Jombi alimwa kupatwa akimega tunda la jirani Krismasi

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Sunday, December 31  2017 at  17:00

Kwa Muhtasari

GITHUNGURI, KIAMBU

KALAMENI mmoja kutoka eneo hili, atavuka mwaka akiuguza majeraha, kufuatia kichapo kikali alichopata baada ya kupatikana akitafuna tunda la jirani yake.

 

Kulingana na mdokezi, kalameni alinyakwa akirushana roho na mke wa jirani yake.

Duru zinasema kabla ya tukio, kalameni alikuwa amemuaga mkewe huku akimueleza kwamba angekesha kanisani.

Inadaiwa badala ya polo kwenda moja kwa moja hadi kanisani kwa kesha, aliamua kupitia kwa boma la jirani. Hii ni baada yake kupata habari kwamba jirani hakuwa nyumbani.

Jirani alikuwa kwa rafiki yake wakiburudika walivyozoea mwishoni mwa mwaka.

Penyenye zinaarifu kulikuweko na uvumi kwamba kalameni na mke wa jirani walikuwa wakiendeleza uhusiano wa kimapenzi kisiri jambo ambalo jirani aliamua kulifanyia uchunguzi bila ya kumchukulia polo hatua.

Inasemekana polo alipofika kwa jirani alianza kurina asali ya mwenyewe bila kujali.

Baada ya muda mfupi, jirani aliwasili na jamaa akajaribu kurukia kwa dirisha lakini mwanya wa dirisha ulikuwa mdogo sana kwake.

“Nilikuwa nikifikiri mambo yaliyokuwa yakienea kukuhusu wewe na mke wangu ni uvumi tu. Leo nimekupata. Utanitambua,” mwenye boma alimfokea polo.

Polo alijaribu kutafuta namna ya kutoroka lakini ikawa ngumu. Jirani alimrukia na kuanza kumpa kichapo bila kujali mjeledi ungeanguka sehemu gani ya mwili.

“Wewe ni jirani wa aina gani! Nilikuwa nikifikiria kuwa wewe ni mtu mzuri. Kama ni ujirani wacha uishe leo,” jirani alimkaripia polo.

Alipoona polo akiendelea kujeruhiwa, mwanadada alikimbia na kuufungua mlango. Polo alipopata nafasi ya kutoroka, alichomoka mbio bila kuangalia nyuma.

 

 

Mke taabani kwa kukosa kuandaa busaa Krismasi

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Thursday, December 28  2017 at  20:36

Kwa Muhtasari

KOTUR, TESO

WENYEJI wa eneo hili walipigwa na butwaa polo alipomzomea vikali mke wake kwa kukosa kuandaa busaa ya Krismasi.

 

Kulingana na mdokezi, polo alikuwa akitarajia kipusa amuandalie busaa. Alishangaa sana alipogundua kwamba kipusa hakumuandalia kinywaji chake ambacho anakienzi sana.

Inasemekana polo alikuwa akiandaliwa busaa na mkewe kwa miaka mingi. Duru zinasema siku ya Krismasi ilipofika, polo alimueleza mkewe kwamba marafiki zake wangejumuika naye jioni. Polo alimuelekeza mkewe ajitayarishe kuwandalia busaa.

“Mara hii sijaunda busaa. Hao marafiki zako nitawapikia chai,” kipusa alimueleza polo. Inadaiwa polo alimuangalia kipusa na kunyamaza kwa dakika tatu. “Wewe ni kama umepagawa. Hujui unalosema. Krismasi bila busaa si Krismasi. Wageni wangu wanakuja jioni na ni lazima wanywe busaa,” polo alisema kwa ukali.

Kipusa alimlaumu polo kwa kumkanganya kwani hapo awali polo alikuwa amedai kuachana na busaa.

“Wewe uliniambia mambo ya busaa umeachana nayo. Ulitaka nitengezee nani anywe? Isitoshe nimetoka kwetu nikiwa nimechelewa. Sikuwa na wakati,” kipusa alijibu.

Polo alianza kumzomea mkewe huku akiapa kumpa adabu.
“Mimi sikukuambia nimeacha kabisa. Ni kupunguza tu. Isitoshe Krismasi ni sherehe kubwa sana. Utaacha uvivu,” polo alimzomea mkewe huku akitishia kumtimua.

“Mimi sitaki mtu wa kuniletea aibu hapa. Bila busaa hutakaa hapa. Uliona kwenu ni kuzuri kushinda kwangu,” polo alimzomea mkewe.

Majirani wa polo walianza kukusanyika pembezoni kutazamia sinema ya bure. “Wanawake wote kijijini humu walienda kwao na wakarudi kwa wakati kuandalia waume zao krisimasi ya kukata na shoka. Wewe je?” polo alizidi kufoka. Kipusa aliamua kunyamaza.

“Sijawahi ona sherehe ovyo kama hii kwangu. Maandalizi yamekuwa duni kabisa. Na ni wewe umekuwa sababu,” polo alimzomea kipusa.

 

 

Mhubiri afumaniwa akirina asali ya mke wa askari barabarani

Na Mary Wangari

Imepakiwa - Sunday, December 17  2017 at  13:57

Kwa Muhtasari

NDEIYA, Limuru

KIOJA kilizuka hapa, baada ya mhubiri mashuhuri kufumaniwa akichovya asali ya mke wa afisa mmoja wa polisi kando ya barabara.

 

Kwa mujibu wa mdaku wetu, mchungaji na mke wa afisa huyo yamkini walizidiwa na mahaba ambapo kasisi aliliegesha gari lake kando ya barabara na wakaanza kula uroda.

Yasemekana pasta huyo aliacha mkewe na watoto nyumbani na kukutana na mke wa afisa huyo kabla ya kuanza kucheza miereka kando ya barabara!

Mdaku wetu alitujuza kwamba wawili hao walipatikana na maafisa wengine wa polisi waliokuwa wakishika doria katika barabara hiyo.

Maafisa hao waliposimama kulikagua gari hilo lililokuwa limeegeshwa kando ya barabara, waliwapata katika kilele cha kurushana roho.

 

 

Pasta abomolea mwanawe nyumba kuigeuza ‘danguro’

Na  Kimani Wa Njuguna

Imepakiwa - Sunday, December 17  2017 at  13:54

Kwa Muhtasari

BANANA, Kiambu

PASTA wa hapa, alibomoa nyumba aliyomjengea mwanawe, akimlaumu kwa kuitumia kama danguro.

 

Yasemekana jamaa ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu alikuwa akiwaalika marafiki zake na wapenzi wao nyumbani tabia ambayo haikumfurahisha baba yake.

Siku ya kisanga, jamaa alitoka baa akiwa na mpenzi wake na walipofika nyumbani mzee aliwasikia wakizungumza na akatoka nje.

“Kwa hivyo hata baada ya kukuonya dhidi ya ushetani hutaki kunisikia na umegeuza nyumba niliyokujengea kuwa danguro? Leo utakuwa mwisho wako kuishi hapa kwangu,” alifoka mhubiri na kuanza kubomoa nyumba hiyo.

Jamaa na kidosho wake walilazimika kutimua mbio.

 

 

Ahepa mkewe kuhusu bajeti kali ya Krismasi

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Sunday, December 17  2017 at  13:51

Kwa Muhtasari

CHAKOLI, TESO

KIZAAZAA kilizuka eneo hili, baada ya kipusa kumpa polo bajeti ya krismasi. Kulingana na mdokezi, polo alimzomea kipusa huku akimkumbusha jinsi maisha yalivyomkalia vibaya mwaka mzima.

 

Kipusa hakufurahishwa na matamshi ya polo. “Maisha gani yamekuwa magumu! Mwaka ulipoanza ulikuwa mlevi. Kwa mama pima hujakuwa ukikosa. Ukora utaacha,” kipusa alimkaripia polo.

Duru zinasema kipusa alimlazimisha polo kuipokea bajeti hiyo. “Chukua haraka. Hivi vitu navihitaji kesho kutwa. Nusu yake navipeleka kwetu hata mama yangu pia afurahie kidogo,” kipusa alimueleza polo.

Penyenye zinasema polo alipoona kipusa amezidi, aliamua kutafuta mbinu ya kuhepa jukumu hilo.
Polo alibeba suruali zake tatu na shati kadhaa na kuanza safari. “Nitarudi jioni. Hivi vitu vyote umeniambia nilete nitaleta. Usijali,” polo alimueleza kipusa huku akianza safari.

Kipusa alishangazwa na polo na kumuuliza alikokuwa akienda.

Polo aliendelea na safari yake bila kujali maneno ya kipusa. “Hii begi naenda kubebea vitu vya krismasi. Nitarudi jioni. Jipange kuenda kwenu kesho kutwa,” polo alimueleza kipusa.

Bila kujua kilichokuwa ndani ya begi, kipusa aliamua kumwamini polo. Jioni ilipofika, polo hakuonekana. Kipusa alipompigia simu, polo hakuchukua ila alituma ujumbe.

“Hebu jipange hii krismasi. Mimi siko karibu. Tutaonana mwaka ujao Desemba,” ujumbe ulisema.

Kipusa naye alimshtumu polo kwa uamuzi wake. “Una ujinga sana. Hivyo vitu vichache tu ndivyo vinakufanya utoroke boma. Umejiaibisha mwenyewe,” kipusa alimzomea polo.

Polo alimgombeza kipusa kwa kuwajali watu wa kwao tu. “Siwezi kuwalisha watu wa kwenu. Hebu jipange. Tutaonana mwaka ujao,” polo alimueleza kipusa huku akiizima simu yake.

 

 

Amzomea mumewe kumuachia kijibaridi usiku kucha

Na JOHN MUSYOKI

Imepakiwa - Tuesday, November 28  2017 at  17:44

Kwa Muhtasari

SIAKAGO, EMBU

DEMU mmoja kutoka sehemu hii alishangaza wapangaji plotini kwa kukemea mumewe kwa kumuacha kwenye baridi na kwenda kuhudhuria kesha kanisani bila kumwarifu.

 

Inasemekana kalameni alitoka chumbani mwendo wa saa kumi na moja jioni na kwenda moja kwa moja hadi kanisani kuungana na waumini wengine katika kesha.

Inadaiwa kuwa kalameni aliendelea kufanya maombi usiku kucha lakini cha kushangaza ni kuwa hakuarifu mkewe. Kulingana na mdokezi, jamaa alizima simu jambo lililomkasirisha mkewe.

Jamaa alifika nyumbani asubuhi iliyofuata na kudai alihisi usingizi lakini mkewe akamfokea. “Eti unahisi usingizi, kwanza ninataka unielezee wazi ulipokesha,” demu alisema.

Kalameni kwa upande wake alijitetea na kusema alikuwa kesha kanisani. “Nilikesha kanisani na wenzangu tukiomba. Kuna shida gani nikikesha kanisani,” kalameni alisema.

Demu alimkatiza jamaa na kuendelea kumfokea. “Wacha nikwambie, siku hizi umekuwa mtu bure kabisa. Yaani uliniacha kwenye baridi bila hata kuniarifu. Kuanzia leo utajipanga. Sitavumilia tabia hiyo tena.Haujui una majukumu ya kufanya nyumbani,”demu aliwaka.

Kalameni alijaribu kujitetea lakini demu alimpuuza na kutisha kumuacha iwapo hatarekebisha tabia yake.

 

 

Pasta pabaya kwa kuahidi miujiza hewa

Na ORNELIUS MUTISYA

Imepakiwa - Tuesday, November 28  2017 at  17:41

Kwa Muhtasari

KATHIANI MJINI

WAUMINI wa kanisa moja mjini hapa walizua kasheshe walipomzomea pasta wao peupe baada ya miujiza aliyokuwa amewaahidi kukosa kutimia!

 

Kulingana na mdokezi, pasta aliwaambia waumini waliokuwa na mahitaji mbalimbali wajitokeze mbele ya madhabahu ili awaombee. Aliwaahidi kuwa watapata miujiza baada ya muda wa siku tisini.

“Nimepata maono kutoka kwa Mungu kwamba baada ya muda wa siku tisini, kila mmoja wenu atakuwa na ploti yake mjini hapa,” pasta aliahidi waumini wake.

Inasemekana kwamba waumini hao walijawa na furaha ghaya na asilimia kubwa wakajipanga foleni mbele ya madhabahu waombewe ili wapokee miujiza hiyo.

“Mtu wa Mungu alimtaka kila mmoja apande mbegu ili apate miujiza iliyokuwa njiani yaja,’’ alieleza mdaku wetu.
Penyenye za mtaa zaarifu kuwa, siku tisini zilipita na utabiri wa pasta ukadhihirika kuwa mzaha.

Waumini walipandwa na hasira za mkizi na wakaapa kumkabili awarejeshee hela walizopanda mbegu la sivyo, wamuonyeshe cha mtema kuni.

Siku ya tukio, waumini walifika kanisani mapema kuliko siku zingine na wakakaa kwa utulivu mwingi. Ibada iliendelea kama kawaida hadi wasaa wa kutoa sadaka ulipowadia na kwa kauli moja wakakataa kutoa matoleo yao

Duru zaarifu muumini mmoja alinyanyuka kwa ghadhabu na akamtaka pasta awarejeshee hela alizowalaghai akiwaahidi miujiza hewa. Waumini kadha waliingilia na kuzua purukushani humo kanisani.

“Kanisa liligeuka ulingo wa masumbwi huku baadhi ya waumini wakimtetea pasta,’’ alisema mdokezi wetu.
Penyenye zaarifu kuwa pasta aliwaambia baraka kutoka kwa Mungu huja polepole na hivyo hawakuwa na budi ila kuwa na subira. “Kanisa hilo liligawanyika kutoka siku hiyo,” alisema mdokezi.

 

 

Mganga amuonya vikali mhubiri kumvurugia kazi

Na DENNIS SINYO

Imepakiwa - Wednesday, November 15  2017 at  10:47

Kwa Muhtasari

Malaha, Webuye

TABIBU wa mitishamba eneo hili alitishia kumchukulia hatua kali mhubiri mmoja akidai amekuwa akimharibia kazi kwa kudai yeye ni tapeli.

 

Inasemekana jamaa alilalama kwamba biashara yake imekuwa ikidorora kila uchao kutokana na penyenye za mhubiri huyo.

Yasemekana jamaa alikuwa muumini wa kanisa la pasta kabla ya uhusiano wao kuvunjika alipoanza kupata wateja wengi kuliko washirika waliohudhuria ibada.

“Huyo mtu ni mkora na kila mtu anamjua. Anajifanya anawapa watu dawa ilhali ukweli ni kwamba analetea tu watu shida na balaa tupu,” alisema pasta.

Faida ya jamaa ilipoanza kupungua aliamua kumwendea pasta huyo na kumuonya aache kumharibia kazi au amchukulie hatua kali.

 

 

Marafiki watibuana sababu ya kidosho

Na JOHN MUSYOKI

Imepakiwa - Wednesday, November 15  2017 at  10:45

Kwa Muhtasari

Kamandio, Kitui

URAFIKI wa makalameni waliokuwa wakiishi katika chumba cha kupanga sehemu hii ulifikia kikomo waliporushiana makonde wakizozania demu mgeni katika ploti.

 

Inasemekana wawili hao walianza kuzozana huku mmoja akimlaumu mwenzake kwa kumpiku kuwahi kichuna huyo aliyehamia plotini siku chache zilizopita. Mzozo ulianza chumbani walichokuwa wakiishi jamaa akimlaumu mwenzake kwa kumnyemelea mwanadada huyo.

“Haujui huyo ni mrembo wangu. Mbona unajaribu kunipima akili na unajua huyo ni mrembo wangu tangu aingie katika ploti hii? Usianze kunisumbua ama nikuonyeshe cha mtema kuni,” kalameni alisema.

Inasemekana jamaa kwa upande wake alimgeukia mwenzake na kumfokea vikali. “Wacha ufala jamaa. Demu huyu alikuja hapa na hakuna mmoja aliyekuwa anamjua. Wacha kujishasha eti huyu ni demu wako. Nina uhuru wa kumtongoza na hautakatiza mpango wangu,” kalameni alisema.

Ni katika purukushani hiyo wawili hao walipoanza kutwangana na kushtua wapangaji plotini. Baadhi ya wapangaji walionya makalameni hao dhidi ya kuzua zogo na kuvuruga amani. “Wanaume nyinyi hamna adabu kupigana kama wajinga. Kuna wanawake wengi kila mahali. Acheni ufala,” mpangaji mmoja alisema.

Kulingana na mdokezi, kichuna alidai kwamba alikuwa ameolewa na alikuwa na watoto wawili. “Yaani mnapigana kwa sababu yangu. Poleni sana. Mimi nimeolewa na nina mume na watoto wawili kwa hivyo acheni ujinga. Kila mtu ajipange na muache kunipigania,” demu alisema.

Inasemekana demu alipomwaga mtama makalameni walishangaa sana. Baadaye wawili hao walihama ploti hiyo na inasemekana kila mmoja alienda kukodi chumba chake. Haikujulikana ikiwa walisameheana baada ya uadui kuzuka kwenye tukio hilo.

 

 

Akasirikia pasta kwa kukataa kumfanya mpishi wake

Na  JOHN MUSYOKI

Imepakiwa - Wednesday, November 15  2017 at  10:43

Kwa Muhtasari

Ngetani, Masinga

KIOJA kilishuhudiwa sehemu hii mama mmoja aliponunia pasta wake kwa kutomchagua kuwa mpishi jikoni kila Jumapili.

 

Inasemekana mama alikuwa jirani wa karibu wa pasta lakini alikasirika pasta alipokataa kumchagua kuwa mpishi. Mama alishindwa kuzuia hisia za machungu na kusikika akifoka baada ya kuchujwa na pasta.

“Yaani pasta amenipuuza tu na mimi ni jirani yake, hataki niwe mpishi. Wallahi ameniudhi sana na kuanzia leo sitaongea naye wala kumpa salamu zangu. Ajipange na kwangu asiwahi kutia guu kwa sababu nitahama niende kanisa nyingine,” mama alisema.

Inasemekana waliomsikia akipayuka walipigwa na mshangao mkubwa na kumshauri huku wengine wakitia chuki na kuangua vicheko.

“Pole sana dada yangu. Badala ya kununa heri uende ukapikie familia yako. Kwani ukipikia pasta utapata faida gani. Sio lazima uwe mpishi wa pasta hata kama wewe ni jirani wake wa karibu,” muumini mmoja alimwambia mama huku wengine wakiangua vicheko.

Inasemekana ibada ilipoisha mama alitangulia kuondoka kanisani na haijulikani iwapo alirejea katika kanisa hilo tena.

 

 

Sms ya mpango wa kando usiku yalisha demu kichapo

Na Victoria Nduva

Imepakiwa - Wednesday, November 8  2017 at  10:52

Kwa Muhtasari

Kyumbi, Machakos

MWANADADA wa hapa alilazimika kuhepa usiku kuepuka kichapo mumewe alipogundua alikuwa na mpango wa kando.

 

Yasemekana walikuwa wakilala mwanadada alipotumiwa ujumbe wa mapenzi kwenye simu na mpango wake wa kando. Kulingana na mdokezi, mume wa mwanadada alichukua simu na kukasirika baada ya kusoma ujumbe huo.

“Alimwamsha mkewe kwa mateke akitaka kujua aliyeutuma ujumbe huo saa sita usiku akimtakia usingizi mnono,” alisema mdokezi.
Mwanadada alijinasua kutoka mikono ya jombi akafungua mlango kimiujiza tu na kutoka nje akatokomea gizani. Jamaa hakuwa la jingine isipokuwa kulala na huo ukawa mwisho wa ndoa yao.

 

 

Lofa mtafuna ‘vifaranga’ afurushwa na wananchi

Na KIMANI WA NJUGUNA

Imepakiwa - Monday, November 6  2017 at  14:04

Kwa Muhtasari

KAIRI, Kiambu

Jamaa alilazimika kutoroka hapa baada ya wakazi kuapa kumwadhibu wakimlaumu kwa kuwadhulumu kimapenzi wasichana wa umri mdogo.

 

Yasemekana jamaa alikuwa na tabia ya kuwatongoza wasichana bila kujali, jambo ambalo halikuwafurahisha wakazi. 

Siku ya kisanga, jamaa alifumaniwa kichakani na mama mmoja akiwa na msichana wa shule ya upili. “Msichana huyo alianza kupiga kelele zilizomvutia mama aliyekuwa akipita,” alisema mdokezi.

Mama huyo alichukua kipande cha mti na kunyemelea hadi wawili hao walipokuwa  wakipapasana. 

“Kwa hivyo, unadhani unaweza kutuharibia wasichana wetu kwa tabia hii? Utajuta,” alifoka mama huyo. Bila kujali mama huyo alimuangushia jombi kipande cha mti kichwani.

Kuona hivyo, jombi alifaulu kuchomoka kama mshale na kutoroka asijulikane alipo.

 

 

Kisura atimua dadake kwa kunyemelea mumewe

Na EDISON WANGA

Imepakiwa - Monday, November 6  2017 at  14:01

Kwa Muhtasari

KIEMBENI, MOMBASA

Kipusa aliyeolewa na mzungu mjini hapa alimtimua dada yake aliyekuwa akiishi naye akidai alikuwa na njama za kumnyemelea mumewe. Kipusa huyo alianza kwa kushuku tabia ya dada yake ya  kuvalia nguo fupi fupi.

 

Inasemekana mwanadada huyo alipoanza kuishi na dadake, alikuwa akivalia nadhifu lakini baada ya miezi mitatu, mambo yalibadilika akaanza kuvalia sketi fupi, suruali za kubana na blauzi fupi zilizoacha mgongo ukiwa wazi hadi kamba za sidiria zikawa zaonekana waziwazi.

Juhudi za kipusa kumkataza dadake ziliambulia patupu. “Hizi nguo za aibu aibu usizivalie hapa kwangu. Usidanganyike eti wanaume watakupenda na upuzi wote unaovaa.

Watafanya kukutamani tu bali hawatakupenda. Watakutumia na kukutupa kama masimbi,” kipusa alimweleza dadake. Kulingana na mdokezi, binti alimjibu dada yake kwa madharau akimwambia alikuwa na uhuru wa kuvaa apendavyo.

“It’s my dress my choice, huwezi kunizuia kuvaa ninavyotaka mimi. Heri nipendeze roho yangu,” alijibu kwa kiburi na kejeli.

Hali iliendelea hivyo hadi kipusa akaja kugundua dada yake alivalia hivyo kwa nia ya kumnasa mumewe kimahaba. Ilibidi azibe ufa badala ya kujenga ukuta.

Aliamua kutumia ujanja kumtimua. Alimwambia kwamba alipanga safari na mumewe kwenda ng’ambo. “Chukuwa vitu hivi umpelekee mama. Pamoja na hizi pesa. Mimi na mume wangu tunasafiri juma lijalo. Nikirudi nitakuarifu,” kipusa huyo alimweleza dada yake.

Kulingana na mdokezi wetu, inasemekana dada huyo hakurudi tena. Haikujulikana ikiwa hofu ya mwanadada ya kupokonywa mumewe na dada yake ilikuwa ya kweli au la, japo alisikika akisema hatakaribisha mwanamke mwingine kwake tena.

 

 

Mpishi wa hoteli akutwa ameficha mahamri kwa suruali

Na JOHN MUSYOKI

Imepakiwa - Thursday, November 2  2017 at  11:23

Kwa Muhtasari

KYONDONI, MACHAKOS

KALAMENI mmoja kutoka sehemu hii alikiona cha mtema kuni alipofumaniwa na mwenye hoteli jikoni akiwa ameficha mahamri kwenye mifuko ya suruali yake.

 

Inasemekana kalameni alikuwa mpishi hoteli hiyo lakini alikuwa mlafi. Siku ya kioja kalameni alijipata kona mbaya alipofumaniwa na mwenye hoteli hiyo jikoni akiendelea kutafuna mahamri huku akiyatoa kwenye mfuko wake wa suruali.

Mwenye hoteli kwa hamaki alianza kumfokea jamaa.

“Yaani ni wewe huiba mahamri yangu? Kuanzia leo tamaa yako imefikia kikomo. Hautawahi kutafuna mahamri yangu tena,” mdosi alimkemea kalameni na kumwangushia kofi moto usoni.

Kalameni alipiga nduru zilizovutia waliokuwa karibu lakini hakuna aliyemtetea kwa sababu wengi walidai jamaa alikuwa mwenye tamaa sana na alikuwa akila chakula bila ruhusa.

“Wacha fisi afunzwe funzo. Nilimuonya siku nyingi aache kula mahamri ya boss lakini alikataa ushauri wangu, leo amepatikana, wacha atwangwe,” weita alisikika akiarifu wenzake huku vita vikichacha jikoni.

“Leo utalala polisi kwa sababu umeniudhi sana na kuharibu biashara yangu,” mdosi aliwaka.

Ni katika hali hiyo kalameni alipopata nafasi nzuri ya kuchomoka aliposikia kuwa angepelekwa polisi.

 

 

Mimba ni yangu, polo apayuka kuzima harusi

Na  TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Thursday, November 2  2017 at  11:15

Kwa Muhtasari

BUTULA, BUSIA

Kalameni mmoja kutoka eneo hili aliwashangaza wengi aliposimamisha harusi akidai kwamba bi harusi alikuwa na mimba yake.

 

Kulingana na mdokezi, kalameni alipata ujumbe kutoka kwa rafiki yake mmoja kuwa mpenzi wake alikuwa akipanga kuelekea jijini na polo fulani.

Vilevile alimueleza kuwa kabla ya kuondoka, kulikuwa na mpango wa wao kufunga harusi kwanza. Duru zinasema kalameni alianza kufanya uchunguzi.

Inasemekana alipobaini kwamba ni ukweli mrembo wake alikuwa akipanga kufunga harusi na polo mwingine, aliamua kutulia hadi siku ya harusi yenyewe.

Siku ilipowadia, kalameni hata hakungojea pasta aulize wale waliopinga harusi wajitokeze. Kalameni aliinuka kutoka kwenye kiti na kumrai pasta asimamishe harusi.

“Pasta nakuheshimu sana lakini nakuomba usimamishe hii harusi,” kalameni alimrai pasta. Pasta alibaki ameduwaa asijue la kufanya. “Huyu msichana alikuwa mpenzi wangu.

Kwa sasa ana mimba yangu. Kama mnataka kuendelea na harusi basi tusikilizane atakapojifungua aniletee mtoto wangu,” kalameni alimueleza pasta.

Duru zinasema pasta alibaki mdomo wazi. Kalameni aliketi huku waliohudhuria harusi wakishangaa. Penyenye zinasema polo aliyekuwa akifanya harusi na mrembo alikuwa ametoka tu jijini. Alielekea kwa akina mrembo na kumzuzua kwa hela alizokuwa nazo.

Inasemekana alipoona hela za polo, mrembo aliamua kubadilisha penzi lake. Duru zinaarifu kipusa alianza kuhepa simu za mpenzi wake wa hapo awali.

“Nataka kila mtu ajue hivi, nimegharamika sana kumtunza huyu msichana. Mara kwa mara alikuwa akija kwangu. Hadi tukasikilizana tupate mtoto. Mimi ninataka mtoto wangu,” kalameni alisisitiza. Ilibidi pasta asimamishe uchaguzi.

 

 

Demu azaba fisi kofi kwa kumpapasa matiti baani

Na JOHN MUSYOKI

Imepakiwa - Wednesday, November 1  2017 at  06:26

Kwa Muhtasari

WOTE, MAKUENI

KIZAAZAA kilishuhudiwa kwenye kilabu moja mjini hapa kalameni alipoangushiwa kichapo na mhudumu wa kilabu hiyo akimlaumu kwa kumpapasa matiti.

 

Kulingana na penyenye, kalameni aligusa demu huyo makusudi hali iliyomkasirisha na kuanza kufokea.

Hali iliyoonekana kuwa mzaha iligeuka kuwa ukumbi wa vita mwanadada alipogeukia jombi na kumlisha makofi usoni. “Bure kabisa, nani amekupa ruhusa ya kupapasa matiti yangu?,” demu aliwaka.

Inasemekana jombi alijitetea akisema hakuwa na nia mbaya bali alijipata tu amerusha mkono wake na kupapasa mwanadada huyo aliyeketi kando yake.

“Jamaa huyu ni fisi sana.Anapenda kumezea mate wake za watu. Wacha apate funzo aache tabia yake,” mteja mmoja alisema. Jamaa alilazimika kuondoka

 

 

Pasta apiga marufuku mke aanikaye ushuhuda wa ndoa kanisani

Na JOHN MUSYOKI

Imepakiwa - Wednesday, November 1  2017 at  06:28

Kwa Muhtasari

KIAMBERE MJINI

PASTA wa kanisa moja mjini hapa alishangaza waumini kwa kudai kwamba mke wake hajui kuficha siri za nyumbani.A

 

Kulingana na penyenye, pasta alimlaumu mkewe kwa kutoa ushuhuda kila mara kanisani akisema alikuwa akifichua siri nyingi za boma.

Inasemekana pasta alikerwa na tabia ya mkewe ya kufichua kila kitu kuhusu boma lake na kuapa kumzima kutoa ushuhuda kanisani.

“Ndugu zangu, mke wangu anajaribu kutoa siri za nyumbani kwangu kinyume cha matarajio yangu na kwa hivyo kuanzia leo hatakuwa akitoa ushuhuda.

Siku hizi watu wamesahau kutoa ushuhuda mzuri na kuanza kufichua mambo ya kisiri ya boma zao wakidhani wanaongozwa na roho kufichua mambo ambayo hayafai mbele ya wengine,” pasta alisema.

Inasemekana mke wa pasta hakusita kutoa ushuhuda licha ya mume kumkashifu.

“Siwezi nikaficha yaliyo moyoni. Kila mtu ana ushuhuda wake na hakuna mtu wa kuzuia ushuhuda wa mtu mwingine,” mama alisema. Waumini walishangaa sana huku wengine wakiangua vicheko.

“Jameni huenda pasta na mke wake wamekosana,” waumini walisikika wakisemezana.
Hata hivyo, haikujulikana kilichojiri baada ya kioja hicho.

 

 

Kalameni ahama ploti mke kuolewa na jirani

Na  EDISON WANGA

Imepakiwa - Wednesday, November 1  2017 at  06:23

Kwa Muhtasari

CHAANI, MAGONGO

JAMAA wa hapa aliamua kuhama ploti baada ya kugundua mkewe waliyetengana naye alikuwa ameolewa na jirani yake.

 

Duru zilizotufikia zinasema kuwa jamaa ambaye ni mlevi, alishindwa kukidhi mahitaji ya familia na akawa anarudi nyumbani usiku wa manane kumpiga mkewe akitaka chakula.

Ilibidi mkewe afanye vibarua ili kupata riziki. Jamaa hakujali hayo. Aliendelea kumpiga mkewe kama ngoma. Mkewe alipochoka na kichapo, alirudi kwao mashambani.

“Jamaa alifurahia hatua ya mkewe na hata akampa nauli. Mke alifunganya kilichokuwa chake na kurudi kwao mashambani,” alisema mdokezi.

Baada ya miezi mitatu, jamaa alitoka kazini na kumkuta mkewe kwenye roshani akipiga gumzo na wanawake wenzake.
“Wewe ni nani aliyekuleta hapa? Si nilikupa nauli ukarudi kwenu, umekuja kufuata nini? Naomba uondoke, sitaki kukuona hapa kwangu!” jamaa alimfokea mkewe.

“Wewe hapo ulipo wajua kumtunza mke? Kula, kunywa na kuvaa ujue wapi? Ulinitesa kwa njaa, sasa nimepata mume mwenzako, ananitunza kama malkia. Kwako hutaniona ng’oo! Utasubiri sana,” kipusa alimjibu jamaa kwa bezo.

Jamaa alifanya uchunguzi kutaka kujua ni nani aliyemleta mkewe na kidudu mtu alimweleza ni jirani yake aliyejishindia mwanadada huyo.

Aliposikia hayo jamaa alienda kwa landilodi na kumwambia amrejeshee deposit yake atafute nyumba kwingine.
Alisema asingeishi na mume mwenza katika ploti moja. Alisema ingemuuma kumuona mkewe akiingia na kutoka kwa jirani.

Landilodi alimuomba jamaa ampe muda wa wiki moja amrejeshee pesa zake. Landilodi pia alimuunga jamaa mkono akimwambia kisa hicho ni cha aibu.

 

 

Mapolo wazuia pasta akijisaidia kwenye choo cha klabu

Na JOHN MUSYOKI

Imepakiwa - Monday, October 2  2017 at  12:48

Kwa Muhtasari

Kyondoni, MASINGA

WALEVI kutoka sehemu hii, walishangaza wengi walipomzuia pasta kuingia kwenye choo cha kilabu kwa haja ndogo.

 

Duru zinasema kuwa pasta alikuwa akipita karibu na kilabu hiyo lakini akakazwa na haja na akaamua kuingia msalani.

Makalameni waliokuwa wakinywa pombe walipomuona akikaribia, walianza kumrushia maneno na kumwambia asiingie kwenye choo hicho.

“Wewe pasta unaenda wapi? Nani alikuambia kuwa choo hiki ni cha kanisa? Unataka nini hapa? Kama unataka kukojoa nenda mahali pengine,” makalameni walisema.

Hata hivyo, mtu wa mungu alisisitiza kuwa alikuwa amekazwa lakini walevi hao hawakujali mbali waliendelea kumfukuza .

“Hakuna shida yoyote mimi kuingia kwenye choo. Nimekazwa sana na hakuna haja kuninyima nafasi ya kujisaidia. Hapa hakuna pahali pengine ambapo ningeendakujisaidia,” pasta alieleza.

Makalameni walizidi kuzua fujo huku wakitaka pasta aondoke kwenye choo cha kilabu.

Inasemekana pasta hakuwa na lingine la kufanya ila kuondoka kwa sababu walevi hao walikataa katakata kumruhusu kuingia chooni. Haikujulikana iwapo pasta alifaulu kupata pa kwenda haja.

 

 

Azomea vipusa kumkejeli kwa kufulia mchumba wake sidiria

Na JOHN MUSYOKI

Imepakiwa - Monday, October 2  2017 at  12:41

Kwa Muhtasari

THIKA MJINI

KALAMENI mmoja mjini hapa, alishangaza wapangaji plotini alipowazomea vipusa wawili waliomkejeli kwa kumpata akifua nguo za mwanamke nje ya chumba chake.

 

Duru zinasema kalameni alikuwa akimfulia demu wake sidiria, sketi na rinda wakati vipusa hao walipompata na kuanza kidomodomo chao huku wakimsema. Kwa hamaki kalameni alienda kuwafokea vikali.

“Mnacheka nini? Mnadhani sijawasikia. Kama wapenzi wenu hawawezi kuwafulia nguo mimi hufulia mpenzi wangu,” kalameni alisema.

Inasemekana demu wa jamaa huyo hakuwa karibu na jamaa alichukua fursa hiyo kumfulia nguo zake zilizokuwa chumbani.

Inasemekana kalameni aliendelea kufua nguo za mpenzi wake na kuzianika kwenye kamba zikauke.

 

 

Aanikwa hadharani na mpenzi wake wa zamani kwa kuwa ovyo kitandani

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Monday, October 2  2017 at  12:21

Kwa Muhtasari

Suna, MIGORI

WENYEJI wa eneo hili, walibahatika kutazama sinema ya bure baada ya mrembo kumzomea vikali mchumba wake wa zamani.

