7/9/2017 comment

 

Makamu wa Rais azindua Kamisheni ya Kiswahili

MAKAMU wa Rais, Samia Hassan Suluhu amezindua rasmi Jumatano Septemba 6, 2017 shughuli za Kamisheni ya Kiswahili Afrika Mashariki, lengo  likiwa ni kuisogeza karibu taasisi hiyo muhimu ya lugha kwa  soma zaidi...


26/7/2017 comment

 

MWAMKO MPYA: Kamusi Kuu ya Kiswahili yenye maneno ya kidijitali yazinduliwa

WIZARA ya Elimu inapania kupeleka mswada katika Bunge la Afrika Mashariki kwa lengo la kuhakikisha mwanachama anakitumia na kukienzi Kiswahili. Haya ni kulingana na Waziri wa Elimu, Sayansi na  soma zaidi...


18/4/2017 comment

 

Athari za Fasihi Simulizi katika Fasihi Andishi

Fasihi Andishi imeathiriwa pakubwa na Fasihi Simulizi kimaudhui na kifani kadri inavyobainika katika vipengele vifuatavyo:  soma zaidi...


18/4/2017 comment

 

Uambishaji katika vitenzi vya Kiswahili

KATIKA uzoefu wangu wa kufundisha Kiswahili, hakuna wakati darasa linapochangamka zaidi kama wakati wa mada ya Uambishaji, na mahsusi kuhusu vitenzi.  soma zaidi...


18/4/2017 comment

 

Mabadiliko ya mitaala yanavyochangia mabadiliko katika uandishi na ufundishaji wa Kiswahili

DHANA mtaala imeelezwa kwa namna mbalimbali na wataalamu tofauti wa elimu. Bobbit (1968 katika Okech & Asiachi 1992) kwa mfano amedai kuwa mtaala ni ule mfululizo wa vitu ambavyo watoto na vijana  soma zaidi...


18/4/2017 comment

 

Kiswahili sanifu na kaida za ushairi wa kimapokeo

KATIKA utunzi wa ushairi wa kimapokeo unaofuata kaida za arudhi, mambo yanakuwa magumu zaidi kwa uteuzi wa vipashio vya maneno, maana kunaingia haja ya vipimo vya maneno kwa mujibu wa mizani.   soma zaidi...


18/4/2017 comment

 

Kiswahili sanifu na lahaja ya Kipemba

KWA muda mrefu, dhana ya Kiswahili Sanifu imejadiliwa sana na katika kazi mbalimbali za Fasihi ya Kiswahili – fikra ya kwamba fasihi inayostahiki kusomwa miongoni mwa watu wetu wa Afrika Mashariki  soma zaidi...


19/2/2017 comment

 

Vipengele vinavyojenga na kukuza tofauti kati ya fasihi ya watoto na ya watu wazima

FASIHI ya watoto ni sanaa inayotumia lugha kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyo chini ya umri wa miaka 18.  soma zaidi...


19/2/2017 comment

 

Uchotara wa lugha ya Kiswahili una msingi katika chimbuko na asili yake

WATAALAMU wa lugha wameandika kuhusu Kiswahili kama lugha ya taifa na lugha rasmi inayokadiriwa kutumiwa na watu wapatao zaidi ya milioni 60 duniani kote.  soma zaidi...


19/2/2017 comment

 

Mchango wa Wizara ya Elimu katika maendeleo ya lugha

WIZARA ya elimu nchini Kenya ni mojawapo ya asasi mbalimbali zenye nafasi muhimu katika ukuzaji wa lugha ya Kiswahili.  soma zaidi...


19/2/2017 comment

 

Nafasi ya sayansi katika uchunguzi wa Isimu na Lugha

MATUMIZI ya lugha rasmi aghalabu hutegemea matukio, wakati, idadi ya walengwa, uhusiano baina ya mzungumzaji au mwandishi na hadhira yake pamoja na uwezekano wa habari kuwa ama za kibinafsi au kwa  soma zaidi...


19/2/2017 comment

 

Uendelezaji wa Kiswahili katika enzi za dijitali

KUNA haja ya kushirikisha vyombo mwafaka na wadau mbalimbali wa lugha, ikiwa ni pamoja na wasomi na wataalamu katika kutangaza, kueneza, kuendeleza na kuinua hadhi ya Kiswahili na utamaduni wake  soma zaidi...


19/2/2017 comment

 

Hatua za uchapishaji wa miswada ya vitabu

UCHAPISHAJI wa miswada ya vitabu hupitia hatua mbalimbali. Hatua hizi hata hivyo zinaweza kuwa ama nyingi au chache kwa kutegemea shirika au kampuni husika ya uchapishaji.   soma zaidi...


