http://www.swahilihub.com/image/view/-/1537176/medRes/412062/-/7tge3kz/-/Tirikii.jpg

 

Watiriki wanaishi Mkoa wa Magharibi

Watiriki

Mtiriki na mwanamuziki William Ingosi acheza ngoma za Watiriki katika Shaviringa. Picha/ISAAC WALE 

Na SWAHILI HUB

Imepakiwa - Friday, October 19  2012 at  15:19

Kwa Muhtasari

Tumepata fursa mwanana ya kugusia machache kuhusu kabila la Watiriki kililo Mkoa wa Magharibi kwa minajili ya kutizama baadhi ya mila kama vile kifo hususan urithi.

 

KENYA ni taifa lenye makabila mbalimbali ambayo chini ya kivuli cha lugha ya Kiswahili huletwa pamoja na kushirikiana kwa mambo mengi pasina kuegemea ukabila.

Ijapokuwa lugha ya Kiswahili imefanikiwa kuunda taifa imara kupitia mwito wa itifaki ulio uti wa mgono wa iktisadi ya nchi yetu, hatuna budi kukumbuka kwamba kunazo lugha za kikabila ambazo ni mwandamizi wa mila na desturi za Kiafrika.

Watiriki ni tawi la Abaluhya ambao ni Wabantu wanaoshikilia nafasi ya pili kwa ukubwa nchini. Watiriki wana mila zilizohitilafiana na Waluhya wengine kwa kiwango fulani. Hata hivyo, tofauti hiyo ni kidogo sana.

Tutaangalia jinsi ambavyo desturi zao zinavyoshughulikia mambo ama tukio la kifo na urithi.

Wahedi, kifo kilichukuliwa kama shuku kutoka kwa washirikina ama mashetani (Shisyuzu) ama laana. Kiongozi wa kijiji alitakiwa kuongoza shughuli za kufariji waliofiwa umoseni wakati wa mazishi i1i kudumisha amani na utulivu hasa ikiwa kifo kilidhaniwa kutokana na uchawi. Shughuli hizo ilimbidi azitimize kwenye kaburi.

Watiriki huamini kwamba roho ya mtu inaweza kutoweka anapokuwa analala na kutumia wakati wake ama kushirikiana na mashetani ama majini, jambo arnbalo baadaye lilikumbukwa kuwa ndoto, za mazingaombwe. Pepo huyo mwenye uwezo wa kuhamisha roho alijulikana kama shinini.

Roho ya shinini ilibadilika kuwa wa mizuka ama pepo shisyuzu mtu alipoaga dunia, pepo huyo alimzunguka maid kwa muda wa siku kadha.

Ikiwa mazishi yalihudhuriwa kwa wingi na omuseni ni kufanikiwa kupunguza na kuondoa shaka ya uchawi, pepo alitulizwa katika hali ya kifo na kutulizwa kwenye roho ya aliyekufa hujulikana kama misambwa.

Pepo anayezunguka maiti na kushambulia watu hujulikana kama shinanyenzo. Iliaminika kwamba sababu iliyofanya jamii kushambuliwa na pepo ni kutokana na ibada ya mazishi kufanywa kwa njia isiyotimia na pia kuhudhuriwa kwa uchache.

Urithi nao ulifikiwa na kuamuliwa baada ya mzee mwenye boma kuaga dunia. Jamaa hivo ilihudhuriwa na wazee wa vijiji na wale jirani zao, lilijulikana kama libego aliyekuwa na malalamiko kuhusu mali iliyoachwa alitakiwa kuwasilisha malalamiko yake kwenye kikao hicho lubego.

Ni katika kikao hicho ambapo urithi wa mke unazungumziwa. Kama kawaida ndugu wenye uhusiano wa damu na aliyekufa ndiye hukubaliwa kumrithi mjane, desturi hiyo ya Watiriki kuhusu urithi wa wake, ilikubaliwa na majirani wao wa Maragoli.

Kuhusu urithi wa mashamba, Watiriki hawakukubali urithi uende kwa wale wasiohusiana kidamu. Aghalabu wenve uhusiano utokanao na ndoa kama vile mukwasi na nakhobizala walikubaliwa kurithi mashamba. Watu hawa walitakiwa kutoa kuku na mbuzi ikiwa walitaka kuidhinishwa kuwa wamilikaji wa mali ya aliyekufa.

Hata hivyo, walichotoa hakikuwa kimelingana na thamani ya shamba, bali kilikuwa kama chombo cha kuonyesha jinsi mtu alivyo miliki ardhi hiyo omwene.