http://www.swahilihub.com/image/view/-/1531444/medRes/409391/-/8fmpljz/-/Turkanaa%255D%2523.jpg

 

Hofu na mashaka za Waturkana

Picha/Makhtaba

Picha/Makhtaba 

Na SWAHILI HUB

Imepakiwa - Friday, October 12  2012 at  11:52

Kwa Muhtasari

Waturkana hatimaye walitengana na ndugu zao Wamaasai na Wasamburu waliohamia sehemu za nyanda za juu na pia tambarare kama nyika za Lorogi na kingo za Ziwa Turkana.

 

KWANZA kabisa pongezi na furaha zangu ziwafikie Wakenya na wakarimu po pote walipo waliojawa na roho ya kiutu kwa ushirikiano wao wa hali na mali, kuwasaidia ndugu zetu Waturkana wakati walipokumbwa na baa la njaa la kuogofya hgivi majuzi.

 Kabila hili la Turkana hupatikana katika mkoa wa Bonde la Ufa kwenye mitiririko na kingo za Ziwa Turkana.

 Na kwa vile vile mbare zote ni lazima ziwe na msingi Fulani za kuambatana na kuwasili na chanzo zhao nchini, hawa waliandamana na ndugu zao Wamaasai na Wasamburu waliokuwa wakisikilizana nao kama pete na chanda.

 Mnamo karne ya 18 na 19, kulitokea mavutano za hapa na pale kati ya makabila tofauti tofauti, jambo lililofanya wengine wahamie mahali mbali mbali. 

Waturkana hatimaye walitengana na ndugu zao Wamaasai na Wasamburu waliohamia sehemu za nyanda za juu na pia tambarare kama nyika za Lorogi na kingo za Ziwa Turkana.

 Waturkana walienda kujinyakulia ardhi sehemu za Lotikipi na pia huko pande za Kakuma. Hat hivyo, Waturkana wengi bado hupatikana kwenye miji ya Lodwar na Marich.

 Mila walizo nazo zinatofautiana kuliongana na nyakati mbali mbali.

 Waturkana ni watu wanaooza mabinti zao wakati wangali wachanga, mradi tu mzazi apate mahari kutoka kwa wakwe.

 Vyakula pia wanavyotumia ni vile vya kiutamaduni kwani amini usiamini, kitoweo cha damu aidha kilichopikwa au kisichopikwa na kisha kikachanganywa na maziwa ndicho chakula chao cha kutaka na shoka!

 Akina mama wa kabila hili huwa wanapaswa saa zote kuchanja chale usoni huku ntwele zikipakwa ngeu. Akina baba nao, hutakiakana kuvaa aina ya nmguo zaniazotufautiana na za vijana.

 Hofu na mashaka kuhusu kabila hili ni kwamba linakumbwa na hatima ya kutoweka kwa mambo yao ya kitamaduni kwani wamekodolewa macho na matatizo mengi ya kimaumbile kama njaa. Kutokuwa na maji safi au ukosefu wa chemichemi za maji katika eneo hilo lao.

 Zaidi ya hayao, ni ushambalizi wa mara kwa mara kutoka kwa majirani zao ambao wana mazoea ya kuwaiba mifugo.

 Waturkana pia ni wavuvi ambapo huvua samaki toka Ziwa Turkana – ziwa la pekee linalowasaidia na maji.