http://www.swahilihub.com/image/view/-/2831668/medRes/1090180/-/12hnm7tz/-/shoka.jpg

 

KISA KUKOSA AJIRA?

Shoka

Shoka. Picha/HISANI 

Na BEATUS KUSAGA ‘Sauti ya Kasuku’

Imepakiwa - Thursday, May 3  2018 at  16:09

Kwa Mukhtasari

Kosa ajira au pesa ujue tabia ya mpenzi wako.

 

MUDA wote hasira,
Kukunjiana sura,
Naonekana hasara,
Nyoka sina madhara.
Mara sina ubora,
Naishi kama chura,
Unasema nazurura,
Unasema sina sera,
Naishia kukuchora.

 

Sitakiwi kucheka,
Wala siwezi kudeka,
Naonekana mateka,
Mara umenichoka,
Mara nmepauka,
Mara napepesuka,
Mara eti ninanuka,
Nikiongea naropoka.

 

Jamii inaniona pimbi,
Sinyi wala sijambi,
Mtaani sijigambi,
Wala silijali vumbi,
Popote natia kambi,
Lakini pesa silambi.

 

Kutwa na mibahasha,
Usahili wa kutisha,
Maswali ya kutosha,
Tamaa kunikatisha,
Nkicheka najichekesha,
Nikurudi nakuchosha,
Mbali wankumbusha,
Enzi hzo nakuogesha,
Enzi nakunogesha,
Enzi hizo nakulisha,

Kusoma nimesoma.

Ila natia huruma,
Elimu hii inapima,
Nikajua tansukuma,
Ubaguzi unanitema,
Wengine husema,
Ulimwengu ndo mama.

 

Simezi wala sitemi,
Ukikosea sisemi,
Mpnz mekua kichomi,
Sipumui wala sihemi,
Unanambia sikomi,
Eti umbali sipimi,
Eti nichunge ulimi.

 

Ipo siku nitapata,
Majina yote taniita,
Hapo ndo utajuta,
Mishuzi itakupita,
Kukumbk yalopita,
Polepole tajikata.

 

Eti nione aibu,
Eti nakupa tabu,
Eti nina majaribu,
Eti siishiwi gubu,
Eti naonkana babu,
Eti kanisan nkatubu,
Eti sina adabu.

 

Mara mzungu wa nne,
Mara ununenune,
Mara uende kwingine,
Mara hutaki nikukune,
Mara hutaki nikuone,
Nikiugua nisipone,
Mara oh tuachane,
Mara unitukane.

 

Ujumbe

Kosa ajira au pesa ujue tabia ya mpenzi wako.


Beatus Kusaga
Sauti ya Kasuku
+255719368158