Nchi yaomboleza kufuatia kifo cha Michuki

Waziri John Michuki

Picha/MAKTABA Waziri wa Mazingira John Michuki, akihutubia wanahabari afisini mwake mwaka 2011. 

Na MWANGI MUIRURI  ( email Mwandishi)

Imepakiwa - Wednesday, February 22  2012  at 15:3

Kwa Mukhtasari

Rais Mwai Kibaki, alimtaja kama “rafiki wa ndani, mshauri wa kuaminika na kiungo thabiti katika Serikali yangu.” Wabunge nao walitumia takriban saa nzima kumuomboleza.

 

BIWI la simanzi lilitanda kote nchini Jumatano habari za kifo cha Waziri wa Mazingira John Michuki huku wengi wakieleza masikitiko yao kutokana na tanzia yake.

Rais Mwai Kibaki, alimtaja kama “rafiki wa ndani, mshauri wa kuaminika na kiungo thabiti katika Serikali yangu.”

Hadi kifo chake, alikuwa amemuidhinisha Bw Uhuru Kenyatta, kama mrithi mwafaka wa Rais Kibaki, hali ambayo iligeuza mkondo wa kisiasa kuwa na upinzani mkali kwa wagombezi wengine katika eneo hilo.

Wabunge walitumia takriban saa nzima kumuomboleza.

Majonzi aidha yalitanda katika Kaunti ya Murang’a na viunga vyake huku vyombo vya habari vinavyotangaza kwa lugha ya Kikikuyu ikiwemo Kangema FM aliyokuwa akimilki vikitoa mitambo yao ili wananchi watume risala zao za rabirabi kwa mwendazake.

Bw Michuki akiwa na umri wa miaka 80 na ambaye pia alikuwa Waziri wa Mazingira aliaga dunia usiku wa kuamkia Jumatano mwendo wa saa tatu kutokana na maradhi ya moyo.

“Sitaki kuamini habari hizo ni za ukweli. Lakini kwa upande mwingine vyombo vya habari haviwezi kunidanganya haswa ikiwa ni Rais Mwai Kibaki amethibitisha habari hizo. Nitamkosa. Mungu aiweke roho ya mbunge wangu mahali pema peponi,”  akasema Bi Mary Karanja, mkazi wa Kangema.

Katika eneo bunge la Kangema, majonzi yalitanda katika nyumba nyingi ikizingatiwa kuwa zaidi ya asilimia 50 ya wenyeji  hujumuika kama familia yake.

Hali hiyo inatokana na kuwa, babake Michuki Mzee Michuki Kagwi alikuwa na mabibi 47 na ambapo yeye alikuwa kifungua mimba wa Bi Marion Wanjiku ambaye alikuwa bibi nambari 45.

Umaarufu na kupendwa kwa marehemu Michuki kulijidhihirisha wazi, huku shughuli za kawaida katika maeneo mengi zikikwama watu walipojikusanya vikundivikundi kujadili suala hilo.

Miongoni mwa masuala yaliyomshidia umaarufu katika eneo hilo ni rekodi yake ya maendeleo, kutositasita kwake kukabiliana na masuala nyeti ya jamii, kuwa aliyejitokeza kuungana na watu wake wakati wa sherehe mbalimbali na pia misimamo yake mikali ya mujibu wa sheria.

Ulainishaji wa sekta ya matatu kupitia Sheria za Michuki na pia kusambaza maji na umeme kote katika eneo bunge lake kulimfanya awe kiongozi wa hadhi kuu katika jamii za Mlima Kenya na taifa lote kwa jumla.

Add a comment maoni

Share Bookmark Print

Rating

 

 

 

 

 

 

Nukuu muhimu alizotoa marehemu Michuki

John Michuki akiwa kijana.

John Michuki akiwa kijana. 

Na ANTHONY NYONGESA  ( email Mwandishi)

Imepakiwa - Wednesday, February 22  2012  at 14:41

Kwa Mukhtasari

Marehemu Michuki alijulikana kwa hotuba na taarifa zake zilizojaa uzito wa maneno na maana.

