Dunia tambara bovu

Na Ibrahimu G. Mzava

Imepakiwa - Tuesday, November 29  2016 at  13:04

Kwa Mukhtasari

Mi tuli nimetulia dunia,

Mambo yanayotokea, katika hii dunia,

Ni wazi yanatishia, kuta watu wanalia,

Dunia tambara bovu, limeoza linanuka.

 

Vitisho vya kuuwana, kusikia kawaida,

Watu wanavyochinjana, ulimwengu una shida,

Kila siku twapigana, vita visivyo faida,

Dunia tambara bovu, limeoza linanuka.

 

Dini zaficha uovu, siku hizi kuna mambo,

Imani za kipotevu, watu wana majigambo,

Washindana fuga ndevu, kuta kuchapana,

Dunia tambara bovu, limeoza linanuka.

 

Kanisani fujo tupu, waumini visirani

Akilini kwenye vikapu, si kupeana imani,

Kwa imani ni watupu, hawakosi kanisani,

Dunia tambara bovu, limeoza linanuka.

 

Uchawi umekithiri, wazee si vijana,

Hakuna cha sirisiri mambo yote ni bayana,

KIla mtu ni hatari, uchawi umetubana,

Dunia tambara bovu, limeoza linanuka.

 

Hakuna muaminifu, dunia imetusomba,

Hata akirudi mtu, kufa tena ataomba,

Mambo yapo rafurafu, na hayaendi sambamba,

Dunia tambara bovu, limeoza linanuka.

 

Chuki wivu usiseme, kazini na majumbani,

Nasema acheni seme, yamenikaa  kooni,

Vipi  nijihemeheme, wa kumuogopa nani?

Dunia tambara bovu, limeoza linanuka.

 

Haki za kibinadamu, ni maficho ya madhambi,

Binadamu kwa haramu, ni fundi mpika dhambi,

Vitu vyote vya haramu, afanya ajali dhambi,

Dunia tambara bovu, limeoza linanuka.

 

Ndoa ya jinsia moja, eti siku hizi  ruksa,

Mimi kwangu ni kioja, wao waziita fursa,

Mungu wangu ni mmoja, ni nusuru na mikasa,

Dunia tambara bovu, limeoza linanuka.

 

Dhambi ukizikemea, we adui wa dunia,

Watu watakuchukia, ukweli inakwambia,

Kila utapoingia, gaidi watakwambia,

Dunia tambara bovu, limeoza linanuka.

Mungu dunia ya kwako, binadamu tunapata,

Ilinde dunia yao, iyepushe na vita,

Najua uwezo wako, unashinda vyote vita,

Dunia tambara bovu, limeoza linanuka.

 

Leo nasimama hapa,  shairi limeishia,