 

Inasemekana mrembo alichukua hatua hiyo baada ya kugundua kwamba polo alikuwa akimchafulia jina kijijini.
Kulingana na mdokezi, kabla ya wawili hawa kukosana, mrembo na polo walikuwa wakijulikana kijiji kizima.

Inadaiwa kwamba baada ya kuachana, mrembo alianza kusikia hadithi mbaya mbaya zikisambaa kijijini kumhusu.

Kulingana na mrembo, baadhi ya hadithi hizo zilikuwa ni habari ambazo walikuwa wamesikilizana na polo ziwe siri yao.
Penyenye zinasema mrembo alianza kufanya uchunguzi kubaini zilikotoka habari hizo. Inasemekana muda mrefu haukupita kabla ya mrembo kugundua kwamba mdaku alikuwa mchumba wake wa zamani.

Duru zinasema mrembo alifululiza moja kwa moja hadi kwa polo. “Shida yako ni gani. Si mimi nilikataa mambo yako. Mbona unatembea ukiniharibia sifa,” kipusa alimkaripia polo.

Inadaiwa kuwa polo alibaki mdomo wazi. “Hadithi zote nimezipata. Tangu lini nikawa bure kitandani. Tulipokuwa wachumba ulikuwa ukirina asali kila wakati bila kulalamika.

Leo hii unatembeza habari kinyume. Kweli nyani haoni kundule,” mrembo alizidi kumzomea polo. Aliendelea kubaki kimya tu!.

“Huyu jamaa anatembea akidai eti mimi napenda kula sana. Ni lini nimekuja kwako ukaninunulia hata soda pekee? Nikome kabisa,” mrembo alimshtumu polo.

Inasemekana polo aliamua kuondoka ili kuepa aibu na kumuacha mrembo pale.

“Umesahau kuwa ni mimi nilikuacha. Sema ukweli. Ni wewe ulikuwa ovyo kitandani ndiposa nikaamua kutafuta mwingine,” mrembo alimzomea polo huku vicheko vikitawala angani.

 

 

Amlipa kimada laki moja asitoboe siri

Na DENNIS SINYO

Imepakiwa - Saturday, July 8  2017 at  12:07

Kwa Muhtasari

BUTULA, BUSIA

JOMBI wa hapa alilazimika kutoa zaidi ya Sh100,000 kwa mpango wake wa kando kumshawishi asimharibie ndoa yake.

 

Inasemekana jamaa huyo alikuwa ameweka kimada licha ya kuwa na mke nyumbani na watoto watatu ambao walikuwa wakimtegemea.

Hali hiyo ilimlazimu kumtafutia mwanadada huyo nyumba mbali na kwake ili asikutane na mkewe. Kulingana na mdokezi, kipusa huyo alikuwa akinunuliwa kila kitu na jamaa huku akiahidiwa kujengewa boma.

Penyenye zinadai jamaa alianza kumhepa demu huyo alipogundua kwamba alitaka kuwa mke wake. “Nimechoka kuishi pekee yangu hapa mjini, kama hutaki kunipeleka nyumbani kama mkeo, nitafutie makazi yangu niishi,” kipusa alimwambia jamaa huyo.

Kusikia hivyo, jamaa alilipuka kwa hasira. “Kama hutaki kuishi hapa, shida ni yako. Sina mpango wala pesa za kukunulia shamba popote!’alifoka jamaa.

Kipusa huyo alimuonya jamaa kwamba alikuwa akicheza na moto na angejuta.

“Demu alisema alikuwa tayari kumkabili mke wa jamaa ili ukweli ubainike. Aidha, alidai kwamba iwapo jamaa hakuwa na haja ya kumuoa, alikuwa tayari kumwanika katika vyombo vya habari.

“Ulidhani singejua mkeo, ninamjua na nitahakikisha kwamba amejua kila kitu, hata wanahabari pia watakutafuta na kukuanika wazi,” alisema kipusa huyo.

Inasemekana jamaa alishtuka na kulazimika kumpa mwanadada huyo zaidi ya Sh100,000 ili asidhuhutu kumharibia ndoa yake.

Yasemekana kwamba mwanadada huyo alihama mara tu alipokabidhiwa hela hizo. Jamaa aliyeonekana kuvunjika moyo alidai kwamba alikuwa amepata pigo na funzo la mwaka akiapa kuachana na mipango ya kando.

 

 

Pasta asahau Biblia kwa hawara baada ya kuonjeshwa asali

Na CECIL ODONGO

Imepakiwa - Tuesday, May 30  2017 at  15:36

Kwa Muhtasari

KAMKUYWA, BUNGOMA

PASTA wa mji huu alijipata kwenye kona mbaya alipoenda kutoa huduma ya maombi kwa nyumba ya mwanamke moja bila kufahamu kwamba alikuwa hawara.

 

Inasemekana kwamba mwanamke huyo alijifanya mgonjwa na kwa kuwa pasta huyo alikuwa akitoa huduma hiyo kutoka nyumba hadi nyingine alikubali ombi lake bila kujua alikuwa na nia mbaya.

Penyenye ziliambia meza ya dondoo kwamba pasta aliingia nyumba hiyo na kukaribishwa kwa mapochopocho na vinywaji.

Alipomaliza kula jamaa alitekwa na usingizi mnono na alipozinduka alijipata uchi kitandani kando ya mwanadada aliyedai alikuwa mgonjwa.

Inasemekana alivaa nguo zake haraka na kuondoka bila kuongea na mwanamke huyo hata akasahau Bibilia yake.

 

 

Pasta amramba kofi muumini mpenda anasa kwa kusinzia

Na KIMANI wa NJUGUNA

Imepakiwa - Tuesday, May 30  2017 at  15:31

Kwa Muhtasari

MWEA, KIRINYAGA

KASISI wa kanisa moja eneo hili aliwaacha wafuasi vinywa wazi alipomtimua muumini aliyesinzia alipokuwa akihubiri neno la Mungu.

 

“Kalameni aliyehusika anajulikana kwa kupenda anasa za kila aina na hasa ulevi wa kupindukia,” alisema mdokezi. Mkewe kalameni ni mcha Mungu na kiongozi wa kanisa na wazee walisisitiza ni lazima mumewe awe akihudhuria ibada kwa sababu ya cheo cha mkewe.

“Jamaa hangetaka mke wake akose cheo na akaamua kuwa akiandamana naye kanisani,” akaeleza mdokezi. Hata hivyo, jamaa alijipata kwenye kibarua kigumu kwani aliendelea kushiriki burudani vilabuni na kumfanya awe akisinzia kanisani Ibada ikiendelea.

Jamaa alihudhuria tamasha la burudani lililoporomoshwa na msanii marufu eneo hili hadi chee, alisimulia mdokezi.

Na siku iliyofuata walipohudhuria ibada, jamaa alikuwa mchovu na akalala fo fo fo na kuanza kukoroma jambo lililomfanya kasisi kukasirika. Inasemekana pasta alimuendea na kumzaba kofi lililomwamsha kalameni.

“Ikiwa unadhani kanisa ni chumba cha kulala ukichoka na kuhudumia Serrano jua kwamba mimi sivumilii upuzi kama huo,” alichemka mhubiri.

Jambo lililowashangaza waumini ni kwamba kasisi huyo alimtimua kalameni na kumuonya dhidi kukanyaga kanisani akiwa ametoka kuhudumia shetani.

Penyenye zinasema mke wa jamaa na baadhi ya waumini hawakufurahishwa na kitendo cha pasta na wakaondoka kanisani wakiteta.

Walimlaumu pasta kwa kushindwa katika kazi yake ya kuwalea waumini kiroho na kugeukia nguvu za mwili kuwakosoa.

Kikao cha wazee wa kanisa kiliandaliwa na pasta akaonywa vikali kurekebisha tabia au achukuliwe hatua za kinidhamu.

 

 

Atandikwa na sponsa kwa kunyemelea asali

Na SAMMY MURAYA

Imepakiwa - Monday, May 29  2017 at  13:08

Kwa Muhtasari

MABROS, GITHURAI

SINEMA ya bure ilishuhudiwa katika duka moja mtaani hapa kalameni alipoangushiwa mangumi mazito na buda kwa kumpata akitongoza mpango wake wa kando katika biashara aliyomwekea.

 

Yasemekana polo alizoea kumtembelea kimwana huyo katika biashara yake kumrushia mistari ya mapenzi. “Jamaa alikuwa ameonywa na kidosho huyo kwamba alifadhiliwa kuanzisha biashara na sponsa wake, lakini hakusikia la mwadhini wala la mteka maji msikitini,” alisema mdokezi wetu.

Duru ziliarifu meza ya dondoo kwamba siku ya kioja, polo alienda katika duka la mwanadada huyo kumrushia mistari ya mapenzi kama ilivyokuwa kawaida yake. Inasemekana siku hiyo kipusa hakutaka kuongea na jamaa. “Hae, nimekuja, ni muda sijakuona.” kalameni alimueleza mwanadada.

Kulingana na mdokezi, kidosho alikimya na kujaribu kumuepuka jamaa. Muda wa kuku kumeza punje ya mahindi, gari la kifahari lilifika na kuegeshwa karibu na duka hilo na buda aliyeunga akashuka.

“Wewe ndiye nasikia huwa unasumbua mke wangu?” mzee huyo aliuliza. “Ati mke wako? Miaka yako na ya mrembo huyu haiambatani,” kalameni alimjibu kwa dharau.

Kabla ya jamaa kuongeza neno, mangumi na mateke yalimshukia akaramba sakafu. “Ukijitazama kuanzia utosini hadi unyayoni unaweza kutunza mwanamke kama huyo?” aliuliza buda akihema kwa hasira.

“Huwa namkanya aache kuja hapa na humweleza mimi ni mke wa mtu lakini huwa hasikii,” alishtaki kipusa huyo.

Kalameni huyo ambaye alizidiwa na kichapo hakuwa na budi ila kuchukua gari nambari mguu niponye na kutimka kama swara huku waliotazama kioja hicho wakicheka.

 

 

Kidosho mwizi wa penzi plotini afurushwa

Na KIMANI wa NJUGUNA

Imepakiwa - Monday, May 29  2017 at  12:44

Kwa Muhtasari

RUIRU, KIAMBU

KIZAAZAA kilizuka hapa wanawake walipoungana na kumtimua mwanadada mmoja wakimlaumu kwa kuwanyakua wanaume wa wenyewe.

 

Penyenye zinasema haikuwa mara ya kwanza mwanadada huyo kulaumiwa kwa kuwanyemelea wanaume.

“Alikuwa ameolewa lakini kwa sababu ya tabia yake, alifukuzwa na mume wake na akahamia hapa,” alisema mdokezi.

Kulingana na mdokezi huyo, mwanadada huyo amejaliwa umbo na sura nzuri ambayo inadaiwa amekuwa akiitumia kuwachota wanaume wapendao uroda na kuzini nao.

“Mara tu alipohamia hapa na kupangisha nyumba yake ya kuishi, aliendelea na tabia yake ya kupenda maisha ya anasa na kuwatongoza wanaume,” alieleza mdokezi.

Kilichowaudhi wanawake wa hapa ni kuwamezea mate wanaume ambao wameoa.

Siku ya tukio, mwanamume mmoja ambaye ni jirani wa mwanadada huyo alikosa kufika kwake na vile vile, kidosho huyo hakurudi kulala kwake siku hiyo.

Ni kwa sababu hiyo mke wa jirani huyo alishuku kwamba mumewe alikuwa akijivinjari na mwanadada huyo.

Inasemekana kuwa alimshtaki mwanadada huyo kwa majirani akidai alitoweka na mumewe na alipowasili asubuhi, aliwapata majirani hao wakimngojea.

Walivamia kwake wakimlaumu kwa kuwapagawisha kimapenzi waume zao hadi wakasahau familia zao. “Kamwe hatuwezi kukubali uharibu familia zetu kwa ndumba zako tukinyamaza na leo hii utatambua sisi ni nani,” alifoka mwanamke mmoja na kuungwa mkono na wenzake.

Wanawake hao walitisha kumshambulia mwanamke huyo kabla ya kumfurusha kutoka hili. Hata hivyo, mwanamke huyo alidai hakuwa na uhusiano wa kimapenzi na mume wa mtu na kuwalaumu wanawake hao kwa kushindwa kukidhi wanaume wao kimapenzi.

 

 

Kizaazaa kipusa kupata chupi kwa sanduku la polo baada ya harusi

Na SAMMY WAWERU

Imepakiwa - Thursday, May 25  2017 at  20:39

Kwa Muhtasari

MUGOIRI, MURANG'A

KIZAAZAA kilitokea katika boma moja mtaani hapa kipusa alipotisha kumpa jamaa talaka saa chache baada ya kufunga pingu za maisha alipopata chupi ya mwanamke kwenye sanduku la nguo la polo.

 

Kalameni alikuwa amechumbia kidosho kwa kipindi cha miaka mitatu na wawili hao walikuwa miongoni mwa vijana waliokuwa mstari wa mbele kuhudumu kanisani,” akasema mdokezi.

Siku ya kuvishana pete ilikamilika na maharusi hao wakasindikizwa na wasimamizi wao. Boma lao lilijaa furaha tele kwa polo kupata mke.

Yasemekana kulingana na sheria za kanisa lao, ni lazima wasimamizi wa harusi wakeshe kwa polo wakiwatakia heri njema ya kuanza familia.

Ulipofika wakati wa kulala, jamaa na kimwana waliwaaga wageni wao na kuenda katika chumba cha kulala. Kipusa alichakurachakura chumba akitafuta vazi la kuvaa alale.

Aliingia kwenye sanduku la nguo la kalameni na dakika chache baadaye furaha kageuka karaha. “Hiyo miaka yote tuliyochumbiana nimekuwa mwaminifu kwako kumbe wewe umekuwa ukileta wanawake huku?” aliwaka kipusa akionyesha polo chupi ya mwanamke.

“Naapa mbele ya Mungu hakuna mwanamke nimewahi kuleta huku tangu tuanze kuchumbiana,” jombi alijitetea. “Kwa hivyo hii chupi ina miguu ikajiingiza kwenye sanduku lako?” kipusa aliuliza kwa hamaki.

Maji yalizidi unga mwanadada huyo aliposhikilia katu hangelala huko na wageni waliokuwepo wakataka kujua kulikoni kelele zilipochacha.

“Mmenileta kwa mzinifu, hebu tazameni nilichopata kwenye sanduku lake!” kimwana akawaonyesha ile chupi na wakasalia kinywa wazi.

Yasemekana wazazi wa polo kutoka pande zote waliarifiwa na pasta wafike boma hilo usiku kutatua suala hilo.

 

 

Afurusha walevi kwa kumkosesha usingizi

Na JOHN MUSYOKI

Imepakiwa - Thursday, May 25  2017 at  15:42

Kwa Muhtasari

KISANGA kilizuka hapa mama alipovamia kilabu kimoja usiku na kuwatimua walevi akiwalaumu kwa kumkosesha usingizi kwa kelele.

 

Mama huyo alijitoma katika kilabu hicho akibeba rungu na kuwaagiza walevi kuondoka kwenda nyumbani akisema hangevumilia kelele zao.
Inasemekana kuwa mama anaishi karibu na kilabu hicho na kila mara alilalamikia kelele za mapolo walizokuwa wakipiga hasa usiku wa manane. Siku ya kioja mama aliamua kuwafunza adabu. Aliamka usiku na kujitoma kilabuni na kuwaangushia walevi kichapo kikali.

“Mapolo walipigwa na butwaa kuona mama akiwaangushia kichapo bila huruma hali iliyowafanya kutimua mbio na kuacha muhudumu wa kilabu hicho akikabiliana na mama huyo,” alisema mdokezi.

Penyenye zaeleza kuwa mama alipata kuwa hata mhudumu wa kilabu hicho alikuwa mlevi kupindukia. Baada ya walevi kutoroka, mama alimkemea mhudumu huyo na kumpa kichapo kikali na kumuacha na maumivu.

“Utakuwa ukifunga kilabu mapema. Hakuna haja ya kupigia watu kelele kiasi hiki hadi wanashindwa kupata usingizi. Kutoka leo ambia wateja wako wapunguze kelele na usipofanya hivyo nitawachukulia hatua kali,” mama alifokea mhudumu wa kilabu. Inasemekana mama huyo aliamuru mhudumu huyo kufunga kilabu mara moja na kuondoka.

“Jombi alifanya alivyoambiwa huku akisimamiwa na mama huyo. Baada ya kilabu kufungwa, mama alirudi kwake na kulala. Kuanzia siku hiyo kelele zilikoma kwa sababu wateja hawakuruhisiwa katika kilabu hicho baada ya saa tatu usiku,” alisema mdokezi.

Mama alisema alichotaka ni haki yake ya kupata usingizi.

 

 

Aonja kofi la mkewe kwa kuzubaia kidosho

Na CECIL ODONGO

Imepakiwa - Wednesday, May 24  2017 at  15:28

Kwa Muhtasari

MUTINDWA, NAIROBI

KULITOKEA kisanga kwenye steji ya kuabiri matatu eneo hili jombi alipopigwa kofi kali na mkewe kwa kuwakodolea macho vipusa.

 

Siku ya kisanga, polo na mkewe walikuwa kituoni kuabiri gari mrembo moja mwenye sura ya kupendeza alipotokea.

Polo alimkodolea macho mwanadada huyo na akamsahau mkewe aliyekuwa akizungumza naye kwa kuwa akili yake yote ilimgandia kipusa yule.

Inasemekana mkewe alikasirika na kumwangushia kofi kali iliyomgutusha huku akimkemea vikali.

“Saa hii tunapanga mambo yetu na wewe hapa umepagawishwa na msichana. Kama sikutoshi niambie nijisort hata mimi,” mama aliwaka.

Jombi alijaribu kujitetea lakini mkewe alizidi kumkemekea hadi walipoingia kwenye gari na kuacha waliokuwa stejini wakicheka.

 

 

Kalameni ashambuliwa na kisura kwa kununulia rafiki keki

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Wednesday, May 24  2017 at  15:20

Kwa Muhtasari

KENYATTA UNIVERSITY, NAIROBI

KIOJA kilizuka katika chuo hiki baada ya polo kushambuliwa na mrembo kwa kumnunulia rafiki yake keki siku yake ya kuzaliwa.

 

Inasemekana wawili hawa ambao ni wapenzi, walikutana kwa rafiki yao mmoja aliyekuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa iliyokuwa ikifanyika chuoni humu.

Kulingana na mdokezi, mrembo alishangazwa na zawadi aliyokuwa amenunua polo. Inasemekana polo alikuwa amenunua keki ya kifahari sana. Kwa upande wake, mrembo alikuwa amekuja mikono mikavu.

Duru zinasema baada ya kuitazama keki hiyo kwa muda, mrembo aliamua kumuuliza polo iwapo ni yeye alikuwa ameinunua.

Inadaiwa kuwa polo alimueleza mpenzi wake kuwa aliamua kumnunulia keki kama rafiki yake wa karibu. “Wewe unajua tu vizuri huyu demu hana mchumba wa kugharimia bethdei yake. Aliniomba nimsaidie,” polo alisema.

“Babe, juzi nilikiwa na bethdei, ulininunulia zawadi ya aina gani? Mbona pia hukuninunulia keki kama hii? Ungejua vile siku hiyo niliaibika,” mrembo alianza kumkaripia polo.

Inasemekana mrembo alianza kumhesabia polo makosa aliyomfanyia tangu waanze kuchumbiana. “Hakuna haja ya kuleta fujo hapa. Acha tupange siku nije tusuluhishe mambo,” polo alimrai mrembo.

Hata hivyo kipusa alimuonya polo dhidi ya kukanyaga kwake. “Ndio nimegundua sasa hunipendi. Kwangu usikanyage hata kidogo. Mapenzi yetu acha yaishe leo. Endelea kumpenda huyu kwanza,” kipusa alimueleza polo huku akiondoka karamuni.

Polo alijaribu kumzuia mrembo asiondoke lakini akamchapa kofi. “Huyu demu ni mimi nilikutambulisha kwake. Iweje leo unadai kumpenda kuliko mimi? Endeleeni na yeye,” mrembo alidai huku akiondoka.

 

 

Jombi aacha mlo hotelini kuhepa mke na mwanawe

Na LAWRENCE ONGARO

Imepakiwa - Wednesday, May 24  2017 at  12:28

Kwa Muhtasari

Murera, RUIRU

JOMBI aliwaacha wateja katika hoteli moja eneo hili wakiangua kicheko alipoacha chakula alichoagiza na kutoroka baada ya kumuona mkewe na mtoto.

 

Inasemekana jombi alikuwa amemwambia mkewe hakuwa na pesa za kununua chakula.

Lakini ilibainika jombi alikuwa akipitia hotelini kula kabla ya kufululiza hadi kazini huku familia ikiwa na njaa nyumbani.

Majirani wake walimwarifu mkewe kuhusu tabia hiyo ambayo ilimkata maini mama watoto. Bila kupoteza muda alifululiza moja kwa moja hadi hotelini alikokuwa mumewe na kwa kweli buda alinaswa peupe akitafuna nyama na ugali.

Jamaa alipomuona mkewe alichomokea mlango wa nyuma na kutoroka.

Wateja waliokuwa hapo walishangaa mkewe alipowasimulia masaibu aliyokuwa akipitia huku mkewe akitafuna vinono hotelini.

 

 

Jombi atandikwa kofi na mke kwa kumwaga mtama

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Wednesday, May 24  2017 at  12:24

Kwa Muhtasari

Masinga, MACHAKOS

KIOJA kilizuka eneo hili baada ya polo kuzabwa kofi kali na mkewe akimlaumu kwa kuwafichulia ndugu zake tabia zake.

 

Kulingana na mdokezi, ndoa ya wawili hawa ilikuwa na msukosuko mwingi sana kwani kila wakati walikuwa wakigombana.

Inadaiwa ugomvi wao ulitokana na madai kwamba kipusa alikuwa na macho ya nje. Duru zinasema polo alikuwa akipata habari kutoka kwa majirani jinsi wanaume walipokuwa wakiingia kwake akiwa kazini.

Inasemekana polo alijaribu kumuuliza kipusa iwapo madai ya majirani yalikuwa ya kweli. “Achana na hizo porojo za watu. Lakini kumbuka pia mwanamke anahitaji kutunzwa,” kipusa alimueleza polo.

Duru zinasema jibu la mwanadada lilimchoma polo rohoni. “Sasa unasema mimi sikutunzi vizuri?” polo alimuuliza kipusa. 

Inasemekana polo aliwaita ndugu za kipusa. “Nimewaita kwenye kikao hiki ili niwaeleze tabia ya dada yenu,” aliwaeleza mashemeji zake.

Kulingana na mdokezi, polo aliwaeleza mashemeji zake yote kumhusu dada yao mbele ya mkewe mwenyewe.

Penyenye zinasema baada ya polo kutoa kauli zake, mkewe alisimama na kuelekea alikokuwa polo. 

“Huyu mtu anadai eti mimi nina mipango ya kando, umewahi nipata na mmoja? Mbona unaniaibisha hivyo? mama alimkaripia polo.

Duru zinasema kabla ya polo kujibu swali, kipusa alimzaba kofi moja kali sana lililomuacha akibabaika. “Wuuui. Ameniumiza,” polo alilia.

Inasemekana kipusa alikula kona huku akiwaacha ndugu zake wakimpa polo huduma ya kwanza. 

“Na akipona mwambieni ujinga ndio mimi sipendi. Yeye hata kunitunza hawezi. Halafu ananiaibisha hadharani eti mimi namcheza. Hata yeye acha apate aibu kidogo,” kipusa alisema huku akienda zake.

 

 

Jombi auza bidhaa za nyumba na ploti ili aponde raha

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Monday, May 22  2017 at  18:23

Kwa Muhtasari

AKIRIAMET, TESO

KALAMENI mmoja kutoka eneo hili aliwashangaza wengi alipouza ploti ili apate hela za kuponda raha.

 

Inasemekana polo alipenda sana maisha ya anasa na kila wakati akipata pesa alishinda baa akilewa na vidosho na kula nyama choma.

Duru zinasema baada ya kuuza kila kitu kwa nyumba, polo aliamua kuuza ploti.Inasemekana aliamua kuzungumza na mama pima ili waweke mkataba.

Inadaiwa polo alimueleza mwenye baa amruhusu awe akinywa kiwango fulani cha pombe pamoja na kula kilo moja ya nyama choma kila siku.

Kulingana na mdokezi, mkataba huo ulikuwa uchukue mwaka mmoja ambapo inakisiwa kuwa pesa ambazo polo alikuwa ametumia zilitoshana na bei ya ploti yake.

Inasemekana mwenye baa alikubaliana na polo na wakaweka sahihi kwenye mkataba. Penyenye zinasema habari hizi ziliwaacha wengi midomo wazi.

“Mtu anawezaje kupeana ploti kwa sababu ya nyama na pombe jamani! Huku ni kurogwa,” mtu mmoja alisikika akishangaa.

Hata hivyo jamaa hakujali akisema ploti ni yake na alifanya uamuzi peke yake.

 

 

Aliyepoteza mchujoni pia apoteza msupa

Na NICHOLAS CHERUIYOT

Imepakiwa - Monday, May 22  2017 at  18:18

Kwa Muhtasari

KERICHO MJINI

MASAIBU ya polo aliyepoteza katika kura za mchujo hivi karibuni yalizidi kuongezeka kisura mpenzi wake wa kando alipomtema.

 

Inasemekana kuwa jamaa alikuwa akiishi mji huu na demu huyo licha ya kuwa ana mke na watoto ushago.

Kipusa alikuwa akipewa raha ya kipekee na polo hadi juzi alipofilisishwa na kampeni.

“Demu alivumilia wakati wa kampeni akiamini polo akishinda maisha yatakuwa shwari. Mambo yalienda kombo polo alipobwagwa kwenye mchujo.

Demu alimwamuru asimtembelee tena. Alimwambia akikanyaga kwake angekiona cha mtema kuni,” mdaku akaeleza.

Polo alitamauka zaidi na kuelekea kwa mkewe mikono mitupu.

 

 

Mama amshtaki polo kwa kumnyima asali

Na LEAH MAKENA

Imepakiwa - Monday, May 22  2017 at  18:05

Kwa Muhtasari

Soko Mjinga, THARAKA NITHI

MAMA wa hapa alishangaza wanakijiji kwa kumshtaki mumewe kwa wazee wa jamii akidai alikataa tendo la ndoa alipofika nyumbani baada ya kuwa mbali naye kwa zaidi ya miezi mitatu.

 

Kulingana na mdokezi, jamaa huyo alikuwa akifanya biashara zake maeneo mbali mbali na juzi alifika nyumbani kutembelea familia yake.

Duru zasema kuwa jombi alipata udaku kwamba jirani alikuwa akimnyemelea mkewe.

“Haikuchukua muda mrefu kwani jamaa alidokezewa yaliyokuwa yakijiri nyumbani na akaapa kumpa mama ‘adhabu’,” alisema mdokezi.

Inasemekana kuwa polo alipowasili nyumbani, alipunguza mazungumzo na mkewe na hakushughulika na tendo la ndoa. Mkewe alishuku mumewe alikuwa amebaini mienendo yake ya kula fuska na jirani na akabuni mbinu za kujitakasa.

Hapo ndipo alipofika mbele ya baraza la wazee na kuangua kilio akidai mumewe alimtesa kwa kuikataa asali yak.
Juhudi za wazee hao za kuwaunganisha ziliambulia patupu kwani polo aliapa kutolala na mke wake tena akisema hakutaka kuambukizwa maradhi.

Alisema alikuwa na habari mkewe alikuwa akishiriki mipango ya kando na jirani.

Yasemekana kuwa baada ya wiki moja, jamaa alirejea mjini na kumuacha mkewe mashakani kwani hakujali kutafuta jawabu la tatizo hilo. Minong’ono yasema kuwa mama aliamua kurejea kwao bila kufurushwa akisema mumewe alikosa kumtimizia haja zake.

“Mama alisingizia kuwa mumewe alikuwa hajali hisia zake japo wakazi walifahamu ukweli. Walimlaumu mama huyo kwa kumsaliti mumewe ambaye ana bidii ya kufanya kazi ili familia yake isiteseke,” alisema mdokezi.

Hakuna aliyejua iwapo polo alijipatia mke mwengine au la.

 

 

Kioja wasanii wawili kupigania steji ya magari

Na CORNELIUS MUTISYA

Imepakiwa - Sunday, May 21  2017 at  14:02

Kwa Muhtasari

MACHAKOS MJINI

WAKAZI wa mji huu juzi waliwaonya wasanii wawili walio na mazoea ya kuzozania sehemu ya kituo cha magari wanayotumia kuwatumbuiza mashabiki.

 

Kulingana na mdokezi, msanii mmoja ambaye kwa kawaida huwa anatumbuiza wananchi katika steji ya magari mjini hapa alikosa kufika kwa wakati na msanii mwingine alipofika alianza kutumbuiza hadhira.

Penyenye zaarifu kuwa, ilipotimu saa tano hivi za asubuhi, msanii wa pili alifika katika uwanja huo akiandamana na kikosi chake na akapata uwanja umechukuliwa na msanii mwingine.

Alipandwa na hasira za mkizi na kuanza kumtusi mwenzake huku akimlaumu kwa kuingilia himaya yake ya kutumbuiza mashabiki na kuuza kanda zake.

“Nimekuwa nikitumbuiza wananchi kwa miaka mingi hapa. Mbona sasa umeanza kuniingilia?’’ alilalamika msanii huyo.

Inasemekana kwamba, msanii wa kwanza alianza kujitetea akisema kwamba hakuwa na nia mbaya kwa kuhubiria injili katika uwanja huo maana hata naye alikuwa na haki ya kufanya hivyo kwa sababu alikuwa amelipa ada inayostahili.

Hapo ndipo msanii wa pili alipomparamia mwenzake mithili ya simba marara na kumkwaruza kwa kucha zake usoni kabla ya wakazi kuingilia kati ya kuwatenganisha kisha wakawaonya wakome kuzozania uwanja kila mara.

 

 

Kipusa adai malipo kwa kuishi na jombi

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Sunday, May 21  2017 at  13:56

Kwa Muhtasari

SIRISIA, BUNGOMA

WENYEJI wa eneo hili walibahatika kutazama sinema ya bure kipusa alipomlazimisha polo kumlipa fidia kwa muda aliokaa naye.

 

Inasemekana kipusa alikasirishwa na hatua ya polo ya kumuoa mke wa pili licha ya kukaa naye kwa miaka mingi.

“Nimevumilia kukaa na wewe miaka hiyo yote kwa taabu nyingi na mambo yanapoanza kuwa mazuri, unaamua kuoa mke mwingine. Wewe ni mwanamume wa aina gani? Ukora ndio mimi sipendi,” kipusa alimkaripia polo.

Penyenye zinasema polo alikuwa amepanga kuoa mke wa pili kwa siri.

Wakati haya yote yakifanyika, duru zinaarifu polo alikuwa ametulia tu bila wasiwasi wowote. “Mimi ninarudi kwetu. Tulipooana haukuwa hivi. Nimekulisha na kukulinda kama mtoto mdogo. Watoto wawili nimekuzalia. Lazima unilipe muda huo wote nimeishi na wewe,” kipusa alimueleza polo.

Inadaiwa kuwa polo aliposikia neno kulipa, alipigwa na butaa. “Eti nikulipe nini? Nani amekufuza hapa?” alimuuliza kipusa.

Inasemekana kipusa alianza kumhesabia polo mambo yote aliyomfanyia na kudai malipo.

Inadaiwa kipusa alianza kuvipanga vitu vyote alivyodai alivinunua. “Acha nikwambie hii nyumba tulipooana ilikuwa na godoro peke yake. Hivi vyote ni mimi nilinunua kwa jasho langu. Naenda navyo,” kipusa alimueleza polo.

Duru zinasema polo alianza kujitetea lakini maji yalikuwa yameshamwagika. “Kabla sijaondoka hapa, lazima utoe fidia ya miaka yote nimeishi nawe,” kipusa alimshurutisha jamaa.

Kulingana na mdokezi, majirani wa polo walibaki kutazama tu sinema kwa mbali.Inasemekana kipusa alimpa polo muda wa saa tatu awe ametoa hela alizohitaji kama fidia.

 

 

Akataa mlo baada ya kusikia jirani 'aliokoa jahazi' kwake

Na LAWRENCE ONGARO

Imepakiwa - Thursday, May 18  2017 at  18:20

Kwa Muhtasari

KALAMENI aliyekataa kumpatia mkewe pesa za kununua chakula alikasirika kusikia ya kwamba mwanamume jirani yake aliokoa jahazi.

 

Penyenye zasema kwamba jamaa alimnyima mkewe pesa za kununua chakula akisema alikuwa amesota na hakutaka kusumbuliwa.

Hata hivyo, kalameni jirani aliyezoea kuwasiliana na mkewe, alisikia wawili hao wakizozana kuhusu pesa.

Inasemekana kuwa jamaa aliporejea kutoka kazini jioni alipata ametayarisha ugali na nyama na akashangaa alikotoa pesa. Bila kumficha alimwarifu wazi kuwa ni jirani yao aliyeokoa jahazi kwa kumpatia Sh500 akanunua chakula.

Majibu hayo yalimkasirisha jamaa aliyekataa kula chakula hicho kisha akaondoka kujiunga na marafiki zake kutazama mechi ya soka katika baa iliyo karibu na kwake hadi usiku wa manane.

 

 

Polo achemka kisura kumrushia mistari

Na SAMMY WAWERU

Imepakiwa - Thursday, May 18  2017 at  18:04

Kwa Muhtasari

KIAMBU ROAD, KIAMBU

SINEMA ya bure ilishuhudiwa kwenye basi linalohudumu barabara hii kalameni alipozusha akiteta kuwa kimwana aliyeketi kando yake alikuwa akimkatia ilhali ana mke.

 

Yasemekana jamaa aliabiri matatu hiyo jijini Nairobi kuelekea Kiambu naye kidosho aliingia baadaye kidogo na kuketi kando yake.

Duru zaarifu kwamba gari hilo lilipojaa na kuanza safari, mwanadada alivunja kimya kwa kumsalimia jamaa, “Umeshindaje baba? Umevalia nadhifu kweli,” kidosho alianza.

“Nimeshinda salama nashukuru,” mzee alijibu. Kulingana na mdokezi, mwanadada huyo aliendelea kuongea huku kalameni akionekana kutotaka mazungumzo.

“Inaonekana una mke anayekujali mzee. Hata hivyo, nikipata fursa ya kuolewa nitamjali mume wangu ili asiwe na mpango wa kando. Hata wewe naweza kukufanyia makuu na matamu,” kipusa alimweleza jamaa akimgusa mikono.

“Hei, kwani hili gari huwa mnabeba abiria wa aina gani wasiowapa abiria wengine amani?” jamaa alifoka.

“Huyu mwanamke amekuwa akinizungumzia tangu nilipoingia na anaonekana kuwa na mambo mengine, hajui mimi nina mke na watoto?” aliwaka kila mmoja akionekana kushangazwa na tukio hilo.

Inasemekana jamaa alichemka akisema kuwa yeye ni mzee wa kanisa aliyeheshimika kanisani na kijijini. “Mimi nina heshima zangu si tu kijijini bali pia kanisani.

