Aina za matendo uneni zilizoboreshwa pamoja na dhana ya uolezi

Na MGENI WETU

Imepakiwa - Friday, December 22  2017 at  06:27

Kwa Muhtasari

Katika makala iliyotangulia tuliangazia kwa kina kuhusu matendo uneni.

 

KATIKA makala iliyotangulia tuliangazia kwa kina kuhusu matendo uneni.

Hii leo tutachambua kuhusu aina ya matendo uneni yaliyoboreshwa jinsi ifuatavyo:

1. Ahadi

Haya ni matendo uneni ambayo humfunga mnenaji katika utekelezaji wa kile alichokinena kwa siku za baadaye.

Mfano wa vitenzi kwa tendo uneni hii ni; tuza, ahidi, zawadi, na kadhalima ni lazima utekeleze.

2. Maelekezo/ Directives

Haya ni matendo uneni ambayo hulenga kuchochea jambo fulani lifanyike na msikilizaji kama atakavyo msemaji.

Vitenzi vinavyoweza kutumika ni pamoja na; amrisha, omba, onya, shauri, pendekeza, sihi na kadhalika.

Kwa mfano:

Tunapendekeza jaribio la Pragmatiki lifanyike Alhamisi badala ya Jumatano

Nakusihi uachane na kile kivulana chako cha chuo

3. Hisia (Expressive)

Haya ni matendo uneni ambayo hudhihirisha hisia, imani, mitazamo au mawazo ya msemaji juu ya jambo fulani. vitenzi kama vile; shukuru, pongeza, sifu, fariji, samehe na kadhalika hudhihirisha.

Kwa mfano:

Nimeamua kukusamehe rafiki yangu

Nashukuru kwa wema wako

4. Matamko

Ni matendo uneni ambayo hunenwa kwake hubadili ukweli fulani wa mambo katika dunia.

Vitenzi vinavyoweza kutumika ni kama vile; jiudhuru, achisha kazi, fungua (mkutano), funga (mkutano), hukumu, oza(mke au mume), tangaza, kupa jina na kadhalika.

Kwa mfano;

Kuanzia leo nimekuachisha kazi

Kuanzia sasa natangaza kwamba Wiliam na Helena ni mume na mke

Naufungua mkutano rasmi, mjisikie huru kuchangia hoja

5. Uwakilisho

Haya ni matendo uneni ambayo hueleza kile ambacho mnenaji haamini kuwa ni kweli au si kweli. Matendo uneni ya aina hii hujumuisha maelezo, shadidia au mahitimisho

kwa mfano:-

Lulu hakumuua Kanumba.

Wanaume si waaminifu katika uhusiano.

Wasichana wa mjini hawana mapenzi ya kweli.

Wanaume sio waaminifu katika uhusiano.

Kada yule hatapitishwa na chama chake kugombea urais na chama chake mwaka huu.

Yule mwanao wa pili wa kiume ni shoga.

DHANA YA UOLEZI

Uolezi ni uoneshaji maalum wa vitu, mahali, watu, hali na kadhalika katika muktadha husika wa mazungumzo kwa kutumia maneno (violezi) tofauti na uoneshaji wa kawaida wa kutumia viungo vya mwili hususan vidole.

Si rahisi kwa mtu asiyejua muktadha kujua ni kitu gani kinachojerejelewa.

Kwa mfano

‘ukija yeye utamkuta pale, itabidi usubiri kwa dakika 40 kisha tutakwenda kule kuwaona wale tuwarejeshee hiki nao wapate kile

Hapa maneno yote yaliyopigiwa mstari ni violezi.

Marejeo

1. Massamba P. B. D (2004) Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam: TUKI.