http://www.swahilihub.com/image/view/-/2843572/medRes/1099906/-/pm4nub/-/DNGORVERSESAFC2308cc.jpg

 

CHUI MNYAMA MKALI

Mashabiki wa AFC Leopards

Mashabiki wa AFC Leopards wakitembea barabara za jiji la Nairobi Agosti 23, 2015. Picha/EVANS HABIL 

Na SHUGULI BARAZA NYIKA wa Ukunda, Kwale

Imepakiwa - Tuesday, March 13  2018 at  07:09

Kwa Muhtasari

Zama zile zamani, Leopards tuliamini,

Tufikapo uwanjani, tulicheza kwa makini.

 

ZAMA zile zamani, Leopards tuliamini,
Tufikapo uwanjani, tulicheza kwa makini,
Sasa ni namna gani, kwenu hatuna imani,
Chui mnyama mkali, na mbio hawezekani.

Siku hizi mko hoi, mumepoteza ukali,
Na mbio hamkimbii, zile zenu za awali,
Mumepoteza bidii, hamna yale makali,
Chui mnyama mkali, na mbio hawezekani.

Wawapi kina Masiga, wachezaji wa zamani,
Wapinzani wakibwaga, magoli kuweka ndani,
Mpira wakiupiga, kuwashinda wapinzani,
Chui mnyama mkali, na mbio hawezekani.

Suluhu tuliyopata, hapa petu uwanjani,
Tamaa tumeshakata, tuendako ugenini,
Watatupeleka puta, kule kwao uwanjani,
Chui mnyama mkali, na mbio hawezekani.

Twawaombea bahati, muendako ugenini,
Mola tupe kisimati, cha kushinda uwanjani,
Maana shatii sharuti, goli moja ugenini,
Chui mnyama mkali, na mbio hawezekani.