22/9/2012 comment

 

Mauya Omauya : Uhuru usitumiwe kuudhi Waislamu duniani

Mataifa ya Magharibi yameeneza taswira kwamba Uislamu ni dini isiyopalilia uhuru na demokrasia .  Kamwe hayawezi kutetea utangamano duniani ikiwa yanaruhusu uhuru ndani ya mipaka yake kuzidi  soma zaidi...


18/9/2012 comment

 

Mauya Omauya : Tuambiane ukweli kuhusu Sheikh Rogo

Alipokuwa hai, Sheikh Rogo limiminia sifa wapiganaji wa al-Shabaab na al-Qaeda na kuhimiza vijana waige mfano wa 'muhajidin' hao. Huku waliomuua Rogo wakisakwa na natumai waadhibiwe, tuambiane  soma zaidi...


24/8/2012 comment

 

Mauya Omauya : Waorma na Wapokomo wajue ghasia huzaa ghasia

Kiini cha uhasama kati ya Waorma na Wapokomo kingali,  hasa uchochezi wa wanasiasa na kukurukakara za  kujitafutia riziki. Kwa mazoea na uzembe wa kutenda, nina hakika  mauaji zaidi yaja.  soma zaidi...


11/8/2012 comment

 

Mauya Omauya : Miungu walimpa Baraza kamba, akajinyonga

Miungu walimpa kamba Naibu Jaji Mkuu Bi Baraza afunge na kudhibiti zimwi la dhuluma katika jamii, akajitia kitanzi kwayo. Mwiba wa kujidunga hauambiwi pole.  soma zaidi...


4/8/2012 comment

 

Mauya Omauya : Mwisho wa Assad umefika, hakuna wa kumwokoa

Kuna msemo usemao kwamba miungu wanapoamua kuangamiza mja, mwanzo wanamtia wazimu. Baada ya kumtia kichaa, miungu hawana haja tena kuhusika kwa sababu wameamsha mfululizo wa hatua ambazo  soma zaidi...


28/7/2012 comment

 

Mauya Omauya : MRC wajue chuma chao ki motoni

Iwapo MRC walitamani au kuzoea vya kunyonga sasa Mahakama imewapatia fursa kujizolea vya kuchinja na kama hawawezi uamuzi huu wa mahakama utakuwa ndio mwanzo wa mwisho wa safari yao. Kisheria, sasa  soma zaidi...


23/7/2012 comment

 

Mauya Omauya : Kitabu cha Miguna bila malipo, balaa kuu!

Ni huzuni kwamba hata kabla ya wiki kupita tangu kuzinduliwa kwa kitabu cha Miguna Miguna, nakala ilikuwa ikisambazwa mtandaoni. Wizi huu usipokomeshwa hakika sekta ya uchapishaji itadorora na  soma zaidi...


13/7/2012 comment

 

Mauya Omauya : Miguna: Kitabu cha kuku kuhusu mwewe?

Huku tukisifu juhudi za aliyekuwa Mshauri wa Waziri Mkuu Miguna Miguna, ni bayana kuwa kitabu  chake kingekuwa na ladha tofauti mno ikiwa hangekiandika katika mazingira ya mgaragazano wake na bosi  soma zaidi...


11/7/2012 comment

 

Mauya Omauya : Hata Kony aje tu! 'Hakuna matata’

Katika mazingiria tuliyo nayo Kenya, hapana ajabu tukialika Joseph Kony aje Nairobi. Karibu Komredi Kony, kasri lako tayari, njoo na wandani wote wa Lords Resistance Army, njoo kwenye Paradiso ya  soma zaidi...


9/7/2012 comment

 

Mauya Omauya : Raia ni nguzo kuu katika vita dhidi ya ugaidi

Ukweli ni kuwa katika mashambulizi yote tuloshuhudia mijini Nairobi, Mombasa na  Garissa, kuna raia waliofahamu kilichotendeka na waliokitenda lakini wamefyata ndimi. Raia ndio tu wanaweza kusaidia  soma zaidi...


