http://www.swahilihub.com/image/view/-/1533648/medRes/410305/-/135w3k1/-/Garrii.jpg

 

Wagarri

Sharti mvulana alete ama ngamia au ng’ombe mmoja ili aruhisiwe kumpeleka mchumba wake nyumbani.Picha/JARED NYATAYA 

Na MAKAVAZI YA TAIFA LEO

Imepakiwa - Monday, October 15  2012 at  14:23

Kwa Muhtasari

Wagarri ana desturi tofauti sana na makabila mengine humu nchini Kenya.

 

Garri ni moja kati ya yale makabila yaliyo madogo zaidi nchini kutokana na idadi yao.

Wagarri hasa hawazaidi laki moja kwani wengi wao wamemezwa na ndugu zao Wasomali. Katika safari yetu mkoani Kaskazini Mashariki, ambayo ilijuimisha matatizo mengi ya usafiri na jua la kuyeyusha haikuwa rahisi kwetu kulipata kabila hili la Garri.

Safari yetu hii ilitufikisha katika mpaka wa Moyale na Mandera ambapo tulifanikiwa kuwapata ndugu zetu hawa ambao wanafanana na Wasomali kwa sura na umbo.

Baada ya utafiti wa kina, tulitanabahi kabila hili halina uhusiano wo wote na Wasomali isipokuwa tu imani ya kidini. Wote ni Waislamu.

Na jamii ya ufugaji hivyo maisha ya kuhama hama wakitafuta maisha bora na maji safi ni baadhi ya desturi zao.

Wanaishi kwa vikundi vidogo ndani ya nyumba za udongo na nyasi mkao ambayo huachwa kama mahama wanpongoa nanga kuelekea mahali kwingine.

Ni nadra sana kupata nyumba za kudumu katika sehemu hii. Wagarri hufuga wanyama kama vile ng’ombe, punda, ngamia, mbuzi na kondoo ni kwa idadi ndogo mno.

Kutokana na imani yao na msimamo wao zanifu, huwezi kumpata mbwa miongoni mwa wanyama wanaofugwa na Wagarri. Mavazi yao ni ngozi zinazotokana ni mifugo hao. Aidha ngozi hizo hutumika kwa kulalia kama matandiko no godoro malazani.

Tulipochungua swala la ndoa, tuligundua kwamba Wagarri ana desturi tofauti sana na makabila mengine humu nchini Kenya.

Mvulana humtongoza msichana kwa majani chai ni kahawa spesheli iitwayo “Buna” vitu hivi viwili hupelekwa hadi katika boma atokako msichana ambapo humpikia mvulana na uchumba unaanza papo hapo.

Zama za mababu wa mababu zao, ilikuwa ni mwiko kufanya mapenzi kabla ya ndoa. Hivyo, basi watoto hawangezaliwa nje ya ndoa.

Siku ya kufunga ndoa, lazima idadi Fulani ya mahati itolewe. Sharti mvulana alete ama ngamia au ng’ombe mmoja ili aruhisiwe kumpeleka mchumba wake nyumbani.

Tangia hapo, sehemu nyingine ya mahari inayosalia hupelekwa baadaye. Nayo ni asali na mifugo kadhaa.

Garri huthamini sana imani ya dini ya Kiislamu kuliko kablia. Watoto wao hupewa majina ya Kiislamu pekee na wala si ya kabila lao.