http://www.swahilihub.com/image/view/-/2106350/medRes/641168/-/5jswolz/-/DNNakuruUASU0709y.jpg

 

HAKI ZAO HADI LINI?

Mgomo wa wahadhiri

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Egerton, Njoro waondoka chuoni awali. Picha/SULEIMAN MBATIA 

Na LUDOVICK MBOGHOLI 'Al Ustadh Luqman: Ngariba Mlumbi (001)'

Imepakiwa - Saturday, March 10  2018 at  09:03

Kwa Mukhtasari

Wahadhiri wanagoma, mishahara hawaoni,

Wanadai haki zao, nauliza kunani?

 

NILIPOANZA kusoma, chekechea darasani,

Wahadhiri wanagoma, mishahara hawaoni,

Na walimu walalama, maisha yao ni duni!

Wanadai haki zao, nauliza kunani?

 

Niko shule ya msingi, bado hali hiyo hiyo,

Ni wahadhiri kwa wingi, na walimu wako mbiyo,

Haki zao za msingi, zazibiwa masikiyo!

Wananyimwa haki zao, nnauliza kunani?

 

Na nikiwa sekondari, mambo bado ni magumu,

Walemewa wahadhiri, na wenzao waalimu,

Serikali yaghairi, kuwalipa yawa sumu!

Hawapawi haki zao, nnauliza kunani?

 

Nikenda chuo kikuu, nikaona wahadhiri

Nyoyo zao ziko juu, mno zimejaa shari

Hawaipati nafuu, serikali yaghairi!

Kupatiwa haki zao, nauliza hadi lini?

 

Leo nnafanya kazi, bado tuu wang’ang’ana,

Wahadhiri wako bizi, na walimu nawaona,

Malipo yao ajizi, serikali imetuna!

Hailipi haki zao, nauliza kunani?