5/7/2012 comment

 

Mauya Omauya : Uadui wa kidini? Tazameni Nigeria

Waliopofuka kwa imani iendeshayo chuki hawasikii nasaha na hawapendi kuipata. Mjadala kuhusu ukweli wa imani katika dini hauna dawa wala hatima. Tazameni Nigeria, taifa linalozidi kuoza kwa sababu  soma zaidi...


3/7/2012 comment

 

Mauya Omauya : Wakenya wajulishwe walanguzi wa mihadarati

Nasubiri siku raia wa Kenya watafahamu hata punje kuhusu wanaolangua dawa za kulevya! Hadi siku hiyo tutateremea kuogelea kwenye bahari hii ya 'hatujui’ na 'heri sahau’.  soma zaidi...


20/6/2012 comment

 

Mauya Omauya : Amkeni tumalize kejeli kwa Afrika

Wiki hii Shirika la Ndege la Korea Kusini lilijulisha wageni kwamba wakija Kenya watajionea na kukutana na watu 'walio na ari kuu ya ukosefu wa ustaarabu'. Sijali iwapo hili la Korea ni kosa la  soma zaidi...


13/6/2012 comment

 

Mauya Omauya : Malawi kukiuka AU kuhusu Bashir ni ushujaa

Rais wa Malawi Joyce Banda wa Malawi amesema waziwazi kwamba nchi yake itachukua mwelekeo tofauti na amekataa kumkaribisha Rais wa Sudan Omar al-Bashir anayetafutwa na ICC kwa makosa ya uhalifu wa  soma zaidi...


12/6/2012 comment

 

Mauya Omauya : Hukumu ya  Mubarak ni onyo mwafaka kwa madikteta

Hukumu ya Rais Hosni Mubarak ni ujumbe na onyo mwafaka kwa madikteta waliozoea minofu ya ukuu huku raia wakiguguna fupa la dhiki. Demokrasia halisi itawasili wakati viongozi watachukua jukumu lao  soma zaidi...


9/6/2012 comment

 

Mauya Omauya : Heri kuwapa sindano wanaotumia mihadarati

Tusizibe macho kwa ndwele hizi katika jamii. Kuwapa sindano wanaotumia dawa za kulevya kutawatoa gizani, serikali itawafahamu waliko, itawapa mafunzo nasaha kuepuka uraibu huo na itawaokoa kutokana  soma zaidi...


1/6/2012 comment

 

Mauya Omauya : Tusipoziba ufa wa MRC tutalazimika kujenga ukuta

Wanasiasa watatumia kilio cha MRC kujishindia ushabiki wa muda. Wanafaa wafahamu kwamba wanapanda mbegu ya kuchochea uhasama kwa kudhalilisha utawala wa katiba, na baadaye hakika taifa hili  soma zaidi...


1/6/2012 comment

 

Mauya Omauya : Ni vigumu kujivunia hali yetu kama Wakenya

Ni vigumu kujivunia kuwa Mkenya. Historia yetu imejawa na ukabila, ufisadi, ujinga, barabara mbaya, ajali barabarani, elimu duni, ghasia za kisiasa, ubinafsi wa viongozi, wizi wa kimabafu,  soma zaidi...


26/5/2012 comment

 

Mauya Omauya : Samahani Uhuru, siamini ukombozi umefika

Haidhuru, Mgalla muue na haki mpe; Bw Uhuru Kenyatta aliandaa sherehe iliyowaacha wengi wametanua vinywa wazi kwani kila hatua ilivutia hisia, bila shaka ilimgharimu kitita kinono mno. Si hoja,  soma zaidi...


17/5/2012 comment

 

Mauya Omauya : Ushoga Amerika: Pilipili usiyoila yakuwashiani?

Yaliyokubalika juzi, yalikanwa jana, yaliyokanwa jana, yanakubalika leo. Rais Obama alipokubali ndoa za watu wa jinsia moja alifahamu kwamba jamii ya Amerika ina raia wa kila nui. Tunaomkashifu  soma zaidi...


Zilizopata Umaarufu