Wewe mwanadada unanichukulia vipi ukisema niwe mpango wako wa kando?” kalameni alipaza sauti. Mwanadada huyo aliaibika kiasi kwamba alilazimika kushuka.

“Kweli kuna watu wasio na adabu, yaani amekosa mume aanze kunyemelea waume wa wengine?” aliuliza mama mmoja na kusababisha abiria wote kuangua kicheko.

 

 

Ashindwa ampe mke yupi zawadi aliyopewa na rafikiye

Na DENNIS SINYO

Imepakiwa - Wednesday, May 17  2017 at  13:20

Kwa Muhtasari

Mosoriot, NANDI

MZEE mwenye wake wawili alitokwa na kijasho aliposhindwa ni mke yupi wa kumpa zawadi aliyotunukiwa na rafiki yake.

 

Jamaa huyo alikuwa ameandamana na wake wawili kwenye sherehe aliyoalikwa na rafiki yake wa dhati.

Kulingana na mdokezi, wake hao walikuwa wakigombana mara kwa mara wakiwa nyumbani. Walipowasili kwenye sherehe hiyo, waliketi karibu na mumewe licha ya uhasama wao wa muda mrefu.

Kabla ya kutamatisha sherehe, mwenyeji wao alianza kuwatuza wageni wake aliodai walikuwa wamesimama naye kwa miaka mingi.

“Jamaa aliitwa kupatiwa blanketi kama zawadi. Mke wake wa kwanza alimfuata kwenye jukwaa naye mke wa pili akaingiwa na wivu na kumfuata pia. Alipopewa zawadi yake, jamaa huyo alishindwa ni mke yupi wa kumpa kwani wote wawili walikuwa wamesimama na yeye pamoja,” alisema mdokezi.

Inaarifiwa wanawake hao walikuwa wamenyoosha mikono kupokea zawadi hiyo ila jamaa akahisi kwamba angesababisha balaa kama angempa mmoja na kumwacha mwingine.

Wageni waliokuwa wameketi walitazama kioja hicho kwa muda kabla ya mwanaume huyo kuamua kushikilia zawadi hiyo mwenyewe mkononi hadi alipotoka kwenye jukwaa.

 

 

Mzee wa kanisa ajuta kuonja tunda haramu

Na LEAH MAKENA

Imepakiwa - Wednesday, May 17  2017 at  13:12

Kwa Muhtasari

MACHAKOS MJINI

POLO wa hapa alipata aibu ya mwaka pale ilipobainika kuwa alivamiwa na kuadhibiwa baada ya kumfumaniwa akichovya asali kutoka mzinga wa mwanamume mwingine na wala hakuwa amepata ajali jinsi alivyodai.

 

Duru zasema kuwa jamaa huyo alikuwa mzee wa kanisa japo alikuwa akiwamezea mate akina dada licha ya kuwa na mke na watoto sita.

Inasemekana kuwa jamaa alianza kunyemelea mama mmoja kanisani ambaye mumewe alikuwa akifanya kazi mbali na nyumbani.

Minong’ono yasema kuwa wawili hao walianza kurushana roho kwenye lojing’i na baada ya muda mama alianza kumualika kwake nyumbani.

Kulingana na penyenye za mtaa, jirani mmoja alimpigia simu mume wa mwanamke huyo kumuarifu jinsi mkewe alivyokuwa akigawa asali. Hapo ndipo jamaa alipanga safari ya ghafla na kufika kwake usiku wa manane.

Yasemekana kuwa vuta nikuvute ilishuhudiwa pale mama alipodinda kufungua mlango. Hata hivyo, kwa kuhofia kuvutia umati, jamaa aliufungua na kuanza kumenyana na mwenye boma.

“Wawili hao walimenyana nusura mla vya watu auawe baada ya kukabwa koo lakini alinusurika na kuponyoka akiwa na majeraha mabaya yaliyomlazimu kulazwa hospitali kwa muda,” alisema mdokezi.

Polo alikuwa akihadaa washiriki waliofika hospitalini kumjulia hali kwa mara ya kwanza kuwa alivamiwa na wakora. Hata hivyo, mambo yalianikwa wazi mume wa mama huyo alipowaelezea washiriki jinsi alivyompata jamaa huyo akila uroda na mkewe katika kitanda chao cha ndoa.

Inasemekana baada ya kupona, jamaa hakukanyaga kanisani huku mke aliyezini naye akiamua kurudi kwa wazazi wake katika kaunti jirani.

 

 

Buda achemka kufumania mkewe kilabuni na mapolo

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Tuesday, April 11  2017 at  15:16

Kwa Muhtasari

ZIMMERMAN, NAIROBI.

KIZAAZAA kilizuka hapa polo alipomzaba mkewe makofi makali baada ya kumpata ndani ya kilabu akiketi kati kati ya makalameni akitazama mpira. Inasemekana mkewe alikuwa amekamata chupa ya pombe mkononi.

 

Kulingana na mdokezi, polo alikuwa akirejea nyumbani kutoka kazini aliposikia kelele zisizo za kawaida kilabuni na akaamua kuingia ndani kushuhudia kilichokuwa kikiendelea.

Kulingana na mdokezi, polo alipotupa jicho katikati ya makalameni, hakuamini macho yake alipomuona mkewe akiwa katikati ya makalameni watano.

Penyenye zinasema kipusa alikuwa na furaha nyingi sana kuwa katikati ya makalameni wale. Kulingana na mdokezi, timu aliyoshabikia kipusa ilifunga bao.

Kipusa aliruka juu huku mkononi akishikilia chupa ya pombe. Inasemekana polo alienda moja kwa moja na kumuinua kipusa juu. “Nani kakuleta hapa?” polo alimuuliza kipusa huku akimkodolea macho.

Duru zinasema kipusa alibaki mdomo wazi. “Unafanya nini hapa?” polo alizidi kumuuliza kipusa ambaye hakujibu maswali ya polo.

Inasemekana kipusa aliachilia chupa ya pombe na ikaanguka chini huku jamaa akimzaba kipusa makofi.

“Tafadhali usinichape tena. Ni mara yangu ya kwanza kuja huku,” kipusa alimrai polo. Inasemekana polo aliendelea kumzaba kipusa makofi.

“Huna aibu hata kidogo. Juzi uliniambia uliacha ulevi, hiyo chupa ilikuwa na sharubati ama maji ndani?” polo alimuuliza kipusa huku hasira zikizidi kumpanda.

Penyenye zinasema kila wakati jamaa akienda kazini, mkewe alikuwa akishika njia kuwatafuta marafiki zake.

“Leo hana bahati. Acha apewe adabu. Mwanamke mzima kila wakati kufuatana na wanaume!” sauti ya jamaa mmoja ilisikika ikisema.

 

 

Landilodi mashakani kwa kutupa chambo plotini

Na JOHN MUSYOKI

Imepakiwa - Wednesday, March 15  2017 at  13:32

Kwa Muhtasari

NGETANI, Masinga

KIOJA kilitokea sehemu hii landilodi alipokabiliwa vikali na wapangaji na mkewe kwa tabia ya kunyemelea wake wa watu plotini.

 

Siku ya kioja, landilodi alipatikana katika chumba cha mwanamke mmoja mpangaji akimrushia mistari ya mapenzi. Hata hivyo, juhudi zake ziliambulia patupu mkewe alipofika kwenye ploti huku akibeba upanga na kufoka kwa ukali.
“Unafanya nini katika nyumba ya mwanamke.

Umekuwa kahaba? Leo umepatikana na lazima nikupe funzo,” mke wa jamaa alifoka na kuingia chumbani.
Wakati huo jamaa alijawa na hofu tele na kuanza kutetemeka ungedhani alikuwa ameugua maradhi ya kifafa.

Inasemekana mkewe alianza kuwakemea vikali. “Wewe ni mwanamke sampuli gani unamchukua mume wangu na kumfanya mumeo.

Nitawaonyesha kilichomtoa kanga manyoya,” mama alianza kumpokeza mwanamke kichapo huku jamaa akipata nafasi ya kuhepa.

Jamaa alipotoka nje, alipata mlango wa ploti ukiwa umefungwa kwa kufuli kubwa na baadhi ya wapangaji wakiwa wameshika fimbo nzito tayari kumkabili mwizi wa mapenzi.

Penyenye zinasema kati ya wapangaji hao alikuwemo mume wa mwanamke aliyekuwa alipokezwa kichapo chumbani.
Kwa hasira walimrukia na kuanza kumtandika jamaa kisanga ambacho kilivutia watu wengi akiwepo pasta.

Vita hivyo, vilizimwa baada ya Mtu wa Mungu kuingililia kati na kuwatenganisha. “Acheni kupigana nina ujumbe kwenu,” pasta alisema.

Ni katika hali hiyo pasta alipowahubiria na kuwaomba kudumisha amani. Hata hivyo, landilodi alipiga magoti mbele ya mtumishi wa Mungu huku akikiri makosa yake. Baadaye pasta aliwaombea wote na kuwaambia uzinifu ni dhambi.

 

 

DONDOO: Kimada na mama boi wapapurana hadharani

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Thursday, March 2  2017 at  15:08

Kwa Muhtasari

OL KALOU, Laikipia

KIZAAZAA kilizuka eneo hili baada ya kidosho kumvamia mke wa polo akimlaumu kwa kumzuia mumewe kumuoa mke wa pili.

 

Kulingana na mdokezi, kidosho alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na polo. Inasemekana polo alikuwa amemuahidi kidosho kuwa atamuoa awe mke wake wa pili.

Duru zinasema kidosho alipoona kuwa polo alikawia sana kutekeleza ahadi yake ya kumuoa, aliamua kumkumbusha. “Nakumbuka ulikuwa umeniahidi kuwa mwezi huu tutaishi pamoja. Ninapokuona ni kama huna dalili zozote,” kidosho alisema.

Inasemekana kuwa polo alimueleza jinsi alivyozomewa na mke wake nyumbani. “Mimi hata sijui ni nani alimuambia mama boi eti napanga kukuoa. Amenizomea sana,” polo alimueleza kidosho.

Kulingana na mdokezi, polo alimueleza kidosho awe na subira hadi mkewe atakapotulia. “Kwani huyo mwanamke ndiye hukuamlia cha kufanya?” kidosho alimuuliza polo kwa hasira.

Inasemekana kidosho alielekea hadi kwa boma la polo na kuanza kumshambulia mkewe kwa maneno. “Wewe una shida gani? Kama humlindi bwana wako vizuri acha kumpa masharti,” kidosho alimuonya mke wa jamaa.

Duru zinasema mama alimuonya kidosho aachane na mumewe kabisa. “Acha ujinga. Nani alikuambia simlindi vizuri bwanangu? Porojo sitaki. Kwenda huko. Sikutaki katika hili boma,” alimzomea kidosho.

Kulingana na mdokezi, wawili hao walianza kurushiana matusi huku majirani wakibaki kutazama sinema ya bure. “Upende usipende lazima nitaolewa katika hili boma. Huna uwezo wa kumzuia mumeo kuoa,” kidosho alifoka.

Habari zilizotufikia zinasema karibu wawili hao wakabane koo. “Sitaki usaidizi wowote kutoka kwako,” mama alimuonya kidosho.

 

 

Jombi na mkewe wagongana kilabuni kila mmoja akiwa na mpango wa kando

Na MAGDALENE WANJA

Imepakiwa - Monday, October 10  2016 at  12:44

Kwa Muhtasari

FREE AREA, Nakuru

Kizaazaa kilizuka katika baa moja eneo hii baada ya jamaa na mkewe kukutana kila mmoja akiwa na mpango wa kando.

 

Kulidaiwa kua kuwa jamaa alimuaga mkewe na wanawe akisema anakwenda seminari ya kiikazi siku tatu na alimpigia mkewe simu jioni hio akidai alifika salama.

Hakufahamu kuwa jombi hakuwa amesafiri popote bali alikuwa amekodisha chumba katika baa moja hapa mjini alikoishi na mpenzi wake wa zamani.

Jamaa alikua akimpigia mkewe simu kumjulia hali ,na alipogundua mkewe alikuwa ameingia boksi, aliamua kumpeleka mpenzi wake matembezi ya jioni na  baadaye wakarudi ndani ya baa na kuagiza mvinyo.

Kulingana na mdokezi, mkewe naye alimpigia simu mpenzi wake wa zamani wakutane wajiburudishe akilini akijua mumewe hayuko karibu.Baada ya kutaniana kwa muda, wawili hao walikubaliana wakutane katika baa ambayo jombi na kimada wake walikuwa wakijivinjari.

Haikuchukua muda kabla mama huyo kufika pale na kuelekea ndani ya baa walimokuwa mumewe na mpango wake wa kando na kuagiza vinywaji.

Walipokuwa wakinywa na kupiga gumzo macho ya mama huyo yalikutana ana kwa ana na mumewe na akalipuka kwa hasira.

“Hapa ndio seminari?’’ mama alianza kufoka huku akipandWa na hasira “Na huyu ni nani?” mumewe naye akamuuliza mkewe.

Badala ya kupeana majibu mke alimrukia mpango wa kando wa mumewe naye mumewe akamurukia kalameni aliyekuwa na mkewe.

Wahudumu wa baa walilazimika kuingilia kati kabla purukushani hiyo kusababisha hasara katika baa hiyo.Penyenye zinasema huo ndio ulikuwa mwisho wa ndoa ya jamaa na mkewe.

 

 

Polo watwangana kwa sababu ya githeri

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Monday, September 26  2016 at  06:58

Kwa Muhtasari

Makalameni waliokuwa kazini hapa Zimmerman waliwashangaza wapita njia baada ya kupiganana wakizozania githeri.

 

ZIMMERMAN, Nairobi

MAKALAMENI waliokuwa kazini hapa waliwashangaza wapita njia baada ya kupiganana wakizozania githeri.

Makalameni hao ambao ni waashi waliokuwa wakijenga ghorofa moja mtaani humu, walianza kutwangana makonde baadhi walipowamalizia wenzao githeri.

Inasemekana kuwa baadhi ya makalameni walikasirishwa na hatua ya mapolo wenzao kutangulia kwa siri kwa mama mmoja aliyekuwa akiwaandalia chakula na wakala kila kitu.

Duru zinaarifu kuwa mapolo waligundua chakula kilikuwa kimemalizwa na wenzao baada ya kufika kwa mama huyo huku njaa ikiwakeketa.

“Wenzenu wamekuwa hapa wakala kila kitu. Waliniambia kwamba nyinyi leo hampo kazi,” mama aliwaambia mapolo.

Mapolo hao walishangaa jinsi wenzao walivyotoroka kwenda kula bila kuwaarifu.

“Hawa jamaa kwani walikuwa na njama gani? Wanawezaje kutumalizia chakula? Leo watakiona,” polo mmoja aliapa huku akiwaeleza wenzake waende kuwatafuta makalameni.

“Nyinyi mnaezaje kula githeri yote?” polo alimuuliza mwenzake kwa hasira.

Inasemekana kuwa yule jamaa aliyeulizwa alianza kucheka tu. “Sasa unacheka na nani?” polo alimuuliza mwenzake huku akimpa kofi.
Inasemekana wawili hao walianza kutwangana huku wale waliotangulia kula wakimsaidia mwenzao.

Kulingana na mdokezi, makalameni waliokuwa na njaa pia walijiunga na mwenzao kuwapa wenye shibe adabu.

Ujenzi wasitishwa

Duru zinaarifu kuwa shughuli za ujenzi zilisitishwa kwa muda.

“Ukora sisi hatutaki. Ulafi mtaacha,” makalameni waliokosa githeri waliwaeleza wenzao huku wakiwalemea kwa nguvu.

Habari zilizotufikia zinasema iliwabidi wapita njia waingilie kati ili kusuluhisha mgogoro baina ya mapolo.

“Sisi tuliona wamechelewa sana. Tukaamua kwenda kula,” mapolo walianza kujitetea.

Kulingana na mdokezi, ujira wa mapolo wa siku hiyo ulipunguzwa kama njia moja ya kuwapa wote adabu.

Dondoo za Hapa na Pale ni visa vinavyojiri kila siku sehemu tofauti nchini na kimataifa. Tuma habari kwa:dondoo@ke.nationmedia.com / taifa@ke.nationmedia.com au swahilihub@ke.nationmedia.com

 

 

Jombi amtoroka 'mpango wa kando' ndotoni uchi

Na TONY NYONGESI

Imepakiwa - Sunday, September 4  2016 at  18:37

Kwa Muhtasari

KANGEMI, Nairobi

WAKAZI wa hapa walishabikia kisa cha kushangaza jombi alipochomoka nyumbani uchi wa mnyama akiwa kwenye ndoto akidai alikuwa akikimbizwa na mpango wa kando.

 

Jamaa ambaye huchapa vinywaji wikendi  aliamua kulala mapema ili kuepuka kuchelewa kazini kumbe alikuwa akialika mkosi uliomweka mashakani.

Ilipotimia saa tatu usiku, jombi ambaye kawaida  hulala bila mavazi aliangua kilio usingizini akitaja jina la mpango wa kando.

“Wewe  unanihangaisha kwa nini na nilikuwa nimekulipa? Mbona wataka kunikatakata Jessi na nimegharamia kila kitu?” alilia jombi kwa sauti ya juu akiwa usingizini.

Mkewe na wanawe waliokuwa wakiandaa chakula cha jioni, waliingiwa na wasi wasi na  ghafla bin vuu, jombi alichomoka kwenye chumba cha kulala na kutoka nje mbio akiangua kilio na kumtaka Jessi amwachilie.

“Wewe Jessi, ukiendelea hivi sitarudi hapa tena,” jombi alipiga kelele huku akitembea nje ya ploti. Ajabu ni kwamba wakati huu wote, kalameni alikuwa amevalia chupi bila shati wala kaptula ya kulala.

Kilio cha mkewe kilifuata  huku akitaka kumjua Jessi alikuwa nani.

Inasemekana kuwa mama alizuiwa kumhangaisha mumewe kwani alielezwa na baadhi ya watu kwamba si vyema kumsumbua mtu akitembea akiwa usingizini kwa sababu anaweza kunyakuliwa na mashetani.

Kulingana na mdokezi wetu, mzee alizunguka nje ya ploti na ajabu ya Musa, alirudi nyumbani na kujilaza kitandani huku akiendelea kukoroma.

Dakika chache baadaye aliamushwa na mkewe akitaka kujua Jessi alikuwa nani.

“Leo nimejua kimada wako ni Jessi na lazima utaniambia ni nani na alikufanyia nini. Sitaishi kwa hofu kila mara namna hii,” alichemka kwa hasira mama huku jombi akijitia hamnazo.

 

 

Seremala ala makofi kwa kumtamani kidosho

Na SAMMY WAWERU

Imepakiwa - Tuesday, August 30  2016 at  09:18

Kwa Muhtasari

Kioja kilitokea kwenye matatu moja inayohudumu eneo hili la Wang'uru jombi alipoangushiwa kichapo kikali na buda kwa kukatia mwanadada akiahidi kumfungulia biashara.

 

WANG'URU, Kirinyaga,

KIOJA kilitokea kwenye matatu moja inayohudumu eneo hili la Wang'uru jombi alipoangushiwa kichapo kikali na buda kwa kukatia mwanadada akiahidi kumfungulia biashara.

Minong’ono inaarifu kuwa polo ni seremala mtaani hapa.

Siku ya sinema, kalameni alikuwa akienda kwa mteja wake akiwa amebeba vifaa vyake vya kazi.

Kipusa mmoja aliingia kwenye matatu akiandamana na baba yake ingawa waliketi katika viti tofauti.

“Kidosho aliketi karibu na polo naye baba akaketi nyuma yao,” alisema mdokezi aliyesimulia kuwa jamaa alivunja kimya na kuanza kumrushia kimwana huyo mistari ya mapenzi.

“Madam ninahitaji mke na ninaona Mungu ndiye amekutuma kwangu,” polo alimweleza akimnyoshea mkono wa salamu.

Kipusa hakukataa kumsalimia jombi, alimtazama japo hakusema lolote.

“Ninaelekea kazini na nimebeba vifaa vyangu vya kazi. Nitakufungulia biashara uwe mke wangu,” polo aliendelea kurusha mistari ya mapenzi, akimuonyesha vifaa vyake vya kazi.

Mwanadada asalia kimya

Kalameni aliendelea kuzungumza huku mwanadada huyo akisalia kimya.

Baba wa kidosho aliposikia mazungumzo hayo alimrukia polo na kumuangushia magumi mazito mazito.

“Unasafiri kuenda kazini ama kudanganya wasichana?” alifoka buda akimcharaza kalameni.

“Unadhani kazi unayofanya ndiyo itamlisha binti yangu? Unajua gharama ya kuzaa na kutunza binti kama huyu kweli? Hebu safiri kwa utulivu na uache msichana wangu ama nikuonyeshe kilichomtoa kanga manyonya,” alichemka mzee huyo.

Inasemekana abiria waliingilia kati na kumuokoa polo.

“Pole bwana, umejifunza hufai kumtongoza kila kipusa unayemwona,” alisema mama mmoja na kusababisha watu waangue kicheko.

Penyenye zaarifu kwamba alitulia hadi aliposhuka.

 

 

Kisura azabwa konde kwa kumtemea mate X wake

Na JOHN MUSYOKI

Imepakiwa - Monday, August 29  2016 at  12:20

Kwa Muhtasari

MASINGA, Machakos

Kisura mmoja sehemu hii alijipata pabaya alipozabwa kofi kwa kumtemea mate jamaa baada ya kumtema.

 

DEMU mmoja sehemu hii alijipata pabaya alipozabwa kofi kwa kumtemea mate jamaa baada ya kumtema.

Inasemekana mwanadada huyo  alimtemea mate polo kwa kushuku alikuwa na wapenzi chungu nzima. Kioja kilizuka mwanadada huyo alipomtemea jamaa mate huku akimfokea.

"Mwanadada huyo alikuwa amechochewa na wenzake huku akiambia jombi huyo aliyekuwa mpenzi wake hakuwa mtu mzuri. Kwa hamaki alimtemea jamaa mate kichwani kwa dharau huku akiringa kwa madaha,” alisema mdokezi.

Jamaa hakuweza kuvumilia aibu aliyopata kwa kutemewa mate.

Alimgeukia kipusa huyo na kumzaba kofi hadi akaona vimulimuli. Baada ya kumpa adhabu hiyo jamaa alienda zake na kumuacha demu akilia na kuapa kumchukulia hatua za kisheria.

 

 

Buda na kipusa wazua sinema ya bure kwa baa

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Thursday, August 25  2016 at  11:12

Kwa Muhtasari

MWIHOKO, GITHURAI 45

KIOJA kilizuka katika baa moja inayopatikana eneo hili baada ya polo na kipusa kuraruliana nguo hadharani wakizozania bili ya pombe.

 

Inasemekana kuwa wawili hao walikabana koo baada ya kutofautiana kuhusu nani alifaa kulipa bili ya vinywaji walivyokunywa.

Kulingana na mdokezi, polo na kipusa waliingia katika baa pamoja. Inasemekana kuwa polo alimwambia kipusa kuitisha aina ya pombe anayopenda. Duru zinasema kuwa polo naye aliitisha kinywaji chake.

Inasemekana kuwa kadri muda ulivyozidi kusonga, ndivyo walivyozidi kuitisha kileo. Kulingana na mdokezi, meza yao ilikuwa imejaa vileo.

Penyenye zinasema kuwa muuzaji alipogundua kuwa polo na kipusa walikuwa wamelewa, aliwaendea na kuitisha pesa, naye polo alimueleza atulie kidogo.

Duru zinasema kuwa ulifika wakati kipusa alitaka kuondok na kulingana na mdokezi, polo alimueleza kipusa alipe nusu ya bili naye alipe nusu. “Ni wewe ulinileta hapa. Kwa hivyo lipa bili,” kipusa alimkaripia polo. Inasemekana kuwa polo aliingiza mikono mifukoni na kuchomoa Sh100 peke yake.

“Unaniambia nikulipie bili ni kama ni mimi nilikunywa hizi chupa zote. Leo sina pesa. Kila wakati ni mimi nakulipia. Hata na wewe lipa leo. Sio kunikamua tu kama ng’ombe,” polo alimueleza kipusa.

Duru zinasema kuwa kipusa aliinuka na kumshika polo shati kwenye shingo. “Sikia, ujinga ndio sitaki,” kipusa alimsomea polo

Kulingana na walioshuhudia kisa hiki, polo alimkaba koo kipusa na wakaanza kurushiana makonde. “Kama unajua umesota, why call me here?” kipusa alimuuliza polo. Iibidi muuzaji wa baa hiyo kutisha kuwaita polisi ndipo jamaa akalipa bili.

 

 

King'asti msomi atimuliwa kwa kuposwa na taniboi

Na KIMANI NJUGUNA

Imepakiwa - Wednesday, August 24  2016 at  17:21

Kwa Muhtasari

THARAKA-NITHI, Meru

KIPUSA mmoja kutoka hapa alilazimika kutoroka kwao baada ya wazazi wake kumkataa mpenzi wake walipogundua kwamba alikuwa makanga wa matatu.

 

Yasemekana kuwa msichana huyo alimaliza chuo kikuu miaka mitatu iliyopita. “Bahati iliendelea kumfuata msichana huyo kwani mara tu alipofuzu kutoka chuo kikuu, aliajiriwa na kampuni moja ya kibinafsi mjini Nairobi,” akasema mdokezi.

Ni akiwa kazini katika kampuni hiyo ambapo alijuana na kupendana na kijana mmoja makanga wa matatu. “Wawili hao walipendana sana. Hata hivyo, kwa sababu msichana huyo ni Mkristo aliyeokoka, waliamua kutofanya mapenzi kabla ya kufunga ndoa.

Ni kwa sababu hiyo wawili hao waliamua kwenda nyumbani kwa kina msichana huyo ili wawaeleze wazazi wake kuhusu uamuzi huo wa kuoana.

Walipowasili, walipokelewa vizuri na wazazi wakidhani jamaa alikuwa mshiriki wa kanisa lao. Mambo yalipasuka mara tu jamaa alipoeleza kilichomleta na kazi anayofanya.

“Ati nini? Wewe makanga umuoe binti yangu ambaye nimesomesha hadi chuo kikuu ili awe fahari kwa familia yetu. Nikubali binti yangu aolewe na makanga wa matatu? Wewe kijana unataka kumpotosha binti yangu na sitakubali kamwe,” mzee alifoka.

Mzee huyo alijitoma ndani ya nyumba na kuchomoka amebeba rungu mkononi. Bila kujali alimkaribia jamaa huyo aliyechomoka kama mshale ili kujinusuru.

Kuona hivyo, msichana alichomoka na kumfuata mapenzi wake huku akilia kwa sauti ya juu. Kulingana na mdokezi, msichana huyo aliapa kutorejea kwa wazazi wake hadi wamruhusu kuolewa na barafu ya moyo wake.

Haikujulikana iwapo mzee alibadilisha nia na kukubali wapenzi hao kuoana.

 

 

Kipusa amgeuka pasta mumewe siku ya harusi

Na BENSON MATHEKA

Imepakiwa - Tuesday, August 23  2016 at  16:37

Kwa Muhtasari

EMBAKASI, Nairobi

KIOJA kilitokea hapa demu alipokataa kufunga harusi baada ya kugundua kwamba mchumba wake ambaye ni pasta alikuwa na mpenzi mwingine.

 

Wiki moja kabla ya siku ya harusi, mwanadada huyo alichukua simu ya mkewe akitaka kuwasiliana na kamati ya harusi kwa sababu hakuwa na mjazo katika simu yake.

Ni katika harakati za kuwaandikia wanakamati arafa alipopata jumbe ambazo mumewe alitumiwa na mama mmoja aliyemfahamu akimpongeza kwa mapenzi yake motomoto.

“Aliposoma arafa hizo, mwanadada huyo alikasirika hadi akashindwa kupumua. Alimwendea mumewe aliyekuwa chumba cha kulala na kumuuliza kwa nini alikuwa na wachumba wengine ilhali walikuwa wanakaribia kufanya harusi,” alieleza mdokezi.

Inasemekana kuwa maandalizi yote yalikuwa yamekamilika na mwanadada huyo alijipata amechanganyikiwa.

“Badala ya jamaa kuomba msamaha, alimwambia kipusa aamue ikiwa wataendelea na mipango ya harusi au la.

Lilikuwa tamko lililozidisha uchungu katika moyo wa mwanadada huyo. Alishindwa kulala kwa sababu ya mawazo na siku iliyofuata aliamua kusitisha harusi,” akasema mdokezi.

Kulingana na msimulizi wetu, mipango ya harusi ilipokuwa ikiendelea, jamaa alikuwa amepagawisha kimapenzi na mwanadada mwingine tajiri aliyemzidi kwa umri.

“Baada ya harusi kusitishwa jamaa alinyakuliwa na mama sukari huyo huku wakazi wakimsimanga mwanadada kwa kuwahadaa alikuwa na harusi ili wamchangie pesa. Mwanadada huyo alikosa amani, ikawa vigumu kufanya lolote kwa sababu ya masaibu yanayomwandama,” alisema mdokezi.

Demu alipowaeleza wazazi wake sababu za kusitisha harusi walikubali uamuzi wake lakini wakawa na wakati mgumu kuwaeleza watu walioalika kushuhudia binti yao akifunga pingu za maisha.

“Kwa sasa demu anatafuta mchumba, huku jamaa akiendelea kupata joto kutoka kwa mama sukari,” akasema mdokezi.

 

 

Nataka harusi rasmi, mama watoto awakia polo

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Thursday, August 18  2016 at  14:19

Kwa Muhtasari

GASHORORO, Juja

Mwanadada mmoja kutoka hapa alizomewa vikali na mumewe alipomtaka wafunge ndoa kanisani ilhali hakuwa tayari kufanya hivyo.

 

MWANADADA mmoja kutoka hapa alizomewa vikali na mumewe alipomtaka wafunge ndoa kanisani ilhali hakuwa tayari kufanya hivyo.

Kulingana na mdokezi, kipusa huyo alitoka kuhudhuria harusi ya rafiki yake katika mtaa jirani na aliporejea nyumbani, alimueleza polo kilichokuwa moyoni mwake.

“Baba Boi, tumeishi miaka mitatu sasa. Mtoto wa kwanza ndiye huyu tushapata. Mbona basi tusifunge ndoa?” kipusa alimuuliza polo.

Inasemekana kuwa polo alimuangalia kipusa kisha akanyamaza tu. “Wewe angalia watu wanafunga harusi. Kwani tutazidi kuhudhuria harusi za wengine hadi lini?” kipusa alizidi kumuuliza polo.

Duru zinasema kuwa polo alimuangalia kipusa na kucheka. “Wewe umewahi kuniona nikienda kuhudhuria hizo harusi zenu?” polo alimuuliza kipusa.

Penyenye zinasema kuwa polo hangedhubutu kuandaa harusi kwani huko nje hakuwa mchache. Inasemekana kuwa jamaa alikuwa amepanda mbegu kila mahali.

“Kwa hivyo, alikuwa anaogopa kujiletea fedheha,” alieleza mdokezi. Polo alimuonya mkewe dhidi ya kumsukuma wafunge harusi. “Mambo hayo sitaki kuyasikia tena. Kama unataka harusi, basi tafuta mwanamume mwingine mfunge harusi,” polo alimueleza kipusa.

Inasemekana kuwa kipusa aliendelea kusisitizia polo umuhimu wa harusi. “Harusi inadhihirisha mapenzi yako kwangu. Hata na mimi nataka watu waje hapa washerehekee. Nimechoka kualikwa kila mara,” kipusa alimueleza polo.
Kulingana na mdokezi, polo alimkaripia.

“Toka hapa. Kwa nini unanilazimisha kufanya jambo ambalo siko tayari kulitenda? Ninaweza kuwa na nia ya kuoa mke wa pili. Shughulika na mambo yaliyokuleta huku. Achana na mambo mengine kabisa," polo alimkaripia kipusa.

 

 

Kalameni ajuta kurina asali ya bawabu

Na KIMANI wa NJUGUNA

Imepakiwa - Friday, August 12  2016 at  19:45

Kwa Muhtasari

GITAMBAYA, Ruiru

Kalameni wa hapa alijipata pabaya alipofumaniwa akichovya asali kutoka mzinga wa jirani yake ambaye ni bawabu.

 

POLO wa hapa alijipata pabaya alipofumaniwa akichovya asali kutoka mzinga wa jirani yake ambaye ni bawabu.
Habari zilizotufikia zasema kwamba jirani huyo hufanya kazi usiku na kurejea kwake asubuhi na mkewe hufanya vibarua mitaani.

Inasemekana kuwa polo mhusika alimaliza kidato cha nne mwaka uliopita. “Polo hutegemea vibarua vya hapa na pale ili kujikimu kimaisha na kwenye harakati za kutafuta vibarua, alikutana na mke wa bawabu mwenye sura na umbo la kupendeza,” alisema mdokezi.

Wawili hao walifanya urafiki ambao uliota mizizi na akaanza kumtembelea mama huyo jioni. Isitoshe, mara kwa mara alikesha nyumbani kwa mama huyo wakila fuska kwani mwanamke huyo alidai alihitaji mtu wa kumkinga na baridi usiku!

Wawili hao hawakuwa na bahati kwa sababu mwenye mzinga alipashwa habari kuhusu uhusiano wao na wadaku wa mtaa.

Siku arobaini za walaghai hao wa mapenzi zilipotimia, hawakuweza kuepuka. Siku hiyo, bawabu aliamua kuacha kazi yake na kurejea nyumbani usiku wa manane. Badala ya kubisha mlango, aliuvunja kwa kishindo na kujitoma ndani ya chumba cha kulala alipowafumania wakiwa kitandani uchi wa mnyama.

“Nyinyi kweli mna akili timamu? Kijana, ikiwa hujui siku za kuchovya asali katika kila mzinga zilipita na wakati huu ni hatari, basi nitakufunza leo,” alifoka mzee na kuanza kumtwanga jamaa kwa rungu yake.

Vurugu hizo ziliwavutia majirani ambao walifika kujua kilichokuwa kikiendelea. Ni wakati huo ambapo polo alipata mwanya na kufyatuka kama mshale akiwa uchi.

Ajabu ni kwamba bawabu hakusema lolote kwa mkewe kuhusu kitendo hicho.

 

 

Kalameni na kipusa wake wafumaniwa wakila uroda shambani

Na SAMMY WAWERU

Imepakiwa - Wednesday, August 10  2016 at  12:19

Kwa Muhtasari

TOEZZ, GITHURAI 45

Jombi mmoja na kidosho wake walijipata pabaya hivi majuzi walipofumaniwa na bwanyenye mmoja wakila uroda kwenye ua wa boma lake.

 

KALAMENI mmoja na kidosho wake walijipata pabaya hivi majuzi walipofumaniwa na bwanyenye mmoja wakila uroda kwenye ua wa boma lake.

Minong’ono iliyofikia meza ya Dondoo inaarifu kwamba wawili hao walifika karibu na boma la buda huyo mwendo wa saa moja za jioni. “Waliopita waliwaona wakipokezana mabusu,” akasema mdokezi.

Yasemekana kwamba wawili hao walizama kwenye starehe zao wakisahau kwamba walikuwa kwenye ua wa boma la mwenyewe.

Vituko vyao vilisikika na buda huyo aliyetoka akishika kurunzi na nyahunyo mkononi na kuwafumania wawili hao.

