Aina za uolezi pamoja na mahusiano ya ukweli

Na MGENI WETU

Imepakiwa - Friday, December 22  2017 at  15:18

Kwa Muhtasari

Uolezi ni uoneshaji maalum wa vitu, mahali, watu, hali na kadhalika katika muktadha husika wa mazungumzo kwa kutumia maneno (violezi) tofauti na uoneshaji wa kawaida wa kutumia viungo vya mwili hususan vidole.

 

KUNA aina zifuatazo za uolezi:-

1. Uolezi nafsi

Huu ni uolezi unaotumia viwakilishi vya nafsi. Uolezi huu una violezi sita (6) vinavyogawanyika katika makundi matatu jinsi ifuatavyo:

1. Kundi la nafsi ya kwanza- hapa kuna violezi mimi na sisi

2. Kundi la nafsi ya pili - hapa kuna violezi wewe na ninyi

3. Kundi la nafsi ya tatu - hapa kuna violezi yeye na wao

Uchanganuzi wake ni kama ifuatavyo;

Mimi/sisi - hurejelea wazungumzaji au mzungumzaji.

2. Uolezi Wakati

Hujumuisha kutambulisha kipindi tamko fulani linatolewa. Uolezi huu hutofautisha wakati wa kutolewa tamko na wakati tamko lilipopokelewa na msikilizaji.

Kwa mfano:

i. Andika barua yako sasa hivi

ii. Tutaenda kesho

iii. Seni alizaliwa tarehe ishirini na sita mwezi wa Kumi na Mbili Mwaka elfu moja mia tisa na themanini

iv. Nitakuja kwako Jumapili ijayo

v. Habari za asubuhi

Pia njeo za wakati katika sentensi huweza kubainisha uolezi wakati.

Kwa mfano

mwalimu wetu alikuwa anachekesha

3.Uolezi Mahali

Ni aina ya uolezi ambao huashiria mahali ambapo mawasiliano yanafanyika (Muktadha).

Katika lugha ya Kiswahili kuna viashiria kadha wa kadha vinavyoashiria mahali

kwa mfano:

hapa, pale, huku, kule, huko, humu, mule na kadhalika.

4. Uolezi Uelekeo

Huu ni uolezi ambao hurejelea uelekeo. Kwa mfano: mbele-nyuma, kulia-kushoto, chini juu nk

5. Uolezi Jamii

Katika aina hii ya uolezi maana ya tungo hutegemea uhusiano wa kijamii kuweza kueleweka.

Uhusiano huo hurejelewa na maneno fulani fulani ambayo hupata maana kamili yanapotumiwa na watu wa kaida mbalimbali katika jamii.

Huonyesha uhusiano wa aina mbalimbali

kwa mfano

cheo, hadhi au umri wa msemaji na msikilizaji.

Kwa mfano:

Ndiyo mzee nimekuelewa!

Mahusiano ya Ukweli

Mahusiano ya ukweli yako ya aina mbili:-