 

“Tukijua wewe unataka kuingia kwa Wakikuyu bila ya kupitia kwa Uhuru wa Kenyatta, sisi tutatwanga wewe kisiasa. Uhuru wa Kenyatta ndio kiongozi wa Wakikuyu. Mtu yeyote anayetaka kuzungumza na Wakikuyu, azungumze na Uhuru na Uhuru atatuambia ,” ndio matamshi ya mwisho ya kisiasa ya aliyekuwa waziri wa mazingira John Michuki akiwa Murang’a Oktoba 2011

Aliwapuuza viongozi wengine wa eneo hilo wanaompinga Uhuru huku akisisitiza kwamba katika uchaguzi mkuu ujao, Uhuru ndiye anayepasa kuungwa mkono.

“Ukimchokora nyoka, kuwa tayari kuumwa na nyoka huyo,” ni msemo ambao kamwe hautasahaulika kwa urahisi ambapo Michuki alikuwa akiwajibu wanahabari baada ya afisi za Standard Group kuvamiwa na magaidi wa kukodishwa.  Ilikuwa Machi 2006. Matamshi haya yaliwakera mno wanaharakati na mabalozi waliomtaja Michuki kiongozi kiimla.

“Wacha niseme hapa wazi wazi kwamba aliyekuwa mbunge wa Kabete Paul Muite anayo matatizo chungu nzima yaliyompelekea kupoteza kiti chake cha ubunge. Asijaribu kutafuta nafasi kwa magazeti kwa kujihusisha nami,” waziri Michuki akimwonya Muite mnamo Aprili 2009 aliyedai kwamba maisha yake yalikuwa hatarini

 

“Ati kwa maana unamilki matatu chache sasa unataka kujionea mtu 'special’? Haiwezekani kabisa,” Michuki akiwaonya wanaoendesha biashara ya matatu nchini mnamo Agosti 2008

 

“Hatuna starehe na muda wa kupoteza kwa kuendelea kuhairisha mipango ya kuboresha mazingira. Mataifa yanayostawi yanapasa kuweka makubaliano mengine sawa na yale ya Kiyoko ili kutulinda kimazingira kati ya 2013 na 2017,” alisema Michuki Desemba 2011 alipokuwa jijini Durban, Afrika Kusini kwenye kongamano la mabadiliko katika hali ya anga. Hii ni moja wapo ya kazi ya mwisho ambayo aliitekeleza waziri Michuki kabla ya kuelekea Uingereza kwa matibabu.

 

“Nilipokuwa kwenye wizara ya uchukuzi, niliwatafuta maafisa wa trafiki mimi mwenyewe. Haijalishi ilikuwa saa ngapi au siku gani. Wakati mwingine nilichukuliwa adui na maafisa wa na wenye matatu,” alieleza waziri waziri Michuki mwishoni mwa 2009 alipoingia katika wizara ya mazingira.

 

“Watu wa kuomba omba hawana namna. Kwa kweli sisi tumefanywa watu wa kuomba. Tumefanywa watu wa kuomba omba katika hali ambayo inastahili kuwa haki yetu,” alieleza akilalamikia mataifa yaliyostawi kuyanyanyaza yale yanayokuwa kwenye kongamano OneClimate at COP15 jijini Copenhagen mnamo Desemba, 2009.

Add a comment maoni

Share Bookmark Print

Rating

 

 

 

 

 

 

Aliyechapwa na mkewe aondoa kesi

Mwenyekiti wa chama cha Maendeleo ya Wanaume, Bw Nderitu Njoka.

Picha/MAKTABA Mwenyekiti wa chama cha Maendeleo ya Wanaume, Bw Nderitu Njoka ambaye amekuwa akitetea wanaume akihutubia wanahabari Desemba 17, 2009. 

