Uchambuzi wa riwaya ya Takadini

Na MGENI WETU

Imepakiwa - Tuesday, April 10  2018 at  15:07

Kwa Muhtasari

Riwaya ya Takadini imeandikwa na Ben Hanson na kuchapishwa na Mathew Books and Stationers, Dar es Salaam mwaka 2004.

 

Utangulizi

TAKADINI ni mtoto aliyezaliwa akiwa sope (mlemavu wa ngozi) baada ya mama yake, Sekai kukaa miaka tisa bila kupata mtoto.

Makwati, mume wa Sekai alitarajia kupata mtoto wa kiume kwa Sekai baada ya wake zake watatu wote kumzalia watoto wa kike. Wakunga walitaka kumuua mtoto kwa kuwa alikuwa sope, Sekai alikataa. Baada ya Makwati kupata taarifa juu ya kuzaliwa kwa mtoto wa kiume akiwa sope, alimtuhumu kuwa alitoka nje ya ndoa na mtoto alikuwa kama adhabu.

Kwa kuwa Sekai alitaka mtoto aishi, ilimpasa yeye na mwanawe kuuawa. Baada ya Sekai kupata taarifa hiyo kutoka kwa mumewe, aliamua kujitoa mhanga kwa kutoroka yeye na mtoto wake. Alikutana na Chivero ambaye alikuwa akitafuta kuni, aliwachukua na kwenda kuongea na Mtemi Masasa na hatimaye walikubaliwa kubakia pale kijijini. Wanakijiji hasa wanawake waliwakataza watoto wao kucheza na takadini. Takadini alinyanyaswa na kuonewa na watoto wenzake lakini alipata faraja pekee kutoka kwa mama yake na kwa Chivero kama baba yake.

Shingai mtoto wa Nhariswa aliangukia katika penzi zito la Takadini ingawa ilikuwa kwa siri. Wazazi wa Shingai walitaka mtoto wao aolewe na Nhamo lakini Shingai hakumpenda. Wiki mbili kabla ya harusi ya Nhamo na Shingai, Shingai alitoroka na kwenda kwa Takadini. Shingai alishika ujauzito na kuzaa mtoto wa kiume ambaye hakuwa sope. Sekai alirudi kijijini kwao na familia yake mpya.

 

1:Wahusika

Sekai

Ø Mke wa Makwati

Ø Mama wa Takadini

Ø Jasiri

Ø Mwanamapinduzi

Ø Ana mapenzi ya dhati

Makwati

Ø Mume wa Sekai

Ø Ana mapenzi ya dhati kwa wake zake

Ø Ana wake wa nne (ndoa za mitalaa)

Takadini

Ø Mtoto wa Makwati na Sekai

Ø Mume wa Shingai

Ø Sope

Ø Mpigaji mbira

Shingai

Ø Mke wa Takadini

Ø Mtoto wa Nhariswa

Ø Mwanamapinduzi

Ø Mwenye mapenzi ya dhati

N’nanga Chivero

Ø Baba mlezi wa Takadini

Ø Mkarimu

Ø Mwenye busara

Ø Jasiri na shujaa

Mtemi Masasa

Ø Mwenye hekima na busara

Ø Rafiki wa Chivero

Ø Shujaa

Tendai

Ø Mke mdogo wa mtemi Masasa

Ø Ameolewa akiwa na umri mdogo

Ø Rafiki wa Sekai

Pindai

Ø Mke wa pili wa Makwati

Ø Mama wa Pamidzai na Netsai

Dadirai

Ø Mke wa tatu wa Makwati

Rumbidzai

Ø Mke wa nne wa Makwati

Ø Mwenye kejeli, roho mbaya

Ambuya Tukai

Ø Wakunga