http://www.swahilihub.com/image/view/-/4024400/medRes/917755/-/a8xxn3/-/DNFidel0801vv.jpg

 

Ngonjera: Jubilee Vs Nasa

Uhuru Kenyatta na Raila Odinga

Rais Uhuru Kenyatta na mwaniaji urais wa NASA Bw Raila Odinga awali. Picha|BILLY MUTAI  

Na JIMMY NAIBEI

Imepakiwa - Thursday, July 20  2017 at  14:46

Kwa Muhtasari

Jubilee

JUBILEE pia guru, twasimama kama wani,

Kumpa Mkenya uhuru, kufanya yalo moyoni,

Japo chache haidhuru, mengi yapo machoni,

Nasa hamtuwezi ng'o, baba ashakua babu.

 

Nasa

Unga pia na sukari,gharama tu hatusemi,

Mwajiita tu serikali, Mkenya tu ni ukemi,

Mwatujengea tu mochari, kateni yenu ulimi,

Nasa tutawanasa, wakati ndio sasa.

Mkenya

Kwa upole nauliza,langu swali peupeni,

Vipi tumbo kutuliza, sima bei i angani,

Bajeti kutuliza,viongozi zindukeni,

Hurumia wazalendo, gharama chunguzeni.

Nasa

Virago vyenu fungeni, Mkenya ashasema

Kama vipi twawambieni, vintu vichenjanga

Wakora kwaherini, Kenya yetu i majanga

Nasa tutawanassa, wakati ndio sasa

Jubilee

Korti hiyo mwatumia, kubadili tu katiba,

Kujizolea pia silimia, mmebaki mwatiba,

Akili Mkenya tumia, si eti tu ni baba,

Nasa hamtuwezi ng'o, baba ashakua babu.

Kauli ya wote

Twashikana mikono,pawani saidiana,

Sisi sote tuwe wino, tuache kupigana,

Tuyaache ya ujino, tubaki kupendana,

Kenya yetu tuilinde, pia kesho twahitajika.

Ngonjera na Jimmy Naibei, kaunti ya Bungoma

Simu - 0705832873

Shukrani.