Na CHARLES MWANIKI  ( email Mwandishi)

Imepakiwa - Wednesday, February 22  2012  at 19:24

Kwa Mukhtasari

Bw Patrick Kimaru Mwangi, aliambia Hakimu Mkuu Mkazi wa Nyeri,  Bi Joan Wambilyanga kwamba alimsamehe mkewe, Bi Eunice Wairema Gaitho, baada ya kuombwa msamaha na kuhakikishiwa kwamba asingechapwa tena.

 

MWANAUME ambaye alikuwa wa kwanza kujitokeza hadharani  kwa kudai kuchapwa na mke wake sasa ametupilia mbali kesi dhidi ya mwanamke huyo mahakamani.

Bw Patrick Kimaru Mwangi, aliambia Hakimu Mkuu Mkazi wa Nyeri,  Bi Joan Wambilyanga kwamba alimsamehe mkewe, Bi Eunice Wairema Gaitho, baada ya kuombwa msamaha na kuhakikishiwa kwamba asingechapwa tena.

Bi Wairema alishtakiwa  Januari 23 kwa madai ya kupiga na kumuumiza Bw Kimaru mnamo Januari 1, katika kijiji cha Ngangarithi, Nyeri.

Wakati Kiongozi wa Mashtaka, Inspekta Bernard Wamalwa alisema kwamba alikwa tayari kuendeleza kesi,  Bi Wairema aliomba kuzungumza, na kueleza kwamba mumewe, ambaye ni msanii mjini Nyeri, alikuwa tayari kuondoa mashtaka hayo dhidi yake.

Hakushurutishwa

Alipoitwa mbele ya korti kuthibitisha ukweli huo, Bw Kimaru alisema kwamba hakushurutishwa na yeyote kuondoa kesi hiyo, bali alifanya hivyo kwa hiari yake.

“Mke wangu ameniomba msamaha na kuniambia kwamba hatarudia kosa hili.  Nimekubali kwani yeye ni mke wangu na sijashurutishwa na yeyote kuondoa mashtaka haya,” akasema Bw Kimaru.

Kwenye kesi nyingine, watu watatu waliioshtakiwa kwa madai ya wizi wa mali kwenye vyumba vya hoteli ya kifahari ya Outspan, wataendelea kuzuiliwa kwenye Kituo cha polisi cha Nyeri hadi Ijumaa kufuatia ombi kutoka kwa upande wa mashtaka.

Add a comment maoni

Share Bookmark Print

Rating

 

 

 

 

 

 

Wabunge waomboleza Michuki

Waziri John Michuki

Picha/MAKTABA Waziri wa Mazingira John Michuki, akihutubia wanahabari afisini mwake mwaka 2011. 

Na JUMA NAMLOLA  ( email Mwandishi)

Imepakiwa - Wednesday, February 22  2012  at 14:54

Kwa Mukhtasari

Kwa zaidi ya saa nzima, wabunge walisimama na kumtaja Bw John Michuki kuwa mwanasiasa aliyekuwa na msimamo; ndani na nje ya bunge.

 

BUNGE Jumatano lilitumia muda wa Mawasiliano kutoka kwa Spika kutuma rambirambi kwa ndugu na jamaa ya marehemu John Michuki.

Kwa zaidi ya saa nzima, wabunge walisimama na kumtaja Bw Michuki kuwa mwanasiasa aliyekuwa na msimamo; ndani na nje ya bunge.

Naibu wa Spika Bw Farah Maalim alianza kwa kulifahamisha bunge kuhusu kifo cha Bw Michuki, na kukitaja kuwa msiba mkubwa.

Mbunge wa Dujis Bw Aden Duale alisema kuwa alimtambua Bw Michuki kuwa mpole lakini aliyependa kutoa masharti yake kwa watu aliokaribiana nao.

“Bw Spika, nataka kusema kuwa nimewahi kukaa na marehemu mheshimiwa Michuki. Alikuwa mwepesi wa kukufanyia lolote, mradi utii masharti yake. Angekununulia chai na mzungumze, lakini usitumie simu yako,” akasema.

“Nakumbuka siku moja tulikuwa tunakunywa naye chai na mheshimiwa Keynan kwa kutumia simu yake tukiwa pamoja,” akasema.

