Hali na maendeleo ya Kiswahili nchini Rwanda

Na CHRIS ADUNGO

Imepakiwa - Tuesday, April 18  2017 at  14:56

Kwa Mukhtasari

KWA kipindi kirefu sana kabla ya ukoloni, nchi ya Rwanda ilikuwa na utawala wa kifalme. Ni katika baadhi ya nchi nyingi za kiafrika ambapo Kiswahili huzungumzwa kwa nadra sana. 

 

Kudunishwa huku kwa lugha ya Kiswahili kunaweza kuhusishwa na desturi za watawala wa kijadi ambao hawakukubali kutangamana na wageni kwa kipindi kirefu.

Watawala wa kijadi nchini Rwanda walikataa katakata wafanyabiashara waliozungumza lugha tofauti na Kinyarwanda kuingia katika chi yao.

Shughuli nyingi za kibiashara ziliendeshwa na majirani wa Wanyarwanda waliomudu kuizungumza lugha ya Kinyarwanda.

Hao ndio pekee walioruhusiwa kuuza na kununua bidhaa kwawanyarwanda. Kutokana na kutokutana kwa wanyarwanda na wafanyabiashara wa Kiswahili, Wanyarwanda hawakuweza kujifunza wala kuzungumza Kiswahili.

Kutokana na vizuizi hivi Kiswahili kilichelewa sana kuingia katika nchi ya Rwanda.Hata hivyo, kufikia mwishoni mwa karne ya kumi na tisa, wakati wa utawala wakijerumani, kiswahii kilianza kuingia japo kwa kujikokota.

Kama Burundi,wajerumani waliingia na watumishi waliokuwa weledi katika mazungumzo ya lughaya Kiswahili.Kipindi cha wajerumani kilikuwa na vichocheo kadha wa kadha vilivyochangia kuenea kwa Kiswahili. 

Mojawapo ya vichocheo hivi ni kuwa watawala wa kijerumani walikuwa wamezoea kutumia lugha ya Kiswahili nchini Tanganyika kwa hivyowaliendeleza kasumba za Kiswahili.

Dini ya kiislamu halikadhalika ilichangia sana katika kukieneza Kiswahili. Wengi wawatumishi wa wajerumani walikuwa ima waarabu au wafrika kutoka Tanganyika.Wote hawa walikuwa waislamu. 

Katika kueneza dini yao walitumia lugha yaKiswahili ili kuwaingiza wanyarwanda katika dini yao. Baadhi ya wanyarwandawalifuata mafunzo ya dini ya kiislamu na kujifunza Kiswahili.

Lugha ya Kiswahili ilisambaa baada ya Wanyarwanda kuwaruhusu Wajerumani nchini mwao kama watawala karne ya 19.

Waswahili waliwasaidia Wajerumani kama wapagazi na wakalimani. Kwa kutumia fursa hii, Waswahili na bila shaka waislamu walieneza dini yao kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Lugha ya Kiswahili pia ilitumika katika elimu kwa mfano katika kufundishia shule za kijadi. Chifu wa Rwanda Yuki Musinga alikubali kujifunza Kiswahili pamoja na watawala wa Rwanda wa wakati huo ili kukuza mahusiano baina yao na Wajerumani.

Katika kipindi hiki Wanyarwanda walionekana kukikumbatia Kiswahili hukukikitumika katika shule za watawala wa kijadi. Kufika mwaka wa 1900 Mfalme Yuki Musinga alikubali kuwa yeye na wasaidizi wake wafunzwe lugha ya Kiswahili!

Baada ya kuondoka kwa watawala wa Kijerumani, eneo la Rwanda lilikaliwa na wakoloni wa kibelgiji. Wabelgiji walipinga sana dini ya kiislamu kwani walikuwa waumini wa dini ya Kikristo. 

Mbeligiji hakukipenda Kiswahili hata kidogo kwani kilihusishwa na dini ya Kiislamu.Baada ya uhuru nchini Rwanda juhudi za kukiimarisha Kiswahili zilianza.

Mnamo mwaka wa 1976 hadi 1977 lugha ya Kiswahili ilianza kufundishwa katika shule zaupili na chuo Kikuu Cha Rwanda. 

Walimu waliofunza lugha ya Kiswahili walikuwawametoka nchini Tanzania.Katika juhudi za kuimarisha Kiswahili shuleni na vyuoni, serikali iliunda kitengo chaKiswahili katika Taasisi Ya Elimu chini ya Wizara Ya Elimu Ya Taifa. 

Kitengo hikikilidhamiriwa kushughulikia vyema ukuaji na ufundishaji wa Kiswahili.Kufikia mwaka wa 1961 idhaa za matangazo ya redio zilianza kupeperushamatangazo kwa lugha ya Kiswahili. 

Baadhi ya vipindi vya Kiswahili vilikuwa : Taarifa Ya Habari, Ulimwengu Tuishio, matangazo ya mpira na vipindi vya salamu.

Maenezi ya Kiswahili nchini Rwanda hayakukosa matatizo ya hapa na pale. Mathalani walimu wa Kiswahili walikuwa wachache sana. Hivyo basi ufundishaji ulikuwa nachangamoto kemkem. 

Ukosefu wa vitabu vya kiswahili lilikuwa tatizo jinginelililotishia kudidimiza maendeleo ya lugha hii. Vitabu vingi vilivyopatikana vilikuwa vimeandikwa kwa lugha za kigeni.

Wanyarwanda wamesawiriwa kuwa watu waliojipenda sana na kwa kiwango fulaniwaliokuwa na kiburi. Walishikilia kikiki lugha yao ya Kinyarwanda na hawakutaka.