http://www.swahilihub.com/image/view/-/1533702/medRes/410334/-/cd105f/-/sagwe.jpg

 

Wasagwe ni kama wametoweka!

Sagwe

Mbuzi wajikinga dhidi ya jua kali kustahimili hali ngumu ya ukame. Picha/JARED NYATAYA 

Na MAKAVAZI YA TAIFA LEO

Imepakiwa - Monday, October 15  2012 at  15:16

Kwa Muhtasari

Wasagwe ni watu waliopenda kufuga wanyama sana lakini maeneo wanamokalia ni kama jangwa. Siku hizi wao hufuga tu wanyama wanaoweze kustahimili hali ngumu ya ukame kama mbuzi na ngamia.

 

Napenda nikujulishe kwa ndugu zetu wa kabila la Sagwe wanaopatikana wilayani Wajiir, mkoa wa Kaskazini Mashariki.

Hapo wilayani utawapata wakiishi maeneo ya milimani kama Gurar, Bute, Ajau Gollo na Tarbaj. Kulingana na usemi wazee wa kabila hili, inasemekana waliwasili hapa nchini yapata miaka 400 iliyopita wakitoka sehemu za Abyssinia (siku hizi Ethiopia) wakiandamana na makabila kama Gabbra, Ogaden, El-Molo, na Rendille.

Hata hivyo, hivi sasa, robo tatu ya Wasagwe wanaopatikana humu nchini wamebadilika kabisa kimila kutokana na kuoana kwao na majirani zao, nao wanaishi sehemu kama kadno kando ya mito Laga Born a Laga Hoichof.

Khadhalika kuna kundi linguine ndogo linalopatikana miji midogo kama Giriftu, Tarbej na Buti Halu – wote bado wakitathamini mila na desturi zao.

Kimila na kitamuduni Wasage huwa ni wafuasi wa dini ya Kiislamu ambapo huamini kuwa Allah ndiye mpeanji wa kila kitu na kwamba mbali na kuabudiwa hupaswa kupewa sadaka kama ya fedha, vyakula, mazao na hata kuchinjwa mifugo.

Na ili maombi yamfikie Allah, mawasiliano hufanywa kupitia Nabii Abagada tu.

Wakiwa wanatii mambo ya kimila vilivyo, Wasagwe hufanya tohara huku shughuli hizi zikienda sambamba na tfrija motomoto kama nyimbo ngoma kwa wanawili unywaji tembo kwa wazee na pia michezo aina mbali mbali.

Kutokana na hali ya mabadiliko ya kimaumbile na hali ya anga. Wasagwe ni watu waliopenda kufuga wanyama sana lakini maeneo wanamokalia ni kama jangwa. Siku hizi wao hufuga tu wanyama wanaoweze kustahimili hali ngumu ya ukame kama mbuzi na ngamia.

Wasagwe wanasema ifikapo tfrija za Buffat, sio lazima wachinje fahli bali wanaweza kuchinja mnyama yeyote bora tu damu imwagike chini na pia kwa vile ni siku kuu iliyotenegewa vijana, hakuna amri inayosema kuwa ni lazima mnama mkubwa afe, kinyume cha ndugu zao Waborana wanaochinja ng’ombe siku hiyo ya Buffat.

Wasagwe hujenga nyumba zao zikimulika mji mtakatifu wa Mecca. Kabila hili ambalo baadhi yao huongea Kisomali halijatilia maanani mambo ya kisiasa kwani limekumbwa na hali ya umasikini na kutokana na uchache wao, ni kana kwamba hawepo nchini!