Naibu Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni Bw Amos Kimunya, alisema Bw Michuki hakuwa waziri tu bali rafiki na mtu aliyemshawishi kuingia kwenye siasa.

“Najua Wakenya wengi hawana habari. Mheshimiwa Michuki, Rais Kibaki na mheshimiwa George Muhoho waliniketisha chini Aprili 2002 na kunishawishi niingie katika siasa,” akasema.

Serikali ya kwanza ya muungano

Mbunge huyo wa Kipipiri alisema kwamba mwaka 2008, alishirikiana na Bw Michuki kujadili jinsi ya kubuni serikali ya kwanza ya muungano kwa kuruhusu wabunge wa chama cha ODM Kenya.

“Tuliketi na Bw Michuki tukajadiliana na kukubaliana kubuni muungano huo. Alikuwa mara kwa mara akiniambia kwamba ukiwa kiongozi, huna budi kufanya uamuzi bila kujali kama watu wataukubali au kuukataa. Nataka niseme kuwa nimempoteza rafiki wa kweli,” akasema.

Bw Kimunya ambaye anasimamia wizara ya Uchukuzi, iliyoimarika wakati ikiwa chini ya Bw Michuki, aliwaomba wabunge wawaombee wanasiasa wengine aliosema wanaugua.

Add a comment maoni

Share Bookmark Print

Rating

 

 

 

 

 

 

Madavadi asema hakujadili siasa na Museveni

Waziri Mkuu Raila Odinga na naibu wake Musalia Mudavadi.

Picha/PMPS Waziri Mkuu Raila Odinga (kulia) na naibu wake Musalia Mudavadi wazungumza katika dhifa ya jioni iliyoandaliwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni nyumbani kwa Bw Odinga eneo la Bondo. 

Na AGGREY MUTAMBO  ( email Mwandishi)

Imepakiwa - Tuesday, February 21  2012  at 11:41

Kwa Mukhtasari

Mudavadi asema alihudhuria hafla hiyo nyumbani kwa Waziri Mkuu, Bondo, kama afisa wa serikali wala sio mwanachama wa ODM.

 

Naibu Waziri Mkuu Musalia Mudavadi amekanusha madai kwamba alifanya kikao cha faragha na Rais Yoweri Museveni wa Uganda kuzungumzia siasa za ODM, na uhasama wa kisiasa kati yake na Waziri Mkuu Raila Odinga.

Jumatatu, Bw Mudavadi aliambia wanahabari katika Kaunti ya Kiambu kuwa alihudhuria hafla hiyo nyumbani kwa Waziri Mkuu, Bondo, kama afisa wa serikali wala sio mwanachama wa ODM.

Mudavadi alisema ilikuwa kawaida kwake, akiwa afisa mkuu wa serikali, kuhudhuria hafla ya kiongozi wa taifa lingine aliyezuru Kenya.

“Kwa kawaida, kiongozi wa taifa lingine anapotembelea nchi hii, maafisa wa Serikali kama mimi na wengine hutarajiwa kuhudhuria hafla anazohudhuria ili tuwe sehemu ya ziara hiyo na pia kuhakikisha Kenya imewakilishwa,” akaeleza.

Bw Mudavadi aliongeza kuwa suala la mgogoro kati yake na Bw Odinga halikuzungumziwa wakati wa hafla hiyo ya Jumamosi.

“Tulijadili masuala mengi yanayohusu nchi zote mbili na ni hayo tu. Kwa hakika, Museveni hangeweza kuingilia siasa za ODM. Alizungumzia masuala yanayoathiri Jumuiya ya Afrika Mashariki,” akasema Mudavadi. “Nataka tuheshimu hilo kwa sababu tunamzungumza kuhusu kiongozi wa taifa.

Itakuwa vibaya kuripoti uvumi kuhusu kiongozi wa taifa jirani.”

