http://www.swahilihub.com/image/view/-/4318456/medRes/1893514/-/wn445mz/-/renyatta.jpg

 

KUELEWANA

Uhuru Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta ahutubu Busia Februari 24, 2018, baaada ya yeye pamoja na Rais Yoweri Museveni kufungua kituo cha huduma ya pamoja mpakani Kenya na Uganda. Picha/PSCU 

Na JUSTIN GUNGA CHEA akiwa Mariakani, Kilifi

Imepakiwa - Tuesday, May 22  2018 at  16:22

Kwa Muhtasari

Si vizuri kugombana, katika mipaka yetu,

Vizuri kuelewana, na jirani ndugu zetu.

 

NI vyema kuelewana, majirani ndugu zetu,
Si vizuri kugombana, katika mipaka yetu,
Jambo zuri la maana, tuishi na ndugu zetu,
Vizuri kuelewana, na jirani ndugu zetu.

Mi nachukizwa sana, tokea uhuru wetu,
Twaishi tukigombana, sisi pamwe ndugu zetu,
Hatuna kuelewana, katika mipaka yetu,
Vizuri kuelewana, na jirani ndugu zetu.

Hasira zimejazana, katika mitima yetu,
Hatuwazi kupatana, mabaya maisha yetu,
Sifa zetu kugombana,sisi na wale wenzetu,
Vizuri kuelewana, na jirani ndugu zetu.

Kila tunapozozana, hakuna faida kwetu,
Halafu tukipigana, ni nini faida yetu,
Tuishi kwa kupendana, tuwe na sifa za utu,
Vizuri kuelewana, na jirani ndugu zetu.

Baraka tutaziona, tukijenga ushirika,
Kazi zetu zitafana, na uchumi kadhalika,
Mafao tutafaana, tutakalo tutashika,
Vizuri kuelewana, na jirani ndugu zetu.

JUSTIN GUNGA CHEA
Mariakani, Kilifi