Merille ni kama hawako tena

Merille

Wamerille wakibeba samaki kutoka Ziwa Turkana 

Imepakiwa - Tuesday, November 20  2012 at  14:09

Kwa Muhtasari

Sehemu Merille wanayoishi ni kando kando ya Ziwa Turkana na joto kali.

 

Merille ni kabila ambalo hupatikana kaskazini mwa Kenya kando kando ya Ziwa Turkana.

Utafiti katika sehemu hiyo hivi majuzu, ulifichua kwamba idadi yao ni ndogo sana hivi kwamba kwa sasa huishi kama familia moja tu!

Sehemu wanayoishi ni kavu na joto kali. Mtu anaweza kutembea yapata hata kilomita kama ishirini hivi bila hata kupata maji ya kukomesha kiu huku ukitembea kwenye udongo uliokauka usio na rotuba.

Licha ya matatiza mengi yanayowakabili, lakini Wa-Merille wanazidi kudumisha utamaduni wao, kwani utapata katika boma moja watoto wasiozidi wanane huwa wanaishi na wazazi wao hata wale waliofikisha umri wa kuoa ama kuolewa.

Lakini utapata kuwa binti aliyepata moto nje ya ndoa, hulazimishwa kwenda kuishi mbali na wazazi wake.

Kadhalika binti kama huyo akaozwa, mahari itakayotolewa huwa ni duni kwa sababu ataonekana ni kama ‘si msafi kimila’

Kilemwe au kilembwezeka aliyezaliwa na mamake pia hapaswi kubebwa na nyanyake au babuye wakati angali mchanga.

Mvulana barobaro ambaye pia hajaozwa msichana, huwa hatakiwi awe na uhusiano wowote na mwanamwali na akipatikana, basi atapaswa aidha aende kuishi katika kijiji kingine au kupotea kabisa bila kuonekana tena na huyo msichana pahali pasipo julikana kabisa!

Mmerille ambaye amevaa manyoya ya ndege kicwani, kisha akaweka vipuli masikoni na awe ni mwanamume, au akionekana amevaa shumizi wakati anapoingia jandoni, itamaanisha eti ameuwa adui wake vitani na atachukliwa kama shujaa wa kijiji chake huku akutunukiwa heshima na wanakijiji.

Kijana kama huyo pia atatunukiwa msichana mrembo wa kuishi naye.

Wasichana wa Ki-Merille huwa na urembo wa kukata na shoka kama bado wangali wadogo, na huwa hawaruhusiwi kurithi  mali ya familia.

Wakati angali chini ya ulinzi wa wazazi wake, msichana kama huyo kazi yake ni kama kutafuta kuni, kuteka maji, kupika na kazi zote za kinyumbani.

Naye mvulana hupaswa kukaa na babake kila mara ndiposa aambiwe namna ya kuwinda wanyama, kulisha mifugo, kuchunga boma kutokana na maadui, pamoja na kazi zote za kiume.

Ajabu ni kwamba, motto wa kiume hutakiwa kuanza shughuli hizi akiwa na umri wa miaka sita tu.

Katika sehemu hiyo yao inayopakana na Ethiopia, hamna shule kwani watoto hawapelekwi kusoma, somo lao ni kuchunga mifugo.