Kuonyesha umoja katika ODM

Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Idara ya Habari ya Waziri Mkuu baada ya hafla hiyo ilisema kuwa Mudavadi alihudhuria hafla hiyo kuonyesha umoja wa chama cha ODM na kuondoa dhana ambao imeenea miongoni mwa watu wengi, kwamba kuna mgogoro wa kisiasa kati yao.

Lakini msemaji wa Bw Mudavadi, Bw Kibisu Kabatesi, alituma taarifa nyingine kwa vyombo vya habari, akisema mkutano huo haukuhusu chama cha ODM.

Hapo jana, Bw Mudavadi alikiri kuwa aliruhusu taarifa hiyo itumwe kwa vyombo vya habari, lakini akasema hakuna mgogoro wowote katika chama cha ODM kutokana na nia yake ya kuwania tiketi ya urais kwa chama hicho.

Wakati huo huo, Bw Mudavadi alisema wanachama wengi wa ODM wanaunga mkono ushindani kati yake na Bw Odinga, na akakanusha madai kwamba baadhi ya wabunge wa ODM walimwendea wiki jana wakimtaka amwachie waziri mkuu nafasi hiyo.

Add a comment maoni

Share Bookmark Print

Rating

 

 

 

 

 

 

Hofu ya serikali yawafanya wahamishe wanafunzi

Mwenyekiti wa KEPSA, Bw John Mwai

Picha/MAKTABA Mwenyekiti wa Chama cha Shule za Kibinafsi, Bw John Mwai (kushoto) akiwa na Mwekahazina wa chama hicho, Bw Kabiru Ndiritu, kwenye kikao na wanahabari Januari 18, 2012. 

Na WAANDISHI WETU  ( email Mwandishi)

Imepakiwa - Saturday, February 18  2012  at 18:7

Kwa Mukhtasari

Wazazi wanahamisha wanafunzi kutokana na mfumo wa uteuzi wa wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza, ambao kwa miaka mitatu sasa umeonekana kuwapendelea wanafunzi wa shule za umma.

 

WAZAZI wengi wameanza kuwaondoa watoto wao kutoka shule za msingi za kibinafsi na kuwapeleka kwa zile za umma.

Chama cha shule za kibinafsi na kile cha wazazi, vimekiri kuwa kuna uhamishaji wa kiwango cha juu wa wanafunzi, hasa wa madarasa ya saba na nane.

Shule nyingi za msingi za umma sasa zina msongamano mkubwa wa wanafunzi.

Hali hii inatokana na mfumo wa uteuzi wa wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza, ambao kwa miaka mitatu sasa umeonekana kuwapendelea wanafunzi wa shule za umma.

Baadhi ya wazazi wameshutumiwa kwa kuungana na walimu wakuu wa shule za msingi za umma, ili watoto wao wasajiliwe kufanya mitihani yao ya KCPE huko, licha ya kuendelea kusoma katika shule za msingi za kibinafsi hadi mtihani wa KCPE uanze.

Usajili wa wanafunzi si siri

Katibu Mkuu wa Chama cha Wazazi (KNAP), Bw Musau Ndunda, alisema usajili wa wanafunzi kutoka shule za kibinafsi katika shule za umma sio siri.

“Sera ya serikali kuwapa wanafunzi wa shule za umma kipaumbele wakati wa kujiunga na kidato cha kwanza imewasababisha wazazi wengi kuungana na walimu wakuu ili watoto wao wasajiliwe kufanya mitihani yao, huku wakiendelea kusoma katika shule za kibinafsi,” alisema.

Bw Ndunda aliambia Taifa Jumapili kuwa, licha ya hatua hii kukiuka sheria, wazazi hawapaswi kulaumiwa kwani kila mmoja ana haki ya kumtafutia mwanawe masomo mema.

Mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa shule za kibinafsi KEPSA, Bw John Mwai, alisema mfumo huu mpya pia umesababisha wazazi wengi kuwahamisha watoto wao katika shule za umma za malazi.