“Nyinyi mmefanya ua wangu kuwa lojing’i mfanyie hizo tabia hapa?” alichemka mzee huyo akiwaangushia mijeledi moto moto.

“Ama hamna nyumba niwatafutie moja mpangishe?” aliwafokea. Kioja hicho kilivutia watu waliofika hapo kujionea kalameni na kipenzi chake wakitiwa adabu.

Yasemekana waliokolewa na mama mmoja aliyeomba buda huyo kuwaonea huruma na kuwasamehe. “Mzee hata wewe wakati mmoja ulikuwa kama wao ukitafuta mke, japo wamepata funzo hayo mambo si ya kufanyiwa hadharani,” mama huyo alieleza bwanyenye huyo na kusababisha watu kuangua kicheko.

 

 

Kipusa afumania rafiki mnafiki akimwibia penzi

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Tuesday, August 9  2016 at  12:07

Kwa Muhtasari

Kioja kilizuka katika baa moja hapa mtaani Mwiki baada ya kipusa kumfamania mpenzi wake akijivinjari na kidosho rafiki yake.

 

MWIKI, Nairobi

KIOJA kilizuka katika baa moja hapa mtaani Mwiki baada ya kipusa kumfamania mpenzi wake akijivinjari na kidosho rafiki yake.

Duru zinaarifu kuwa kipusa aliwapata wawili hao pembeni wakiwa wamejaza chupa za pombe na nyama choma mezani.

Kulingana na mdokezi, kipusa alipowaona, alianza kuwatusi huku akitaka kuvua nguo jambo lililowashtua wateja wengine.

Penyenye zinasema kuwa kipusa alikuwa amemtambulisha rafiki yake wa dhati kazini kwa mpenzi wake.

Kulingana na mdokezi, siku ya kisanga, rafiki yake aliondoka kazini mapema bila kumueleza ilivyokuwa kawaida yake.

Inasemekana kuwa kipusa alishangaa kugundua kuwa rafiki yake aliondoka bila kumfahamisha.

Duru zinaarifu kuwa kipusa alijaribu kumpigia simu rafiki yake, lakini alikuwa mteja.

Kulingana na mdokezi, kwa sababu ya urafiki wao, kipusa hangeweza kumshuku kwa sababu walikuwa wamefanya mambo mengi pamoja.

Penyenye zinasema kuwa kipusa alipofika mtaani humu, alikutana na jirani yake mmoja aliyemueleza kuwa alikuwa amekutana na rafiki yake.

“Na leo rafiki yako wa dhati alikuacha wapi? Nimekutana na yeye akiingia kile kilabu akiwa na spidi kali sana nikafikiria pengine ulikuwa kule,” jirani alimueleza kipusa.

Kwa raha

Duru zinasema kuwa kipusa naye alifululiza moja kwa moja hadi katika hicho kilabu na kumpata rafiki yake na mpenzi wake wakitulia kwa raha zao.

“Kwa hivyo, ulitoka kazini mapema ndio uje ukutane na mpenzi wangu? Wewe ni rafiki wa aina gani?” kipusa alimuuliza rafiki yake.
Inasemekana kuwa polo alitamani ardhi ipasuke ajifiche ndani.

“Unawezaje kunifanyia haya, Unawezaje kumtongoza rafiki yangu. Nyinyi wawili ni bure kabisa,” kipusa alimkaripia polo huku akiirukia meza na kuanza kumuaga pombe chini hadi akafukuzwa na walinzi.

 

 

Yaya na shambaboi wafumaniwa na mdosi wakila busu

Na SAMMY WAWERU

Imepakiwa - Monday, August 8  2016 at  10:34

Kwa Muhtasari

GITHUNGURI, Kiambu

Kipusa aliyekuwa akifanya kazi katika boma moja kijijini hapa alipigwa kalamu alipofumaniwa akipigana mabusu na shamba boi ambaye alikuwa mpango wa kando wa bosi wake.

 

KIDOSHO aliyekuwa akifanya kazi katika boma moja kijijini hapa alipigwa kalamu alipofumaniwa akipigana mabusu na shamba boi ambaye alikuwa mpango wa kando wa bosi wake.

Yasemekana yaya huyo aliajiriwa kazi miezi minne iliyopita. “Mume wa bosi wake husafiri sana ughaibuni kwa sababu ya biashara,” akasema mdokezi wetu.

Kwa mujibu wa mdokezi, bosi huyo hukatia shambaboi wake na wanaokubali kumzuzua kimahaba huwaongezea kitita cha mshahara.

Siku ya kioja kipusa alienda kumpelekea shambaboi chakula cha mchana kwenye bustani alipokuwa akifanya kazi. Kidosho kwa sababu alimmezea polo mate aliamua kufungua roho yake.

“Huwa ninakutamani uwe mpenzi wangu, kila nikikutazama nakuwaza,” yaya alimweleza. “Ungenieleza kitambo sasa hivi tungekuwa mbali,” kalameni alimjibu.

Wawili hao walianza kupokezana mabusu moto moto hadi kupusa akasahau alikuwa na majukumu aliyopewa na bosi. Saa moja iliisha mama huyo akisubiri yaya arejee hadi akaamua kujua kwa nini alikawia.

Alifululiza kwenye bustani na kumfumania yaya na shamba boi wakiwa wamezama katika mapenzi. “Wewe nilikuajiri kufanya kazi ama kuniharibia shamba boi wangu?” boss lady alimfokea. Penyenye zinaarifu kwamba mama alimpiga kalamu papo hapo.

“Unanidai mshahara wa shilingi ngapi hadi kwa sasa? Kazi kwangu imeisha,” akachemka na kumpokeza mshahara wake na kumuagiza kuondoka kwake kisha akamgeukia shamba boi.

“Na wewe ni nini ulichokosa hadi ukaamua kwenda kwa yaya. Ninakulipa mshahara mkubwa sio kwa kazi ya shamba bali ni kwa sababu ya kuniburudisha?” mama huyo alimweleza shamba boi akitisha kumtimua pia.

 

 

Mke ala makonde kwa kufagia minofu ya nguruwe peke yake

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Sunday, August 7  2016 at  14:39

Kwa Muhtasari

Jombi aliwaacha wenyeji wa eneo hili vinywa wazi baada ya kumpa mkewe kichapo kikali akidai alimmalizia kitoweo cha nyama ya nguruwe.

 

JOMBI aliwaacha wenyeji wa eneo hili vinywa wazi baada ya kumpa mkewe kichapo kikali akidai alimmalizia kitoweo cha nyama ya nguruwe.


Yasemekana polo alinunua nyama ya nguruwe kilo moja na mkewe akaamua kuipika yote japo mumewe hakutaka nyama hiyo ipikwe yote.
“Mbona umepika nyama yote? Si ungebakisha nusu ili ipikwe kesho,” polo alifoka. Penyenye zinasema kuwa kipusa alimueleza polo kuwa hawangekula yote.


“Wewe usijali. Hii nyama ni nyingi sana. Tutabakisha nyingine itumike kesho,” mke huyo alimueleza polo. Inasemekana kuwa polo alikubaliana na mke lakini kwa shingo upande.


Duru zinaarifu kuwa kulipopambazuka, polo alienda shughuli zake za kila siku huku akimuacha mkewe nyumbani. Inasemekana kuwa mchana mke huyo alitayarisha chakula na kukila kwa nyama iliyosalia jioni ile kama kitoweo. 


Lakini kwa bahati mbaya, yamkini kutokana na utamu wake, mke akaufagia mnofu mzima bila kubakisha. Jamaa aliporejea kwake kwa hamu ya kufakamia kitoweo chake cha nguruwe, alishtuka.


“Jamaa hakuamini macho yake alipoandaliwa ugali kwa mboga za kienyeji,” alieleza mdokezi. Inasemekana kuwa polo alichungulia tena kwenye sahani ili kuthibitisha alichoona.


“Nguruwe ya jana kwani umesahau kuleta?” polo aliuliza. Duru zinasema kuwa mkewe alimueleza kuwa nyama ya nguruwe iliisha.
“Wewe ukiondoka asubuhi, uliniachia pesa za mboga kweli? Nilipika ugali mchana nikala na hiyo nguruwe,” kipusa alimueleza polo.
Duru zinasema kuwa polo aliinuka na kuanza kumzaba mkewe makofi kwa hasira.


“Mimi sikuoa mke mlafi. Unawezaje kula nusu kilo ya nyama ya nguruwe peke yako?” polo alimuuliza kipusa huku akiendelea kumpa makofi.
Inasemekana kuwa majirani walishangazwa na sababu ya polo kumchapa mkewe.

 

 

Pasta afumaniwa akimchuna ngozi kondoo wake

Na CORNELIUS MUTISYA

Imepakiwa - Thursday, August 4  2016 at  07:44

Kwa Muhtasari

KISSONI, Machakos

Mhubiri wa kanisa moja eneo hili alipokezwa kichapo cha mbwa koko na wakazi alipofumaniwa akirushana roho na mke wa muumini wa kanisa lake katika chumba chake kanisani.

 

PASTA wa kanisa moja eneo hili alipokezwa kichapo cha mbwa koko na wakazi alipofumaniwa akirushana roho na mke wa muumini wa kanisa lake katika chumba chake kanisani.


Kulingana na mdokezi, pasta alihamishiwa kanisa hilo mwaka uliopita. Staili zake za mahubiri na mienendo yake ziliwatia hofu waumini mpaka baadhi yao wakaanza kususia ibada. Licha ya waumini kulalamika kuhusu hulka zake, hakuna hatua yoyote ya kinidhamu aliyochukuliwa na wakubwa wake.


“Pasta aliondokea kuwa na tabia potovu. Alikuwa akiwatongoza akina mama kanisani bila kuogopa chochote,’’ alisema mdokezi.


Penyenye za mtaa zaarifu kuwa, pasta alianza uhusiano wa kimapenzi na mama mmoja. Mapenzi yao yalivuma mno mpaka mumewe akapata habari akiwa jijini Nairobi anakochapa kazi. Aliamua kuajiri 'makachero’ wa kuchunguza nyendo za pasta na mkewe ili akiwafumania, awafunze adabu ya mwaka.


Siku ya tukio, Pasta alimpigia simu mama huyo mwendo wa saa mbili unusu usiku akimtaka amletee maji chumbani mwake. Mama alifika akiwa na mtungi wa maji na akajibanza kwa kiti sebuleni. Baadaye walijitoma katika chumba cha kulala na kujibanza kitandani ambako walianza kurushana roho.


Inasemekana kwamba walipokuwa wamezama katika shughuli zao, 'makachero’ , walimpigia simu mume wa mwanamke huyo na akafika mara moja.


Kulingana na mdokezi, mke wa polo alitoroka kupitia dirishani mambo yalipochacha na kumuacha pasta akitandikwa vikali. Hata hivyo, aliokolewa na maafisa wa usalama waliokuwa kwenye doria.


Duru zaarifu kuwa, polo alisikika akiapa hatamkubali mkewe tena kwa sababu ya uzinzi.

 

 

Apigwa kalamu kwa kung'ara kuliko bosi

Na OSCAR KAKAI

Imepakiwa - Thursday, August 4  2016 at  07:48

Kwa Muhtasari

MAKUTANO, POKOT

Kipusa mmoja mjini hapa alipoteza kazi kwa kuvalia vizuri kuliko mke wa mdosi wake.

 

DEMU mmoja mjini hapa alipoteza kazi kwa kuvalia vizuri kuliko mke wa mdosi wake.
Demu huyo ambaye alikuwa akifanya kazi ya kuuza katika duka moja alikuwa akifika kazini akiwa amevalia nguo na mapambo ya bei ghali.
Yasemekana kuwa mwanadada huyo alipoajiriwa kazi hakuwa na nguo za maana na alikuwa ameparara.
Baada ya kufanya kazi katika duka hilo kwa muda wa miezi mitatu, demu huyo alibadilika na kuanza kununua nguo nyingi ambazo alibadilisha kila siku.
Juzi demu huyo alifika kazini akiwa amevalia nguo na viatu vipya na kufanya mwajiri huyo kushtuka.

 

 

Polo aliyedhani ndoa ni asali tu ajua ukweli

Na CORNELIUS MUTISYA

Imepakiwa - Sunday, June 12  2016 at  14:56

Kwa Muhtasari

KAVIANI, Machakos

Polo wa eneo hili alijipata pabaya alipokataa kuwajibikia mimba aliyompachika mwanadada akisema alikuwa akisingiziwa.

 

POLO wa eneo hili alijipata pabaya alipokataa kuwajibikia mimba aliyompachika mwanadada akisema alikuwa akisingiziwa. Hata hivyo, mtoto alipozaliwa na wakapimwa chembechembe za DNA, iligunduliwa alikuwa mtoto wake halisi.


Penyenye zinaarifu kuwa polo alianza uhusiano wa kimapenzi na mwanamke huyo ambao ulinoga hadi demu akahamia kwa polo katika ndoa ya 'njoo tuishi’.


“Polo na demu walikuwa wakiishi pamoja kama mume na mke. Hata hivyo, hawakuwa wamefuata utaratibu unaotakiwa kulingana na mila na desturi za jamii ya hapa,’’ akasema mdokezi.


Inasemekana demu aliishi na jamaa huyo kwa muda wa miezi minane na akabeba mimba yake. Alipomwambia polo kuhusu mimba hiyo, alikasirika na akamfurusha kinyama.


“Jombi aliposikia kuwa demu alikuwa mja mzito, alikasirika na kufoka kuwa mimba haikuwa yake. Alimwamuru kufunganya virago vyake na kutokomea,’’ akasema mdokezi.


Inasemekana kwamba jitihada za demu kumtuliza polo zilipoambulia patupu, aliamua kwenda kuripoti kisa hicho kwa naibu wa chifu ili suluhisho lipatakane.


Duru zinaarifu kwamba chifu aliposikiliza madai ya demu huyo, alimshutumu kwa kuamua kuishi na polo huyo kana kwamba alikuwa amemuoa. Alimwambia ikiwa alikuwa na hakika mimba ilikuwa ya polo huyo, basi asubiri mtoto atakapozaliwa wapimwe damu ili ukweli udhihirike.


Na mtoto alipozaliwa na wote wakapimwa, ilidhihirika bayana kuwa alikuwa wa polo huyo. Walienda kwa naibu wa chifu na polo akaamriwa agharamie malezi na elimu ya mtoto wake hadi atakapotimu umri wa miaka 18.


“Polo alikubali kugharamia mahitaji ya mtoto huyo, lakini alikataa katakata shinikizo za wazazi wake kumuoa mwanadada huyo,’’ akasema mdokezi.

 

 

Mpango wa kando alijileta chumbani singekataa tunda, buda ahadithia

Na GRACE KARANJA

Imepakiwa - Sunday, May 29  2016 at  15:13

Kwa Muhtasari

KOMAROCK, Nairobi

Buda wa mtaa huu aliwaacha majirani midomo wazi alipokiri kwamba alianza mpango wa kando na kipusa jirani kwa sababu alijileta kwake mwenyewe.

 

BUDA wa mtaa huu aliwaacha majirani midomo wazi alipokiri kwamba alianza mpango wa kando na kipusa jirani kwa sababu alijileta kwake mwenyewe.


Kulingana na mdokezi, mke wa jamaa alikuwa akishuku mienendo ya mumewe lakini hakufahamu kwamba demu jirani ndiye alikuwa mpango wa kando wa mumewe.


Inasemekana kuwa kipusa alikuwa akimpigia simu buda lakini hakujibu na ikambidi kumwandikia ujumbe mfupi ambao mkewe aliusoma jamaa akiwa bafu.

“Nilijua tu una mpango wa kando lakini sikudhani anaweza kuwa ni jirani. Haya pokea ujumbe kutoka kwa jirani yako anakualika mjini,” mkewe alimwambia buda baada ya kutoka kuoga.


Yasemekana kwamba buda alipogundua alikuwa amepatikana, alijaribu kujitetea kwa mkewe na kukiri kwamba demu alijileta kwake.


“Najua umeudhika sana lakini naomba msamaha tu, sikuwa na la kufanya kwa sababu demu alijileta mwenyewe kwangu na kuniambia ananipenda.


Usilojua ni kwamba ninampenda pia na furaha yangu ni kwamba umejua,” buda alikiri mbele ya mkewe na majirani waliofika kujua walichokuwa wakigombania.

Haikubainika kilichofuata kwa sababu demu hakuweko lakini mke wa jamaa aliingia ndani ya nyumba huku majirani wakishangazwa na tukio hilo.

 

 

Jombi arudi ocha kusaka aliyemroga

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Monday, May 23  2016 at  14:34

Kwa Muhtasari

CHWELE, Bungoma

Kalameni aliwashangaza wenyeji wa eneo hili aliporejea kutoka jijini kwa lengo la kumsaka mtu aliyeshuku alimroga. Inasemekana kuwa lengo la polo lilikuwa ni kumwadhibu aliyemroga.

 

KALAMENI aliwashangaza wenyeji wa eneo hili aliporejea kutoka jijini kwa lengo la kumsaka mtu aliyeshuku alimroga. Inasemekana kuwa lengo la polo lilikuwa ni kumwadhibu aliyemroga.


Kulingana na mdokezi, polo alikuwa akioa lakini hakuna mwanamke aliyeishi naye kwa muda mrefu. “Wote walikuwa wakimtoroka baada ya muda mfupi,” alieleza mdokezi. Inasemekana kuwa jambo hili lilimkasirisha polo hadi akaamua kuhamia jijini.


“Kwani mimi nina shida gani? Watoto wa juzi wameoa na wanaishi na wake zao vizuri. Lazima kuna mtu anayeniangalia na jicho baya,” polo alisema.


Duru zinasema kwamba polo alipofika jijini, alimpata kipusa mwingine ambaye walioana lakini pia hawakuishi kwa muda mrefu.


Inasemekana kuwa polo alipokuwa anarejea kwake wakati wa jioni kutoka kazini, aliona kibango ambacho kilikuwa na maandishi yasemayo mganga wa kulinda ndoa.


Duru zinasema kuwa polo aliamua kumtembelea mganga huyo akiwa na matumaini ya kupata suluhisho la tatizo lake. Inasemekana kuwa mganga alimfichulia polo mtu aliyemfanya asiishi na mke.

“Wazee wananiambia kuwa wewe ulifungwa. Hakuna mke atakayeishi na wewe. Aliyekufunga ni jirani yako,” mganga alimueleza polo.


Kulingana na mdokezi, polo alitoka kwa mganga akiwa na hasira na kuelekea moja kwa moja hadi kwao kijijini kumsaka mtu aliyetajwa na mganga,” alieleza mdokezi.


Inasemekana kuwa alipofika kijijini, polo alielekea kwa wazazi wake ambapo aliwaeleza shughuli iliyomleta. “Mimi nimekuja kumtafuta mtu asiyenitakia mazuri. Nimetoka kwa mganga na akaniamba kuwa ni jirani yetu ndiye ananiroga. Lazima nimwadhibu leo,” polo aliwaeleza wazazi wake.


“Umehadaiwa bure na mganga, jirani yetu si mchawi,” polo alielezwa na wazazi.

 

 

Mama afumaniwa juu ya paa kwa jirani akifanya sarakasi

Na HASSAN POJJO

Imepakiwa - Saturday, May 21  2016 at  14:21

Kwa Muhtasari

CHAANI, Mombasa

Kulizuka kioja katika mtaa hapa baada ya mama mmoja kupatikana kwenye paa la nyumba ya mwenyewe usiku akifanya vituko vya uchawi.

 

KULITOKEA kioja katika mtaa hapa baada ya mama mmoja kupatikana kwenye paa la nyumba ya mwenyewe usiku akifanya vituko vya uchawi.


Inasemekana kwamba watu walikuwa wakishuku mama huyo kwamba alihusika na ushirikina.

Kulingana na mdokezi, ilikuwa saa nane usiku wapangaji wa nyumba moja mtaani hapa waliposikia kishindo kikubwa juu ya nyumba yao na wakatoka nje.

Baada ya kuchunguza walipata mama akiwa uchi wa mnyama akishika vitambaa vyeusi mkononi.

Baada ya kushurutishwa ashuke chini alianza kulia na kuomba msamaha.

Umati uliojawa na hasira kwa kusumbuliwa usiku na wachawi juu ya ulianza kumtandika huku wakumuuliza alikokuwa akienda.

 

 

Polo arukwa na akili baada ya Sportpesa kunyonya hela zake

Na DENNIS SINYO

Imepakiwa - Friday, May 20  2016 at  16:52

Kwa Muhtasari

KABRAS, Malava

MAMA kutoka eneo hili aliwashangaza wakazi kwa kutisha kumripoti mumewe kwa polisi akidai alichanganyikiwa baada ya kupoteza pesa nyingi kwenye mchezo wa bahati nasibu katika Sportpesa.

 

MAMA kutoka eneo hili aliwashangaza wakazi kwa kutisha kumripoti mumewe kwa polisi akidai alichanganyikiwa baada ya kupoteza pesa nyingi kwenye mchezo wa bahati nasibu katika Sportpesa.

Yaarifiwa kwamba mume wa mama huyo alikuwa akishiriki kamari hiyo kila siku huku akiwa na matumaini kwamba angeshinda hela nyingi na kuishi maisha ya raha mstarehe.

Hata hivyo, jamaa huyo anasemekana kuwa mkali zaidi akikosa kushinda pesa kwenye mchezo huo. Kulingana na mdokezi, hali hii ilikuwa ikimfanya jamaa kutotulia usiku kucha huku akiamka kila mara kutazama iwapo alikuwa ametumiwa ujumbe wa kushinda kwenye simu yake.

Hali ilipoonekana kuwa mbaya zaidi, mama huyo alimjuza shemeji yake na kumuomba amshauri jamaa kuacha kushiriki michezo hiyo.

Hata hivyo, inasemekana ndugu ya jamaa aliogopa akisema kwamba jamaa hangemsikiza hata kidogo. Hali hii ilimfanya mama huyo kutisha kupiga ripoti kwa polisi kwamba mumewe alikuwa hatulii nyumbani na kukataa chakula baada ya kukosa kushinda.

Kukataa chakula

“Usiku hulali hata kidogo, kila mara ni simu tu, anapogundua kwamba hujashinda kitu, huwa na mawazo mengi sana

kukataa chakula,” alieleza mama huyo.

Ilisemekana kwamba jamaa alikuwa amepoteza pesa nyingi sana kwenye michezo hiyo ya kubashiri matokeo ya spoti ila hakuwa akibahatika kushinda kitita alichonuia.

Licha ya mkewe kumrai kuacha uraibu huo, jamaa alikuwa akimfokea na kumtaka kuachana naye kabisa.“Nimetumia njia zote kukusaidia ila nimeshindwa, sasa hii lazima ifike polisi,” mama huyo alimtisha mumewe.

Hata hivyo, wakazi walimshauri mama huyo kumtafutia jamaa ushauri nasaha aitwe kusaidiwa kuepuka majuto ya kutoshinda michezo ya bahati nasibu.

Wakazi walimlaumu vikali mama huyo kwa kumtakia mumewe mabaya kwa kutisha kumshtaki kwa polisi.

 

 

Wang'ang'ania polo kama mpira wa kona mbele ya mke wake

Na GRACE KARANJA

Imepakiwa - Thursday, May 19  2016 at  12:37

Kwa Muhtasari

DANDORA, Nairobi

Kioja kilizuka mtaani hapa vipusa wawili walipomenyana vikali wakimng’ang’ania polo mbele ya mke na watoto wake.

 

KIOJA kilizuka mtaani hapa vipusa wawili walipomenyana vikali wakimng’ang’ania polo mbele ya mke na watoto wake.


Kulingana na mdokezi, wawili hao walikuwa wamealikwa na polo kuhudhuria sherehe za kuzaliwa kwa mwanawe.


Inasemekana kuwa polo hufanya biashara ya kupika na kuuza chakula na wawili hao walikuwa wateja wake lakini hawakuamini kwamba alikuwa na mke. Kila mmoja alikuwa akimmezea mate.


Siku ya kisanga wawili hao walifika kwa jamaa wakiwa wamevalia mavazi ya kisasa huku wamejipodoapodoa kwelikweli kisha wakaketi karibu na polo.


“Usiniambie hata wewe uko hapa. Mimi nitaketi karibu naye hata kama ana mke sijali,” mmoja alimwambia mwenzake.
Hapo ndipo mwenzake alisimama na bila kuona haya akaanza kumpapasa polo mkono mbele ya mkewe na mtoto.


“Naona una mke na mtoto tuliyekuja kumsherehekea lakini najua mapenzi ndiyo yalikufanya unialike. Sasa amka tuanze kula ngoma,” alimuomba polo.


Hata hivyo, polo alisimama na kuwaonya vikali dhidi ya kumharibia sherehe za mwanawe.


“Niliwaalika hapa ndio mjue kwamba nina mke na mtoto na siwezi kumwacha kwa sababu yenu, nawaheshimu kama wateja wangu lakini mengine mwajidanganya tu. Kwa sasa, ondokeni kwangu kwa sababu hamna nia nzuri,” polo aliwaonya wawili hao ambao tayari wana watoto nje ya ndoa.


Hapo ndipo walianza kukabiliana wenyewe kwa wenyewe wakilaumiana vikali. Hakuna aliyewatenganisha na mara moja, mke wa polo akawafurusha nje.


“Hamna haya, nendeni mkatafute baba za watoto hao wenu, mwacheni mume wangu,” mke wa polo aliwaonya wawili hao.

 

 

Walishana bakora kukosa kuelewena kuhusu ukali wa pombe

Na AMIMO ZACCHAEUS

Imepakiwa - Wednesday, May 18  2016 at  09:59

Kwa Muhtasari

Kulizuka hali ya taharuki katika boma la mama pima mmoja wa hapa Wire, Oyugis walevi walipoanza kulishana bakora baada kukosa kuelewana kuhusu ukali wa pombe waliokuwa wakiteremsha.

 

WIRE, Oyugis

KULIZUKA hali ya taharuki katika boma la mama pima mmoja wa hapa Wire, Oyugis walevi walipoanza kulishana bakora baada kukosa kuelewana kuhusu ukali wa pombe waliokuwa wakiteremsha.

Kulingana na mdokezi, walevi hao walikuwa wakiburudika kwa mama pima pale mmoja wao alipoanza mjadala akidai pombe hiyo haikuwa kali kama ya siku iliyotangulia.

“Leo ni kama imeongezwa maji ama nini wenzangu? Hii sio kali kama ile ya jana! Nateremsha na bado sipati stimu,” alisema jamaa moja.

Kilichomshangaza ni kwamba, hakuna aliyemjibu, badala yake, wenzake  waliendelea kuchapa dozi wakiagiza kinywaji zaidi.

Inasemekana kuwa jamaa aliyelalamika, alichukua bakuli iliyokuwa na pombe na kuiangusha akisema pombe hiyo haikuwa na ladha.

“Nimewaambia pombe si kali na ni kama hamsikii. Kwani midomo yenu imewekwa nini kiasi kwamba hamuwezi kugundua pombe imeongezwa maji,” jamaa alilalamika huku akimwita mama pima.

Mama pima atolewa kijasho kwa maswali

Mama pima alipofika jamaa alimkabili kwa maswali magumu.

“Kwani siku hizi unaongeza pombe maji kwa nini? Unajua nakulipa kwa huduma yako na hivyo basi ningependa nipate dhamana ya pesa yangu. Yaani nataka ile inawasha koo yangu,” alisema mzee huyo.

Kwa hasira, mmoja wa walevi wengine walimwambia aachane na ujinga na kuondoka badala ya kusumbua watu.

“Unajua wewe una ujinga mwingi sana ukilewa.Unasemaje pombe si kali ilhali umelewa.Kama haujalewa si uamke uende kwako nyumbani?” akafoka jombi mmoja.

Wawili hao walianza kubishana na haikuchukua muda kabla ya mmoja kumwangushia mwenzake bakora mgongoni.

“Jinga wewe! Chukua hiyo. Nyinyi ndio mnaharibu biashara hapa,” alimfoka huku akimwambia mama pima amrudishie jamaa pesa zake. Mama huyo alilazimika kuwafurusha walevi wote na kufunga mlango akiogopa ghasia.

 

 

Nusura pasta avunjike guu baada ya kufumaniwa akimla kondoo

Na SAMMY WAWERU

Imepakiwa - Tuesday, May 17  2016 at  13:22

Kwa Muhtasari

KAGUMO MJINI

Pasta anayehubiri katika kanisa moja mjini hapa nusura avunjike mguu akitorokea dirishani alipofumaniwa akizini kwa mshirika wa kanisa lake.

 

PASTA anayehubiri katika kanisa moja mjini hapa nusura avunjike mguu akitorokea dirishani alipofumaniwa akizini kwa mshirika wa kanisa lake.


Inasemekana kuwa muumini huyo ni mke wa mtu na mama wa watoto watatu. Penyenye zinaarifu kuwa mhubiri huyo alikuwa na uhusiano wa kimahaba na mama huyo.


Mume wa mama huyo aliarifiwa na majirani kuwa mchungaji huyo alikuwa akionekana kwake jioni na walishuku alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe.

Siku ya kioja, mume wa mama huyo alifika nyumbani wikendi bila kumuarifu mkewe baada ya kupashwa habari kuwa pasta alionekana kwake. Alibisha mlango na mkewe akamfungulia mhubiri akiwa katika chumba cha kulala walikokuwa wakila uroda.


“Kwa nini ukaja bila kuniarifu, utakula nini ilhali chakula kimeisha na maduka yamefungwa?” mama huyo alimuuliza kwa ukali. “Huku ni kwangu na si lazima nikufahamishe ninapokuja,” mumewe alimjibu.

Pasta aliposikia sauti ya mwenye nyumba, aliamua kurukia dirishani. Hata hivyo, hakuwa na bahati mzee wa boma alipomfumania katika harakati za kutoroka.

“Hii ndiyo injili ambayo umekuwa ukija kueneza kwangu?” mzee alichemka akimuangushia pasta kichapo.

 

 

Jombi adinda kulipa mahari akidai mke ni mvivu

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Monday, May 16  2016 at  12:59

Kwa Muhtasari

LUANDA, Vihiga

Kalameni kutoka eneo hili, alishangaza mashemeji wake baada ya kuwaeleza kuwa wasitarajie mahari yoyote kwa sababu dada yao alikuwa mvivu.

 

KALAMENI kutoka eneo hili, alishangaza mashemeji wake baada ya kuwaeleza kuwa wasitarajie mahari yoyote kwa sababu dada yao alikuwa mvivu.


Kulingana na mdokezi, polo alikuwa amechoshwa na safari za mara kwa mara za mashemeji nyumbani kwake wakidai mahari.


Inasemekana kuwa jamaa aliamua kuwaita nyumbani. Kulingana na mdokezi, mashemeji hao hawakukawia kwenda wakidhani aliwaitia mahari.


“Mimi nimewaita hapa ili tuweze kujadiliana mambo kadhaa,” jamaa alianza kuwambia mashemeji zake. “Ninajua ya kwamba nimekaa na msichana wenu kwa muda mrefu bila kuwaletea chochote. Nyinyi mnafikiria kuwa nimewahepa,” polo aliwaeleza mashemeji zake.

 
Kulingana na mdokezi, shemeji mmoja alisimama na kuanza kuzungumza. “Shemeji sisi hatukatai chenye unasema. Lakini mtu huleta kitu kidogo kidogo.” Duru zinasema kuwa jamaa alisimama tena na kuanza kuzungumza huku hasira zikimpanda.


“Ati kitu kidogo kidogo? Kitoke wapi? Ebu niwaulize, mlipoingia katika hili boma, mmeona ng’ombe, kondoo au mbuzi wangapi? Dada yenu kwanza ni mvivu namba one. Sasa mnataka niwape nini?” polo aliwauliza mashemeji zake.


Inasemekana kuwa mashemeji walianza kuangaliana. “Sasa unamaanisha nini?” polo mmoja alimuuliza. Kulingana na walioshuhudia kisa hicho, polo na mashemeji zake walianza kurushiana cheche za matusi.

“Kila mara mnakuja hapa mkitaka mahari, please tell your sister aanze kutafuta hiyo mahari. Mtu anayelala mpaka saa tano mchana. Ninamlisha tu kama ndege. Halafu mnanisumbua hapa eti mahari. Kwendeni huko,” polo aliwazomea mashemeji zake.

 

 

Demu aanika wazi ufisi wa polo kwa harusi

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Sunday, May 15  2016 at  13:53

Kwa Muhtasari

NDAUNI, Makueni

Kizaazaa kilizuka katika kanisa moja eneo hili kipusa alipomtaka pasta kusimamisha harusi akidai alikuwa na mimba ya bwana harusi.

 

KIZAAZAA kilizuka katika kanisa moja eneo hili kipusa alipomtaka pasta kusimamisha harusi akidai alikuwa na mimba ya bwana harusi.


Kulingana na mdokezi, kipusa aliingia kanisani na kuelekea moja kwa moja hadi kwenye altari. “Wewe akili yako inafanya kweli? Kwa nini unapenda kuchezea mademu?” kipusa alimuuliza polo.

Inasemekana kuwa waumini kanisani walisimama wote kujionea yakiendelea. “Nimeuliza unafanya nini hapa?” kipusa alizidi kumuuliza polo.


Penyenye zinasema kuwa polo alikuwa amepanga harusi hiyo kwa siri bila hata kuwaeleza baadhi ya marafiki zake.
Kulingana na mdokezi, pasta alisimama na kujaribu kumshawishi kipusa kutulia.

“Wewe pia achana na mimi kabisa. I’m carrying his child. Na leo ananifanyia haya,” kipusa alimueleza pasta. Inasemekana kuwa pasta alipigwa na butwaa aliposikia maneno ya kipusa. “Una uhakika na yale unayosema?” pasta alimuuliza kipusa.


Duru zinasema kuwa kila mtu kanisani alianza kucheka. “Huyu jamaa alikuwa ameahidi kunioa. Hata tulikuwa tumepanga kwenda kujitambulisha kwa wazazi. Leo ananifanyia haya. Huyu ni mtu wa aina gani?” kipusa alimuuliza pasta.


Inasemekana kuwa polo alimweleza pasta aliachana na kipusa yule. “Pasta achana naye. Nilimtema kitambo. Mchumba wangu kwa sasa ndiye huyu. Kama ana mimba yangu mimi sijui. Wewe endelea na harusi,” polo alimueleza pasta.


Kwa hasira, kipusa alimvamia polo kwa matusi “Unaambia nani hivyo? Wewe ni mjinga sana. Leo ujanja wako lazima ukome. Pasta hakuna harusi itaendelea hapa. Hii mimba nimebeba hata yeye mwenyewe anajua ni miezi sita. Saa hii anajaribu kuniruka. Kwani niliipata through osmosis?” kipusa alisimama kidete.

Ilibidi harusi iahirishwe kwa muda.

 

 

Aibu ya mwaka kwa mwalimu kudaiwa madeni na wanakijiji hadharani

Na DUNCAN MWERE

Imepakiwa - Saturday, May 14  2016 at  13:09

Kwa Muhtasari

MUKARO, NYERI

Shughuli katika shule moja ya msingi zilisimama kwa muda wa saa mbili baada ya mwalimu mmoja kudaiwa madeni na wanakijiji wa eneo hili.