19/2/2017 comment

 

KONGAMANO LA CHAWAKAMA KENYA LILIVYOFUA DAFU MWAMBAO WA PWANI

KONGAMANO la Kiswahili lililoandaliwa na Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili katika vyuo vikuu vya Afrika Mashariki (CHAWAKAMA-Kenya) katika Chuo Kikuu cha Pwani lilifanikiwa pakubwa jinsi  soma zaidi...


19/2/2017 comment

 

Sababu za wanafasihi kuchelewa kubainisha utanzu wa Ngomezi katika Fasihi Simulizi

HISTORIA ya ngomezi ni kongwe kama ilivyo historia ya uumbaji wenyewe. Katika sehemu nyingi za Afrika, ngomezi hutumika kama njia ya mawasiliano, kutoa tahadhari na kuburudisha watu katika makasri  soma zaidi...


19/2/2017 comment

 

Sanaa si kiwakilishi cha maisha halisi ya wanajamii nyakati zote

INGAWAJE kazi ya fasihi kwa kawaida huwa yamithilisha au kujaribu kuumba upya maisha kwa njia moja au nyingine, tunatambua ukweli kwamba yaliyotungwa na mwanafasihi si katika sanaa yake si  soma zaidi...


19/2/2017 comment

 

Upekee wa sifa ya makundi ya jamii katika matumizi ya lugha

LUGHA inazidi kutegemewa pakubwa katika jitihada za kuleta mabadiliko na maendeleo kwa wanajamii na huwa na athari chanya na hasi kwa kutegemea watumiaji wake, yaani wasemaji na wasemewa.   soma zaidi...


19/2/2017 comment

 

Changamoto zinazoikabili Wizara ya Elimu katika kukuza Kiswahili

ILI kufanikiwa katika jitihada za kukuza na kutukuza Kiswahili, Wizara ya Elimu inastahili kuzielewa na kuzikabili changamoto mbalimbali zinazoikumba katika utekelezaji wa majukumu yake.   soma zaidi...


19/2/2017 comment

 

Umuhimu wa kufundisha watoto wenye umri mdogo kwa lugha za asili

UHUSIANO kati ya lugha, mazingira ya binadamu na mirathi ya jamii kwa jumla huenda ukafahamika angalau kwa wepesi zaidi, iwapo tutazingatia mambo mawili.   soma zaidi...


19/2/2017 comment

 

Uhusiano uliopo kati ya lugha, fani na utaalamu wa mtu

INGAWA ufahamu wa kina wa Kiingereza hauna maana ya kuwa mtaalamu katika eneo lako la kazi, hakuna ubishi kwamba kujua Kiingereza si sifa ya ubora.   soma zaidi...


19/2/2017 comment

 

Nafasi ya ushairi katika Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi

USHAIRI wa Kiswahili una dhima kubwa mno katika Fasihi Simulizi na Andishi. Ushairi umetumiwa sana katika tanzu mbalimbali za fasihi kwa sababu mbalimbali.  soma zaidi...


19/2/2017 comment

 

Kiswahili ni fimbo ya wanyonge dhidi ya teknolojia za mataifa makuu

KISWAHILI ambacho kinaongoza kwa ukubwa na umaarufu zaidi miongoni mwa lugha kuu za asili barani Afrika kinazidi kushuhudia mwamko mpya.  soma zaidi...


22/2/2017 comment

 

Mipaka baina ya Fani na Maudhui katika Ushairi wa Kiswahili

FANI na maudhui ni vipengele vya ndani vinavyojenga shairi. Kuna uhusiano mkubwa kati ya fani na maudhui ambayo ni jumla ya fikira au mawazo ya mtunzi yeyote wa kazi ya sanaa. Ni kama pande mbili  soma zaidi...


22/2/2017 comment

 

Nguvu ya lugha za kigeni katika kuathiri utunzi na uwasilishaji wa Fasihi ya Kiafrika

MATUMIZI ya lugha aghalabu husadifu kuwa ndio msingi wa kuendeleza na kukuza, na hata pia kubuni uzushi mpya katika mirathi ya utamaduni, mila na hulka za kijamii.  soma zaidi...


22/2/2017 comment

 

Utata wa kubaini mzizi wa kitenzi ng'ang'ania

JE, ni kweli kwamba kuna kitu kinachoitwa ‘Kiswahili Sanifu’ katika udhati wake, au hii ni dhana ya kitaalamu tu inayotumiwa kuelezea hali isiyokuwapo katika lugha, lakini kwa mantiki ya kuifanya  soma zaidi...


22/2/2017 comment

 

Dhana na msisitizo wa sajili umo kwenye matumizi ya lugha katika taaluma husika

SAJILI ni aina ya lugha katika lugha moja kwa kutegemea kazi mbalimbali. Kila taaluma au uwanja wa kikazi hudhihirisha tofauti za kipekee katika matumizi ya lugha.  soma zaidi...