Karo imezidi

“Nyingi ya shule hizi ni za hali ya juu na hata karo imezidi inayolipwa katika shule nyingi za kibinafsi. Tofauti na  shule nyingi za kibinafsi, shule hizi kama Nairobi Primary, Muthaiga Primary na Nyeri Complex zina vifaa bora na hivyo zinatoa fursa kwa wanafunzi kukubaliwa katika shule za kitaifa,” asema.

Add a comment maoni

Share Bookmark Print

Rating

 

 

 

 

 

 

Wengi wataka Uhuru awanie urais na Ruto

Bw Ruto na Bw Kenyatta

Picha/MAKTABA Bw Ruto (kushoto) na Bw Kenyatta wakiwa kwenye mkutano wa hadhara. 

Na LUCY KILALO  ( email Mwandishi)

Imepakiwa - Monday, February 20  2012  at 20:21

Kwa Mukhtasari

Kulingana na uchunguzi uliofanywa na Ipsos Synovate, asilimia 32 iliidhinisha ugombeaji wa Bw Kenyatta akiwa na Bw Ruto ikilinganishwa na asilimia 14 iwapo Bw Kenyatta atamchagua Bw Musyoka kama mgombeaji mwenza.

 

WAKENYA wengi wangependa Naibu Waziri Mkuu, Bw Uhuru Kenyatta awanie urais akiwa na Mbunge wa Eldoret Kaskazini, Bw William Ruto kama mgombeaji mwenza chini ya muungano wa G7, kura ya maoni imeonyesha.

Kulingana na uchunguzi uliofanywa na shirika la utafiti la Ipsos Synovate, asilimia 32 iliidhinisha ugombeaji wa Bw Kenyatta akiwa na Bw Ruto ikilinganishwa na asilimia 14 iwapo Bw Kenyatta atamchagua Bw Musyoka kama mgombeaji mwenza.

Wagombeaji wengine wanaopendelewa katika kura hiyo ni Bw Musyoka na Bw Eugene Wamalwa pamoja na wagombeaji wengine wakichukua asilimia nane.

Utafiti ulifanywa kati ya Januari 21 na Februari 2 mwaka huu, lakini haukutolewa mapema kwa sababu uligusia masuala yaliyohusiana na Bw Kenyatta na Bw Ruto.

Raila bado aongoza

Hata hivyo, Waziri Mkuu Raila Odinga bado anaendelea kuwa mgombeaji urais maarufu zaidi akiwa na asilimia 31 na kufuatwa na Bw Kenyatta akiwa na asilimia 24 naye Bw Musyoka na 10. Matokeo hayo yalionekana kuwa sawa na utafiti uliokuwa umefanywa awali.

Wengi wa watu zaidi ya 1,500 waliohojiwa watampigia kura Bw Odinga iwapo kutakuwa na marudio ya uchaguzi kati yake na mmoja wa wagombezi wa urais.

 “Bw Odinga atapata asilimia 44 ilhali Bw Kenyatta atapata 42 katika marudio ya uchaguzi. Na ikiwa ni baina ya Bw Odinga na Bw Kalonzo, watakuwa na asilimia 44 na 41. Uchaguzi ukiwa kati ya Raila na Martha Karua, watakuwa na asilimia 43 na 33 na ikiwa ni kati yake na Bw Ruto, atapata asilimia 50 dhidi ya 33,” kura hiyo ya maoni ilionyesha.

Add a comment maoni

Share Bookmark Print

Rating

 

 

 

 

 

 

Apigwa na kuumizwa na mke wa kakake

Mwenyekiti wa chama cha Maendeleo ya Wanaume, Bw Nderitu Njoka.

Picha/MAKTABA Mwenyekiti wa chama cha Maendeleo ya Wanaume, Bw Nderitu Njoka ambaye amekuwa akitetea wanaume akihutubia wanahabari Desemba 17, 2009. 

Na JAMES KARIUKI  ( email Mwandishi)

Imepakiwa - Friday, February 17  2012  at 18:19

Kwa Mukhtasari

Bw Stephen Macharia aliyelazwa hospitalini alisema alikuwa akizozana na kakake kuhusu watakavyolima shamba la wazazi wao.

