MTUKUFU RAMADHANI

Mzee Mwislamu

Mzee Mwislamu aomba wakati wa kuanza kwa sherehe za Idd ul-Fitri za kuadhimisha mwisho wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan uwanja wa Afraha, Nakuru. Picha/SULEIMAN MBATIAH 

Na Qamdula Msimbe Chamiyago

Imepakiwa - Monday, June 5   2017 at  11:19

Kwa Mukhtasari

MWEZI HUU: Mtukufu Ramadhani,

Sio wa machapunga, wa kulakula njiani,

 

Ni mwezi wa kuyapunga, matendo ya kishetani,

Mtukufu Ramadhani, ndio huyo -kaingia.

 

MWEZI HUU: Mashetani, wamefungwa gerezani,

Wamefungwa wako ndani, nje hawaonekani,

Mwezi huu Rahmani, kaupa nyingi thamani,

Mtukufu Ramadhani, ndio huyo-kaingia.

 

MWEZI HUU: wa ibada, tumwombe sana Munani,

Si mwezi wa kawaida, Ukiandamana angani,

Utakapopita muda,  sitegemee mwakani,

Mtukufu Ramadhani, ndio huyo-kaingia.

 

MWEZI HUU:tenda mema, kwa wa mbali na jirani,

Kisha kuwa na huruma, fanya watu hisani,

Mungu aliowanyima, huo ndio mtihani,

Mtukufu Ramadhani, ndio huyo-kaingia.

 

NAMALIZA : kuandika, Al-Qadr Jeilani,

Mwezi huu wa Baraka, wa amani na imani,

Si wa kucheza Bomboka, Msondo na Kiubani,

Mtukufu Ramadahni, ndio huyo-kaingia.

Qamdula Msimbe Chamiyago

Morogoro.