Mila na tamaduni za Wapokomo

Wapokomo

Wachezaji wa 'Bombolulu Cultural Dancers' wakicheza ngoma ya Wapokomo 

Imepakiwa - Tuesday, November 20  2012 at  11:38

Kwa Muhtasari

Wapokomo hupatikana wilayani Tana River mkoani Pwani.

 

“Ee Mungu nguvu yetu

ulete haraka kwetu,

haki iwe ngao ya mlinzi na tukae na undugu amani na uhuru,

raha tupate na ustawi”

Bila shaka hayo maneno si mageni kwetu hata kidogo huwa yanatajwa katika wimbo wetu wa taifa. Muundo na ustadi wake ulitokana na wimbo wa kumlalisha motto kutoka kwa ndugu zetu Wapokomo.

Wapokomo tangu tulipojinyakuha uhuru wanajivunia sana wimbo huu kutokana na heshimaa iliotunikiwa kitaifa.

Kabila hili hupatikana wilayani Tana River mkoani Pwani. Kable hawakuwa wameelekea mjini Hola na Tana, waliachana na wenzao kutoka kwa jamii ya Ki-Shungwaya waliokuwa kaskazini mwa Malindi.

Wakiwa chini ya unahodha Buu, walitoka katika eneo la pwani miaka mia moja kabla ya kuwasili kwao kundi la Nyika, miaka mingi iliyopita, jamaa hawa walikuwa wanapenda kutumia vyombo vilivyotengenzwa kwa njia ya ufinyanzi.

Usanii huu kwanza una historia katika jamii hii nan i jambo la kuridhisha kwamba kufinyanga vyombo ni ujuzi ambao wengi wao bado juwa wanajigamba nacho.

Wapokomo wafinayanzi walikuwa wakichimba udongo maalaum unaotwa Mahumba anaojulikana kwa ubora wake wa kushikana umbile laini na haufanyi nyufa hata kidogo.

Haikadhalika, Wapokomo pia huwa na kundi maalum kinachokaa kama serikali ndogo, kundi hili huitwa Wakiju. Ni kundi la watu wenye kuogfya mno sio tu kimamlaka au kiumri bali pia ni vile ambavyo wanajivaa.

Wazee kutoka kundi la Wakiju hukutana katika pahali maalum paitwapo Ngaji, jina lililotolewa kutokana na aina ya ngoma inayotengenezwa na mbao kisha kuweka kwenye sebule kinachotengwa kivyake.

Ngaji husimamishwa kistadi kwa vijiti vitatu na kuwekwa kwenye nyika. Wakati ngoma inapochapwa, sauti inayotoka inakusudiwa kufanya vijana walio karibu kuisikia na iwapo kuna mmoja kati yao ambaye hajatahiririwa basi hana budi kutoroka mbio kwani sauti huwa ni wa kutoa nyoka pangoni.

Wakamba huita hii ngoma Mabani ilhali wenzao Wagiriama na Warabai nao huitamka Muanza.

Wasichana vilevile wakati wanapoingia katika umri wa kuwa na mchumba, wanatambuliwa na nywele zilizoshukwa kwani huwa wanatoa vitambaa wakliokuwa wakivaa kama wako wachanga, nywele hutiwa pambo murwa sana na kuzingiriwa na vikumu vilivyopakwa rangi.

Wapokomo hutahirisha vijana pekee, jambo ambalo hutekelezwa na wazee wakongwe wanaopaswa kuvaa shumizi ni kama wanaingia jandoni, wakongwe hawa hufundisha hawa vijana jinsi ya kutumia mishale na podo.