22/2/2017 comment

 

Sheng inavyozidi kuazima msamiati kutoka kwa Kiingereza na lugha asili

KUNA haja ya kuielewa lugha kuwa si tu kielelezo cha utamaduni bali ni njia mahsusi ya kuelezea na kusambazia utamaduni wenyewe. Katika maana hii, Kiswahili kimepewa umuhimu mkubwa sana kama wenzo  soma zaidi...


22/2/2017 comment

 

Umuhimu wa kuzingatia saikolojia katika utunzi wa fasihi

JINSI ilivyo katika sanaa nyinginezo, mvuto ni kitu cha kimsingi sana katika fasihi. Kipengele hiki cha mvuto ni muhimu zaidi katika fasihi ya watoto na vijana.  soma zaidi...


22/2/2017 comment

 

Upekee wa mwandishi kama kipengele cha mtindo katika kazi ya fasihi

FASIHI ni sanaa inayotumia lugha na ambayo hujishughulisha na binadamu pamoja na maisha yake na hugusa au huacha athari fulani na hupatikana katika umbo ambalo linatambuliwa na jamii.  soma zaidi...


22/2/2017 comment

 

Nafasi ya muziki wa kisasa katika maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili

NYIMBO zina majukumu mbalimbali ambayo hutekeleza katika jamii. Dhamira kuu ya fasihi ni ile ya kuielimisha na hata kuiburudisha jamii.  soma zaidi...


22/2/2017 comment

 

Kiswahili kama fumbato la desturi na itikadi za wanajamii

LUGHA hubadilika kadri jamii inavyobadilika. Kama sehemu ya utamaduni, lugha ni amali ya jamii inayoizungumza na ina alama ya umoja wa kitaifa kwa sababu kama kitendo, ni zao la amana ya jamii.  soma zaidi...


22/2/2017 comment

 

Kila lugha ina kanuni za kisarufi zinazodhibiti usahihi wake

SIDHANI yapo manufaa yoyote mengine ya lugha nje ya kutimiza kiini kikuu cha mawasiliano. Mojawapo ya sifa kuu za lugha yoyote ni kwamba hutumiwa miongoni mwa binadamu pekee ili kudumisha  soma zaidi...


22/2/2017 comment

 

Ni madawa ya kulevya au dawa za kulevya?

Taasisi na watu wenye nyadhifa mbalimbali katika jamii wana athari kwa wengine wanapotumia lugha.  soma zaidi...


 

Chimbuko na asili ya lugha

Na CHRIS ADUNGO

Imepakiwa - Sunday, May 8  2016 at  21:36

Kwa Muhtasari

Hakuna maafikiano yoyote miongoni mwa wanaisimu kuhusu ni wapi, lini, namna gani au nani hasa alianzisha lugha.

 

HAKUNA maafikiano yoyote miongoni mwa wanaisimu kuhusu ni wapi, lini, namna gani au nani hasa alianzisha lugha.

Hii inatokana na ukweli kwamba, binadamu alianza kuishi tangu kale katika kipindi cha wakati ambao hata hivyo bado haujajulikana.

Suala ambalo halina upingamizi ni kuwa, lugha inatumiwa na mwanadamu na kila jamiii na lugha yake mahsusi inayodumisha mawasiliano ya kila siku. Hata hivyo, kuna nadharia mbalimbali zinazoeleza chimbuko na asili ya lugha.

MTAZAMO WA KIDINI

Msingi wa nadharia hiini kwamba, lugha iliumbwa na Mungu na akapewa mwanadamu kwa nguvu za Mwenyezi Mungu. Inaelezakuwa, haja ya Mungu kuwasiliana na kiumbe wake Binadamu ndiyo iliyomchochea aumbe lugha.

Inaaminika kuwa, Mungu ndiye alikuwa wa kwanza kutumia lugha, aliumba ulimwengu kwa kutumia neno, na kwa neno kila kitu akiwemo mwanadamu kilifanyika. Inaaminika kuwa lugha zote zilitokana na lugha moja iliyoumbwa na Mungu.

Hata hivyo kuna visasili mbalimbali vinavyoeleza asili ya lugha katika nadharia ya Uungu. Kwanza ni, pale Mungu alipompa Adamu uwezo wa kuzungumza kwa kuwatajia majina wanyama wote na pale ndipo lugha ilipoanza (Mwanzo2:19).

Nadharia hii ya Uungu pia huchagizwa na kisasili kingine cha Wamisri, Wababilonina Wahindi. Kwa mujibu wa kisasili cha Wababiloni, inasemekana hapo kale Mfalme wa Babeli aliamuru kujenga mnara mrefu ulioitwa Mnara wa Babeli ili kumfikia Mungu.

