http://www.swahilihub.com/image/view/-/1620830/medRes/425590/-/gtbdo8/-/wasuba.jpg

 

Wasuba kutoka visiwa vya Rusinga na Mfang’ano

Wavuvi

Wavuvi katika kisiwa cha Rusinga. Picha/MAKTABA 

Na MTAFITI WA SWAHILI HUB

Imepakiwa - Thursday, November 15  2012 at  15:08

Kwa Muhtasari

Wasuba sio tu wanapatikana katika visiwa vya Rusinga na Mfang’ano, ila oia lokesheni jirani kama Kakasingri, Gwassi, Gembe, wilayani Migori na hata kwa Wakuna.

 

HUKU nikizidi kuangaza macho kwa mbare kadha wa kadha ya nchi yetu kihistoria majuzi nilivuka mabonde, mito na milima hadi Nyanza Kusini.

Huku nilijaliwa kukutana na jamii ya Wasuba ambao wengi wao hupatikana kando ya Ziwa Victoria upande mmoja wakiwa wamepakana na Tanzania na upande mwingine Uganda.

Vile inavyosemekana kuwa kila kabila ni lazima liwe na msingi fulani ambayo inaambatana na shina la kabila lenyewe, hivyo basi inasemekana kwamba walitokana na kugawanyika kwao na kabila la Baganda kutoka nchini Uganda kati ya karne ya 17 hadi 18 (1800-1900).

Walipokuwa katika heka na pilka pilka za hapa na pale za kutafuta pa kuishi, walichananyikana na Waluo waliokuwa wakivua samaki kutoka Ziwa Victoria. Ilipotimia mwaka wa 1950, wengi wao walianza kuongea Kijaluo huku wakichanganya ndimi na Ki-ekesuba.

Wasuba sio tu wanapatikana katika visiwa vya Rusinga na Mfang’ano, ila oia lokesheni jirani kama Kakasingri, Gwassi, Gembe, wilayani Migori na hata kwa Wakuna.

Wakati Wasuba walipoanza kuishi katika maeneo haya, walijulikana kwa jina maarufu la Mwalo Pinje Abich. Lugha yao ya Ki-ekesuba huzungumzwa kwenye maeneo ya milima Gwassi na milima Gembe.

Fauka ya haya jamaa hawa wanaweza kutambulika sana kwenye mkoa wa Nyanza huo kutokana na udumishaji wao wa utamaduni, mila na itikadi kama mbare zingine pia.

Kwanza, bila kupoteza wakati, hebu nigusie swala la tamaduni, Wasuba wako na wanawake wapiga ramli stadi wanaoaminika wanaweza kuwasiliana na hali ya anga mpaka mvua ianze kutiririka kwenye eneo wanalotaka.

Lo! Maajabu walio nayo jamii ya Kisuba kweli.

Hupasha wavulana pamoja na wasichana tohara na pia wakati huo, wanatakiwa kukaa na kutembea kwenye nyika huku wakiimba nyimbo na miili yao kupakwa rangi aina ya kijivu.

Kadhalika wao hustahili kuvaa shumizi na ngozi wakibeba sagai, pinde, podo na mishale.

Wasichana nao wanatakiwa kuvaa aina fulani ya ngozi.

Mwanamke wa Kisuba aliyejaliwa kuwa na motto anahitajika kujitambulisha na nguo anazozivaa, ngozi iliyokatwa na likawa kama kamba kasha likakaushwa kwa moto.

Huvaliwa na wanawake kama hawa, basi hakuna mwanamume ye yote atakayestahiliwa aidha kumtaka kwa posa au pengine hata kuonana naye kimwili ila tu mchumba wake pekee.

Wasuba pia ni watu wanaotambulika kwa kupenda kwao kwa wageni na ina ya sherehe anayoandaliwa mgeni wakati ambapo anapowatembelea ndugu zetu Wasuba.

Wakati wa kukaribisha mgeni, kuna aina fulani ya dansi inayoandaliwa na vigoli, wanawali hawana wanaimba nyimbo tamutamu sana kaw sauti inayoweza kusikika yapata umbali wa kilomita 10 hivi.

Wanajipamba na kupambika kwani wakati huu ndio huwa wakati wa urembo wao kutambulika, wasichana hawa huchanja chale usoni, miguuni na mikononi wakivaa vikufu vya shaba na mdomoni wakiweka ndonya huku nyweleni pia wamepaka ngeu.

Isitoshe, masikioni, hau huweka herini na vipuli, kweli bila shaka msomaji usifikirie eti makabila mengine pekee ndiyo wanaotambuliwa kwa urembo wa vigoli, labda uliteleza kidogo na ndiyo maana wasemi nao hawakukuwa na budi kunena kwamba “pwagu hupata pwaguzi”.

Wanaofuata kwenye dansi ni vijana nao wakiingia katika mtindo wa kipekee wakivaa mavazi za kuvutia sana za ngozi za nyani na wakionekana kama mashujaa wa kivita.

Wasuba hupenda kula samaki waliokaushwa ama kuchomwa wanaovua kutoka Ziwa Victoria na maziwa pia wakichanganya na mayai.

Lugha ya Ki-ekesuba imegawanywa mara tatu, wale Wasuba wa kutoka kisiwa cha Mfang’ano wanahanganya ndimi ni Ki-Luganda, au Kinyopre, ilhali Wasuba toka eneo la Kaksingri hupiga gumzo iliyochanganywa na Ki-kuria.

Wakati nao wenao kutoka Gwassi huongea kwa Ki-ungoe, lugha inayofanana na Ki-gwassi, Ki-wirege kinachokaa kama Ki-kuria na Ki-gwassi pia kinachotamkwa Ki-kuria.