http://www.swahilihub.com/image/view/-/1533672/medRes/410323/-/bsk43/-/pokott.jpg

 

Historia ya Wakopot

Pokot

Consolata Limanguria, mchezaji wa 'Sengetwo Traditional Dancers' kutoka Pokot Magharibi. June 21, 2012. Picha/JARED NYATAYA 

Na MAKAVAZI YA TAIFA LEO

Imepakiwa - Monday, October 15  2012 at  14:49

Kwa Muhtasari

Kulingana na historia, Wapokot waliwasili humu nchini kati ya karne ya 18/19 ambapo walilakiwa na wenzao kama Wanandi, Wakipsigis, Wakeiyo na Wamarakwet.

 

Wapokot kama moja za mbare za humu nchini ni wazaliwa wa humu humu Kenya waiiowakilishwa na mababu zao yapata miaka 500 iliyopita.

Je, hawa Wapokot ni kina nani hasa? Je, wanaweza kuwa eti ni wale wezi wa mifugo wa mara kwa mara wilayani Pokot Magharibi, au ni majangili wanaowashambulia watu katika mpaka wa Kenya na nchi jirani za Sudan na Uganda? Jawabu ni: La!

Kulingana na historia, Wapokot waliwasili humu nchini kati ya karne ya 18/19 ambapo walilakiwa na wenzao kama Wanandi, Wakipsigis, Wakeiyo na Wamarakwet.

Hata hivyo, baadaye waliamua kukaa katika sehemu tofauti kutekeleza majukumu yao. Tangu Kenya kujinyakulia uhjuru wake, Wapokot wameishi maisha ya kuhamahama kufuatia mashambulizi kutoka kwa maadui zao kama Wasabaoti na pia majangili kutoka nchi jirani.

Kuhusu nyanja ya kimila watoto wa kutoka jamii hii ni huwa wanavaa shumizi zilizofunika miili yao nusu huku wakionekana wenye nyuso za furaha wakati wote wanapochunga mifugo, kazi ambayo hawa vijana huanza kutekeleza punde tu wafikapo katika miaka ya kwenda shuleni.

Kijana barobaro Mpokot anapohitimu umri wa kutafuta mchumba, atahitajika kujikinga na silaha. za 'kiume', silaha kama mishale, podo, pinde na isitoshe, hata sagaia.

Lengo na shabaha ni kuwa, kijana kama huyu wakati anapochunga mifugo na adui akitokea, atapaswa kupigana kufa na kupona na ashindapo, basi atakuwa ni shujaa ambaye atawavutia wanawali wote wa kiiiji na huwa fahari kubwa sana kwao.

Wapokot huthamini sana mlo wa maziwa na damu ya ng'ombe au ngamia wanaopata kutokana na jitihada zao za kuwafuga. Huwa mara nyingi wanatembea mwendo mrefu sana ndiposa wapate maji safi, shughuli za afya na hata watoto wao kuhudhuria shule zilizo chache sana.

Ndoto za Wapokot huenda zikawa ria ukweli kutokana na ufadhili mbalimbali za miradi za maendeleo zinazopatikana kutokana na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayozidhamini kama SIDA, CARE na Msalaba Mwekundu.

Jamii ya Wapokot pia hujivunia wana wao walioshilia madaraka mbalimbali humu nchini huku wakiwa na maeneo ya uwakilishi bungeni.

Viongozi kutoka jamii hii pamoja na Mawaziri Francis Lotodo, Andrew Kiptoon, waziri msaidizi Joseph Lotodo.

Jambo la kusikitisha ni kuwa visa vya uvamizi vya kila siku wilayani Pokot kuhusu wizi wa mifugo imewafanya wapoteze fahari ya kimilia waliyokuwa nayo kuanzia jedi.