http://www.swahilihub.com/image/view/-/1529026/medRes/408188/-/6vttb8z/-/Wakasaurieni.jpg

 

Wakasaurien wanaamini wako katika ‘Kenya mpya’

Mtu apumzike njiani ya Kacheliba-Alale, Poko Magharib, Agosti 4 2012. 

Na SWAHILI HUB

Imepakiwa - Tuesday, October 9  2012 at  14:39

Kwa Muhtasari

Wakasaurien ni watu warefu, wazito, weusi na wanaogopewa sana kutokana na hasira yao mbaya na ni jamii inayopenda vita na uraibti wa wizi wa mifugo.

 

EWE! Msomaji pengine kwa muda mrefu umekuwa ukidhani ya kwamba Wapokot ni jamii moja.

La! hasha, katika jannii ya Wapokot kunao makabila madogo madogo ndani yake kama vile Wakasuarien wanaoshi maeneo ya "Kenya Mpya" huko wilayani Pokot Magharibi, mpakani mwa Kenya na Uganda.

Wao hupatikana kwa wingi sehemu ya Alale karibu na tarafa ya Kacheliba wilayani Pokot Magharibi eneo ambalo wenyeji hulitamka kama Kochalibai ambalo kwa Kiswahili ni ‘Hajalipa’. Hadi kufikia mwaka wa 1970 eneo nzima ya Kachileba yenye miji mdogo ya Suam, Kapchok, Kasei, Kiwawa, Kases, Chemorongit, Amakuriat, Akoret, Amdat, na Alale, yalikuwa chini ya himaya ya nchi Uganda. Maeneo hayo yalitaifishwa na Rais wa Kwanza wa Jamhuri yetu, hivyo basi Wapokot na Wakasaurien wa maeneo hayo hutaja sehemu hiyo kuwa ‘Kenya Mpya’.

Kiramani, Alale ambayo sasa ni makao makuu ya wilaya ndogo hupakana na Uganda sehemu yake ya magharibi ilhali kaskazini ni Wilaya ya Turkana huku wilaya ya Pokot Magharibi iko sehemu ya mashariki na kusini.

Wakasaurien ni watu warefu, wazito, weusi na wanaogopewa sana kutokana na hasira yao mbaya na ni jamii inayopenda vita na uraibti wa wizi wa mifugo.

Maskani ya watu hawa ni juu mlimani na wengi wao huishi mapangoni hata wa leo. Ingawa wengine wao waliostaarabika huishi kwenye manyatta ndani ya nyumba za kitamaduni iitwayo "Cheptupon".

Ukitembelea wilaya hii ndogo ya Alale, bila shaka utawakuta watu hawa kwenye mlima wa Kadam. Wanaposali wao hutazama mlima "MTukufu" wa Kadam. Mlima wa Kadam ni wa kipekee katioka eneo hilo ambao una miti ya kila namna kama vile miraa, Podo (sosoila), Ueda (Torokwo), Mwiri (Tendwo), Mkorombosi (Siworwo) na Mianzi (Techan).