Kwa lengo hilo, Mungu alikasirishwa sana akaamua kuwachanganya lugha wajenzi wa mnara huo hivyo wakashindwa kuelewana na hatimaye azma yao ikasitishwa.

Kwa hiyo kutokana na imani hiyo waumini wengine wanakubali kuwa, yawezekana lugha nyingi zinazoonekana leo ni tokeo la mnara wa Babeli. Kama hivyo haitoshi,Wamisri wanachagiza nadharia hii kwa kuwa na mungu wao aliyeitwa “Thoth”ambaye ni 'mungu wa lugha’.

Wahindu walihusisha uwezowa mwanadamu wa kuzungumza namungu wao wa kike aliyeitwa “Brahma” ambaye kwaimani yao ndiye mungu muumbaji wa ulimwengu lakini lugha alipewa mwanadamu kutoka kwamke wake aliyeitwa “Sarasvati”.

Suala la msingi katika nadharia hii ni kwamba, lugha za mwanadamu zina chanzo kimoja na ndio maana wanaisimu wa baadaye wamekuwa wakizungumzia suala la sarufi bia.

Udhaifu wake ni kwamba, zinashindwa kujibu maswalikama vile - kwa nini lugha nyingine zinazuka tu siku hizi na hazitoki kwa Mungu.

Vile vile, mtazamo huu haujajikita katika tafiti za sayansi ya lugha, yaani, isimu. Pia haujafuata taratibu za kiuchunguzi wa kiisimu ambazo huunga sayansi ya lugha.

KUIGA SAUTI ZA ASILI

Nadharia nyingine inayoelezajuu ya asili ya lughani ile ya Wigo. Kwa mujibu wa Yule (2010), nadharia hii inashikilia msimamo kuwa, sauti za awali kabisa za lugha ya binadamu ni matokeo ya binadamu kuiga sauti asilia ambazo wanawake na wanaume walizisikia katika mazingira yao.

Nadharia hii inapigiwa upatu na baadhi ya maneno ambayo yanatokana na sauti asilia za milio ya vitu kama vile vitu vinapodondoka au kugongana ambayo huitwa onomatopoeia.

Pamoja na uthibitisho unaoweza kutolewa kwa maneno hayo machache ambayo huenda kila lugha inayo, bado kuna udhaifu katika nadharia hii.

Nadharia hii haijitoshelezi kwa kuwa, kuna maneno mengi tu ambayo kwa asili yake hayatokani na milio ya vitu, kama majina, na vitenzi ambavyo ni matokeo ya njia nyingine za uundaji wa maneno na siyo uigo wa sauti asilia.

MAHUSIANO YA KIJAMII

Nadharia hii inashikilia msimamo kuwa, wakati fulani katika maisha ya mwanadamu, alihitaji msaada wa mwanadamu mwingine katika kufanya kazi.

Katika kazi hizo binadamu hao walitoa milio na sauti mbalimbali za kuhamasishana. Kutokana na sauti hizo yasemekana ndipo lugha ilipoanza.

Hata hivyo, nadharia hii inatupa wazo moja muhimu kwamba maendeleo ya lugha ya mwanadamu yanatokana na mazingira ya kijamii alimoishi mwanadamu.

Kwa hiyo wanadamu lazima waliishi katika makundi ya kijamii, kama hilo linaweza kukubalika, lazima tukubali kuwa, yamkini kulikuwa na kanuni maalum ambazo zilitawala mfumo wao wa mawasiliano katika maisha yao na mahusiano yao ya kijamii.

Pamoja na hayo, nadharia hii bado inatunyima majibu ya swali letu la msingi juu yaasili ya hizo sauti zilizozalishwa.

Kama chanzo cha lugha ni mahusiano ya kijamii, kuna wanyama wengine wanaoishi katika makundi makundi kama vile tumbili na ngedere lakini mawasiliano haya hayaendelei kuwa matamshi ya lugha.

MAUMBILE YA MWANADAMU

Badala ya kuchunguza asili ya sauti za mwanadamu na kutoa tamko kuwa huenda ndizo chanzo na asili ya lugha ya mwanadamu, ni vyema kuangalia sifa za kimaumbile alizonazo mwanadamu.

Uchunguzi huu unajikita katika zile sifa ambazo viumbe wengine (wanyama) hawana (Yule, 2010).

Msimamo wa nadharia hii ni kuwa tofauti ya kimaumbile kati ya mwananadamu na wanyama wengine ndicho kilichokuwa chanzo cha lugha ya mwanadamu.

Lugha hiyo ndiyo nyenzo muhimu anayoitumia binadamu kufanikisha mawasiliano ya siku hadi siku.

 

 

Zilizopata Umaarufu