Jifunze Kiswahili

Kina mama jitokezeni

Na CHARLES ONGADI  ( email Mwandishi)

Imepakiwa - Thursday, October 30  2008  at 14:13

Akina mama wanastahili kujitokeza kuwania nyadhifa mbalimbali wakati wa uchaguzi mkuu ujao.
Kauli hiyo ilitolewa na diwani wa wadi ya Shanzu, kaunti ya Mombasa, Bi Maimuna Salim, hapo jana.
Alisema kwamba akina mama ndio uti wa mgongo wa taifa hili, na wanapswa kujitokeza kukabiliana ana kwa ana na wanaume bila kusubiri kuteuliwa.
Sawa na wanaume, akina mama pia wana uwezo,juhudi na maarifa ya kuleta mendeleo nchini, alinena Bi Maimuna.
Alitoa mwito kwa vijana wajihadhari ili wasiumiwe na wanasiasa kuzua fujo wakati huu ambapo uchaguzi mkuu unakaribia.
Bi Maimuna alikuwa akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi wa mataa ya barabarani katika wadi hiyo, iliyofanyika katika eneo la Saga karibu na hoteli ya kitalii ya Severin.
Wakati huo huo, Bi Maimuna aliwaonya vikali mabwanyenye wanaoziba njia za wananchi kutumia kuelekea ufuoni kwamba siku zao zimefika.
Alisema kwamba ingawa serikali ilitenga nafasi ya njia kwa wananchi kupitia kuelekea ufuoni kujivinjari na wavuvi kuelekea baharini, sasa nafasi hizo zimenyakuliwa na mabwanyenye.
Alishangaa kwamba barabara hizo ndogo zimezibwa na mabwanyenye hao hivyo kuwalazimisha wananchi kutembea mbali ili kufika ufuoni.
Aidha, diwani huyo aliwataka wananchi kuwa na subira wakati huu anaposhghulikia swala hilo, huku akiahidi kwamba suluhisho litapatikana hivi karibuni.

 

Most Popular

Wabunge 175 kutahiriwa Zimbabwe

Wabunge 175 nchini Zimbabwe watapashwa tohara kufikia mwisho wa mwezi ujao katika juhudi za kuhamasisha wanaume

Mwanawe Waziri wa Fedha ajitia kitanzi

MWANAWE Waziri wa Fedha Njeru Githae anadaiwa kujiua nyumbani kwao Runda, Nairobi. Polisi wameanzisha uchunguzi

Polisi waendelea kusaka walioshambulia Mombasa

Polisi wameanzisha msako mkali kutafuta washukiwa waliotekeleza shambulio la kigaidi katika mkahawa wa Bella Vista,

Utengano wakumba ukumbusho wa Wanjiru

Ibada mbili tofauti zilifanywa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha bingwa wa marathon katika Olimpiki Samuel