Mama aonywa dhidi ya kumnyima mumewe mlo

Na NICHOLAS CHERUIYOT

Imepakiwa - Monday, January 11  2016 at  14:17

Kwa Muhtasari

Mama wa hapa, alionywa vikali na wazee wa kijiji dhidi ya tabia yake ya kumnyima mumewe chakula.

 

MAKIMENY, Bomet

MAMA wa hapa, alionywa vikali na wazee wa kijiji dhidi ya tabia yake ya kumnyima mumewe chakula.

Penyenye zasema wazee walichukua hatua hiyo baada ya afya ya jamaa kudhoofika kwa sababu ya njaa. Kulingana na mdokezi, mama huyo alichukua hatua hiyo baada ya mumewe kufutwa kazi.

“Mama huyo aliwachukiza wanakijiji kwa kuchukulia visivyo msemo kwamba mkono mtu haurambwi. Alimtesa sana mumewe ambaye hurauka asubuhi na mapema kutafuta kazi za sulubu ili achumie riziki familia yake,” akasema mdokezi.

Fununu zaeleza kuwa licha ya kalameni kumpatia bibi yake pesa zote alizopata kwa kufanya vibarua alikuwa akimnyima chakula na ikabidi wazee wa ukoo wa mumewe waingilie kati.