http://www.swahilihub.com/image/view/-/1624842/medRes/427793/-/becv2lz/-/wadorobo.jpg

 

Mila na tamaduni za Wadorobo

Wadorobo

Wanawake kutoka kabila ya Dorobo 

Na SWAHILI HUB

Imepakiwa - Friday, November 16  2012 at  14:06

Kwa Muhtasari

Ogiek ama Wadorobo hupenda kukaa pamoja huku wakiimba nyimbo za kivita pamoja na za ushindi.

 

NDUGU msomaji hapana shaka kwa muda wa siku chache zilizopita ulisikia kuwa Wadorobo wanakabiliwa na tisho ya kuondolewa katika ardhi ndogo wanamokalia wilayani Nakuru.

Nikiwaangaza kihistoria, kwanza jamii hii walipata jina la Dorobo au Ogiek kutokana na maisha yao yaliyokuwa yakienda sambamba na kuwinda wanyama wa kuchuna matunda mnamo karne ya kumi na kenda.

Waliungana san asana na jamii za Kalenjin, Keiyo, Kipsigis, Nandi na hata Turgen wakati wa vita na uvamizi. Pia walikuwa marafiki sana na Wamaasai mpaka kuna wakati walikuwa wakibadilisha vitu vya thamani kama pembe za ndovu, asali na hata zana za kivita kama sagai, pinde na mishale.

Huku Wamaasai wakiungana nao wakati wa kutafuta mifugo yao yaliyokuwa yakiibiwa na watu wengine au mifugo zikipotea kutokana na majanga kama ukame, magonjwa na hata matatizo mengine yaliyokuwa yakiwakera.

Hawa watu hupenda sana kula nyama ya wanya na mwitu wanaowawinda kwenye misitu zilizoko huko kwao na asali wanaopata kwenye mzinga ya nyuki pia wanaopata kwenye misitu.

Ogiek ama Wadorobo hupenda kukaa pamoja huku wakiimba nyimbo za kivita pamoja na za ushindi.

Historian a utafiti huonyesha eti wengi wa Wadorobo hupatikana huko Loitokitok na kando na kando mwa mlima Kilimanjaro.

Jamii hii walitokana na kugawanyika kwa Wamaasai na Wakikuyu walipatikana huko Kilimanjaro, waliobakia nao walizaana kisha hao pia wakaendelea kuishi kwa umoja lakini kwa bahati mbaya, vita vilivyokuwa kila mara viliwafanya wakimbilie misitu ambapo walipata makao  mapya kama wakimbizi.

Wadorobo huongea Kimaasai huku wakichanganya ndimi na Kigalla kisha lugha ya Kidorobo likaja. Mila na desturi yao hufanana sana nay a Kimaasai ijapokuwa jambo la vikundi ndilo hawajatilia maanani sana.

Je, hawa Wadorobo wanaweza kuwa eti ni Wamaasai?

Jibu ni kuwa, walikuwa Wakikuyu na Wamaasai waliozaana kisha kabila la tatu likatokea. Hivi ni kuwa, kwenye vitongoji vya mji wa Kijabe kuna familia zingine ambazo ni nusu Wakikuyu na nusu Dorobo, ambapo wanajiita Wakikuyu lakini mila na desturi pamoja na itikadi hayo ni kama Wadorobo.

Ogiek ama Wadorobo wengi bado hawajahudhuria shule, iwe ya msingi au ya upili. Idadi za shule zilizoko ni chache sana kiasi ambacho wanafunzi ambao hufanya mitihani za kitaifa wanapaswa kukaa katika darasa moja tu na kumbuka hawa ni wale wanaotoka katika tarafa moja.

Pia, sababu za kufanya shule ziwe chache huku ni kuwa, walimu wale wanaofuzu kutoka kwa vyuo vya ualimu humu nchini, wengi wao hupenda kuenda kwenye sehemu ambazo zimestahamilika kimaendeleo ambako wanaweza kujimarisha kwa Nyanja mbalimbali kama ya kifedha, kiafya, kimasomo na katika harakati yao ya kimaendeleo.

Wadorobo wengi hutegemea mapato kutokana na mifugo iwe ya kifedha au mlo. Ukitembea katika masoko huku, bila shaka utapata aina mbali mbali ya watu kumi utakaokutana nao, labda mawili tu ndio labda watakuwa wamevaa kuptula na jezi, wani wengi wamebaki wote wako nusu uchi labda shuka tu.

Huduma za afya pia ni jambo linguine serikali linafaa litie maanani, kwani Wadorobo, au Ogiek, hutembea kwa mwendo mrefu yapasa kilomita ishirini hivi ndio angalau wahudumiwe kiafya.

Wadorobo wanaishi tu kama maskwota kwani arshi ndogo waliyo nayo sasa inanyakuliwa na wale wanaojiita wenyeji wa huko na sasa hawana mahali pa kwenda.

Tuwapatie nafasi pia hawa kwani wako miongoni mwetu sisi kama Wakenya ingawaje wako wadogo sana lakini jambo la kutilia shaka ni kuwa tunawahitaji sana katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo na ujenzi wa taifa.

Na isitioshe, ni majivuno yetu sana sisi Wakenya kuwa na jamii ambao bado wanadumisha mila na desturi yao.