Atumbukia mtaroni akihepa anayemdai

Na   GRACE KARANJA

Imepakiwa - Monday, January 11  2016 at  14:18

Kwa Muhtasari

Polo wa mtaa huu, alijipata pabaya alipotumbukia ndani ya mtaro uliojaa maji taka akihepa kulipa deni.

 

KOROGOCHO, NAIROBI

POLO wa mtaa huu, alijipata pabaya alipotumbukia ndani ya mtaro uliojaa maji taka akihepa kulipa deni.

Inasemekana kuwa jamaa huyo alikuwa amelewa alipokutana na jirani aliyemtaka kulipa deni.

“Kama una pesa za kulewa saa mbili asubuhi huwezi kukosa za kunilipa deni langu, nipe pesa sasa,” jamaa alimwambia polo.

Hata hivyo, badala ya kulipa jamaa alitimua mbio lakini kwa bahati mbaya aliingia ndani ya mtaro wa maji taka.