 

SHUGHULI katika shule moja ya msingi zilisimama kwa muda wa saa mbili baada ya mwalimu mmoja kudaiwa madeni na wanakijiji wa eneo hili.

Mwalimu huyu aliyehudumu katika shule hiyo kwa zaidi ya miaka ishirini inaaminika hutangamana na wenyeji wa hapa kiasi cha kwamba huwatembelea nyumbani mwao baada ya masomo na wakati hana vipindi.

Wanakijiji waliokuwa na hasira walimininika shuleni mwendo wa asubuhi huku wakidai haki yao. Kioja hiki kilivutia walimu, wanafunzi na wanakijiji wa kata hiyo na kukatiza shughuli za masomo kote shuleni.

“Haki yetu! Lazima alipe bidhaa zetu ambazo tumemkopesha kwa muda wa nusu mwaka,” wanakijiji waliokuwa na ghadhabu wakapaza sauti. Wengine walisema hawatabanduka shuleni hadi wapatiwe haki yao.

Haya yakijiri mwalimu mkuu alikuwa ofisini akiwa mwingi wa matumaini shida hii itatatuliwa na naibu wake na mwalimu wa zamu. Maji yalipozidi unga ilibidi mwalimu mkuu kuingilia kati ili kupata suluhisho.

Hapo ndipo mambo yalichukua mkondo mpya na joto lililokuwa limepanda kupunguza. “kwanza lazima mtulie kwani sheria za taasisi hii haziruhusu wananchi kuzua rabsha hapa shuleni wakati wowote,” akaonya mwalimu mkuu.

Wote waliokuwa wakipayuka walifyata ulimi kwani walielewa ima fa ima wao ni wazazi shuleni humo. Mkuu wa shule hii aliwaita walimu na baadhi ya wazazi waliokuwa wakidai haki zao.

Wakati wa kikao hicho ambacho nusra kitimbuke kutokana na malumbano kutoka pande zote mbili. Kwa tajriba na hekima ya mwalimu aliweza kukomesha ugomvi huu uliokuwa umezidi.

“Mbona msifuate kanuni na utaratibu unaofaa kutatua tofauti kati yenu,” akauliza mwalimu mkuu akionyesha kukerwa na tukio hilo ambalo halijawahi kutokea shuleni humo tangu ajiunge nayo. Wanakijiji hao walisema wamekuwa wakiahidiwa ahadi za kulipwa na wakaona wanachezewa shere.

"Tumesubiri kwa muda wa siku, miezi na miaka lakini kila wakati tunaambulia patupu,” akasema mmoja wao aliyekuwa mkuu wao. “Kwani

mnadai nini na nini, " akahoji mwalimu mkuu aliyekuwa katika nafasi ya hakimu.

Kila mmoja aliyepata fursa alisema si mara moja aliwahi kumkopesha bidhaa na aina mbalimbali ya vyakula na kukosa kulipwa. Wengine walieleza kuwa waliwahi kumkopesha viumbe ambao hufugwa ila hakuna malipo wamewahi kupata.

Kuku na mbuzi

“Mimi niliwahi kumkopesha kuku wawili na mbuzi lakini kufikia sasa ni muda wa miezi minane na sijapata haki yangu,” akasema mama mmoja. Madai yaliendelea huku mazungmzo yakionekana kutokamilika kwa muda uliotengewa. Taharuki ilizidi kutandaa shuleni kila mmoja aliyekuweko akionekana kujua hatima ya kesi hiyo.

Hatimaye, mwalimu mkuu aliwaomba wanakijiji hao kuandika ni nini wanamdai mwalimu huyo. Baadaye walikubaliana ni lini na ni wapi watapata haki yao na wakaonywa na mwalimu mkuu kuwa macho wanapokopesha walimu na mtu wa aina yoyote bidhaa zake. Kwa mujibu wa wale wanaomfahamu mwalimu walisema halipi madai hadi sheria itumike.

Wanakijiji waliondoka wakiwa na wingi wa matumaini kupata haki yao. Baadaye mwalimu mkuu aliandaa kikao na walimu wote na kuwashauri kuhusu baadhi ya mambo ambayo yatawashushia heshima yao.

Hatimaye alimwita mwalimu mhusika na kumwonya endapo hatabadilisha mienendo yake huenda atapata uhamisho.

 

 

Polo amzaba makonde mke kwa kutumiwa jumbe za mahaba Facebook

Na DUNCAN MWERE

Imepakiwa - Saturday, May 14  2016 at  12:58

Kwa Muhtasari

MBIRIRI, NYERI

Jombi mmoja kutoka eneo hili alimwadhibu mkewe vibaya kwa madai kuwa amejiunga na mtandao wa kijamii. Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka, 55, alishangwa na hatua ya mkewe, 32, ya kujiunga na mtandao wa Facebook.

 

JOMBI mmoja kutoka eneo hili alimwadhibu mkewe vibaya kwa madai kuwa amejiunga na mtandao wa kijamii. Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka, 55, alishangwa na hatua ya mkewe, 32, ya kujiunga na mtandao wa Facebook.

Hali ya kutoelewana kati yao ilitokea wakati mkewe alitumia wakati mwingi kuwasiliana na rafiki wake. Kalameni huyu alipofanya uchunguzi wa kina kuhusu ni kwa nini mkewe anatumia muda mwingi akichokora simu alifahamu kuwa alikuwa akiwasiliana na marafiki na kujenga uhusiano mpya na masaibu wapya.

Mumewe alikiri kuwa mwenzake amebadili mienendo na kuwa mkaidi. “Nimegundua kuwa wewe umekuwa ukitumia muda mwingi ukiwasiliana na watu wa matambaka mbalimbali na kusahau majukumu yako hapa nyumbani, " akasema jombi huyu kwa hasira.

Vuta nikuvute iliendelea kuhusu swali hili. Juhudi za kalameni za kumshawishi agure kwenye mtandao huo zilizidi kuongezeka masaibu maradufu kwani uhasama kati yao ulichangia wao wawili kukosana zaidi.

Kalameni huyo alihofia huenda mkewe akajinasia mwingine hasa kutokana na umri wao kutokuwa sawa. “Nakuomba uachane na mambo ya Facebook kwani mambo yaliomo ni ya kupotosha na hayazingatii maadili katu,” akamweleza akijaribu kutumia mbinu ya kumshawishi kuachana na mtandao.

Mkewe aliyekerwa na jambo hili alisema hayuko tayari kuhama kwani amefahamiana na marafiki wengi wa matabaka tofauti. “Kuwasiliana kupitia mitandao kuna manufaa mengi kwani nimewajua marafiki wengi wa jinsia zote,” akamweleza.

Mpango wa kando

Kauli hii ndio ilifanya jombi huyu kuwaza mwenzake amejinasia mwingine. Kila siku kalameni alianza kuchokora simu wakati hayuko ili kuhakikisha hawasiliani na mwanamume mwingine.

Hali hii iliendelea kwa muda mrefu lakini siku moja alipatikana ametuma ujumbe kwa jamaa mmoja, jambo lilimuudhi na kuamua kumpatia funzo ambalo hatasahau maishani.

Mdaku wa eneo hili alifahamisha meza ya Dondoo kuwa jombi huyu aliamua kumtia mkewe adabu na funzo ambalo hatasahau maishani mwake.

“Nimepata ujumbe wa mahaba kwenye simu yako na sasa ni wazi kuwa kupitia mitandao umejinasia wa kando au siyo,” akauliza mwanamume huyu aliyekuwa amepandwa na mori kupindukia.

Mkewe alijaribu kujitetea lakini juhudi zake za kumwambia nyingi za jumbe kwenye mitandao huwa zina uwazi. “Wengi wa wale wanaotumia mitandao hii hawajali ni lugha gani ambayo wanatumia,” akajitetea. Hapo ndipo mwanamume huyo aliamua kumlisha makonde mkewe kwa vile alikaidi uamuzi wake.

Alimwonya vikali dhidi ya kuendelea kutumia mitandao hiyo. Wadaku wanaarifu kuwa mama huyu huwasiliana kupitia mitambo hii kisiri.

 

 

Jombi ajuta kuwatuma watoto karo kwa wakwe zake

Na DUNCAN MWERE

Imepakiwa - Monday, May 9  2016 at  17:59

Kwa Muhtasari

KIAMAINA, NYERI

Jombi mmoja kutoka eneo hili aliyekuwa na mazoea ya kuwatuma wanawe kwa wakwe zake kuchukua

karo na mahitaji mengine alijipata pabaya baada ya kuzomewa na wanakijiji.

 

Jombi mmoja kutoka eneo hili aliyekuwa na mazoea ya kuwatuma wanawe kwa wakwe zake kuchukua karo na mahitaji mengine alijipata pabaya baada ya kuzomewa na wanakijiji.

Mwanamume huyu mzembe kutoka eneo hili aliwaeleza watoto wake endapo wametumwa nyumbani kwa sababu ya pesa za matumizi shuleni wawe wanaendea kwa wakwe wao.

Ujanja wake uligunduliwa na wanakijiji walipoona watoto wa mzee huyu wa umri wa makamo wakifika boma la wakwe wake wakati vipindi vya masomo vinaendelea.

Awali walidhani kuwa ni mapenzi watoto walikuwa nayo kwa upande ambao mama yao ametoka. Lo! Majibu waliyopata yaliwaacha vinywa wazi kwani watoto hao walio na umri wa miaka kati ya miaka tisa na kumi na mmoja walisema wanaelekezwa na baba yao.

“Baba yangu hutushauri kuendea karo na matumizi mengine katika boma ambalo mama ametoka,” akasema mmoja

wa watoto hao aliye na umri mkuu kati yao.

Kina mama walioona fedheha na kuwaliamuru watoto kwenda makwao na kumhimiza babake kuwajibika. Wakati wa adhuhuri watoto walifika nyumbani na kumkuta baba yao.

Alipowaona wanaye alishangaa sawa na mtu aliyeona sinema ya shani. Baada ya kuwahoji wanaye alimaizi kuwa kitumbua kimeingia mchanga.

Kwani mambo yameendaje mkaja nyumbani ilhali siku zote nimewaelekeza boma ambalo mama yenu ametoka?" akauliza jombi huyo. Watoto waliojawa na woga hawakumfamisha babake ujanja wake umegunduliwa na wanakijiji wenzake.

Aliwarai watoto kwenda kwa wakwe wake kwa azma ya kupata karo. Watoto walishika kiguu na njia na kwenda kule walizoea.

Raundi hii watoto walionekana na wanakijiji wengi kuliko ilivyokuwa hapo awali. Waliamua ni lazima mzee huyu ajue kilicho na mwanzo kina mwisho wake.

Waliamuru watoto kurudi makwao ili mahitaji yao yatimizwe na mzazi wao. Kwa nyota ya jaha walimpata baba watoto akibarizi nje ya boma yake.

Alijaribu kujitetea lakini yote yalikuwa bure bilashi kwani walimweleza kinagaubaga kuwajibikia watoto wake kwa vyovyote vile.

 

 

Kalameni afurushwa chamani kwa dai ni mpishi

Na DUNCAN MWERE

Imepakiwa - Monday, May 9  2016 at  18:25

Kwa Muhtasari

BUSARA, NYAHURURU

Mwanamume mmoja kutoka mji huu alitimuliwa kwenye kikao cha wazee kwa madai hupenda kuingia jikoni kwa lengo la upishi.

 

Mwanamume mmoja kutoka mji huu alitimuliwa kwenye kikao cha wazee kwa madai hupenda kuingia jikoni kwa lengo la upishi.

Jombi huyu ambaye ni baba wa watoto wanne inasemekana hupenda kuingia jikoni kujipikia ilhali mkewe huwa tayari kutekeleza wajibu na majukumu yake barabara.

Uvumi ulianza wakati watoto wake walipoanza kutangazia wenzao mienendo ya babaye. Fununu hizo zilienea si shuleni si nyumbani almuradi watu wa matabaka mbalimbali walikuwa na mwao kuhusu jombi huyu ambaye inasadikika hupenda mlo kupindukia.

Kwa mujibu wa watoto, waliwambia wengine wakati walikuwa wakirudi nyumbani. Hatimaye ujumbe huu uliwafikia wazazi kisha habari zikaenea mithili moto kwenye kichaka kikavu.

“Unajua baba ameteka majukumu ya mama haswa upishi kila wakati," akasema mmoja wa watoto hao.

Watoto wenzake walisaili zaidi ili wapashwe kuhusu baba yao. Udaku huu uliwafikia wazee wa rika lake na kuamua kuwa na kikao na mpishi huyo hodari. Baada ya kuhojiwa na wenzake aliungama bila kusita na kuamuliwa kukaa kando ili uamuzi wa busara utolewe.

Kisha aliitwa ili kujua hatima yake. Mkuu wa kikao hicho alimweleza namna baraza liliamua. Kabla ya hukumu kutolewa jombi huyu aliulizwa endapo yuko tayari kukomesha mienendo yake.

Uraibu wa kupika

“Mimi siko tayari kuacha kupika kwani huu ni uraibu wangu,” akajibu. Mzee huyu alisema yuko tayari kwa lolote lakini ataendelee na hulka yake anayopenda na kuienzi mithili ya moyo yake.

Mkuu wa kikao hicho aliye pia mzee wa kijiji alisimama na kutoa wosia kuhusu majukumu ya mwanamume kuhusu jamii hiyo.

“Kwanza ni lazima mjue kuwa tangu jadi mwanamume hakuruhusiwa kuingia jikoni, endapo kulikuwa na jambo la dharura rafikiye mkewe akiaalikwa ili kuwajibika,” akashauri.

Ni kweli kuwa mwenzetu anatutia doa kutokana na tabia ambazo zinatukera sisi sote,” akaongezea. Wakati wa kutolewa hukumu wazee wenzake walioonekana kuunga mkono uamuzi uliotolewa dhidi ya kalameni na fauka ya hayo hakuonyesha wasiwasi wowote.

"Kwa vile afua ni mbili, lazima uchague moja kati ya hizi kulipa kondoo watano au kupigwa marufuku chamani wala kushiriki mikutano wa kijiji hicho,” akaongezea.

Mzee mpishi alisimama na kusema. “ Mimi nimeamua kutolipa ada yoyote lakini nitakuwa nikihudhuria mikutano ya wazee kwenye baraza,” akajibu.

Jawabu hilo liliwafanya wazee hao kupandwa na mori na kumchukulia hatua kali. “Kutoka leo hutakuwa ukishiriki mikutano ya wazee wa kitongoji hiki na huo ndio uamuzi wa jopo na wazee wenzangu,” akaongezea.

Kutoka siku hiyo hiyo mzee mpishi hajakuwa akihudhuria mikutano wala kushirikishwa katika maamuzi ya baraza la wazee.

 

 

Jombi alisha watoto mijeledi kwa kufikiri walimwita 'punda'

Na DUNCAN MWERE

Imepakiwa - Monday, May 9  2016 at  18:10

Kwa Muhtasari

GITERO, NANYUKI

Watoto wa familia moja katika kitongoji hiki wanajuta baada ya kuadhibiwa vikali na baba yao kwa kutumia lugha ambayo haelewi.

 

Watoto wa familia moja katika kitongoji hiki wanajuta baada ya kuadhibiwa vikali na baba yao kwa kutumia lugha ambayo haelewi.

Kisa hiki kilijiri wakati watoto waliendelea kutumia lugha hiyo ambayo baba hakuelewa katu. Lililomuudhi baba yao ni kuwa wanawe walitumia maneno ya kumshushia hadhi na kumpiga majembe jambo ambalo lilimfanya kupandwa na mori na kuchukua hatua kali. Baba yao ambaye

alidhani baadhi ya maneno hayo ni ya kumtusi.

Aliwaonya vikali watoto hao ambao wanaelewa maneno ya lugha kadri yanavyochipuka kila uchao. Mdokezi wetu alidokeza mwandishi wa Swahilihub kuwa vijana hao wameathirika si haba na hiyo lugha ya mjini almaarufu Sheng.

“Popote wawapo vijana hawa wana mazoea ya kutumia lugha hii jambo ambalo limechangia kukosana na watu kijijini ambao katu

hawaelewi lugha hii,” akasema.

Penyenye ziliarifu kuwa ni kutokana na mazoea haya wameathirika shuleni. “Imekuwa ni kawaida ya walimu wao kulalamika kila wakati kutokana na wanafunzi hao kutumia lugha batili hususan katika uandishi wa insha,” akaeleza mmoja wa walimu kutoka katika eneo hilo wanakosomea watoto hao.

Kilichomkera babake ni namna walivyozoea kumwita. Mmoja wa vijana hao alifika nyumbani na kuuliza babake endapo kulikuwa na chochote cha kula. “Wewe buda leo kuna msosi nimange ,”? kijana akauliza.

Matusi

Swali hilo lilimkasirisha baba mtu na kuamua kumpatia adhabu ambayo hataisahau maishani mwake. “Mbona unanitusi punda ilhali mimi ndiye babako mzazi?,” akauliza babaye.

Kijana alijaribu kujitetea lakini yote yaliaambulia patupu. “ Mimi nimesema buda lakini sijasema punda,” akajitetea. Mara ghafla babake aliwaita watoto wengine ambao waliitikia kwa lugha hiyo bila kumaizi wamerusha jiwe kwenye kituo cha polisi.

“Niaje mbuyu kwani kulikoni,” wakaitikia. Kwa hasira za mkizi baba ambaye hakuonyesha utani wala mzaha aliamua liwe liwalo lazima awatie adadu na wajue kilichomtoa kanga manyoya.

“Leo ni leo msema kesho ni mwongo, lazima mjue kwa nini sangara akachomwa moto," akaeleza bila dhihaka. Baba alichukua bakora na kuwatandika watoto na kuwaonya wasiwahi kutumia lugha Sheng karibu naye na mazingira ya nyumbani mwake.

 

 

Demu alishwa kipigo baada ya kufumaniwa na mpango wa kando

Imepakiwa - Friday, May 6  2016 at  10:45

Kwa Muhtasari

DALAS, Embu

Mwanadada kutoka eneo hili alijipata pabaya mumewe alipompokeza kichapo na kumtema baada ya kumfumania katika hali ya kutatanisha na buda aliyeshuku kuwa mpango wake wa kando.

 

MWANADADA kutoka eneo hili alijipata pabaya mumewe alipompokeza kichapo na kumtema baada ya kumfumania katika hali ya kutatanisha na buda aliyeshuku kuwa mpango wake wa kando.


Penyenye zilizotufikia zasema kwamba mwanadada huyo alikuwa akija nyumbani na pesa nyingi licha ya kutofanya kazi.
“Maisha yake yalibadilika akawa na pesa nyingi licha ya kutofanya kazi,” akasema mdokezi.


Inasemekana kuwa mumewe alipomuuliza alikotoa pesa hizo za kununua vipodozi kila wakati alimwambia kwamba wanaume ni wengi walio na mali.


“Mkewe alimjibu kwa dharau na kumwambia kwamba wanaume ni wengi ambao wana pesa na hawana haja nazo,” alisema mdokezi.


Siku ya kioja, mumewe mama alijipodoa na mumewe akamuuliza alikokuwa akienda, naye akamdanganya kwamba alikuwa akipeleka mchango katika kikundi cha akina mama.


“Kama ni lazima ufahamu ninakoenda kila wakati, leo ni siku ya chama, ninapeleka hela za akina mama,” alijibu.
Ni katika baa moja iliyoko eneo hili alipomfumania mkewe na buda mmoja wakipigana mabusu.


“Shika hizi hela ukanunue kile unachohitaji kwa sasa, kisha mwisho wa mwezi nitakupa zile nilizokuahidi. Kumbuka kuwa mjanja mumeo asijue uhusiano wetu na wewe,” buda alimweleza mwanadada.


Mumewe hakungoja tena, alijitokeza na kuanza kumchapa mkewe.


“Wewe hata hujiheshimu, unajiuza kwa mzee kama huyu rika la baba yako kwa sababu ya pesa,” jamaa alichemka kwa hasira na kuchukua hela alizoficha kwa sidiria na kuzitupa.


Jamaa huyo alisikika akimweleza mkewe kumfuata buda aliyeponyoka na kuingia kwa gari na kutoroka.

 

 

Machozi yamtoka ajuza kuona ndevu za pasta zinafanana na beberu wake aliyeibwa

Na DUNCAN MWERE        

Imepakiwa - Tuesday, May 3  2016 at  17:36

Kwa Muhtasari

MUTHINGA, Nyeri

Ajuza mmoja katika sehemu hii aliwashangaza waumini na mhubiri kwa kuwa na huzuni wakati wa ibada. Mwanamke huyo alifika kanisani mapema ilivyo desturi yake lakini hakuwa mchangamfu.

 

AJUZA mmoja katika sehemu hii aliwashangaza waumini na mhubiri kwa kuwa na huzuni wakati wa ibada. Mwanamke huyo alifika kanisani mapema ilivyo desturi yake lakini hakuwa mchangamfu.

Waumini wenzake hawakujua mwenzao ambaye hakosi kuhudhuria ibada na mikutano ya injili katikati ya juma alikuwa na jambo ambalo limemwendea mvange.

Wakati wa nyimbo za sifa mama huyu mwenye watoto wanane aliimba ilivyo desturi yake. Ilipowadia wakati wa ushuhuda mama huyu hakujitokeza kushuhudia  kwani kila fursa inapopatikana huwa mstari wa kwanza na  anafahamika kuwa kielelezo bora cha kuigwa na vijana wa kanisa hilo.

Kipindi cha mahubiri kilipofika, mhubiri aliyealikwa kutoka parokia jirani alisimama na kujitambulisha. Alikuwa mrefu na mwingi wa maneno ya hekima yaliojikita kwenye biblia takatifu.

Fauka ya hayo alikuwa amefuga msitu wa ndevu ambazo zilitoa taswira ya mitume wanaosimuliwa kwenye misahafu.

Alianza mahubiri yake yaliokuwa na ucheshi na taharuki huku waumini wakionyesha ishara ya kutaka  aendelee. Akiwa katikati ya ibada aligundua kuna mama mmoja aliyekuwa na huzuni.

Ajuza huyu alishika tama kwenye shavu lake la kushoto na kububujikwa na machozi. Ni mhubiri huyu pekee aligundua kuna jambo ambalo linaenda kombo ila alijitia hamnazo na akaendelea na mahubiri yake.

Kadri mahubiri yalivyoendelea ndivyo huzuni ilimzidia ajuza huyu. Kufumbua na kufumbua akashika tama katika shavu lake la kulia na kudodokwa na machozi. Hatimaye ibada ilifika ukingoni nao waumini walifumukana.

Katika pilkapilka za kuondoka mhubiri aliamua kumuuliza ajuza tatizo alilokuwa nalo kutoka awali hadi akheri. “Mbona ulikuwa na huzuni wakati mahubiri yalikuwa yakiendelea,” akauliza mhubiri aliyekuwa na hamu ya kutaka kujua.

“Nilipokuona ukihubiri nilikumbuka beberu wangu aliyeibiwa na wezi  na alikuwa na ndevu sawa na zako,” akajibu mama aliyekuwa mwingi wa huzuni na masikitiko. Kisha mhubiri alimpatia pole na kumuomba awasamehe wezi waliomwibia beberu wake.    

 

 

Machozi yamtoka ajuza kuona ndevu za pasta zinafanana na beberu wake aliyeibwa

Na DUNCAN MWERE        

Imepakiwa - Tuesday, May 3  2016 at  17:36

Kwa Muhtasari

MUTHINGA, Nyeri

Ajuza mmoja katika sehemu hii aliwashangaza waumini na mhubiri kwa kuwa na huzuni wakati wa ibada. Mwanamke huyo alifika kanisani mapema ilivyo desturi yake lakini hakuwa mchangamfu.

 

AJUZA mmoja katika sehemu hii aliwashangaza waumini na mhubiri kwa kuwa na huzuni wakati wa ibada. Mwanamke huyo alifika kanisani mapema ilivyo desturi yake lakini hakuwa mchangamfu.

Waumini wenzake hawakujua mwenzao ambaye hakosi kuhudhuria ibada na mikutano ya injili katikati ya juma alikuwa na jambo ambalo limemwendea mvange.

Wakati wa nyimbo za sifa mama huyu mwenye watoto wanane aliimba ilivyo desturi yake. Ilipowadia wakati wa ushuhuda mama huyu hakujitokeza kushuhudia  kwani kila fursa inapopatikana huwa mstari wa kwanza na  anafahamika kuwa kielelezo bora cha kuigwa na vijana wa kanisa hilo.

Kipindi cha mahubiri kilipofika, mhubiri aliyealikwa kutoka parokia jirani alisimama na kujitambulisha. Alikuwa mrefu na mwingi wa maneno ya hekima yaliojikita kwenye biblia takatifu.

Fauka ya hayo alikuwa amefuga msitu wa ndevu ambazo zilitoa taswira ya mitume wanaosimuliwa kwenye misahafu.

Alianza mahubiri yake yaliokuwa na ucheshi na taharuki huku waumini wakionyesha ishara ya kutaka  aendelee. Akiwa katikati ya ibada aligundua kuna mama mmoja aliyekuwa na huzuni.

Ajuza huyu alishika tama kwenye shavu lake la kushoto na kububujikwa na machozi. Ni mhubiri huyu pekee aligundua kuna jambo ambalo linaenda kombo ila alijitia hamnazo na akaendelea na mahubiri yake.

Kadri mahubiri yalivyoendelea ndivyo huzuni ilimzidia ajuza huyu. Kufumbua na kufumbua akashika tama katika shavu lake la kulia na kudodokwa na machozi. Hatimaye ibada ilifika ukingoni nao waumini walifumukana.

Katika pilkapilka za kuondoka mhubiri aliamua kumuuliza ajuza tatizo alilokuwa nalo kutoka awali hadi akheri. “Mbona ulikuwa na huzuni wakati mahubiri yalikuwa yakiendelea,” akauliza mhubiri aliyekuwa na hamu ya kutaka kujua.

“Nilipokuona ukihubiri nilikumbuka beberu wangu aliyeibiwa na wezi  na alikuwa na ndevu sawa na zako,” akajibu mama aliyekuwa mwingi wa huzuni na masikitiko. Kisha mhubiri alimpatia pole na kumuomba awasamehe wezi waliomwibia beberu wake.    

 

 

Mbwa wararua polo akinyemelea demu

Na KIMANI wa NJUGUNA

Imepakiwa - Tuesday, April 26  2016 at  14:21

Kwa Muhtasari

NKUBU, Meru

POLO wa hapa alipata majeraha aliposhambuliwa na mbwa wakali akimsubiri kipusa aliyekuwa akimmezea mate.

 

Penyenye zinasema jamaa huyo anajulikana kwa tabia yake kuwaandama vipusa kila wakati. Hivi majuzi, alikutana na mwanadada wakiwa kwenye mkutano wa kanisa.


“Wawili hao walianza uhusiano wa kimahaba na ikawa ni kawaida yao kukutana kila Jumamosi ili wale 'tende’ pamoja,” akasema mdokezi.


Inasemekana mama wa mwanadada huyo huwa anahudhuria mkutano wa akina mama kila Jumamosi jioni. Lakini naye baba wa demu huyo huwa anajiunga na marafiki vilabuni kuburudika hadi usiku na akirudi nyumbani mbwa wake wakali huwa wanafunguliwa.


Mambo yalienda mrama Jumamosi iliyopita kwani buda hakuhudhuria kikao cha wazee na kumfanya mkewe kuwa nyumbani kinyume na desturi, ili amshughulikie mumewe.


Kwa sababu ambazo hazikubainika, kidosho hakuwasiliana na jamaa ili wabadilishe mpango wao.


Isitoshe, mbwa wa boma walifunguliwa mapema kwa sababu mzee hakutoka nyumbani. Ilipofika saa mbili jioni, polo alielekea katika boma la mpenzi wake kama ilivyokuwa desturi na kusimama karibu na dirisha la chumba cha kidosho ambapo alibisha.


Kabla ya dakika kupita, mbwa walitokea na kuanza kumshambulia jamaa. Kilio cha polo kiliwavutia wote waliokuwa katika boma hilo.


“Wuuii! Wuuuii! Wuuuui! Mimi si mwizi! Mimi ni shemeji yenu,” akalia jamaa katika juhudi za kujiokoa.


Ilibidi kidosho kuingilia kati na kumnusuru polo huyo dhidi ya kutafunwa na mbwa na kukiri kwamba alikuwa mpenzi wake.


Hapo ndipo wazazi wake kidosho huyo walipomuonya polo na kuapa kumpatia funzo ambalo hatawahi kusahau maishani akirudia tabia hiyo.

 

 

Jombi ampa mke kichapo kwa kukumbatia mwanasiasa

Na DUNCAN MWERE

Imepakiwa - Thursday, April 21  2016 at  14:16

Kwa Muhtasari

MAHIGA, NYERI

MWANAMKE mmoja aliye na tabia ya kukumbatia mwaniaji yeyote wa kiti cha siasa alipata aibu ya mwaka baada ya kupata kichapo kutoka kwa mumewe hadharani.

 

Mwanamke huyu wa makamo alipata kichapo hicho baada ya kukumbatiwa na mwanamume anayedhamiria kuwania kiti kimoja kikuu katika eneo hili kama ishara ya hakikisho kundi la akina mama alilo kinara wake litampigia kura

wakati wa uteuzi na uchaguzi mkuu.

Punde baada ya mgombeaji huyu kuwasili uwanjani alitumbuizwa na kundi la kinamama hao na kisha akaamka kusakata

rumba nao. Katika pilkapilka hizo ndipo kiongozi huyu alianza kuwapa pesa na kuonyesha ishara ya mapenzi kwao.

Alipomfikia mama huyo alimkumbatia mama huyo mchanga kwa muda.

Ghafla bin vuu bwanake mwanamke alijongea kwenye jukwaa kwa hasira na kufoka. “Leo ni leo lazima ujue kilichomtoa kanga manyoya. Ni nani alikuruhusu kuwakumbatia mabwana wa wenyewe namna hii?" akauliza.

Baada ya maneno alimgeukia mkewe na kumtandika kwa fimbo na kumwezeka makofi. Wote waliofika waliduwaa na kushindwa la kufanya kwani walihofia huenda zamu ya kushambuliwa ikawa ni yao.

Hatimaye walijikakamua liwe liwalo wakamwokoa mmoja mama huyo. Mwanamke huyo aliamua kuchana mbuga na kuahidi asithubutu kufika nyumbani siku hiyo.

"Ujue leo hutalala kwangu, kwani naelewa kuna zaidi ya haya nimejionea kwa macho yangu," akasema mwanamume huyo na alijawa na hasira zilizozidi za mkizi.

 

 

Polo ajuta kwa kupelekea wakwe chupi kama nyongeza ya mahari!

Na DUNCAN MWERE

Imepakiwa - Thursday, April 21  2016 at  13:51

Kwa Muhtasari

MATHAKWAINI, NYERI

JOMBI mmoja eneo hili anajuta baada ya kuwapelekea wakwe zake mavazi ya ndani kama nyongeza ya mahari.

 

Jombi mmoja eneo hili anajuta baada ya kuwapelekea wakwe zake mavazi ya ndani yakiwa nyongeza ya mahari.

Kalameni huyu ambaye ni kibarua katika maeneo haya aliandamana na wazee kadhaa kwa lengo la kuwasilisha mahari. Alishangaza wote waliofika baada ya kusema ana zawadi ya ziada.

Cha kushangaza ni kuwa mwanamume huyu hakuwa amewaarifu ingawa alikuwa ameandamana nao. Baada ya

shughuli zote kukamilka za mlo na kutoa mahari ambayo ilikuwa ni pesa taslimu.

Kalameni huyu alisema, “Ninayo furaha kuu kukubalika katika boma hili, nitawazawadi wazazi wa mke wangu kwa

zawadi maalum.” Wote waliofika waliduwaa.

Kalameni akaendelea. “Zawadi kuu ni kwa wakwe zangu ni chupi tano kwa kila mmoja,” akasema. Wenye boma waliojawa na hasira waliamuru kalameni huyo kuondoka na kusema posa hiyo haitakubalika.

Wazee walioandamana na bwana harusi mtarajiwa waliomba msamaha. Hatimaye waliondoka na kumshauri kalameni huyo kuhusu mipaka na adabu kwa wakwe.

 

 

Muziki mchafu wa pasta wafanya waumini kususia ibada

Na  DUNCAN MWERE

Imepakiwa - Thursday, April 21  2016 at  13:36

Kwa Muhtasari

CHAKA, NYERI

WAUMINI wa kanisa moja katika eneo hili walisusia ibada ya Jumapili baada ya pasta kuwa na mazoea kuabiria bodaboda zinazocheza muziki uliokiuka maadili na mafundisho ya dini.

 

Waumini wa kanisa moja katika eneo hili walisusia ibada ya Jumapili baada ya pasta kuwa na mazoea kuabiria bodaboda zinazocheza muziki uliokiuka maadili na mafundisho ya dini.

Mhubiri huyu alifika kanisani asubuhi na mapema ilivyo desturi yake. Baada ya kufanya sala ya kipekee asubuhi, alisubiri waumini kuingia kanisani lakini hakuna hata mmoja aliingia ili kuendelea mbele na ibada.

Pasta alitoka nje na kupata wafuasi wake wakijadiliana kwa sauti za chini. “Kulikoni ni jambo lipi limeenda mrama?" pasta aliuliza.

Wote walinyamaza kwa muda, na muda si muda wakajibu kwa pamoja. “Umetuletea aibu kote mjini, mbona unaabiria bodaboda zinazocheza muziki mchafu unaoshusha hadhi yako na kutuaibisha sisi wafuasi wako,” wakauliza.

Pasta huyu mwenye mbwembwe za kila aina aliomba msamaha na kuahidi hatarudia kuabiria boda boda zinazocheza muziki wa aina hiyo.

Hatimaye ibada iliendelea lakini ibada ikaongozwa na mzee wa kanisa.

 

 

Jombi ampa mkewe red card kwa kuhepesha pesa

Na DENNIS SINYO

Imepakiwa - Monday, April 18  2016 at  12:49

Kwa Muhtasari

MATULO, Webuye

MAMA wa hapa alipata talaka baada ya mumewe kugundua kwamba aliiba pesa zake na kumpelekea mama yake mzazi.

 

Jamaa alidai kwamba mkewe alichukua Sh 8,500 kutoka mfuko wa koti lake aliloacha nyumbani na kumpelekea mama yake akidhani kwamba mumewe hangejua.

Kwa bahati, jamaa huyo alipata fununu kutoka kwa marafiki zake kwamba mkewe alimpatia mama yake mzazi Sh8,000 ili aandalie wajukuu wake sherehe.


Wakati jamaa alipofika nyumbani, alidhibitisha kwamba pesa zake hazikuwa alipoziweka.


“Jamaa alimuuliza mkewe ikiwa akichukua pesa lakini mama alikanusha kuiba pesa hizo. Hali hii ilimuudhi jamaa na akamwambia alikuwa akimwibia pesa


kila mara. Aidha, jamaa alielezea jinsi alivyosaidia familia ya mkewe mara nyingi ila hakuna shemeji hata mmoja aliyemshukuru kwa wema wake.


“Wakati nyumba ya mama-mkwe ilibomoka nilitumia, mshahara wangu wote kumjengea nyumba nyingine, baadaye kaka yako mkubwa


alikamatwa na polisi na nikaitwa kulipa faini akaachiliwa huru. Leo umeiba pesa zangu na akampatia mama yako, mbona nyinyi hamna huruma?” aliuliza jamaa.


