http://www.swahilihub.com/image/view/-/1533730/medRes/410349/-/7k9j2s/-/Terikk.jpg

 

Waterik ‘wamemezwa’ na Wakalenjin

Na MAKAVAZI YA TAIFA LEO

Imepakiwa - Monday, October 15  2012 at  15:51

Kwa Muhtasari

Waterik wanaopatikana viungani vya mji wa Baringo, mji wanaouita Emparing mumaanisha ziwa.

 

Terik ni moja ya makabila ya humu nchini na ambalo si Wakenya wengi wameahi kuwasikia. Wao hupatikana katika mkoani Rift Valley kwenye katika bonde la Kerio. Walikuwa moja va makabila yaliyokuwa yakitafuta maeneo ya milima, mito, na hata maziwa katika shamra na pilka pilka za kuhamhama zilizofanyika miaka za nyuma.

Katika uchunguzi wangu wa hivi karibunikuhusu kabila hili ambalo badaaye limeweza kuiwekwa katika tabaka moja na makabila mengine kama Kalenjin. Turgen, Marakwet, Pokot na Sabaot, utafiti umedhihirisha kwamba katika karne ya 18/19, kulizuka vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe kati ya hawa ndugu.

Jambo hilo liliwafanya Waterik wateremkie kingo za Ziwa Turkana na wengine nao wakahamia nchini Ethiopia. Wale waliobakia Kenya, hatimaye wakanyakua ardhi iliyoko sehemu za Ziwa Baringo na mitiriko ya Mlima Elgon.

Punde si punde wakaanza shughuli za upandaji wa mimea na uwekaji mifugo. 

Watarik huongea kugha ya Kikalenjin ijapokuwa idadi yao inaendelea kukabiliwa na tisho la kudidimia na pia hatima ya kutoweka kabisa kwani wengi wao tayari wameona na Wapokot, Waturgen, Wasaboti, Wamarkwet na hata wengine wakaoana na Wabukusu, hivyo basi mila na desturi kuwahusu ikiendelea pia kutoweka. 

Waterik wanaopatikana viungani vya mji wa Baringo, mji wanaouita Emparing mumaanisha ziwa. Wazee toka kabila hili ni watu wanaoeshimiwa sana kutokana na mawaidha wanaotoa na pia hekima waliotunikiwa.

Wao hukalia Ngorika - aina ya kiti kinachowekwa sebuleni tu wakati wa shughuli fulani. Wanapofanya hivyo, huwa wakati huo wamevalia Ngorigi, aina ya vikuku vinavyovaliwa mwilini na Mintoi yaani vipuli vilivyopakwa rangi nyekundu ambavyo huvaliwa masikioni.

Jamaa hawa pia wako na vikundi vya vijana vilivyo pia na vitengo tofauti wakati wa tohara, kila kikundi kina kiongozi anayejulikana kama Longchayailok anayetarajiwa kufundisha vijana nyimbo za kiutamaduni na jinsi ya kujikinga wakati wa vita na uvamizi.

Isitoshe Longchayailok ambaye ni kama mtawala wa makundi haya, huwa anakumbatwa na mambo mbalimbali magumu dhidi yake wakati wake wa utawala.

Utawala dhalimu wa Longchayailok hutia hofu kubwa kwa vijana licha ya hatua kali anazozichukua i1i azuie mambo fulani yasitekelezwa kama kuna vijana ambao hawapendi mambo ya kitohara na huwa na huwa wanajaribu kwa udi na uvumba ili mzee kama huyu apatikane na janga la huzuni.

Maisha ya Waterik huenda sambamba na shughuli za ufugaji wa ngombe, kondoo na mbuzi ijapokwuka siku hizi wanaanza miradi mbalimbali kama ya kilimo huku wakiyanyuniza mashamba yao maji wakati wa kiangazi.

Kwa kweli Waterik wamekuwa kama maji yaliyokuwa katika nyungu kilichovunjika vigaegae na kisha yakamwagika ndiposa nasisitiza kuwa bado yanaweza kuzoleka tukijimudu na pia tuku jivunia mila na desturi zetu sisi kama Wakenya.

Ni hivyo ndivyo ilivyo na Waterik.