 

MWANAUME amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Nyandarua akiwa na majeraha kichwani na mkononi, akidai aliyapata baada ya kupigwa na mke wa kakake.

Bw Stephen Macharia akizungumza kwa maumivu kutoka kitanda cha hospitali, aliambia Taifa Leo kuwa alikuwa akizozana na kakake kuhusu watakavyolima shamba la wazazi wao.

“Nikiwa sina habari, mke wa kakangu aliingilia kati na kuanza kunishambulia kwa chuma kichwani, mikononi na miguuni. Kakangu naye alienda kwake nyumbani akarudi akiwa na panga na kumsaidia mkewe kunikata,” akasema.

Alisema kwamba aliwachwa akiwa ameanguka chini na kakake akaamuru tingatinga alilokuwa ameenda nalo hapo shambani kulima liondoke.

“Nimepiga ripoti katika kituo cha polisi cha Huho-ini hapa wilayani Nyandarua Magharibi, lakini kakangu na mkewe wangali huru,” akalalama.

Kisa hicho kilitokea katika eneo la Silibwet.

Mzozo kuhusu shamba

Bw Macharia alisema kwamba mzozo huo kuhusu shamba uliwalazimisha nduguze wengine kuondoka, wakihofia kuwa kaka yao na mkewe wangelitekeleza vitisho vyao kuwa 'watatumaliza’.

“Alitimiza vitisho vyake kwa kunishambulia. Kama hakutachukuliwa hatua, nahofia kuwa huenda akarudia jambo hilo, na safari hii anaweza kuua mtu,” akasema.

Mwanaume huyo mwenye watoto watatu, alisema pia alipata majeraha ya ndani ya mwili, hasa kifuani na mgongoni, kutokana na kichapo cha 'nguvu’ alichopokea kutoka kwa kakake na mumewe.

Tukio hilo la Nyandarua linafuatia msururu wa visa vya wanaume kushambuliwa na wanawake katika maeneo ya Nyeri, Ruiru, Kiambi, Bungoma na Kisii.

Add a comment maoni

Share Bookmark Print

Rating

 

 

 

 

 

 

Uhuru na Ruto wasema hawajamtenga Kalonzo

Bw Ruto na Bw Musyoka

Picha/JENNIFER MUIRURI Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka (kulia) ajumuika na Mbunge wa Eldoret Kaskazini William Ruto baada ya mkutano katika hoteli ya Norfolk, Nairobi Februari 17, 2012. 

Na JAMES KARIUKI  ( email Mwandishi)

Imepakiwa - Saturday, February 18  2012  at 17:46

Kwa Mukhtasari

Wakihutubia mikutano ya hadhara katika maeneo mbali mbali ya Nyandarua, wawili hao na wafuasi wao walisema lengo lao ni kudumisha umoja na kuhakikisha Wakenya wanapata viongozi bora.

 

NAIBU Waziri Mkuu Uhuru Kenyatta na Mbunge wa Eldoret Kaskazini Bw William Ruto, Jumamosi walisema hawana nia ya kumtenga Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka.

Wakihutubia mikutano ya hadhara katika maeneo mbali mbali ya Nyandarua, wawili hao na wafuasi wao walisema lengo lao ni kuhakikisha Wakenya wanapata viongozi bora.

Walisema wataungana kuhakikisha Wakenya hawapigani tena kama ilivyokuwa mwaka 2008, ambapo watu wengi waliuawa kutokana na ukabila.

“Kama ni Uhuru, Kalonzo, Murungi, Wamalwa, Ruto au yeyote mwengine, kuweni tayari kuungana nasi ili tumpe nafasi ya kuwapa Wakenya huduma zinazoambatana na sera nzuri,” alisema Bw Ruto.

Aliambia wananchi waliojitokeza katika maeneo ya Ndaragwa, kwa Kung’u, Mairo Inya, Nyahururu, Ol Jororok na Ol Kalou mjini kuwa uongozi wao utashughulikia uhaba wa ajira miongoni mwa vijana na kuwapa wakulima pembejeo za kilimo, miongoni mwa huduma nyingine muhimu kwa wananchi.