Mama huyo alikuwa na wakati mgumu kumshawishi jamaa kwamba hakuiba pesa hizo. Mumewe alimwambia alitaka pesa zake au afuganye virago na kurudi kwao.


Jamaa alimwambia kwamba hakuona haja ya kuishi na mke mwizi asiyeaminika hata kidogo licha ya kutimiziwa mahitaji yote aliyotaka. “Kila kitu unachotaka nakupa, hakuna siku hata moja nimekosa kukupa pesa. Mbona ukachukua pesa zangu na kuharibu mipango yangu?” jamaa alimuuliza mkewe.

Kulingana na mdokezi, jamaa aliamua kumtimua mkewe hadi atakaporejesha pesa hizo.

 

 

Polo alimwa na mke kwa kukataa kutoa namba siri ya ATM

Imepakiwa - Sunday, April 17  2016 at  14:20

Kwa Muhtasari

DANDORA, Nairobi

JOMBI wa mtaa huu alijipata pabaya baada ya mkewe kumkabili bila huruma na kumjeruhi alipokataa kumpa nambari ya siri ya ATM yake.

 

Kulingana na penyenye, haikuwa mara ya kwanza ya jombi kuonekana akinuna mwisho wa mwezi ila hakuna aliyejua masaibu aliyokuwa akipitia.


Inasemekana kwamba jamaa alirejea nyumbani kutoka kazini akiwa amelewa.


Hapo ndipo ugomvi kati yake na mumewe ulipoanza mkewe akitaka pesa za matumizi.


“Wewe ni gwiji wa kulewa tu lakini hukumbuki kwamba tunahitaji chakula. Si kwanza ungeniletea pesa kisha uende kujiunga na walevi wenzako. Nipe ATM na nambari ya siri sasa hivi,” mkewe aliteta.


Ni katika mabishano yao ambapo mama alimpiga mumewe lakini kwa bahati, jirani mmoja alimsikia jamaa huyo akimwambia mkewe kwamba hangempa nambari hiyo.


“Yaani wewe unaweza kuniumiza kwa sababu ya pesa zangu, wacha nikuambie, hata ukitaka kuniua, niue tu lakini nambari ya siri ya kadi yangu sikupi,” jamaa alimwambia mkewe.


Kulingana na mdokezi, jirani alimlazimisha mke wa jamaa kuufungua mlango na alipokataa aliwaita majirani wengine na wakugundua kwamba alikuwa amempiga mumewe na kumjeruhi.

 

 

Mke arukia kalameni kula kwa demu jirani

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Sunday, April 17  2016 at  14:15

Kwa Muhtasari

TENKWEN, Bomet

KALAMENI wa eneo hili alipata aibu ya mwaka alipozomewa na mkewe baada ya kupatikana akila ugali katika nyumba ya kipusa jirani yao.

 

Inasemekana kuwa mke wa polo alikuwa akitoka sokoni kuuza mahindi, alipomuona mumewe katika nyumba ya kipusa huyo.


Kulingana na mdokezi wetu, mume wa kipusa alikuwa jijini anakofanya kazi na fununu za mtaa zilidai polo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na kipusa huyo.

Inasemekana kuwa polo alijaribu kujificha nyuma ya mlango lakini mkewe alikuwa amemtambua kutokana na mavazi yake. “Nimeona mtu hapa kama bwanangu. Kwani ameingia wapi?” mama alimuuliza kipusa. “Ni kama wewe umeona shetani. Bwanako hayuko hapa,” alijibu kipusa.


Duru zinasema kuwa mke wa polo aliamua kuingia ndani ya nyumba ya kipusa na akampata jamaa. “Na huyu ni nani? Nilikuona ukila chakula hapa. Huna aibu hata kidogo,” mama alianza kumzomea polo.

Njaa
“Ni mara ngapi nimekuuliza kuhusu uhusiano wako na huyu mwanamke kisha unapinga?” mama aliendelea kumuuliza polo. “Mimi nilikuwa na njaa. Singekungoja urudi kutoka sokoni ndio unipikie. Niliona ni afadhali nije nile hapa,” polo alimjibu mkewe.


Kulingana na walioshuhudia kisa hiki, mama alianza kumzomea polo bila kuogopa chochote. “Nani hajui mambo yako na huyu bibi? Unajifanya hapa eti una njaa. Kile chakula nilikupikia kwani umemaliza? Mimi najua huyu ni mpango wako wa kando.”


Inasemekana kuwa watu walianza kufurika eneo hilo. “Kila mtu alishangazwa na maneno ya mke wa polo,” alieleza mdokezi. Polo alishindwa kumkabili mkewe. “Sitaki kukuona tena,” mkewe alisema huku akiondoka.

 

 

Polo mtanashati afanya demu na mdosi wapigane

Na CORNELIUS MUTISYA

Imepakiwa - Monday, April 4  2016 at  09:59

Kwa Muhtasari

KIOJA kilishuhudiwa mjini hapa demu alipotwangana na mke wa mwajiri wake waking’ang’ania barobaro aliyekuwa mteja katika hoteli waliyokuwa wakichapa kazi.

 

Kulingana na mdokezi, mke wa bosi alikuwa keshia katika hoteli ya mumewe huku demu akiwa weita.


Huduma yao mufti ilifanya hoteli hiyo kuvuma mno na kupendwa na makastoma wengi.


“Makastoma walifurika katika hoteli hiyo kwa sababu ya mapishi kibao na huduma ya hali ya juu,’’ akasema mdokezi.


Penyenye zaarifu kwamba, miongoni mwa wateja hao alikuwa barobaro mmoja aliyefanya kazi ya kuuza bima.

Utanashati na upole wake ziliwafanya mama na demu huyo kumtamani japo kwa siri.


Inasemekana kwamba, demu alichota fikira za barobaro huyo na wakawa wapenzi wa chanda na pete. Hata hivyo, mama huyo alipogundua kuwa jitihada zake za kumzuzua barobaro huyo zilikuwa zimegonga mwamba, alikasirika.


Siku ya kisanga, barobaro huyo alifika hotelini mwendo wa saa sita adhuhuri kwa chakula cha mchana. Alikaribishwa kwa furaha na bashasha na demu huyo na wakapiga gumzo kwa dakika kadhaa kabla ya kuagiza maankuli. Mama alikuwa akiwatazama akikereka.


Inasemekana mama alianza kumzomea demu huyo huku akimwambia akomeshe tabia ya kuwasumbua wateja wake. Vurugu zilizuka baina yao nusura wachafuane sura.


“Mama alimzomea demu akimwambia hakuwa na ruhusa ya kuingilia wateja wake,’’ alisema mdokezi.


Kulingana na mdokezi, maji yalizidi unga mwanadada alipomfokea mama huyo na kumwambia alikuwa amezeeka.

na alipasa kuwaachia uwanja na vita vikaanza.


Ilibidi wateja kuingilia kati na kuwatenganisha na kuwashauri haikuwa jambo la busara kuzozana mbele ya makastoma.

 

 

Mke alishwa talaka kwa kupakulia mume chakula cha kitoto

Na HOLINESS MWAMBI

Imepakiwa - Sunday, April 3  2016 at  13:16

Kwa Muhtasari

VOI

JOMBI mmoja wa hapa aliwaacha majirani vinywa wazi kwa kumtaliki mkewe akimlaumu kwa kuwa na mazoea ya kumpakulia ugali ambao hakuweza kushiba.

 

Jombi mmoja wa hapa aliwaacha majirani vinywa wazi kwa kumtaliki mkewe akimlaumu kwa kuwa na mazoea ya kumpakulia ugali ambao hakuweza kushiba.

Jamaa huyo alidai kwamba hakuweza kushiba licha ya kushinda siku nzima akifanya kazi kwa bidii kulisha familia yake.

“Usiku uliotangulia,  alimwamsha mkewe na kumweleza kwamba alikuwa akihisi njaa lakini mama alikasirika na kumpuuza. Alimwambia ikiwa alikuwa na njaa angeingia jikoni kupika,” akasema mdokezi.

Asubuhi ilipofika, jamaa alimwamuru mkewe kufuga virago na kurudi kwao akisema hangevumilia mke asiyeweza kumpikia chakula anachoweza kushiba.

 

 

Aibu kwa mzee wa kanisa baada ya kufichuka alizaa na kiruka njia

Na OSCAR KAKAI

Imepakiwa - Sunday, April 3  2016 at  13:11

Kwa Muhtasari

KAPENGURIA MJINI

KIOJA kilizuka katika kanisa moja mjini hapa mzee wa kanisa alipotupiwa mtoto na mpango wake wa kando ibada ikiendelea.

 

Kisanga hiki kilitendeka mama alipofika kanisani kwa  nia  ya kumuaibisha mzee huyo.

Duru ziliarifu kuwa buda huyo alikuwa amekataa kumsaidia kumtunza mtoto huyo.

Yasemekena kuwa jamaa alikuwa akihepa majukumu kama baba ya mtoto aliyekuwa na umri wa mwaka  mmoja.

Buda huyo alikuwa ameificha familia yake kuhusu suala hilo na ni watu wachache walikuwa wanaelewa.

Mama alienda moja kwa moja alikoketi mzee huyo pasta alipokuwa akihubiri.

“Leo ni leo lazima kanisa lijue mambo ambayo huwa unajificha. Huwezi kuzaa mtoto kisha ukose kulea,”alisema mama aliyejawa na ghadhabu.

Baada ya kukosa msaada kutoka kwa wahudumu wa kanisa hilo, mama aliamua kumrushia mzee mtoto huyo.

Ibada  ilisimamishwa kwa muda huku walinzi wa kanisa hilo wakifika kwa haraka ili kumuokoa mzee huyo.

Ilibidi  walinzi hao kumfurusha mama na mtoto haraka.

Mzee huyo alibaki kimya kwenye kiti huku akijifanya  alikuwa amezama katika maombi.

Kisanga hiki kiliwaacha waumini  vinywa wazi kwa sababu buda huyo ni mmoja wa viongozi wakuu katika kanisa hilo.

Mdaku wetu alituarifu kwamba mama alikuwa amemweleza mke  wa mzee huyo ajiandae kwa  kisanga.

“Mke wa kiongozi huyo ambaye alikuwa kwenye kanisa hilo alitulia na kushindwa la kufanya,” akasema mdokezi.

Ilibidi wazee wa kanisa hilo kuingilia kati na kumueleza mama kuwa watamueleza mzee aweze kuwajibika.

“Mama tulia tutamueleza mzee aweze kutoa msaada kwa mtoto,”mzee mmoja alisikika akisema.

Baada ya kuambiwa hayo, mama aliondoka akiapa kumuonyesha mzee cha mtema kuni.

 

 

Mama azuia mwanawe kuoa muuza-baa mke wa pili

Na CORNELIUS MUTISYA

Imepakiwa - Saturday, April 2  2016 at  14:11

Kwa Muhtasari

Polo wa hapa Lita, Machakos alijipata katika njia panda pale jaribio lake la kuoa mke wa pili lilipotibuliwa na mama yake aliyetisha kumlaani.

 

LITA, Machakos

POLO wa hapa Lita, Machakos alijipata katika njia panda pale jaribio lake la kuoa mke wa pili lilipotibuliwa na mama yake aliyetisha kumlaani.

Kulingana na mdokezi, polo ambaye ameoa na kujaliwa watoto wanne alianzisha uhusiano wa kimahaba na mwanamke mwingine mhudumu wa baa.

Uhusiano wao ulimea mizizi na kujidhibiti mpaka wakaamua kufunga pingu za maisha.

Penyenye zaarifu kwamba, habari za mpango wao wa kuoana zilivuma kote mithili na wazaz, ndugu na marafiki wa polo huyo walipokea habari hizo hisia mseto.

Baadhi yao walimuunga mkono na wengine wakapinga vikali mipango yake.

“Azimio la polo kuoa mke wa pili lilipingwa vikali na wazazi na marafiki na kuungwa na ndugu zake. Wazazi walidai polo kuoa mke wa pili, tena mhudumu wa baa, ilikuwa ni kujiletea balaa,’’ akasema mdokezi.

Mama aapa kumlaani mwana

Inasemekana kwamba, mama ya polo aliposikia habari hizo aliapa kumlaani mwanawe endapo angeendelea na mpango wake na kuoa mke wa pili.

Siku ya tukio, polo alifika nyumbani akiandamana na mwanamke aliyenuia kuoa akikusudia kumjulisha rasmi kwa wazazi wake.

Hata hivyo, mama yake alipowaona, alianza kuwatupia cheche za matusi huku akitisha kumlaani polo.

“Nilikuzaa, nikakulea na kukusomesha. Tayari una mke na watoto wanne nyumbani. Mbona unatusaliti kwa kutaka kuoa mke wa pili, tena mhudumu wa baa?" mama alifoka huku akitisha kuvua nguo zake kwa hasira za mkizi.

Duru zaarifu kwamba, kwa kuchelea kukumbwa na laana za mama mzazi, polo aliamua kukatiza mpango wa kuoa mwanamke huyo, lakini shingo upande na akawaomba wazazi na mkewe msamaha.

 

 

Fundi alishwa makonde kwa kuvalia viatu vya kastoma

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Wednesday, March 30  2016 at  13:38

Kwa Muhtasari

DANDORA, Nairobi

FUNDI mmoja wa viatu mtaani hapa, alijipata pabaya baada ya kupatikana akivaa viatu vya kastoma.

 

Inasemekana kuwa fundi alikuwa akitoka sokoni na akaamua kupitia kwa mama pima alikomkuta polo mwenye viatu akijiburudisha kwa kileo.


“Fundi leo unakaa smati sana. Hiki kiatu kiko chonjo tu sana. Ulikinunua wapi?” polo alimuuliza fundi.


Inasemekana kuwa fundi hakujibu swali hilo. “Badala yake alijaribu kuleta hadithi nyingine ili kukwepa kumjibu polo. Lakini polo aliendelea kumuuliza maswali hadi alipopewa jibu sahihi,” alieleza mdokezi.


“Unasema kiatu hiki ni cha kastoma wako ambaye alikawia kuleta pesa. Na hata mimi nilileta viatu vyangu vinavyofanana na hivi kwako ushone. Sijui kama umemaliza kushona?” polo alimuuliza fundi.


“Mimi huwa sijali. Mtu akileta kiatu kushonewa na akawie kuleta hela, nazitumia tu,” fundi alieleza.


Inasemekana kuwa polo alizidi kuuliza maswali na kuhakikisha kuwa fundi alikuwa amevalia viatu vyake, mzozo ulianza.


“Wewe kichwa chako hakifanyi kazi. Nimekuletea viatu jana kisha baada ya kushona umevivaa,” polo alimzomea fundi.


Kulingana na mdokezi wetu, polo alitaka kumtoa fundi viatu miguuni. “Ebu toa hivyo viatu miguuni mwako haraka. Kama ni pesa zako nakupa saa hizi,” polo alimueleza fundi.


“Njoo nyumbani kwangu utavipata huko. Siwezi kutembea bila viatu hadi kwangu.” fundi alimueleza polo.


Inasemekana kuwa polo hakukubaliana na fundi. “Aliinuka tayari kumzaba makofi lakini watu waliokuwa karibu naye wakamkamata,” alieleza mdokezi.


“Na wewe pia, umezoea tabia mbaya. Viatu vya wateja wako si vyako. Itabidi uwaheshimu,” mzee mmoja alimweleza.
Ilimbidi fundi apotee kabla ya mambo kuharibika zaidi.

 

 

Utingo mdaganyifu akutana na saizi yake

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Monday, March 28  2016 at  12:01

Kwa Muhtasari

DANDORA, Nairobi

UTINGO mmoja alijipata pabaya baada ya kukabwa koo na abiria wa kike aliyekasirika baada ya kugundua kwamba alimdanganya.

 

Kulingana na mdokezi wetu, kabla ya abiria huyo kupanda gari, makanga alimuarifu lingepitia eneo alilotaka kushukia. “Kipusa alishawishika na kuliabiri gari,” alieleza mdokezi.


Inasemekana kuwa njiani, utingo alianza kuchukua nauli kutoka kwa abiria. Ghafla gari lilipiga kona kuelekea sehemu tofauti na alikokuwa akienda kipusa.


“Sasa unanipeleka wapi?” kipusa alimuuliza utingo.


Kulingana na mdokezi, kipusa alipandwa na hasira. “Look at this idiot. Wakati nilipanda hili gari uliniambia nini? Leta pesa zangu hapa haraka,” kipusa alimueleza utingo.


“Kiendacho kwa mganga hakirudi. Kama unataka basi shuka,” utingo alimueleza mwanadada kwa dharau.


Ugomvi baina ya utingo na kipusa uliendelea kushika kasi kipusa akisisitiza kuwa ni lazima arejeshewe nauli yake. 
Inasemekana kuwa gari lilipofika kwenye steji lilisimama ili kuwachukua wateja wengine.


“Kipusa alishuka huku akimvuta polo shati. “Nilikwambia ninaenda wapi? Na hapa ni wapi? Mbona mnapenda kukaa vichwa ngumu hivyo? Leo utajua ya kwamba hata sisi tumezaliwa,” kipusa alimkaripia utingo.


Inasemekana kuwa iliwabidi madereva na makanga wengine kuingilia kati ili kumuokoa jamaa. “Alipopata mwanya wa kutoroka, polo alichomoka mbio bila kuangalia nyuma. Alipomuona utingo akila mbio, naye kipusa aliamua kumfuata unyounyo,” alieleza mdokezi.


Kulingana na mdokezi, watu walishangazwa na mbio ya polo.

“Kama huyu mwanadada anatishia huyu mwanamume, je, ingekuwa vipi kama ni mwanamume aliyekuwa akilalamika? Si mambo yangekuwa mengine,” mzee mmoja ambaye alikuwa katika sehemu ya tukio hili alisema.

 

 

Makalameni wazima ulaghai wa mganga

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Tuesday, March 15  2016 at  12:04

Kwa Muhtasari

Ujanja wa mganga mmoja wa eneo hili la Kitale ulifikia kikomo baada ya kuvamiwa na mapolo wawili kwa kuwalaghai Sh10,000 akidai angemtibu ndugu yao.

 

KITALE MJINI

UJANJA wa mganga mmoja wa eneo hili la Kitale ulifikia kikomo baada ya kuvamiwa na mapolo wawili kwa kuwalaghai Sh10,000 akidai angemtibu ndugu yao.

Inasemekana kuwa mganga alipokea pesa hizo akidai angemtibu ndugu ya mapolo hao ambaye alikuwa akiugua kwa muda mrefu.

Mganga aliwaeleza kwamba ndugu yao alikuwa amerogwa na kwamba wangemfahamu mtu aliyekuwa akimfanyia hivyo. Hata hivyo, licha ya hakikisho la mganga, hali ya mgonjwa iliendelea kuwa mbaya.

Kulingana na mdokezi wetu, mapolo wote walikubali kubuni mbinu itakayotumika kubaini ikiwa mganga huyo alikuwa na nguvu za kutibu.

“Waliamua kubuni kisa cha uongo ambapo walimuendea mganga huyo na kumweleza kuwa mwizi alivunja lango la supamaketi yao na kubeba pesa zote,” alieleza mdokezi.

Mganga alianza kupiga ramli huku akiwaita mababu zake waanze kufanya kazi. Inasemekana kuwa baada ya dakika chache, mganga alisitisha vituko vyake.

“Jinsi nilivyowaambia ugonjwa wa jamaa wenu na mtu ambaye kamfanyia hayo madhambi, ndio jinsi nitawataja wezi wa supamaketi yenu ni akina nani,” mganga aliwaeleza mapolo ambao walikuwa wametega sikio ndi kupata maneno ya mganga kwa ufasaha.

“Wezi walikuwa watano. Na hivyo vitu walichukua watarudisha baada ya siku tatu. Hao wezi hawatoki mbali. Wote ni majirani zenu,” mganga aliwaelezea mapolo.

Uwezo tunao?

“Mzee, leo tumejua siri yako. Wewe ukituangalia, tunaweza miliki supamaketi? Kama kujenga kibanda cha kuuza sukuma wiki hatuwezi, je supa nayo?” mapolo walimuuliza mganga.

“Nimesema Mungu akipenda, mtakuja jenga supamaketi,” mganga aliwaeleza mapolo huku akianza kutetemeka. 

“Tumejua kuwa wewe kazi yako ni kuwahadaa watu. Leo umevuliwa nguo hadharani. Pesa tulizokupa ili umtibu ndugu yetu weka hapa haraka,” mapolo walimuamrisha mganga huku wakimtoa ndani ya nyumba wakimzaba makofi bila huruma.

 

 

Pasta alimwa makonde kwa kurushia mistari kisura wa muumini

Na SAMMY WAWERU

Imepakiwa - Monday, February 29  2016 at  13:40

Kwa Muhtasari

MHUBIRI wa kanisa moja mtaani hapa, nusra ajikatie tikiti ya bure ya kwenda jongomeo alipofumaniwa kwa kidosho na mpenzi wa mwanadada huyo.

 

MAKUTANO, Mwea

Kipusa huyo ni mfuasi wa kanisa la pasta huyo. Yasemekana pasta huyu alikuwa akimezea mate kisura huyo na kila wakati alikuwa akizuru kwake kwa madai ya kumuombea.

“Siku mbili hazingepita kabla pasta huyo kwenda kwa kipusa huyo akisingizia alikuwa akilisha kondoo wake chakula cha kiroho” akasimulia mdokezi.

Licha ya mwanadada kumfahamisha alikuwa na mpenzi aliyetarajia kufunga pingu za maisha naye, pasta alitia masikio pamba  na akaendelea kumtembelea kumrushia mistari ya mapenzi.

Yasemekana siku ya kioja, mhubiri huyo aliaga mkewe akimweleza alienda kutembelea waumini kondoo wake waliohitaji maombi.

Ulikuwa mwendo wa saa mbili za jioni akiwa kwa kipusa na baada ya kuandaliwa chakula, pasta alikariri mistari kadhaa ya Biblia kisha akafichua kilichompeleka kwa kipusa.

“Dada katika Yesu, mimi ni binadamu kama wale wengine. Zaidi ya yote mimi ni mwanamume aliye na hisia za mapenzi na kusema ukweli ninakupenda,” alisema mhubiri huyo na kuanza kumpapasa mwanadada huyo.

Mlango haukuwa umefungwa na mpenzi wa kipusa aliyemtembelea  aliingia bila kubisha na kumfumania  pasta akinyemelea asali yake. 

“Huku ndiko kulisha kondoo wako chakula cha uzima? Huyu ni mke wangu mtarajiwa na uniskie vizuri! Huna hata aibu ukiacha mkeo, pasta mzima kutafuta mpango wa kando,” alichemka polo akimcharaza mtu wa Mungu.

Mhubiri huyo alilazimika kuchana mbuga akiwa na Biblia yake mkononi kuepuka aibu. Inasemekana habari hizo zilimfikia mkewe na wafuasi wake kanisani na haijulikani hatua aliyochukuliwa baadaye.

 

 

Mama aungama kula tunda na shamba-boi

Na CORNELIUS MUTISYA

Imepakiwa - Tuesday, February 16  2016 at  09:55

Kwa Muhtasari

Mama wa hapa aliwaacha wakazi kinywa wazi alipoungama kwamba alizini na shamba boi kulipiza kisasi tabia ya mumewe ya kula uroda na yaya.

 

IVETI, Machakos

MAMA wa hapa aliwaacha wakazi kinywa wazi alipoungama kwamba alizini na shamba boi kulipiza kisasi tabia ya mumewe ya kula uroda na yaya.

Kulingana na mdokezi, mama alikuwa amefumania mumewe na mjakazi wao wakirushana roho sebuleni. Kitendo hicho kilimkasirisha na akaamua siku moja angelipiza kisasi.

Siku ya tukio, mumewe alienda kazini na akamuacha mama watoto nyumbani akitekeleza majukumu yake ya kila siku.

Mama alimualika shamba boi sebuleni na akaanza kumrai wafanye mahaba. Wawili hao walijibwaga juu ya kochi na wakaanza kufanya vituko vyao bila wasiwasi wowote.

Walipokuwa  katika bahari ya mahaba, mumewe alifika ghafla na kupata nyumba ikiwa imefungwa kwa ndani. Alipochungulia  dirishani, hakuamini macho yake aliposhuhudia mkewe akirushana roho na shamba boi,’’ akasema mdokezi.

Inasemekana aligonga mlango kwa nguvu huku akipiga kelele zilizovutia majirani walioshangaa kumpata mkewe na shamba boi wakiburudishana.

Walipojaribu kumtandika shamba boi, mama huyo alimtetea vikali.

“Jameni, msimpige kijana huyu bure. Ni mimi ambaye nilimualika aniburudishe kama vile mume wangu anavyoburudishwa na mbochi wetu. Niliamua kulipiza kisasi,’’ akasema mdokezi.

Penyenye zasema wakazi waliposikia tetesi za mama huyo,  baadhi yao waliangua kicheko na wakamlaumu mumewe kwa kuzoea kula uroda na yaya wao.

Waliwashauri wawili hao kusameheana na kuwa waaminifu katika ndoa yao ili isivuruguke kwa sababu ya uzinzi wao.

Inasemekana jamaa na mkewe  waliamua kusahemehean.

Hata hivyo, shamba boi na yaya walipoteza kazi zao.

 

 

Uganga wazua ngumi kati ya wake-wenza

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Monday, February 15  2016 at  12:48

Kwa Muhtasari

WAKAZI wa eneo hili walitazama sinema ya bure pale wake-wenza walipochapana makonde mmoja alipomlaumu mwenzake kwa kwenda kwa mganga kumzuia mume wao kutembelea  boma lake.

 

NAITIRI, BUNGOMA

Kulingana na mdokezi, mke wa kwanza alimvamia na mke wa pili na kuzua rabsha.

“Njama yako nimeijua. Unawezaje kwenda kwa mganga kumzuia baba ya watoto wangu kuja kwangu? Chunga unacheza na simba. Uliolewa hili boma juzi halafu unaanza kuleta ujuaji,” mke alimfokea mwenzake.

“Najua nilikuja hili boma juzi lakini lazima ujue kuwa kila mtu ana kwake.

Nani alikuambia mimi nilienda kwa mganga?  Haikosi hujui kumtunza mzee na ndio maana hataki kuja kwako,” mke wa pili alimjibu mwenzake.

Malumbano yaliendelea kwa muda.

“Nani alikuambia mimi sijui kumtunza  mume? Wewe ukija hapa,  nilikuwa nimeishi na yeye miaka gapi? Baada ya kukuhurumia na nikakubali uwe mke mwenzangu, unaanza kuniendea kwa mganga? Leo utanijua,”  mke wa kwanza alimuambia mwenzake huku akimrukia.

Penyenye zinasema  kabla ya wanawake hawa kuumizana, mume wao alifika.

“Shida yenu ni ipi? Mbona mwaniletea aibu?” jamaa aliwauliza. 

“Baba boi kabla hiki kinyangarika kuja hapa, tulikuwa tumeishi nawe miaka migapi?” mke wa kwanza alimuuliza mumewe.

“Iweje leo  anaenda kwa mganga ili kukuzuia wewe kuja kwangu? Lazima sasa aniondokee,”pili alimuambia mumewe huku akimzaba mwenzake makofi.

Inasemekana jamaa alishindwa kutatua mgogoro huo. “Ilibidi atoweke majirani walipoanza kukusanyika kwa wingi,” alieleza mdokezi.

Kulingana na mdokezi wetu, iliwabidi majirani kuingilia kati ili kuwatenganisha wanawake hao. Baadaye kila mtu alienda zake huku wakitafakari vituko vya wake wenza hao.

 

 

Polo aangushiwa kichapo kwa kukiri alimramba maiti

Na SAMMY WAWERU

Imepakiwa - Sunday, February 14  2016 at  13:06

Kwa Muhtasari

Kioja kilitokea katika ibada moja ya mazishi mtaani hapa jamaa alipoangushiwa kichapo kikali kwa kufichua kwamba marehemu alikuwa mpango wake wa kando licha ya kuwa mke wa mtu.

 

NDUNYU NJERU, Nyandarua

KIOJA kilitokea katika ibada moja ya mazishi mtaani hapa jamaa alipoangushiwa kichapo kikali kwa kufichua kwamba marehemu alikuwa mpango wake wa kando licha ya kuwa mke wa mtu.

Yasemekana jombi alikuwa rafiki wa karibu wa mume wa mama aliyefariki.

“Mume wa marehemu alishangaa kugundua rafiki yake alikuwa akichovya asali yake,” akasema mdokezi.

“Wakati  mume wa marehemu alipokuwa akipigwa picha karibu na jeneza la marehemu mkewe, kalameni alitokea na kujiunga naye akisema ilikuwa hatua ya kumfariji,” alisimulia mdokezi.  Kitendo chake hicho kilishtua waombolezaji kwa sababu hakikuwa cha kawaida.

Wakati wa kutoa rambirambi, kwa jamaa na marafiki, polo aliomba nafasi.

“Nina huzuni mwingi kwa kumpoteza marehemu aliyelala hapa. Jamaa zake mpokee pole zangu. Kwa kweli hakuwa rafiki tu, bali alikuwa mpango wangu wa kando.

Naomba radhi kwa mumewe, ninafahamu hakujua uhusiano uliokuwepo kati yetu,” alisema polo.

Kalameni alipoweka maikrofoni chini, mume wa marehemu alimrukia na kumkaba koo huku  akimuangushia mangumi na mateke.

“Leo utanieleza sababu ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wangu,” mume wa marehemu alichemka.  Kwa dakika kadhaa, ibada ya mazishi iligeuka kuwa uwanja wa vita polo akicharazwa.

Kalameni aliokolewa na pasta aliyeongoza ibada hiyo na waombolezaji waliomsihi mumewe kumsamehe.

“Neno la Mungu kwenye Biblia linasema tusamehe mara saba kwa sabini na jua lisitue kabla hatujasamehe waliotukosea ili tuweze kuurithi ufalme wa Mungu” alisema pasta huyo.

Kizaazaa hicho kilitulia na ibada akaendelea polo akishauriwa kuheshimu ndoa za watu.

 

 

Pasta na polo vitani waking'ang'ania mjane

Na SAMMY WAWERU

Imepakiwa - Thursday, February 11  2016 at  12:34

Kwa Muhtasari

Sinema ya bure ilishuhudiwa kwenye boma moja mtaani hapa pasta na kapera walipolishana makonde waking’ang’ania mjane.

 

GATUNG’ANG’A, Nyeri

SINEMA ya bure ilishuhudiwa kwenye boma moja mtaani hapa pasta na kapera walipolishana makonde waking’ang’ania mjane.

Mama huyo ni mshirika wa kanisa analohudumu pasta huyo na yasemekana tangu afiwe na mumewe miezi sita iliyopita, mhubiri huyo alikuwa akimtembelea mara kwa mara.

Duru zinaarifu kwamba kapera huyo pia alikuwa akipiga kambi kwa mama huyo. “Wote walikuwa na lengo la kumnasa mjane huyo na kuanza uhusiano wa kimapenzi” alisema mdokezi.

Minong’ono inaarifu pasta alikuwa akimtembelea jamaa akidai alitaka kumfariji. “Barobaro naye alikuwa akipata pasta akimhubiria mjane japo hakudhani alikuwa akimmezea mate,” alieleza mdokezi.

Inasemekana siku ya kioja pasta alimtembelea mama huyo jioni na akaandaliwa chakula. Baada ya chakula, wawili hao walizama katika mahaba kwenye kochi sebuleni.

Hawakujua kuwa kapera angefika kwa mjane huyo siku hiyo.

Jamaa alipigwa na butwaa kupata pasta  akimpokeza mabusu moto moto. Kwa hasira, alimporomoshea pasta mangumi na mateke.

“Haya ndiyo mahubiri ambayo huwa unayaleta hapa? Huwezi tulia kwa mkeo? Huyu mama achana naye, tena kaa mbali kabisa, yeye ni mali yangu. Nimemsimamia tangu afiwe na mumewe,” alichemka kapera.

“Hei, koma hapo, nani alikueleza pasta hana hisia za mapenzi? Nimekuwa nikimlisha chakula cha kiroho na sasa anahitaji cha mwili,” alifoka pasta.

Yasemekana mama huyo alipiga kamsa zilizoalika watu wakaenda kuwatenganisha.

Walioshuhudia kisanga hicho waliachwa midomo wazi na baadhi wakaangua kicheko. Wawili hao walifurushwa kwa mama huyo na haikujulikana ikiwa walirudi kwake tena.

 

 

 

Weita atiwa adabu kwa kuwapora walevi

Na CORNELIU MUTISYA

Imepakiwa - Thursday, February 11  2016 at  12:51

Kwa Muhtasari

Mhudumu wa baa katika soko hili aliamua kumkubali Yesu kuwa mwokozi wa maisha yake alipopokezwa kichapo na walevi walipogundua hila yake ya kuwaongezea bili kila wakati wakilewa chakari.

 

KITHUNGUNI, MACHAKOS

MHUDUMU wa baa katika soko hili aliamua kumkubali Yesu kuwa mwokozi wa maisha yake alipopokezwa kichapo na walevi walipogundua hila yake ya kuwaongezea bili kila wakati wakilewa chakari.

Kulingana na mdokezi, kipusa huyo alizoea kuwaongezea walevi bili ya pombe akinuia kuwalaghai hela.  Hakuogopa kuchomoa pesa kutoka kwa mifuko ya wateja wake wakilewa chopi.

“Alizoea kuwatapeli walevi hela zao. Kwa kuwa tabia ni mazoea, aliendelea kuwalaghai makastoma hadi wakapungua,’’ akasema mdokezi.

Inasemekana kwamba, sifa zake mbovu  zilizagaa kote na walevi wakapanga njama ya kumkomesha. Waliamua kujivinjari katika baa hiyo na wakamrai mmoja wao aanze kusinzia akijifanya amelewa chakari.

Duru zaarifu kipusa huyo alipoona jamaa alikuwa akisinzia, alimpelekea risiti aliyoongezea Sh 1,000 juu ya bili yake.

Walevi walikasirika na wakampokeza kichapo kabla ya kuokolewa na mwenye baa aliyefika mara moja aliposikia kelele.

Kufuatia kisa hicho, mwanadada huyo aliacha kazi ya kuuza baa na akaokoka. Kwa wakati huu, yeye ni mwanakwaya shupavu katika kanisa moja la kiroho eneo hili na kiongozi wa kikundi cha wanarika.

 

 

Mpangaji ajipata bila makazi asubuhi kwa kudharau landilodi

Na STEPHEN DIK

Imepakiwa - Thursday, February 11  2016 at  12:53

Kwa Muhtasari

Polo alifukuzwa katika ploti aliyokuwa akiishi baada ya kumrushia landilodi kodi ya nyumba alipoenda kumdai.

 

NDERE, Siaya.

Polo alifukuzwa katika ploti aliyokuwa akiishi baada ya kumrushia landilodi kodi ya nyumba alipoenda kumdai.

Landilodi alimwendea jamaa asubuhi kudai kodi lakini badala ya jamaa kumkabidhi alimrusha chini akisema hangempatia kwa mkono sababu alienda kumdai asubuhi.

“Jamaa alimwambia landilodi kuchukua pesa zake na kuondoka, kisha akaingia ndani ya nyumba na kujifungia,” akasema mdokezi.

