http://www.swahilihub.com/image/view/-/4565094/medRes/1975176/-/k3r6s9/-/New+Document.jpg

KWANNI MIMI?

Na Beatus Kusaga

Imepakiwa - Wednesday, May 16  2018 at  16:48

Kwa Muhtasari

Ng'ombe wa maskini hazai, na kama akizaa huzaa dume lisilo na faida

Laiti ningejua kama yatatokea haya nisingefanya maamuzi ambayo leo hii yananigharimu, kwanza fedhea ambayo naipata sababu kila anayesimuliwa hutamani kuniona, pia nimepoteza muda mwingi kusoma lakini leo naishia hali hii.

Umaskini! Umaskini! Umasikini! Daaaaah Sitosaha...

Tumezaliwa wawili katika familiya yetu nikiwa wa kwanza kuzaliwa ila kwa bahati iliyo mbaya kabisa baba yetu alifariki na kutuacha wadogo. Namshukuru Mungu kwa sababu mama alitulea katika maadili ikiwa ni husia kutoka kwa marehemu baba.

 Ndugu walitudhihaki kwa maneno ya kejeli kila walipokuwa wakipita karibu na nyumbani. Nilikuwa naumia sana, sitosahau siku matokeo ya kidato cha sita yalipotoka kabla sijaangalia nilikuwa na hofu kubwa sababu yalisemwa mengi na ndugu upande wa baba yangu.

Baba mdogo aliahidi endapo nitafaulu basi angejisaidia mafungu mafungu kutoka Kariakoo hadi Ubungo pia shangazi

Alisema akifaulu natembea uchi kutoka nyumbani kwangu hadi gengeni kwenda na kurudi.

 Niliomba dua za kila aina Mungu anisimamie yasije kutimia yale yaliyotegemewa. Ilipofika jioni nilienda kuangalia matokeo yangu na katika siku niliyokuwa na furaha ni siku hiyo maana nilikuwa nimepata Division one ya pointi sita. Mimi, mama na mdogo wangu tulifurahi sana lakini baada ya dakika kadhaa mama alikosa raha na akaanza kulia. Wote tukakosa furaha, niliingiwa huzuni na kutaka kujua mama analia nini wakati mwanae nimefaulu vizuri.

 Mama aliniambia kwa huzuni, “Mwanangu, natamani baba yako angekuwepo, tungesaidiana jukumu hili ila kwa kuwa nilimuahidi kuwa nitawalea wanangu, basi Mungu atanisaidia.

Baada ya muda wa miezi kadhaa, mama alimsimamisha mdogo wangu kimasomo na kumwambia, “Cassogera nimekupa jina la baba yangu ambaye alikuwa na huruma na uvumilivu hivyo naomba usimame kimasomo ili Michael aende shule na endapo atafanikiwa atakusomesha na kutusaidia”. Cassogera alikubali.

 Nami  nilimuuliza mama,  ‘Kwa nini niliitwa Michael?’ Mama alitabasamu na kusema, “Aah! Michael ni jina ambalo ulipewa na baba yako ila kibiblia lina maana ya malaika mlinzi. Baba yako aliamini kuwa wewe ndiye utakayelinda familia hii”, nilifurahi sana.

 Baada ya miezi kadhaa nilianza chuo ambapo nilichaguliwa kujiunga katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, kitivo cha sharia. Baada ya miaka minne nilifanikiwa kumaliza degrii yangu ya kwanza na kusoma mwaka mmoja shule ya sheria (shool of law) na kuwa mwanasheria kamili.

 Ajira ilikuwa tatizo na nilikaa mtaani takriban miaka minne na nikajikuta nakata tamaa, nikafanya maamuzi ambayo mpaka leo najutia.

Umaskini, fedhea na dharau kutoka kwa ndugu ndio vilivyoniponza na chachu ya matatizo haya.

Siku moja nilikutana na rafiki yangu niliye soma naye kuanzia sekondari hadi chuo kikuu akiendesha gari na ana maisha mazuri. Alinipa ushauri ambao mwanzo niliukataa lakini kadri shida zilivyonisonga niliona bora nimsikilize. Aliniambia, Kama ukijiunga huku nilipo, chochote utakachokitaka utakipata, cha msingi ni kufata masharti tu. Akanipeleka kwa mganga ambaye wenyewe walimuita mtaalamu na sharti alilonipa ni kwamba, nihakikishe kuwa nisioge ama kugusa maji ya mvua na kama nikiyagusa hata kwa bahati mbaya niende kwake kabla ya masaa matatu”. Kwa kuwa nilikuwa na shida, nilikubali.

Baada ya wiki mbili niliajiliwa kama mwanasheria wa kampuni ya sigara hapa nchini na pesa zikawa siyo shida tena kwangu. Nikajenga nyumba nzuri ya kifahari. Ndugu walianza kujisogeza na bila kinyongo niliwasaidia kwa kusomesha watoto wao na kadharika.

Siku moja mama aliugua sana usiku kiasi kwamba alikuwa akilia na kututaja majina kisha kumtaja marehemu baba. Nilishikwa na kiwewe na usiku huohuo mimi na mdogo wangu tulimkimbiza hospitali.

 Tulipoianza safari, mvua kubwa ilianza kunyesha. Tulipokaribia hospitali gari lilizima ghafra huku mama alikuwa akilia na kusema “Jamani wanangu... Wanangu nawaacha na nani?”

Nilishuka haraka na kujaribu kufungua huku na kule lakini gari halikutengemaa. Nililoa chapachapa. Ghafra ikapita taksi tukaichukuwa na kuwahi hospitali. Nashkuru Mungu mama alipata matibabu na kuwekwa mapumziko. Nilikuwa na mawazo usiku ule kwamba kama mama angefariki tungepata wapi mapenzi ya kweli?

Usiku ule tulirudi nyumbani tukalala, nikiamini kwamba nikiamka asubuhi tutawahi hospitali. Mpenzi msomaji, mpaka naandika simulizi hii sijawahi kupata msaada zaidi ya kufanywa kama sinema na wananiona kama mhusika jasiri na wa kutisha katika tamthiliya fulani.

Kesho yake nilipoamka asubuhi sikuamini jinsi nilivyokuwa nauona mwili wangu maana mwili ulibadilika na kuwa kama kuku aliyenyonyolewa na kukaushwa vizuri kwa moto huku kichwa changu kikiwa kimebadilika na kuwa cha kuku.

 Nikapoteza sura nzuri niliyokuwa nayo, hivyo kuanzia siku hiyo sikuweza kuongea. Kila nilivyojaribu kutaka kuongea nilijikuta nawika kama jogoo na kilichofata niliandika maelezo haya ili yeyote atakayesoma ajifunze kuwa, “Ng'ombe wa maskini hazai, na kama akizaa huzaa dume lisilo na faida”. Naumia sana hasa ninapomuona mama yangu ambaye baada ya kusikia haya aliangua na kujikuta anapalalaizi mwili mzima na Cassogera ndiyo msaada wetu.

Beatus Kusaga, Kasuku
0719368158