http://www.swahilihub.com/image/view/-/1528934/medRes/408177/-/dad7ke/-/Elmoloo.jpg

 

Waelmolo waongezeka polepole licha ya uvumi

Wapiganaji kutoka jamii yo Elmolo katika Kalacha tamasha ya utamaduni katika mji ya Kalacha wilaya ya Marsabit, Mei 2012. Picha/HASSAN HUKA

Wapiganaji kutoka jamii yo Elmolo katika Kalacha tamasha ya utamaduni katika mji ya Kalacha wilaya ya Marsabit, Mei 2012. Picha/HASSAN HUKA 

Na SWAHILI HUB

Imepakiwa - Tuesday, October 9  2012 at  13:35

Kwa Muhtasari

Waelmolo wanatoka Ziwa Turkana na ni kabila ndogo kuliko nyingine Kenya.

 

Juma hili tumevuka milima na mabonde hadi Mkoa wa Rift Valley kuangaza darubini kwa jamii ambayo kusikika kwao ni nadra.

Ni dhahiri shairi kuwa mtu yeyote ambaye anaifahamu lugha ya Kisushaiti atatambua mahali haswa ambapo jamii hupatikana kwani Elmolo iriamaanisha watu ambao huvua samaki kwenye Ziwa Turkana.

Kabila la Elmolo laendelea kuongezeka maradufu licha ya uvumi kwamba linaangamia.

Maelezo ya jina la Elmolo ni sambamba sawia na jamii ya Dorobo, lakini tofauti ni kwamba Elmolo hawafugi nyuki wala hawafanyi kazi ya usasi.

Ama kweli, Elmolo wanafanana na wenzao Wadorobo. Swala hili limewafanya wengi kuibuka na dhana ya kuzuma kati yao na Wadorobo. Licha ya kwamba jamii hii inashiriki mazingara sawa na jamii ya Kidorobo wao hushiriki tu katika shughuli moja na Wadorobo ambayo ni pato ambalo si halisi bali linakusudiwa kutoa matakwa ya kimsingi yaani chakula tu.

Chakula cha jamii hii si kingine bali ni samaki ambao wapishi yake huibuka punde tu samaki anapoanikwa katika jua. Ingawaje jamii hii kwa wakati huu inajaribu kuiga mbinu za kisasa za mapishi bado mbinu hizi hazijakolea sana.

Watu wa Elmolo wana uwezo wa kuzungumza lugha za majirani zao ambazo wanazungumza kukushaiti ona mashariki. Mbali na kuwa na uwezo wa kuwasiliana kwa kukushaiti cha mashariki wao huchukulia lahaja hii kama ya jadi kwani suala hili ndilo limewaweka imara kama vigogo kwa kuzungumza Kimaasai au Kisamburu.

Vile vile, mtindo wao wa kimaisha una uwiano wa takriban sawa na Wasamburu, Jamii ya Elmolo imewakubali Waturkana wachache kuishi nao. Baadhi yao (Elmolo) hujaribu kufuga mifugo kwa idadi ndogo. Yamkinihuwa

wanajaribu kuiga hali ya maisha ya majirani zao, wao bado wanatilia maanani itikadi za mababu zao.

Kwa upande wa mavazi, jamii hii haijaona umuhimu wa kuvaa nguo za kisasa, kasumba huenda ikawa ndiyo imewayumbisha kusuta kwamba matawi ya mtende ni mufti kwa kutengeneza mavazi ambayo hukusudiwa tu kuficha sehemu za siri, mbali na kutumia mtende kama malighafi ya kutengeneza nguo.

Kadhalika, Elmolo hutumia mtende kutengeneza nyavu ya kushika samaki. Wao huamini kwamba nyavu zao haziwezi kuoza kwa sababu malighafi wartayoitumia kutengeneza ni bora.

Jamii hujawa na vitimbi kochokocho kwa mfano wao hutumia kipande cha mti wa mtende kwa kuogelea aidha kusafiri kwa maji.

Wao hufunga pamoja na Vipande vya miti, na punde si punde huwa wametengeneza chombo cha usafiri hadi kwenye nyumba zao ambazo hutengenezwa kwa kutumia gugu ziwa. Nyumba zao zimejengwa na mawe ambayo hutumika kama kinga dhidi ya upepo "kimbunga" ambao huvuma kwenye ziwa.

Mbali na uvumi kuwa kisasi hiki kinaendelea kikididimia ukweli ni kwamba hii ni jamii ambayo inaongezeka polepole.

Dhana nyingine ambayo huenda ikawa ndiyo ilichangia kuzindua fikra au kupungua kwa Elmolo ni kusukumwa kwa baadhi yao ambao hujulikana kama Beshiati Elmoto hadi katika nchi ya Uhabeshi.

Kitimbi kingine kuhusu jamii hii ni jinsi ambavyo wao hufunga ndoa. Ndoa yao lazima ifanywe karibu na ziwa kwani tukio la mwisho huwa ni kufungia pingu ya maisha mjini kama ishara ya kuonyesba shukrani kwa pato lao la msingi.

 Athari hii hutumiwa kama mtihani wa kujaribu kuona kama wahusika watastahimili mazingira ya ziwa kama makao yao ama watabadilika kuambatana na wakati!