Kitendo hiki kilimuudhi sana landilodi ambaye aliokota pesa hizo na kumwambia jamaa ahame.

Landilodi alisimama mlangoni kwa mshangao na kupaza sauti akimwambia jamaa hakutaka kumuona katika ploti yake.

Alimwambia jamaa kwamba hangevumilia tabia yake aliyotaja kama dharau.

 

 

Apokonywa mkewe kilabuni na jamaa mwenye mfuko mzito

Na STEPHEN DIK

Imepakiwa - Thursday, February 11  2016 at  13:10

Kwa Muhtasari

Jombi alijuta baada ya kupokonywa mke na mwanamume mwingine alipoandamana naye kujivinjari katika kilabu maarufu mjini hapa.

 

WUNDANYI MJINI

KALAMENI alijuta baada ya kupokonywa mke na mwanamume mwingine alipoandamana naye kujivinjari katika kilabu maarufu mjini hapa.

Yasemekana mke wa jombi alikuwa mrembo na kila mtu aliyemuona alimmezea mate.

Kipusa huyo pia alipenda wanaume wenye pesa na alipofika katika kilabu hicho alichotwa na mwanamume aliyejaliwa kipato kikubwa na akamtema mumewe.

Alimwambia mumewe kwamba hakuwa na maana kwake na aliamua kuolewa na mtu ambaye atakidhi mahitaji yake yote. Licha ya mumewe kumrai asimuache, mwanadada huyo alikataa kumsikiliza.

Jombi alisikika akitisha kumshtaki jamaa aliyemnyang’anya mkewe.

 

 

 

 

Mwanadada pabaya kutumia pasta SMS ya mapenzi

Na CORNELIUS MUTISYA

Imepakiwa - Tuesday, February 9  2016 at  09:40

Kwa Muhtasari

Kizaazaa kilizuka eneo hili la Kauti, Kathiani mke wa pasta wa Kanisa moja alipojawa na hasira za mkizi na kumcharaza muumini wa kike kwa kumtumia mumewe arafa ya mapenzi.

 

KAUTI, Kathiani

KIZAAZAA kilizuka eneo hili la Kauti, Kathiani mke wa pasta wa Kanisa moja alipojawa na hasira za mkizi na kumcharaza muumini wa kike kwa kumtumia mumewe arafa ya mapenzi.

Kulingana na mdokezi, mwanamke huyo alikuwa kiongozi wa kwaya ya Kanisa hilo.

Hata hivyo, alikuwa akimmezea mate pasta na majuzi aliamua kumtumia ujumbe katika simu yake akimweleza anavyompenda.

“Mwanamke huyo alikuwa akimtamani pasta wake japo kwa siri. Alishindwa kabisa kumweleza hisia zake hadi majuzi alipoamua kumwandikia ujumbe wa mapenzi,’’ akasema mdokezi.

Inasemekana mke wa pasta alichukua simu ya mumewe kuwasiliana na jamaa zake, aliposikia ujumbe ukiingia kwa simu na akausoma.

Alishangaa kusoma ujumbe huo uliokuwa wa mapenzi.

Alikasirika mno na akamsaka mwanamke huyo ili amfundishe tabia.

“Mke wa pasta aliamua kumsaka mwanamke huyo mitaani ili amfundishe adabu kwa kujaribu kupindua serikali yake. Alimpata katika saluni moja sokoni hapa na ugomvi ukazuka baina yao,’’ akasema mdokezi.

Haki

Inasemekana mke wa pasta alipomuuliza mwanamke huyo sababu ya kumtumia mumewe arafa ya mapenzi, alimpuuza akimwambia alikuwa na haki ya kuwasiliana na yeyote kwa sababu hana mume.

Mke wa pasta alijawa na mori na akamparamia mwanamke huyo mithili ya simba marara.

“Vita viliuma mchanga kati ya mke wa pasta na muumini huyo. Wapita njia walijaribu kuwatenganisha lakini juhudi zao ziliambulia patupu,’’ akasema mdokezi.

Tunaarifiwa kwamba, pasta alipashwa habari kuhusu rabsha hiyo na akafika mara moja na kuwatenganisha.

Hata hivyo, mkewe alianza kumtupia cheche za matusi akimwita mzinifu nambari moja na akatisha kumtaliki.

Kwa bahati, wazee wawili wa kanisa walifika na wakawashauri wakasuluhishe mambo yao nyumbani badala ya kumwaga mtama kwenye kuku wengi.

Dondoo za Hapa na Pale ni visa vinavyojiri kila siku sehemu tofauti nchini na kimataifa. Tuma habari kwa:dondoo@ke.nationmedia.com / taifa@ke.nationmedia.com au swahilihub@ke.nationmedia.com

 

 

Akamatwa akiruka ua wa jirani usiku

Na MWANDISHI WETU

Imepakiwa - Thursday, February 4  2016 at  18:26

Kwa Muhtasari

Siku ya arobaini ilifika kwa polo wa eneo hili la Makongeni, Thika alipokamatwa akijaribu kuruka ua kuingia kwa jirani kuwanyemelea mabinti usiku.

 

MAKONGENI, Thika

SIKU ya arobaini ilifika kwa polo wa eneo hili la Makongeni, Thika alipokamatwa akijaribu kuruka ua kuingia kwa jirani kuwanyemelea mabinti usiku.

Kulingana na mdokezi, jirani ya polo alikuwa akilalamika kwamba kulikuwa na mtu aliyekuwa akiingia kwake wakati wa usiku na kuwaita binti zake kwa majina.

“Kila usiku, huwa ninasikia sauti ya mtu ikiitana nje ya nyumba. Huyo mtu huwa ni nani?” mwenye boma aliwauliza binti zake.

Inasemekana vipusa hao walimwambia baba yao kwamba pia wao walikuwa wakisikia sauti za mtu huyo.

“Dadi hata sisi humsikia tu. Lakini hatumjui,” mabinti walimjibu baba yao.

“Leo lazima atarudi na atanipata. Na sijui yeye hupita wapi,” mzee alisema huku akiapa kumnasa jombi huyo.

Inasemekana kuwa aliamua kumwekea polo mtego kwa kujificha kando ya ua la nyumba yake.

“Saa za polo kuruka ua zilipofika alikunja suruali yake tayari kupanda ua la boma ya jirani yake bila kujua alikuwa amewekewa mtego. Kabla ya polo kuruka upande ule mwingine, alikamatwa na mwenye boma,” alisimulia mdokezi.

Mbona wanyemelea wanangu?

“Kwani ni wewe? Mbona unawanyemelea wasichana wangu? Mbona usiwaongojee huko nje mchana badala ya kuwanyemelea usiku?” mzee alimkaripia polo.

“Haki nisamehe, huwa ninatamani kuzungumza nao,” polo alijitetea lakini mzee aliendelea kumkaripia. “Nilikuwa nikifikiria kuwa wewe ni jirani mwema. Kumbe kikulacho ki nguoni mwako. Una bahati sana. Ningekumaliza saa hizi,” mzee alimweleza polo .

Inasemekana kuwa mzee aliwaita binti zake kumuona mgeni wao wa kila usiku.

“Potea hapa kabisa. Siku nyingine nikikuona kwa hili boma langu hata kama ni mchana, utakiona,” mzee alimweleza polo ambaye alitimka mbio bila kuangalia nyuma.

 

 

Jombi mpenda chupa ala viboko kutelekeza

Na SAMMY WAWERU

Imepakiwa - Wednesday, February 3  2016 at  13:08

Kwa Muhtasari

Buda wa hapa Ngandu, Nyeri alijuta baada ya kuchapwa vikali na mkewe kwa kukosa kufika mbele ya kikao cha wazee wa kijiji.

 

NGANDU, Nyeri

BUDA wa hapa Ngandu, Nyeri alijuta baada ya kuchapwa vikali na mkewe kwa kukosa kufika mbele ya kikao cha wazee wa kijiji.

Yasemekana jamaa huyo alikuwa amezembea katika kutelekeza majukumu kama mume na kiongozi wa familia yake.

“Mkewe ndiye aliyeachiwa majukumu yote ya familia,” mdokezi alieleza. Penyenye zasema jamaa alikuwa amezama kwenye mvinyo na mkewe alikuwa akilalamika kila mara.

“Mimi nimeolewa na pombe, wanawake hawana faida kwangu” kalameni alikuwa akisema akitoka kwa mama pima.

Mkewe alichoshwa na tabia ya mumewe akifahamu walikuwa na mtoto anayefaa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu.

Aliamua kumfikisha mbele ya kikao cha wazee wa kijiji. Jamaa alitumiwa ilani ya kufika barazani. Siku ya kikao, polo alirauka jogoo wa kwanza akiwika na kufahamisha mkewe kuwa angefika kikaoni.

Alifululiza hadi kwa mama pima ili kujiburudisha. Mkewe alijitayarisha na kuelekea kikaoni akitarajia mumewe angehudhuria.

Saa ziliyoyoma na dalili za jombi kuwasili hazikuonekana. Simu ya kalameni ilipopigwa, alikuwa ameizima. Mama huyo aliomba wazee hao ruhusa akamsake mumewe na akaelekea kwa mama pima ambapo alimpata jamaa akiwa mlevi chakari.

“Mwanamke ulidhani kunifikisha kwa wazee wa kijiji ndiyo dawa? Niachie raha zangu,” alifoka jombi.

Gumegume lacharazwa

Mkewe alighadhabishwa na matamshi ya gumegume lake ndiposa akaanza kulicharaza vilivyo.

“Leo utatambua mimi ni huyo mwanamke unayetaja. Utakuwa ukitekeleza majukumu yako bila kuelezwa,” alichemka mama huku akimcharaza. Marafiki wa jamaa walimuunga mama huyo.

“Asidhani akituona hapa huwa hatushughulikii familia zetu, maslahi ya familia kwanza, mengine baadaye,” alisema buda mmoja.

Haikufahamika mzozo wao ulifikia wapi polo alipoagizwa na wenzake kuondoka kwenda kushughulikia majukumu ya familia yake.

 

 

Demu amchemkia polo kwa kumtongoza hadharani

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Tuesday, February 2  2016 at  15:03

Kwa Muhtasari

Umachachari wa polo wa hapa ulimtia mashakani alipozomewa na kidosho kwa kufanyia mzaha maumbile yake ya kuvutia.

 

SIREMBE, SIAYA.

UMACHACHARI wa polo wa hapa ulimtia mashakani alipozomewa na kidosho kwa kufanyia mzaha maumbile yake ya kuvutia.

Kulingana na mdokezi, kipusa huyu alipita mbele ya mapolo wanne ambapo mmoja alivutiwa na maumbile yake.

“Madamu, si huyu amenimaliza na hizo 'fundamentals’ zake. Beib, can I escort you please?” polo  alimuuliza kidosho. Inasemekana kipusa alisimama na kumuangalia polo.

“Unaweza kurudia uliyotamka sasa hivi,” kipusa alimuuliza polo kwa ukali.

“Enyewe uko chonjo tu sana. Nataka tu kuandamana na wewe,” polo alimueleza kipusa huku wenzake wakicheka .

“Ni mimi unaita fundamentals?” kipusa alimuuliza polo naye jamaa akaendelea kumjibu.

“Madam usikasirike. Kusema kweli umezibeba poa,” polo alimueleza kidosho.

Jibu hilo lilimfanya  kidosho kupandwa na hasira na kuanza kumzomea polo.

“Wewe ni mjinga sana. Umeamua kuja hapa kuwapa watu majina?  You must be a very big idler. Mshenzi wewe,” kipusa alimzomea polo. Kulingana na mdokezi, polo alinyamaza kwa sababu kipusa hakumpa ruhusa ya kuongea tena.

“Watu walianza kukusanyika eneo la tukio hili kila mmoja akitaka kujua kilichokuwa kikiendelea,” alieleza mdokezi.

“Angalieni huyu mjinga. Mimi nilikuwa nikipita kisha akaanza kuniita fundamentals. I don’t like that nonsense,” kipusa alieleza umati.

Kwa mujibu wa mdokezi, kipusa aliamua kumpa polo onyo kali sana. “Wewe sikia kuanzia leo, nikisikia tena ukilitamka hilo neno, utajua kilichomnyoa kanga manyoya shingoni,” kidosho alimueleza polo.

Inasemekana kuwa polo na wenzake waliamua pia kutoweka. “Wewe endelea kupayuka. Ukimaliza au ukichoka, nenda kwenu,” polo alimueleza kipusa huku akienda.

“Kipusa naye aliamua kuendelea na safari yake.” alieleza mdokezi.                  

 

 

Agutushwa na makofi ya mkewe kwa kulowesha kitanda

Na SAMMY WAWERU

Imepakiwa - Tuesday, February 2  2016 at  15:23

Kwa Muhtasari

Kalameni wa hapa anajuta baada ya kupokezwa kichapo kikali na mkewe kwa kwenda haja ndogo kitandani.

 

MUGOIRI, MURANGA

KALAMENI wa hapa anajuta baada ya kupokezwa kichapo kikali na mkewe kwa kwenda haja ndogo kitandani.

Yasemekana polo huwa na vituko anapolewa kiasi cha kukojoa kitandani. “Jamaa anapolewa, huwa hawezi  kuzuia mkojo wake,” alisema mdokezi.

Minong’ono inaarifu kwamba mkewe hulazimika kufua malazi ambayo jamaa hulowesha.

“Kila wakati kalameni akipitia kwa mama pima, huenda haja ndogo kitandani na akiulizwa na mkewe huwa mkali,” alisimulia mdokezi. Siku ya kioja yasemekana kalameni alishinda  kwa mama pima.

Alifika kwake mwendo wa saa nne za usiku akiwa chakari. Baada ya chakula, alijilaza kitandani na kuzama kwenye usingizi.

Mwendo wa saa nane za usiku  aligutushwa na makofi mazito aliyoangushiwa na mkewe alipogundua  alikuwa amelowesha kitanda kwa mkojo.

“Wewe umekuwa mtoto wa kukojoa kitandani ovyo ovyo? Una tofauti gani na  watoto jamani? Huna hata aibu ukikojoa kitandani mzee mzima kama wewe!

Leo utanitambua na kamwe sitavumilia tabia kama hii,” alichemka mama huyo akimuangushia kichapo kikali.

Kulingana na mdokezi, wiki mbili sasa zimepita buda hajaonekana kwa mama pima tena.

Yasemekana kwamba huwa anaonekana akishughulika shambani na kutunza mifugo wake.

 

 

Binti azomewa na kina mama kwa kutovaa sidiria

Na GRACE KARANJA

Imepakiwa - Monday, February 1  2016 at  12:52

Kwa Muhtasari

Demu mmoja mtaani hapa alijipata pabaya, akina mama walipomuaibisha mbele ya umma wakidai alikuwa na mazoea ya kutovalia sidiria.

 

DANDORA, NAIROBI

DEMU mmoja mtaani hapa alijipata pabaya, akina mama walipomuaibisha mbele ya umma wakidai alikuwa na mazoea ya kutovalia sidiria.

Yasemekana haikuwa mara ya kwanza akina mama hao kumuonya binti huyo dhidi ya kutovaa vizuri lakini hakutilia maanani onyo hilo.

Walisema tabia ya mwanadada huyo ilikuwa ikiwaaibisha wanawake na hawangekubali kudharauliwa na wanaume. Baadhi walisema kipusa huyo alikuwa na nia mbaya.

Asubuhi ya kisanga, demu alienda dukani alipokutana na akina mama wawili waliomlazimisha kurudi kwake kuvalia sidiria lakini akawadharau akisema mavazi yake hayakuwahusu.

“Mimi nikikosa kuvalia sidiria inawahusu nini, haya ni maisha yangu, niacheni niishi ninavyotaka,” demu aliwajibu kwa dharau akina mama.

Majibu hayo yaliwakera sana akina mama hao na wakamgeukia demu kana kwamba walitaka kumvua nguo wamwache uchi.

“Kama hutaki kuvalia vizuri itakubidi uhame hapa kama sivyo wacha tukuvue hii nguo ya juu utembee hivyo watu wakuone vizuri,” akina mama waliojawa na ghadhabu walimwambia demu. Hata hivyo, mwanadada huyo hakushtushwa na vitisho vyao.

Kulingana na mdokezi masaibu ya demu yalizidi  akina mama wengine walipofika na kuelezwa kilichokuwa kikiendelea na wakawaunga  mkono wenzao wakimwambia demu kwamba ni kwa manufaa yake kuvaa vizuri.

Hata hivyo, walipinga hatua ya kutaka  kumvua nguo mwanadada huyo wakisema ni tendo la uhalifu na wanaweza kushtakiwa kwa kufanya hivyo.

“Heri tumuache kwa sasa kisha akubali kuacha  shughuli zake arudi akavalie sidiria. Sio vizuri kumvua mtu nguo. Mnaweza kufungwa jela kwa kufanya hivyo,” alisema mama aliyemwonea huruma demu huyo.

Kulingana na mdokezi, demu alitimka mbio asionekane tena eneo hilo la kisanga.

 

 

Jombi alishwa mijeledi na chifu kwa kumbeza

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Friday, January 29  2016 at  11:34

Kwa Muhtasari

Kalameni aliyejidai jasiri zaidi alijipata pabaya baada ya kumtusi chifu wa eneo hili.

 

NYASERO, NYAMIRA

KALAMENI aliyejidai jasiri zaidi alijipata pabaya baada ya kumtusi chifu wa eneo hili.

Inasemekana kuwa polo alianza kumtusi chifu alipomuita ofisini baada ya kupata malalamishi  kutoka kwa wakazi kwamba alikuwa 'akiwaharibu’ wasichana wao.

“Nimekuita hapa ili unieleze ikiwa madai niliyoyasikia kukuhusu ni ya kweli,” chifu alimueleza polo.

Hata hivyo, polo hakushtushwa na maneno ya chifu.

Inasemekana kuwa baada ya chifu kumfafanulia madai yote, polo alianza kupandwa na hasira.

What is the problem with that? Mlitaka nimtafute wapi mchumba? Hata mwenye kuleta kesi kama hiyo kwako hana aibu hata kidogo. Kwani alitaka kumuoa msichana wake?” polo alimuuliza chifu kwa hasira.

“Kwanza si huyo pekee yake. Kuna wengine wawili ambao walileta malalamishi kama hayo tu. Wote wanadai kuwa wewe unawaharibu wasichana wao ilhali wangali wanasoma,” chifu alimueleza polo.

“Kwani hauna kesi nyingine ya kusikiza? Tafuta kesi kubwa ya kusikiza. Jina lako ni kubwa sana kuliko hii kesi yangu. Acha aibu ndogondogo bwana chifu. Kama huna kazi nitakutafutia,” jamaa alimueleza chifu.

Inasemekana kuwa chifu pia alipandwa na hasira na kuanza kumzomea polo ila polo akamzima.

“Wewe ni mjinga sana. Hayo madai si ya kuniita hapa,” polo alimzomea chifu huku akiondoka.

“Sasa umeamua kunitusi? Unanidharau sasa? Basi tuone nani ataumia!” chifu alifoka.

Kulingana na mdokezi wetu, chifu aliwaita polisi tawala wake. “Nao polisi walifika kwa haraka sana ambapo walimpata polo akiwa bado anamrushia chifu cheche za matusi. Polisi walimweka pingu na kumuelekeza kituoni,” alisimulia mdokezi.

Inasemekana polo alipewa viboko visivyohesabika. “Aliapa kutorudia makosa hayo,” alieleza mdokezi.

 

 

Purukushani polo akilazimishwa kumpenda mkewe

Na GRACE KARANJA

Imepakiwa - Friday, January 29  2016 at  11:27

Kwa Muhtasari

Rabsha zilizuka katika boma eneo hili, jamaa alipolazimishwa na wazazi wake kuandamana na mkewe mjini baada ya kumtelekeza mashambani.

 

NDITHINI, THIKA

RABSHA zilizuka katika boma eneo hili, jamaa alipolazimishwa na wazazi wake kuandamana na mkewe mjini baada ya kumtelekeza mashambani.

Kulingana na mdokezi, jamaa hufanya kazi mjini na ni nadra sana kumtembelea mkewe mashambani.

“Tangu aoe alimuacha mkewe ocha, hamjali na alimaliza mwaka bila kumtembelea,” mdokezi alieleza.

Yasemekana  majuma mawili kabla ya tukio, mkewe alimpigia simu na kumfahamisha nia yake ya kutaka kumtembelea mjini lakini jamaa alikataa.

Hapo ndipo mkewe alipochukua hatua ya kuwaeleza wakwe zake.

“Mimi nimechoka kukaa hapa peke yangu. Ikiwa sikuolewa kama wanawake wengine nijulishwe mapema. Mpigieni simu mwana wenu aje kunichukua na kama hatafanya hivyo nitaenda zangu,” mwanadada alisema.

“Usiwe na hofu hata mimi siwezi kukubali ndoa kama hiyo. Nilipomuoa huyu mama yako sikumwachia wazazi wangu. Nilikwenda naye popote pale nilikuwa nikifanya kazi. Niachie hayo nitasuluhisha,” baba mkwe alimtuliza mwanadada.

Inasemekana kuwa, jamaa alipigiwa simu na baba yake na kufahamishwa aende nyumbani haraka iwezekanavyo kushughulikia  jambo la dharura.

Alipofika nyumbani hakuamini alipogundua kwamba lililokuwa la dharura ni takwa la mkewe.

“Baba mimi huwezi kunilazimisha kumbeba mke hadi mjini, gharama itakuwa juu sana,”  jamaa alijaribu kujitetea.

Hata hivyo wazazi wake hawakumpa nafasi mbali walimwambia ikiwa hangeenda na mkewe  mjini, amtaliki mara moja.

“Mimi sina haja na mke mwingine, nilitosheka na mama yako. Kama huendi na huyo wako, mrudishie wazazi wake mara moja na ujue kwamba hutaoa mwingine umlete hapa,” jamaa alionywa vikali na baba yake.

Kulingana na mdokezi, jamaa hakuwa na budi ila kurudi na mkewe mjini ingawa shingo upande.

 

 

Atwangwa kwa kupatikana ndani ya mzinga wa rafiki yake

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Friday, January 29  2016 at  11:17

Kwa Muhtasari

Kalameni wa hapa nusura ajikatie tiketi ya bure  kwenda ahera alipofumaniwa akichovya asali ya mke wa rafiki yake.

 

GITHURAI 45, NAIROBI

KALAMENI wa hapa nusura ajikatie tiketi ya bure  kwenda ahera alipofumaniwa akichovya asali ya mke wa rafiki yake.

Jamaa huyo ni mhudumu wa teksi mtaani hapa. Kulingana na mdaku,  polo alifurusha mkewe miezi minne iliyopita ili aweze kuwa na uhusiano haramu wa kimapenzi na mama huyo.

Duru za kuaminika zinasema mke wa polo na mama huyo walikuwa marafiki wakubwa kabla ya kufurushwa. Hata hivyo, hakujua kwamba mumewe alikuwa akimnyemelea rafiki yake.

“Mke wa jamaa hakujua kilicho mla kilikuwa nguoni mwake,” alisimulia mdokezi wetu.

Minong’ono inasema kwamba  jamaa alitahadharishwa na watu aepuke uhusiano na mwanadada huyo lakini hakusikia la mwadhini wala la mteka maji msikitini.

Siku ya kioja, mwendo wa saa kumi na mbili hivi za jioni, kalameni alimualika mpango wake wa kando alikoegesha teksi yake na wakazama kwenye raha zao.

Yasemekana mume wa  mama huyo alifika nyumbani na kumkosa mkewe na alimpigia  simu  hakuijibu.

Aliamua kwenda kumsaka mkewe sokoni na kwa bahati jirani mmoja alimdokezea kwamba alimuona akiingia teksi ya polo.

Inasemekana kuwa alielekezwa polo alikoegesha teksi yake na kumpata akimumunyana na mkewe. “Polo aliangushiwa kichapo. Alipohisi mauti yakibisha hodi, alipiga magoti na kuomba msamaha,” akasema mdokezi.

“Ulifukuza mkeo ili uharibu wanawake wa wenyewe? Leo nitakufunza adabu iwapo hukufunzwa na mama yako ?”kalameni alichemka akihema kwa hasira huku mkewe akitimka mbio kama swara.

Polo aliokolewa na maafisa wa polisi waliopigiwa simu na watu waliofika kujionea sinema hiyo ya bure. Hadi wakati mdokezi alipotoka kwenye eneo la kioja hicho hakuna aliyejua alikoelekea mwanadada huyo mgawa asali.

 

 

Polo amtandika mkewe kwa kupeleka hela kwao kisiri

Na  TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Tuesday, January 26  2016 at  14:10

Kwa Muhtasari

Kizaazaa kilizuka eneo hili baada ya polo kumwadhibu mkewe alipogundua kwamba alipeleka pesa alizonuia kujenga nyumba kwao kisiri.

 

GATUNDU, KIAMBU.

KIZAAZAA kilizuka eneo hili baada ya polo kumwadhibu mkewe alipogundua kwamba alipeleka pesa alizonuia kujenga nyumba kwao kisiri.

Penyenye zasema polo alimpa mkewe pesa hizo aziweke akiwa na mipango ya kuongeza zingine ili ajenge nyumba.

Lakini baada ya muda, polo aliona mienendo ya mkewe ikibadilika jambo

lililomtia wasiwasi mwingi sana.

Jamaa alimwambia mkewe ampe pesa hizo ili aanze kupanga mradi wake.

“Mama watoto ebu nipe zile pesa. Ninataka kumuita fundi juma lijalo ili aanze ule mradi niliokuambia,” polo alimueleza mkewe.

Duru zinasema mkewe  hakutoa pesa na akaamua kumweleza  mumewe ukweli kwamba alimpa mama yake pesa hizo.

“Unasema pesa ulimpelekea mama yako? You are jocking. Nakupa nusu saa uniletee hizo pesa. Kimbia kwenu uzilete,” polo alimwamuru mkewe.

“Kwani watu wa kwetu pia hawawezi kula chako? Acha kukaa mkono gamu. Hizo pesa zitatumika kama mahari,” mwanadada alimweleza mkewe.

Inasemekana polo alipandwa na hasira. “Eti mahari? Kwa hivyo hii nyumba ikianguka tutaenda kuishi kwenu?” polo alimuuliza mkewe kwa hasira.

Kulingana na mdokezi, jamaa alianza kumzaba mkewe makofi.

“Nimekwambia ukimbie kwenu uniletee pesa, alafu unaniangalia. Nataka pesa saa

hizi,” polo alimfokea mkewe.

Inasemekana mkewe  aliamua kulia kwa sauti na kuwavutia majirani.

“Mimi najikaza ili nimpe mke wangu maisha mazuri kisha nikimpa pesa aweke, anapeleka kwa wazazi wake  eti hiyo ni kama mahari. Tangu lini wanawake wakaanza kutoa mahari?” polo aliuliza majirani kwa hasira.

Kila mtu alibaki akicheka tu na kuwaacha wawili hao kusuluhisha mambo yao.

Mwishowe mwanadada alilazimika  kwenda kwao na haikufahamika ikiwa alimrudishia  mumewe pesa zake.

Dondoo za Hapa na Pale ni visa vinavyojiri kila siku sehemu tofauti nchini na kimataifa. Tuma habari kwa:dondoo@ke.nationmedia.com/ taifa@ke.nationmedia.com au swahilihub@ke.nationmedia.com   

 

 

Mbunge achomolewa pochi akipanda jukwaani

Na BENSON MATHEKA.

Imepakiwa - Tuesday, January 26  2016 at  14:13

Kwa Muhtasari

Mbunge mmoja nusura atokwe na machozi wachomozi walipotoweka na pochi lake alipokuwa akipanda jukwaani kujiunga na wanasiasa wenzake wakati wa mkutano wa hadhara.

 

MACHAKOS  MJINI

MBUNGE mmoja nusura atokwe na machozi wachomozi walipotoweka na pochi lake alipokuwa akipanda jukwaani kujiunga na wanasiasa wenzake wakati wa mkutano wa hadhara.

Mkutano huo uliohudhuriwa na vinara wa upinzani ulivutia umati mkubwa uliozunguka jukwaa.

Ni wakati mheshimiwa huyo alipokuwa akipanda jukwaani ambako mwanamuziki mmoja maarufu alikuwa akitumbuiza wachomozi walipata fursa ya kuchomoa pochi lake lililokuwa kwenye mfuko wa long’i yake.

Ingawa aling’amua kwamba pochi lake lilikuwa limechomolewa, mheshimiwa huyo alivumilia hadi mkutano ulipokamilika dakika chache kabla ya saa moja usiku ambapo alimwendea mwelekezi na kumfahamisha kilichokuwa kimetendeka.

“Jamani kuna tangazo hapa. Mheshimiwa huyu amepoteza pochi lake. Halina pesa, ni kadi za kibiashara na benki zilizo ndani.

Tafadhani ikiwa umechukua kipochi hicho mrudishie mheshimiwa, hautachukuliwa hatua zozote za kisheria. Tutakupatia zawadi ya Sh2000 ukipata kipochi hicho,” mwelekezi alitangazia watu ambao walikuwa wameanza kuondoka uwanjani.

Dondoo za Hapa na Pale ni visa vinavyojiri kila siku sehemu tofauti nchini na kimataifa. Tuma habari kwa:dondoo@ke.nationmedia.com/ taifa@ke.nationmedia.com au swahilihub@ke.nationmedia.com   

 

 

Jombi afurusha kina mama waliofika kwake kumwombea

Na  COLLINS ONGALO

Imepakiwa - Tuesday, January 26  2016 at  14:16

Kwa Muhtasari

Jombi wa hapa aliwashangaza wengi kwa kuwatimua akina mama walioenda kumuombea akiwa mgonjwa.

 

MANYONYI, Lugari.

JOMBI wa hapa aliwashangaza wengi kwa kuwatimua akina mama walioenda kumuombea akiwa mgonjwa.

Inasemekana kuwa mkewe aliwaalika wanawake  marafiki zake kumuombea jamaa ambaye alikuwa akiugua kwa muda.

Hata hivyo, wanawake hao walipofika nyumbani kwa jombi  aliwatimua akidai   kwamba yeye hakuwa 'hafifu’ na wala hakuhitaji  kuombewa.

“Nani aliwaambia ninahitaji maombi? Mnadhani mimi sina uwezo wa kujiombea? Maombi pelekeni kanisani lakini sio hapa,” jombi aliwafokea.

Kwa mujibu wa mdokezi,  jamaa alikuwa amemuonya  mkewe dhidi ya kualika watu kuomba katika boma lake.

Juhudi za mkewe kumrai akubali kuombewa ili Mungu amponye ziligonga ukuta kwani jamaa alikataa kutoruhusu maombi katika boma lake.

 

 

Demu atemwa kwa kuzidiwa na tamaa

Na GRACE KARANJA

Imepakiwa - Tuesday, January 26  2016 at  14:01

Kwa Muhtasari

Mwanadada kutoka mtaa huu, hakuamini macho yake alipotemwa na mumewe kwa kuwa na tamaa ya kutaka kila kitu.

 

MAKONGENI, Thika

MWANADADA kutoka mtaa huu, hakuamini macho yake alipotemwa na mumewe kwa kuwa na tamaa ya kutaka kila kitu.

Duru zaarifu kwamba, wawili hao walikuwa wameishi katika ndoa kwa mwaka mmoja lakini kila mara walisikika wakigombana.

“Hawakuweza kukaa hata siku tatu bila kurushiana maneno. Ilikuwa ni mabishano, ugomvi na hasira,” mdokezi alisema.

Sababu ya ugomvi huo ilikuwa tabia ya mwanadada ya kumlazimisha mumewe kumfanyia mambo ambayo hangeyamudu.

Yasemekana  mumewe alikuwa amemuonya mara nyingi dhidi ya tabia ya kutamani maisha ya juu.

“Jamaa alikuwa amemwambia mkewe kwamba mambo hufanywa kwa mpango lakini hakusikia,” akasema mdokezi.

Jioni ya kisanga, jamaa alirudi nyumbani bila viatu ambavyo mwanadada alikuwa amemwitisha jambo lililomfanya mkewe kumfokea mbele ya majirani.

“Mbona leo hukuniletea chochote na uliniahidi viatu,” mwanadada alitaka kujua.

Swali hilo lilimkera sana jamaa na kumwambia mkewe kwamba alimkosea heshima mbele ya majirani.

“Nyamaza, unataka kuwajulisha majirani ndio wafanye nini? Ni mara ngapi nimekuonya dhidi ya kutaka maisha ya juu usiyoyaweza? Ni nini ambacho sijakununulia tangu nikuoe, una jozi ngapi za viatu hata zingine hata huvai? Sijui unata zingine za kupeleka wapi?

Mimi sikuapa kuishi maisha hayo na kuanzia dakika hii kwa sababu ya kuniabisha mbele ya majirani, kesho uamke uende utafute kazi uwe tajiri uweze kujipa chochote utakacho maishani,” jamaa alimwambia mkewe kwa hasira.

Hata hivyo, mwanadada huyo alichukulia matamshi ya jamaa kama mzaha tu na hakutilia maanani onyo hilo.

Kulingana na mdokezi, siku iliyofuata, jamaa aliamka na kumfukuza mwanadada huyo dhihirisho kwamba hakuwa akifanya mzaha alipomwambia alikuwa amechoshwa na tabia yake.

 

Dondoo za Hapa na Pale ni visa vinavyojiri kila siku sehemu tofauti nchini na kimataifa. Tuma habari kwa:dondoo@ke.nationmedia.com/ taifa@ke.nationmedia.com au swahilihub@ke.nationmedia.com   

 

 

Polo asusia pilau akishuku ina sumu

Na GRACE KARANJA 

Imepakiwa - Sunday, January 24  2016 at  12:27

Kwa Muhtasari

Kioja kilizuka katika nyumba moja mtaani hapa  jombi aliposusia pilau akishuku kwamba viungo vilivyowekwa na mkewe vilikuwa sumu.

 

DANDORA, NAIROBI

KIOJA kilizuka katika nyumba moja mtaani hapa  jombi aliposusia pilau akishuku kwamba viungo vilivyowekwa na mkewe vilikuwa sumu.

Penyenye zaarifu kwamba ilikuwa mara ya kwanza kwa mke wa jombi kuweka pilau masala kwa wali jambo ambalo lilimshtua.

“Jamaa alishtushwa na pilau masala kwa sababu mkewe hakuwa ameitia kwa wali hapo awali,” mdokezi alieleza.

Inasemekana kwamba wawili hao walikuwa waking’ang’ana na maisha kwa muda mrefu na ilikuwa tatizo kupika vyakula vya aina tofauti.

Usiku wa kioja, jamaa alitoka kazini kama kawaida na kupumzika kitini ili apikiwe na mkewe.

“Leo hutaamini chakula  nilichokupikia, ni pilau,” mkewe alimwambia jamaa.

Hapo ndipo alipoweka mezani sinia iliyojaa pilau na kumkaribisha mumewe ale.

Badala ya jombi kufurahia chakula, alimrudishia mkewe pilau na kumwambia kwamba ikiwa alikuwa na mpango ya kumuua siku hiyo, hangefaulu.

“Si ungesubiri tu niwe na mali kiasi ndio uniue ubaki nayo, mipango yako imesabaratika. Hicho chakula chako unachokiita pilau sikitaki.

