Siwiji alobingika, ambaye ataka tengwa,
Atwambe amelimka, mjuzi asiyepingwa,
Kama yuko kwa hakika, ni mrongo amerengwa,
Hakuna bingwa wa bingwa, wala gwiji wa daima!
Tungajipa kuswifika, swifa hazina kupangwa,
Kwani huku kutajika, kwengine kuvungwavungwa,
Hata tukijashtuka, si kweli yaliyorongwa,
Hakuna bingwa wa bingwa, wala gwiji wa daima!
Kuna wasopumzika, wakitefuta kuwangwa,
Na juu wakijipeka, wakitaraji kuengwa,
Mwishowe hugundulika, wakabaki kusimangwa,
Hakuna bingwa wa bingwa, wala gwiji wa daima!
Baadhi huhangaika, kupitiya zote nyangwa,
Si watu huambilika, wamekubuhu kwa nongwa,
Hujiona wamefika, muhali kwao kuzongwa,
Hakuna bingwa wa bingwa, wala gwiji wa daima!
Fundi wa kujibandika, twabiyaye nda kugungwa,
Uganga anoushika, ajuwe kunavyogangwa,
Ima atafedheheka, kuringiya amalingwa,
Hakuna bingwa wa bingwa, wala gwiji wa daima!
Tangu nyaka na vikaka, majagina wangalungwa,
Ipo siku hutoweka, yao yasazwe kudungwa,
Wangine wakaibuka, nao piya wakajengwa,
Hakuna bingwa wa bingwa, wala gwiji wa daima!
Wabunge 175 nchini Zimbabwe watapashwa tohara kufikia mwisho wa mwezi ujao katika juhudi za kuhamasisha wanaume
MWANAWE Waziri wa Fedha Njeru Githae anadaiwa kujiua nyumbani kwao Runda, Nairobi. Polisi wameanzisha uchunguzi
Polisi wameanzisha msako mkali kutafuta washukiwa waliotekeleza shambulio la kigaidi katika mkahawa wa Bella Vista,
Ibada mbili tofauti zilifanywa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha bingwa wa marathon katika Olimpiki Samuel