Mama wa thamani

 

Imepakiwa - Wednesday, June 13  2018 at  16:45

 

Dua njema nakombea,

Mama ngu ulonilea,

Mpaka Leo nimekua,

Japo kwako ni mtoto.

 

Mengi nimeyapitia,

Kipindi kile nakua,

Leo mama natambua,

Jinsi ulivyonilea.

 

Hakika uliumia,

Machungu ukasikia,

Ulipoona nalia,

Hukusita bembeleza.

 

Cha kukulipa ni nini,

Cha thamani duniani,

Hata kama ni madini,

Yawezi kutosheleza.

 

Namuomba Rahamani,

Akupe sana Imani,

Muumba wetu manani,

Akuzidishie kheri.

 

Izidi yako Imani,

Mama yangu wa thamani,

Mfano e duniani,

Hakuna wakutokea.

 

Moyo wapata Amani,

Furaha yatoka ndani,

Najiona wa thamani,

Nikonapo mama yangu.

 

Thamaniyo kubwa sana,

Kwako mama najichana,

Nywele uliponchana,

Hakika nilipendeza.

 

Idd Ninga, Arusha, 255624010160,