Mbona wali umebadili rangi? Sitaki, kula mwenyewe, ndio maana umeweka nyama kwa sababu wajua naipenda,” jamaa alimfokea mkewe.

Kulingana na mdokezi, ilibidi mkewe kutafuna vijiko kadhaa na kuvimeza ili kumhakikishia mumewe chakula hakikuwa na sumu.

“Miaka hiyo yote nimekaa nawe mbona niamue kukuua leo. Hii ni pilau masala niliyoweka ili wali unukie vizuri. Kama huamini wacha nile vijiko kadhaa nife kwanza tuone,” mkewe alimweleza jombi.

Inasemekana kwamba jombi alimwomba mkewe msamaha kisha wakaendelea kula pamoja na bila hofu ya kuangamizwa.

Baadaye jamaa alimsifu mkewe kwa kumpikia chakula kitamu sana na mara kwa mara akawa anamuomba ampikie pilau.

 

 

Meidi afichua siri za 'Baba Boi' asifutwe kazi

Na TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Saturday, January 23  2016 at  14:02

Kwa Muhtasari

Buda wa eneo hili alitamani ardhi ipasuke immeze akiwa hai baada ya meidi kumweleza mkewe kwamba alikuwa akialika wanawake nyumbani akiwa kazini.

 

KAKAMEGA MJINI

BUDA wa eneo hili alitamani ardhi ipasuke immeze akiwa hai baada ya meidi kumweleza mkewe kwamba alikuwa akialika wanawake nyumbani akiwa kazini.

Penyenye zasema kuwa baada ya mkewe kwenda  kazini, polo alikuwa akialika vimada nyumbani.

Kulingana na mdokezi wetu, meidi aliamua kutoboa siri hiyo kwa mke wajamaa ili asifutwe kazi.

“Mama Boi nasikia eti unataka kunifuta kazi. Unafikiria utapata wapi mtu wa kukuchungia boma kama mimi?” meidi alimshawishi mdosi.

Inasemekana kuwa meidi alipoona ushawishi wake unaambulia patupu, aliamua kumfichulia vituko vya mumewe.

“Mama boi wacha nikuambie siri. Isije baadaye ukasema eti sikukuambia wakati nimeenda. Kila wakati unapoenda kazini, baba Boi huleta hapa wanawake  tofauti.

Kila wakati wakija, yeye huniambia niwapikie chai kisha ananipa Sh200 niende sokoni ninunue ninachotaka. Nikirudi huniambia nisimuambie mtu,” alisimulia meidi.

Maneno ya meidi yalimshtua mke wa polo sana. “Mbona hukuniambia mapema?” mama aliuliza.

“Nilitaka kukuambia lakini niliogopa. Hata jana ulipoondoka tu hivi, demu fulani alikuja hapa. Nikaambiwa ni msichana wa ukoo wenu. Lakini bado nilipewa off ya saa tatu,” meidi alizidi kuelezea.

Kulingana na mdokezi wetu, haya yote yakiendelea, polo hakuwepo. “Sasa wewe ukinifuta kazi, nani atakueleza hii siri?” meidi alimuuliza mdosi wake.

Polo alipowasili, mkewe alianza kumrushia cheche za maneno,” alieleza mdokezi.

“Kila siku mimi nikitoka hapa, wewe huwaleta nani katika hii nyumba? Jana ni msichana yupi alikuwa hapa? Meidi unamzubaisha kwa kumpa Sh200 kisha unamfukuza ndio asijue kinachoendelea. Wewe ni mtu wa aina gani?” mama alimfokea mumewe.

Inasemekana kuwa baada ya polo kugundua siri  ilikuwa imefichuliwa, aliamua kutoroka ili kuhepa kuzomewa na mkewe.

 

 

Jombi sasa ni skwota baada ya kuuza shamba alipe mganga

Na JOHN MUSYOKI

Imepakiwa - Saturday, January 23  2016 at  14:10

Kwa Muhtasari

Polo amepiga kambi katika mitaa ya mji huu baada ya kukosa makao alipouza shamba lake ili amlipe mganga aliyemhudumia.

 

EMBU MJINI

POLO amepiga kambi katika mitaa ya mji huu baada ya kukosa makao alipouza shamba lake ili amlipe mganga aliyemhudumia.

Penyenye zasema kwamba jamaa aliamini familia yake ilikuwa imerogwa ikasambaratika na akaamua kutafuta huduma za mganga maarufu.

Inasemekana mganga huyo alifika na kufanya vituko vyake katika boma la jamaa huyo na kuahidi kwamba mambo yangekuwa shwari na  mke na watoto wake waliokuwa wamehama wangerudi.

Hata hivyo, badala ya mambo kuwa mazuri kwa jamaa, yaliendelea kuwa mabaya zaidi na akasita kumlipa mganga. Kulingana na mdokezi, jamaa alikuwa ameafikiana na mganga huyo kwamba angemlipa baada ya kuona matunda ya kazi yake.

“Lakini jamaa alikosa kuona mabadiliko katika muda ambao alikuwa ameahidiwa na mganga huyo. Fauka ya yote, alifutwa kazi hata kabla ya kipindi hicho kukamilika akawa hana mbele wala nyuma,” akasema mdokezi.

Inasemekana mganga alianza kumtisha jamaa angekiona cha mtema kuni asipomlipa na ikabidi auze shamba. Kwa sasa anahangaika mitaani akiombaomba sababu familia yae imemkataa.

 

 

Demu azua kizaazaa kilabuni kwa kuzaba mpenziwe makofi

Na JOHN MUSYOKI

Imepakiwa - Saturday, January 23  2016 at  14:12

Kwa Muhtasari

Kizaazaa kilizuka katika baa kipusa alipompiga mpenzi wake kwa kumpata akisakata densi na kidosho mwingine.

 

KITHIMANI, MACHAKOS

KIZAAZAA kilizuka katika baa kipusa alipompiga mpenzi wake kwa kumpata akisakata densi na kidosho mwingine.

Inasemekana kwamba mwanadada huyo alikuwa akishuku jamaa alikuwa na tabia ya kuburudisha vipusa wengine na akaamua kuchunguza ili kubaini ukweli.

Siku ya kisanga alimpigia jamaa simu wakutane kujivinjari lakini akamfahamisha alikuwa na shughuli nyingi na hangepata nafasi.

Mwanadada huyo alipata habari kutoka kwa makachero wake kwamba polo alionekana akiburudika na kipusa mwingine. Alipofika, aliwapata wakinengua viuno na bila kusita alimzaba jamaa makofi makali yaliyoshtua wateja wengine.

“Mwanamume malaya wewe. Ulidhani sitakupata, usiwahi kunikaribia tena,” kipusa alimfokea jamaa na kuondoka kwa hasira.

 

 

Polo ajuta kudandia lori la polisi usiku

Na SAMMY WAWERU

Imepakiwa - Friday, January 22  2016 at  17:03

Kwa Muhtasari

Polo wa hapa Kiangoma, Nyeri alilazimika kukesha kwenye seli kwa kudandia lori bila kujua lilikuwa la polisi.

 

KIANGOMA, Nyeri

POLO wa hapa Kiangoma, Nyeri alilazimika kukesha kwenye seli kwa kudandia lori bila kujua lilikuwa la polisi.

Yasemekana jamaa huyo alikuwa amelewa chakari alipotekeleza kitendo hicho.

Kulingana na mdokezi, kalameni ni alikuwa akitoka kwa mama pima kuzima mwasho wa koo lake kwa chang’aa.

Alipofika barabara iliyoelekea mtaa anaoishi jamaa, aliona lori likielekea alikokuwa akienda huku likiendeshwa taratibu.

Bila hata kukagua nambari za usajili, polo alilidandia na kujilaza juu ya mizigo iliyokuwa ndani na kwa sababu ya ulevi alizama kwenye usingizi na kujisahau.

Kulingana na mdokezi, lori hilo lilifululiza mwendo na kituo cha kwanza kusimama kikawa ni kambi ya polisi. Maafisa wa polisi walipoanza kupakua mizigo waliyobeba walipata jombi akikoroma.

“Hei mkubwa uliona uwe miongoni mwa mizigo yetu?” aliuliza afisa mmoja wa polisi akimuamsha.

Kalameni hakuwa na budi ila kutiwa seli hadi siku iliyofuata kwa sababu giza lilikuwa limeingia tayari.

“Jamaa alishtuka kisha akaeleza alivyodandia lori akielekea nyumbani na kuomba msamaha,” akasema mdokezi.

Kufyeka nyasi

Asubuhi iliyofuata, jamaa alipewa adhabu ya kufyeka nyasi kwenye kituo hicho na kuonywa dhidi ya kudandia magari ya polisi.

“Siku nyingine usidandie gari usilolifahamu, hiyo ni kuhatarisha maisha yako kwa sababu hujui watu walilonalo wana nia gani,” alishauriwa na afisa mmoja wa polisi alipoachiliwa huru.

Yasemekana polo alifululiza hadi kwa mama pima na alipohadithia watu kisa hicho waliangua kicheko.

“Jana nimelala seli kama mahabusu kwa kupanda gari la polisi, nitapunguza hii cham na niwe mwangalifu sasa,” alisema polo kila mmoja akimsikiliza na kucheka.

Dondoo za Hapa na Pale ni visa vinavyojiri kila siku sehemu tofauti nchini na kimataifa. Tuma habari kwa:dondoo@ke.nationmedia.com/ taifa@ke.nationmedia.com au swahilihub@ke.nationmedia.com   

 

 

Washangaa kugunua polo hupigwa na mke, si majambazi

Na CORNELIUS MUTISYA

Imepakiwa - Monday, January 18  2016 at  13:40

Kwa Muhtasari

Polo wa hapa aliwaacha wakazi vinywa wazi walipogundua kwamba aliwahadaa alikuwa amevamiwa na majambazi baada ya kutwangwa na mke wake.

 

KITHUNGUINI, MACHAKOS

POLO wa hapa aliwaacha wakazi vinywa wazi walipogundua kwamba aliwahadaa alikuwa amevamiwa na majambazi baada ya kutwangwa na mke wake.

Jamaa huyo alipiga nduru zilizowavutia wakazi na walipoenda kujua kilichojiri aliwafahamisha kwamba alikuwa amevamiwa na majambazi waliokuwa na silaha.

Kulingana na mdokezi, polo alikuwa na mazoea ya kumpiga mkewe kila siku akimlaumu kwa makosa madogomadogo. Hali hii ilimfanya mkewe kukasirika na akazua njama ya kulipiza kisasi.

“Polo alikuwa na mazoea  ya kumpiga mke wake kila siku. Hali hii ilimfanya mama watoto kukasirika na akaamua kulipiza kisasi,” akasema mdokezi.

Inasemekana siku ya kioja, mama watoto alipika chakula mapema na akapakulia watoto kikaisha. Aliosha sufuria na akaketi sebuleni kumsubiri mumewe.

“Polo alipofika nyumbani mwendo wa saa tatu usiku, alianza kumwitisha mkewe chakula kwa fujo. Ugomvi ulizuka baina yao na mama watoto akachukua kipande cha ukuni na kumtwangwa mumewe kichwani,’’ akasema mdokezi.

Kulingana na mdokezi, polo alichomoka nje mithili ya swara aliyebumburushwa na akapiga kamsa akidai alikuwa ameshambuliwa na genge la majambazi waliojihami kwa silaha za kila aina.

Wakazi walifurika  kwake kumnusuru lakini wakashangaa walipopata  hakuwa amevamiwa na majangili kama alivyokuwa amedai.

Wakazi waliamua kufanya uchunguzi na wakagundua kuwa alikuwa ametwangwa na mkewe kwa kumsumbua akiitisha chakula ambacho hakununua.

“Wakazi walimuonya polo asithubutu tena kupiga kamsa akidai amevamiwa na wezi anakikosana na mkewe. Walimwambia anafaa kuketi chini na mkewe na kusuluhisha tofauti zao kwa njia ya kiutu uzima badala ya kumwaga mtama kwenye kuku wengi,’’ akasema mdokezi.

Inasemekana mkewe alisikika akimwambia kwamba hatavumilia dhuluma na akaapa kumwadhibu tena akiendelea kumsumbua.

 

 

Siri ya kalameni Krismasi yafichuka

Na GRACE KARANJA

Imepakiwa - Saturday, January 16  2016 at  14:27

Kwa Muhtasari

Jombi wa mji huu wa Thika alijipata pabaya baada ya mkewe kugundua kuwa mwisho wa mwaka jana wakati wa likizo ya Krisimasi, alikuwa kwa mpango wa kando.

 

THIKA MJINI

JOMBI wa mji huu wa Thika alijipata pabaya baada ya mkewe kugundua kuwa mwisho wa mwaka jana wakati wa likizo ya Krisimasi, alikuwa kwa mpango wa kando.

Penyenye zilizotufikia zasema kuwa buda alimwambia mkewe kwamba alisafiri kwenda kuwaona wazazi mashambani kwa sababu alikuwa hajawaona kwa muda mrefu.

“Jamaa alikuwa amekaa miaka mitatu bila kuwatembelea wazazi na mkewe aliamini alikuwa huko,” mdokezi alisema.

Inasemekana kuwa, siku kadhaa kabla ya sikukuu jamaa alikuwa na furaha sana na kila wakati alitaja safari hiyo.

“Naona siku zinakawia sana na ninatamani kuondoka kwenda nyumbani kuwaona wazazi wangu,” kila mara jamaa alimwambia mkewe.

Siku ya kisanga juzi, jamaa alikuwa nje ya nyumba simu yake ilipopigwa na mkewe akaipokea.

“Mbona siku nyingi hujanipigia simu na vile ulinifurahisha likizo yote au umemrudia mkeo? Unaweza kunisahau haraka hivyo?” demu aliropokwa akidhani alikuwa akizungumza na jamaa.

Mama apigwa na butwaa

Mama huyo hakuamini masikio yake na alimpa mumewe simu.

“Haya ongea na huyu uliyemfurahisha wakati wa Krismasi, sikujua kwamba wewe unaweza kunifanyia jambo kama hilo. Ulinindanganya ulienda kuwaona wazazi wako ili ukaburudishe vimada. Ulidhani mimi ni mjinga kwa sababu sikutaka kujua kama ulifika nyumbani au la. Usijali leo nimekushika,” mama alimfokea jamaa.

Juhudi za jamaa kutaka kuzungumza na mpango wake wa kando hazikufua dafu mkewe alimnyang’anya simu na kumwonya kipusa dhidi ya kumchezea mumewe.

“Hata kama mume wangu alikuja kwako usifikiri umepata nafasi ya kumchukua. Keep off my husband,” mama alichemka.

Haikufahamika ikiwa mama alisamehe jamaa baada ya kugundua tabia yake.

Dondoo za Hapa na Pale ni visa vinavyojiri kila siku sehemu tofauti nchini na kimataifa. Tuma habari kwa:dondoo@ke.nationmedia.com/ taifa@ke.nationmedia.com au swahilihub@ke.nationmedia.com   

 

 

Demu azirai kupata baba mkwe lojing'i

Na KIMANI wa NJUGUNA

Imepakiwa - Wednesday, January 13  2016 at  10:14

Kwa Muhtasari

Mwanadada mmoja wa Kiambu Mjini alipoteza fahamu na kuanguka alipoingia ndani ya lojing’i kushiriki mipango ya kando na kumpata baba mkwe akiwa bawabu wa gesti hiyo.

 

MWANADADA mmoja wa Kiambu Mjini alipoteza fahamu na kuanguka alipoingia ndani ya lojing’i kushiriki mipango ya kando na kumpata baba mkwe akiwa bawabu wa gesti hiyo.

“Mwanadada huyo aliolewa miaka mitano iliyopita na jamaa ambaye alikuwa akifanya kazi katika kampuni moja jijini Nairobi na wakabarikiwa na watoto wawili,” akaeleza mdokezi.

Inasemekana jamaa aliangukiwa na bahati alipopata kazi ng’ambo na akamuacha mkewe nchini. Kulingana na mdokezi, jamaa alikuwa akimtumia mkewe pesa za kutosha kuwatunza watoto.

“Baada ya muda, mwanamke huyo alianza kuhisi upweke na kiu cha uroda kwa sababu hakuna mwanamume ambaye alimrushia ndoano,” akaendelea mdokezi.

Ni wakati huo ambapo alikata kauli kutongoza wanamume na akampata barobaro mmoja aliyemaliza kidato cha nne mwaka jana.

Bila kupoteza muda, mwanamke huyo alianza kumtumia arafa moto moto za kimapenzi kijana huyo.

Isitoshe, alimzuzua chali huyo kwa kumtumia pesa za matumizi yake.

Siku ya kisanga, wawili hao walipanga kukutana katika hoteli moja na baada ya mapochopocho na vileo, waliamua kujitoma kwenye lojing’i ili waburudishane faraghani.

Jukumu la kukodisha vyumba

Walielekea katika gesti moja na wakafahamishwa kwamba jukumu la kukodisha vyumba vya kulala lilikuwa la mlinzi wa usiku.

Mara tu alipochomoa pesa za kukodisha chumba na kugundua alikuwa anamkabidhi baba mkewe pesa hizo.

“Ala! Kwa hivyo, mwanangu alimuoa mwanamke ambaye anawalipa vijana wadogo wamburudishe kimapenzi? Tabia kama hii haitafanyika nikiwa hai na lazima nilinde heshima ya familia yangu,” alifoka mzee.

Alipomaliza tu kuzungumza, demu alianguka sakafuni kwa kishindo.

Alipewa huduma za kwanza na akapata fahamu, bawabu huyo aliinua rungu akitaka kumuangushia polo kichwani, lakini akahepa.

Kuona mambo yalikuwa yamepasuka, mwanadada huyo alichomoka kama mshale.

Iliwabidi waliokuwa karibu kumtuliza mzee huyo huku wakimlaumu mwanadada kwa tukio hilo.

Dondoo za Hapa na Pale ni visa vinavyojiri kila siku sehemu tofauti nchini na kimataifa. Tuma habari kwa:dondoo@ke.nationmedia.com/ taifa@ke.nationmedia.com au swahilihub@ke.nationmedia.com

 

 

Wamrukia ndugu yao kufuatia kifo cha baba

Na BENSON MATHEKA

Imepakiwa - Wednesday, January 13  2016 at  10:14

Kwa Muhtasari

Kizaazaa kilitokea hapa Miwani, Machakos jombi alipotandikwa na ndugu zake wakidai alifahamu kilichosababisha kifo cha baba yao.

 

MIWANI, Machakos

KIZAAZAA kilitokea hapa Miwani, Machakos jombi alipotandikwa na ndugu zake wakidai alifahamu kilichosababisha kifo cha baba yao.

Inasemekana kuwa familia ya marehemu, majirani na marafiki walifika mochari iliyoko eneo hili kuchukua mwili kwenda kuuzika.

Hata hivyo, walipomwona ndugu yao walipandwa na hasira na kumtaka kuondoka.

“Unafanya nini hapa? Na unajua kilichomuua baba yetu. Ondoka mara moja, hatutaki kukuona,” ndugu zake walimwambia.

Jamaa aliyekuwa ameegesha gari la kifahari hatua chache kutoka mochari alikaidi agizo hilo na kusema alikuwa na haki ya kuhudhuria mazishi ya baba yake.

“Ni baba yangu aliyenizaa na niko hapa kumpa mkono wa buriani. Hamna haki ya kunizuia,” akasema.

Ndugu wapandwa na hamaki

Lakini matamshi yake yalionekana kuwachemsha zaidi ndugu zake waliomlaumu kwa kukosa kushiriki mipango ya mazishi.

“Sasa ndio amekuwa baba yako eh? Ulikuwa wapi tulipokuwa tukiandaa mazishi? Wacha hayo, hukumtembelea alipokuwa akiugua, tena ulisema wakati wake wa kufa ulikuwa umefika kumaanisha ulijua kilichomuua. Toka hapa na wewe sio ndugu yetu na usikaribie tulipo.”

Mambo yaliharibika alipojaribu kusongea gari la kubeba maiti lilipokuwa ndugu zake walipomuinua juu na kumtandika.

“Shetani ya mtu wewe, hautaendelea kusumbua familia yetu,” walimfokea.

Dondoo za Hapa na Pale ni visa vinavyojiri kila siku sehemu tofauti nchini na kimataifa. Tuma habari kwa:dondoo@ke.nationmedia.com/ taifa@ke.nationmedia.com au swahilihub@ke.nationmedia.com

 

 

Mke wa polo akosa kurudi baada ya kwenda Krismasi

Na COLLINS ONGALO

Imepakiwa - Wednesday, January 13  2016 at  10:14

Kwa Muhtasari

Kalameni wa mtaa huu wa Huruma, Nairobi anahuzunika baada ya mkewe kutorudi mjini tangu mwaka jana alipoenda kuwasalimia wazazi wake msimu wa Krismasi.

 

HURUMA, Nairobi

KALAMENI wa mtaa huu wa Huruma, Nairobi anahuzunika baada ya mkewe kutorudi mjini tangu mwaka jana alipoenda kuwasalimia wazazi wake msimu wa Krismasi.

Inasemekana kwamba jombi na mkewe wanahudumu mjini walikopatana na kuchumbiana miaka sita iliyopita na wamejaliwa watoto wawili.

Mwishoni mwa mwaka jana, mkewe alimuomba kalameni ruhusa ya kwenda kuungana na wazazi wake wanaoishi mashambani kwa sababu hakuwa amewaona kwa miaka mingi.

“Hilo ni wazo zuri, bora uende na urudi kabla ya shule kufunguliwa ili watoto warudi shule,” jamaa alimwambia mkewe.

Kwa mujibu wa mdokezi, walizidi kuwasiliana kwa simu.

Lakini siku mbili baada ya Krisimasi, jombi alipigwa butwaa mama alipokosa kujibu simu au hata kumpigia.

Baadaye alipokea arafa mama akimweleza hangerudi kabla ya kulipa mahari.

Dondoo za Hapa na Pale ni visa vinavyojiri kila siku sehemu tofauti nchini na kimataifa. Tuma habari kwa:dondoo@ke.nationmedia.com/ taifa@ke.nationmedia.com au swahilihub@ke.nationmedia.com

 

 

Polo akaripia mkewe kwa kutupa ugali uliobaki jioni

Na STEPHEN DIK

Imepakiwa - Wednesday, January 13  2016 at  10:14

Kwa Muhtasari

Jombi wa hapa Ndere, Siaya aliwashangaza wakazi kwa kumgombeza mkewe kwa sababu ya kutupa ugali kiporo.

 

NDERE, Siaya

JOMBI wa hapa Ndere, Siaya aliwashangaza wakazi kwa kumgombeza mkewe kwa sababu ya kutupa ugali kiporo.

Kulingana na mdokezi, mkewe aliamka asubuhi na jambo la kwanza kufanya lilikuwa ni kuchukua kiporo na kukitupa kwenye jaa la taka.

“Jamaa alimgombeza mkewe akimwambia alitaka kutafuna kiporo na kuteremsha kwa chai. Alimwambia mkewe aliharibu chakula nyakati hizi ambazo gharama ya maisha iko juu,” akasema mdokezi.

Jamaa amekuwa akinywa chai kwa ugali kila asubuhi siku za hivi karibuni jambo ambalo halikumfurahisha mkewe.

Jamaa alimwambia mkewe kwamba akirudi kutupa chakula atamchukulia hatua ambazo hakutaja.

Dondoo za Hapa na Pale ni visa vinavyojiri kila siku sehemu tofauti nchini na kimataifa. Tuma habari kwa:dondoo@ke.nationmedia.com/ taifa@ke.nationmedia.com au swahilihub@ke.nationmedia.com

 

 

Atandikwa kwa kumpiga bawabu wake

Na COLLINS ONGALO

Imepakiwa - Wednesday, January 13  2016 at  10:14

Kwa Muhtasari

Kalameni wa hapa Webuye anauguza majeraha baada ya kushambuliwa na majirani kwa kumpiga na kumjeruhi bawabu wake alipoingilia mzozo wake na mkewe.

 

WEBUYE MJINI

KALAMENI wa hapa Webuye anauguza majeraha baada ya kushambuliwa na majirani kwa kumpiga na kumjeruhi bawabu wake alipoingilia mzozo wake na mkewe.

Yasemekana jamaa aliona picha za wanaume kwenye ukurasa wa Facebook wa mkewe na akataka kujua uhusiano wake na wanaume hao.

Mama alipojaribu kumweleza walikuwa marafiki tu, jamaa alikasirika na kuanza kumpiga.

Jombi aliposikia nduru za mama alienda kumuokoa jambo ambalo lilimkasirisha kalameni akampiga kwa kipande cha chuma.

Wakazi walimpa kipigo hadi akaomba msamaha.

Dondoo za Hapa na Pale ni visa vinavyojiri kila siku sehemu tofauti nchini na kimataifa. Tuma habari kwa:dondoo@ke.nationmedia.com/ taifa@ke.nationmedia.com au swahilihub@ke.nationmedia.com

 

 

Aibu kwa mama kuhepesha hela za matanga

Na CORNELIUS MUTISYA

Imepakiwa - Tuesday, January 12  2016 at  15:20

Kwa Muhtasari

Mama wa hapa alipata aibu ya mwaka alipokamatwa baada ya kutoroka na pesa za chama cha mazishi.

 

KALUNGA, MACHAKOS

MAMA wa hapa alipata aibu ya mwaka alipokamatwa baada ya kutoroka na pesa za chama cha mazishi.

Inasemekana kuwa mama huyo aliyekuwa mweka hazina wa chama hicho alienda mafichoni lakini akasakwa na kulazimishwa kuzilipa.

Kulingana na mdokezi, mama huyo alichaguliwa mweka hazina wa chama cha mazishi kwa sababu aliheshimiwa na wakazi.Hakuna aliyedhani kuwa angebadilika na kutoroka na pesa za chama.

“Mama alichaguliwa na wakazi kuwa mweka hazina kwa sababu walimheshimu. Hakuna aliyedhani kuwa angetoroka na pesa hizo,’’ akasema mdokezi.

Inasemekna kwamba wanachama walichanga pesa kama ilivyokuwa desturi yao kila mwisho wa mwezi na kumkabidhi mweka hazina azipeleke benki.

Alipopewa hela hizo, badala ya kupeleka benki, aliamua kutoroka  hadi mjini Athiriver alikopanga chumba na kuanzisha biashara ya  mboga na matunda.

Penyenye zaarifu kwamba, wanachama waliingiwa na wasiwasi walipomkosa mama huyo kwa muda.Walishindwa kwa nini hakuwasilisha risiti ya benki kwa katibu wa chama ili aweke katika rekodi za chama.Walimtafuta kujua ukweli wa mambo.

“Mwenyekiti na katibu waliamua kwenda benki ili kuuliza baki ya akaunti yao. Walishangaa mno walipogundua kuwa mweka hazina hakuwa amepeleka pesa hizo benki,’’ akasema mdokezi.

Waliarifu wakazi ambao walianza kumsaka mama huyo na wakapata habari alikuwa akifanya biashara  mjini Athiriver.

Waliamua kumkabili ili awarejeshee hela zao.

“Walimwendea mama huyo mjini na wakamlazimisha arejeshe pesa za chama. Alikubaliana nao na akarejea nyumbani na kuuza ng’ombe kulipa pesa hizo.

Hata hivyo, aliondolewa kabisa kutoka wadhifa wa mweka hazina na akabaki mwanachama wa kawaida.’’ akasema mdokezi.

Duru zaarifu kwamba,  mama huyo hatoki nyumbani kwa sababu ya aibu.

 

 

Ajuta kutolipa vidosho wa kunengua kiuno

Na SAMMY WAWERU

Imepakiwa - Tuesday, January 12  2016 at  15:37

Kwa Muhtasari

Kioja kilitokea kwenye klabu kimoja mtaani hapa buda alipovamiwa na vidosho kwa kudinda kuwalipa hela alizowaahidi baada ya kumnengulia kiuno.

 

GITHUNGURI, KIAMBU

KIOJA kilitokea kwenye klabu kimoja mtaani hapa buda alipovamiwa na vidosho kwa kudinda kuwalipa hela alizowaahidi baada ya kumnengulia kiuno.

Jamaa alifika katika baa kuteremsha pombe na kulingana na mdaku, aliwaambia vipusa waliokuwa wakiburudisha wateja wajibwage jukwaani kusakata densi awalipe donge na kuwanunulia mvinyo.

“Warembo mnasakata densi vizuri, tafadhali  ninengulieni Viuno.  Nitawatuza na kuwanunulia vinywaji mfurahie. Pesa kwangu si hoja,” alisema buda.

Yasemekana jombi aliahidi kuwapa kila mmoja shilingi mia tano. “Vipusa waliingia jukwaani na kuanza kunengua huku jamaa akiwatazama,” aliarifu mdokezi.

Vipusa hao walitumia kila mbinu kumzuzua buda hadi akashindwa kuzuia kicheko. “Yes, utamu wa maisha ni raha kama hizi,” alisema polo kwa kejeli.

Vipusa walikunja jamvi kusakata densi na kudai haki yao. “Raha umepata, tupe mshahara sasa,” alisema kipusa mmoja na kuungwa mkono na wengine.

“Kuna mkataba tulioandikiana nitawalipa? Mmeniongezea faida gani maishani?” alifoka buda huyo. Matamshi hayo yaliwakasirisha vipusa hao na wakamkaba koo jamaa huyo.

“Wewe utajua unacheza na akina nani. Ahadi lazima utatimiza au utakiona cha mtema kuni. Utajua tunatoka Nyeri na hatucheki,” alichemka mmoja wao.

 

 

Polo afungiwa stoo kwa kuibia hoteli sukari

Na  TOBBIE WEKESA

Imepakiwa - Monday, January 11  2016 at  14:08

Kwa Muhtasari

Kalameni wa eneo hili, alijipata taabani baada ya kufungiwa stoo  siku nzima alipopatikana akiiba sukari katika hoteli.

 

MAILI SABA, Kitale

KALAMENI wa eneo hili, alijipata taabani baada ya kufungiwa stoo siku nzima alipopatikana akiiba sukari katika hoteli.

Kulingana na mdokezi, polo aliingia katika hoteli na kuketi karibu na meza iliyokuwa na bakuli iliyojaa sukari kisha akaagiza chai na andazi moja.

Inasemekana kuwa polo alianza kuweka sukari kwa chai huku akiweka nyingine katika mfuko wa long’i yake bila kujua weita mmoja alikuwa akimtazama.

Duru zasema alipokuwa akiondoka, weita alimsimamisha.

“Bosi, umekunywa chai vikombe vingapi?” weita huyo alimuuliza.

“Nimekunywa kikombe kimoja tu na ndicho ninalipia,” polo alimjibu weita. “Kwani kikombe kimoja ndicho kimemaliza sukari iliyokuwa imejaa kwenye hii sahani?” weita alimuuliza polo.

Inasemekana kuwa polo alianza kumzomea weita. “Sasa unafikiria mimi nimeramba sukari? Kwenda huko,” alisema.

Weita alimuagiza polo kutoa kila kitu kilichokuwa ndani ya mfuko  wa long’i yake na sukari ikapatikana ndani ya mfuko huo.

“Huyu jamaa nilikuwa nikiangalia alichokuwa akifanya. Mara tu alipoletewa chai, alijifanya aliumwa na kitu kumbe ni karatasi aliyokuwa akitoa kisha akaanza kuchota sukari na kuweka ndani ya hiyo karatasi,” weita alisimulia.

Ilibidi jamaa kupiga magoti na kuomba msamaha.

“Jamani mnisamehe. Sitarudia tena. Mimi ni kastoma wenu wa kila siku. Na tena najulikana hapa. Tafadhali msiniaibishe,” polo aliwarai wahudumu.

“Hakuna cha msamaha. Huyu jamaa lazima afungiwe hapa hadi bosi wetu aje,” weita mmoja aliwaeleza wenzake.

Inasemekana kuwa polo alipelekwa na kufungiwa katika chumba cha kuhifadhi vyakula. “Kaa huko mpaka upate adabu,” weita mmoja alisema huku akimsukuma polo ndani ya chumba na kumfungia ndani.

 

 

Polo, dadake wazozania kuzika maiti ya mama yao

Na DENNIS SINYO

Imepakiwa - Monday, January 11  2016 at  14:10

Kwa Muhtasari

Kizaazaa kilizuka katika eno hili, wakati jamaa na dadake walipozozana huku kila mmoja wao akitaka kwenda kuuzika mwili wa mama yao.

 

BUMULA, Bungoma

KIZAAZAA kilizuka katika eno hili, wakati jamaa na dadake walipozozana huku kila mmoja wao akitaka kwenda kuuzika mwili wa mama yao.

Kioja hiki kilivutia umati mkubwa huku mwanadada huyo akisimama kidete akitaka aruhusiwe kuuzika mwili wa mama yake.

Hata hivyo, kaka yake alikataa kata kata akisema kwamba mila na desturi za jamii yao haziruhusu msichana kuzika mzazi na kwamba kufanya hivyo kungeletea jamii hiyo balaa kubwa.

Lakini licha ya madai hayo, msichana alisisitiza kuwa mama yake alikataliwa na familia baada ya mumewe kuaga dunia.

Alidai kwamba, shamba lililokuwa na la baba yao na akalazimika kununua shamba na kumjengea mama yake makao.

Hali hii ilizua mvutano mkali huku wawili hao wakikosa kuafikiana siku ya mazishi. Wapita njia na madereva walikuwa na wakati mgumu huku msafara wa mazishi ukisimama kando ya barabara ili wawili hao kuelewana.

Hata hivyo, walikosa kuelewana na mwili ukarudishwa mochari. Kulingana na mdokezi, msichana  huyo alishangaa ni kwa nini ukoo wao ulikuwa ukitaka kuzika mwili wa mama yake  ilhali ulimkataa wakati  alipokuwa hai.

Msichana huyo aliapa kupigana kwa jino na ukucha hadi auzike mwili wa mama yake.

 

 

Jombi ang'oa mlango mke alipokataa kuufungua

Na GRACE KARANJA

Imepakiwa - Monday, January 11  2016 at  14:14

Kwa Muhtasari

Kalameni wa eneo hili, aliwashangaza majirani alipong’oa mlango wa nyumba yake akimlaumu mkewe kwa kukataa kumfungulia baada ya kutoka kazini usiku.

 

KIGANJO, Thika

KALAMENI wa eneo hili, aliwashangaza majirani alipong’oa mlango wa nyumba yake akimlaumu mkewe kwa kukataa kumfungulia baada ya kutoka kazini usiku.

Kulingana na mdokezi, jamaa huyo huondoka kwenda kazini asubuhi na kurudi saa tano usiku.

Inasemekana wakati mwingine mkewe alikuwa akijivuta kumfungulia mlango na jamaa alimuonya dhidi ya tabia hiyo.

Hivi majuzi, alifika saa tano usiku lakini alipompigia simu mkewe ili amfungulie alikataa.

“Imekuwa wimbo, kila siku ni kama ninakubembeleza unifunglie, mimi si mlinzi?” jamaa alisema mkewe alipofungua mlango baada ya kusubiri kwa saa moja.

Jamaa aliamka mapema na kuchukua nyundo, kisha akang’oa mlango wa nyumba. 

“Kutoka leo nimefanya kazi yako kuwa rahisi. Sasa ninaweza kurudi  saa saba usiku bila kukusumbua,” jamaa alimwambia mkewe baada ya kung’oa mlango wa nyumba.