Wawili hao waliandamana na wabunge 20 kusema kuwa G7 ni mtandao mmoja usioweza kuvurugwa na yeyote.

Madai ya kutengwa

Mbunge wa Horr Kaskazini Bw Chachu Ganya, aliongoza wabunge wengine kusema kuwa makamu wa Rais atakuwa sehemu ya kundi hilo.

“Madai kuwa tumemtenga Kalonzo ni ya vyombo vya habari. Kundi letu la G7 linahitaji kura kutoka kwa kila mtu na hatuwezi kumtenga Kalonzo,” akasema.

Mwenzake wa Dujis Bw Aden Duale, alisema kwamba ni viongozi chini ya G7 pekee watakaotambuliwa na viongozi hao.

Chini ya mwito wa “Tuko Pamoja” Waziri Msaidizi Mwangi Kiunjuri aliwaomba vijana wachukue vitambulisho na kujiandikisha kwa wingi kuwa wapiga kura.

Alisema si sawa kwa vijana ambao ndio wenye kauli katika uchaguzi, kuwaachia watu wengine kuwachagulia viongozi.

Add a comment maoni

Share Bookmark Print

Rating

 

 

 

 

 

 

Wawili kizimbani kwa madai ya kuroga

Na JAMES KARIUKI  ( email Mwandishi)

Imepakiwa - Thursday, February 16  2012  at 19:14

Kwa Mukhtasari

WATU wawili wanaodaiwa walisafiri kutoka Kisii hadi Kaunti ya Laikipia ili kuwaroga jamaa waliokosa kulipa deni, Alhamisi walishtakiwa kwa uchawi katika mahakama ya Nyahururu.

 

WATU wawili wanaodaiwa walisafiri kutoka Kisii hadi Kaunti ya 

WATU wawili wanaodaiwa walisafiri kutoka Kisii hadi Kaunti ya Laikipia ili kuwaroga jamaa waliokosa kulipa deni, Alhamisi walishtakiwa kwa uchawi katika mahakama ya Nyahururu.

Laikipia ili kuwaroga jamaa waliokosa kulipa deni, Alhamisi walishtakiwa kwa uchawi katika mahakama ya Nyahururu.

Lakini wawili hao, Bi Judith Nasu Watila, 49  na “mwelekezi wake” Bw Justus Nyakora Mwebi, 40 walikanusha mashtaka hayo mbele ya hakimu mkaazi, Bw Vincent Kiptoon.

Wawili hao waliwachiliwa kwa dhamana ya Sh300,000 na mdhamini wa kiasi sawa na hicho kwa kila mmoja.

Mahakama ilielezwa kuwa usiku wa Februari 13 katika eneo la Gatundia, wilayani Laikipia Magharibi, washtakiwa wakiwa na nia ya kutisha familia ya Bw Jackson Mogusu, walisambaza ndumba yao ambayo ilikuwa majani makavu na mifupa iliyovunjika katika boma hilo, huku wakitamka maneno ambayo hayakueleweka kwa nia ya kuroga familia hiyo.

Waliua ng'ombe

Mahakama pia ilifahamishwa kuwa tarehe hiyo, washukiwa waliua ng’ombe na ndama wake masaa ya alfajiri na pia kuingia katika boma la Bw Mogusu bila idhini.

Bi Watila aliambia mahakama kuwa  alikuwa ameajiriwa na mwanamume ambaye sasa ametoweka. Hata hivyo, alikiri kuwa na ndumba hiyo ingawaje alikanusha kuwa zilitumiwa kumroga mlalamishi.

Mahakama iliagiza kesi hiyo isikizwe Machi 16 na kwamba mshtakiwa apelekwe jela la wanawake la Nyahururu baada ya kushindwa kulipa dhamana.

Add a comment maoni

Share Bookmark Print

Rating

 

 

 

 

 

 

Most Popular