Uhakiki maana kwa mujibu wa Nadharia Anuwai

Na MGENI WETU

Imepakiwa - Tuesday, February 20  2018 at  13:47

Kwa Muhtasari

Jinsi tulivyojadili awali, nadharia za maana ziliibuka kutoka katika mtindo wa mtoano ambapo kila nadharia iliyofuata ilijaribu kujibu mapengo yaliyoachwa na nadharia iliyotangulia.

 

JINSI tulivyojadili awali, nadharia za maana ziliibuka kutoka katika mtindo wa mtoano ambapo kila nadharia iliyofuata ilijaribu kujibu mapengo yaliyoachwa na nadharia iliyotangulia.

Ukweli huu unaweza kuhakikiwa kwa kutumia nadharia za urejeleo, dhana, mwitiko na matumizi jinsi ifuatavyo:

 

MAANA KAMA UREJELEO/ KITAJWA

Kwa mujibu wa nadharia hii maana inaweza kufafanuliwa kama ilivyoainishwa;

 

  1. Maana ya umbo la kiisimu hurejelea umbo hilo.
  2. Maana ya tamko ni kile kinachorejelewa
  3. Umbo la kiisimu lazima liwe na kirejeleo chake.
  4. Mara nyingi inahusu majina maalum ambayo yanarejelewa.

Kwa mfano unaweza kuwa na jina kwa upande mwingine 'kikombe‘ na kisha kwa upande wa pili ukawa na 'umbo halisi la kikombe‘

 

MAANA KAMA DHANA

Iliasisiwa na akina F. Dessassure, Ogrady, Sapier 1923 (aliyeasisi ni Edward Sapier na wengine waliunga mkono hoja yake)

 

Kwa mujibu wa nadharia hii;

Kuna uhusiano wa alama dhana na kitajwa.

Mawasiliano hufanikiwa iwapo tu maneno hayo huchochea dhana au mawazo sawa kati ya msemaji au msikilizaji

 

MAANA KAMA MWITIKO

Nadharia hii iliasisiwa na Bloomfield 1935 na kulingana nayo; Maana ya tamko ni ule mwitiko:

Kama watu wakipokea mwitiko mmoja basi kuna maana moja

Ubora wake ni kwamba katika lugha kuna baadhi ya maneno ambayo mwitiko  wake unafanana.

Udhaifu wake ni kuwa inawezekana kuwa na mwitiko tofauti tofauti.

Kuna maneno katika lugha ambayo ni vigumu kubaini mwitiko wa maneno hayo, kwa mfano; maneno kama 'na‘ 'kwa', na kadhalika.

Wakati mwingine kuna mwitiko tofauti kwa jambo moja. Kwa mfano: Mambo...

 – mwingine anasema 'poa', mwingine 'kwa Yesu‘

 

MAANA KAMA MATUMIZI

Nadharia hii iliasisiwa na Ludwing Wittgenstein katika kitabu chake cha Philosophical Investigation.

Alidai kuwa ni kosa kubwa mno kuweka mipaka ya maana kama ambavyo nadharia zilizotangulia zinavyofanya.

Hii ni kwa sababu kufanya hivyo ni sawa na kuweka mipaka ya thamani ya umbo lenyewe la kiisimu. Kwa hiyo kinachopaswa kuangaliwa ni matumizi ya umbo hilo.

Nadharia hii ina ubora wake; lugha imefungamana na jamii.

Lakini hata hivyo kuna baadhi ya maneno ambayo hupewa maana yake hata kabla ya kutumiwa.

Hakuna mipaka yoyote inayowekwa na nadharia hii

Nadharia hii inapingana na matumizi ya kamusi ambayo inatoa maana ya maneno bila kubainisha muktadha wa matumizi yake.

 

 

Marejeo

1.      Massamba P. B. D (2004) Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam: TUKI.

 2.      Mdee, J. S (1997), Nadharia na Historia ya Leksikografia, Dar es Salaam:TUKI.

 3.      Morris, Charles W. (1971), Writings on the general theory of signs, The Hague: Mouton