JE, UCHAGUZI UTAKAOKUJA UTALETA MAENDELEO ENDELEVU?

Na Hezekiel Gikambi  ( email Hezekiel Gikambi)

Imepakiwa - Friday, February 3  2012  at 7:52

 

Inasikitisha kuwa baadhi ya wanafunzi bora katika mtihani wa KCPE hawatajiunga na shule za kitaifa kufuatia sera ambayo serekali inaitumia kuwateua wanafunzi. Sera hii imewaathiri wanafunzi wengi waliosomea katika shule za kibinafsi walioibuka na alama bora katika mtihani huo. Hili ni jambo la kutamausha sana hasatukizingatia kuwa shule hizi zinachangia pakubwa katika ukuaji wa elimu nchini kwa kufidia upungufu wa shule za serikali.

Iweje kuwa mwanafunzi aliyepata zaidi ya alama 432 katika mtihani wa KCPE ananyimwa fursa ya kujiunga na shule ya kitaifa ilhali alama zake tayari zinaonyesha juhudi kubwa alizozitia katika kutimiza ndoto yake? Kinaya ni kuwa utapata kuwa yule aliyepata alama 350 amepata nafasi katika shule hizi eti kwa kuwa alisomea katika shule ya msingi ya umma. Je, ni nini ambacho kinaifanya serekali kumwacha mwanafunzi kama huyu?

Ukweli ni kuwa nyingi ya shule za kibinafsi zimejitahidi sana kuimarisha viwango vya masomo nchini na hazistahili kuchezewa karata dakika za mwisho mwisho wakati zinastahili kufurahia matunda yake. Hakuna shaka yeyo ambayo ilitolewa na serekali kuhusu matokeo ya shule hizi ambayo ingeifanya serekali kudunisha matokeo yao. Hata hivyo, mbubujiko wa wanafunzi katika shule hizi katika siku za hivi karibuni ni idhibati tosha ya ubora wa shule hizi na thamani ya masomo yaliyopo ikilinganishwa na zile za umma.

Serikali isitarajie kukua kwa viwango vya elimu nchini iwapo itaendeleza mtindo baguzi ambao unaelekea kuwazawadia wanafunzi waliofeli katika mitihani hiii. Hatua hii ni kandamizi, isiyo ya kimaadili na ya kibaguzi.Wakati tunapofikiria kuhusu malengo ya Milenia ya ‘Elimu kwa wote’, serikali inastahili kuhakikisha kuwa hadhi ya juu ya masomo imezingatiwa kwa vyo vyote vile.

Kwa kuwabagua wanafunzi waliosomea katika shule za upili za kibinafsi, serekali inaweka mpaka wa kielimu ambao una hatari ya kushusha viwango vya elimu nchini. Miongoni mwa mambo mengine, mtindo huu utazitamausha shule za kibinafsi na watu wanaokusudia kuwekeza katika elimu nchini. Hili likitokea, mustakabali wa elimu nchini utakuwa mbaya sana.  

Wizara ya Elimu haina budi  kubatilisha mfumo huu na kutumia mfumo ambao utaonekana kuwa wa haki na wa usawa kwa wote. Ni muhumu pia kwa serikali kusikia kilio cha washikadau wa shule za kibinafsi ili isije ikarudisha mipango ya elimu nchini nyuma. Washikadau hawa wanatekeleza mchango muhimu sana katika sekta ya elimu na hawapaswi kupuuzwa.

 Wakati umefika wa serekali kuzihusisha shule za kibinafsi katika shughuli ya uteuzi wa wanafunzi ili zipate fursa ya kushiriki kikamilifu katika mfanyiko wa uteuzi. Serekali iwatendee haki wanafunzi walioongoza katika mtihani wa KCPE.

Kennedy Opindi

Share Bookmark Print

Rating

 

 

 

 

 

 

Most Popular

Wabunge 175 kutahiriwa Zimbabwe

Wabunge 175 nchini Zimbabwe watapashwa tohara kufikia mwisho wa mwezi ujao katika juhudi za kuhamasisha wanaume

Mwanawe Waziri wa Fedha ajitia kitanzi

MWANAWE Waziri wa Fedha Njeru Githae anadaiwa kujiua nyumbani kwao Runda, Nairobi. Polisi wameanzisha uchunguzi

Polisi waendelea kusaka walioshambulia Mombasa

Polisi wameanzisha msako mkali kutafuta washukiwa waliotekeleza shambulio la kigaidi katika mkahawa wa Bella Vista,

Utengano wakumba ukumbusho wa Wanjiru

Ibada mbili tofauti zilifanywa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha bingwa wa marathon katika Olimpiki Samuel