http://www.swahilihub.com/image/view/-/3080946/medRes/1258813/-/pxo04c/-/redio.jpg

 

MAFUNDI WENGI BANDIA

James Okeyo Alara

Licha ya kupooza mikono kwa sababu ya Polio, ubongo wa James Okeyo Alara ulibakia katika ubora wake na hivyo amesalia kuwa fundi stadi wa redio. Picha/NELCON ODHIAMBO 

Na MWINYI HAJI MWALIMU akiwa Lungalunga Mpakani

Imepakiwa - Tuesday, May 22  2018 at  15:58

Kwa Muhtasari

Supea zilizotajwa, heri mpya ninunue,

Mafundi wengi bandia, wa TV na redio.

 

MAFUNDI wengi bandia, wa TV na redio,
Kama wataka kulia, jaribu mafundi hao,
Mimi nimeshakwambia, jaribu uwaonao,
Mafundi wengi bandia, wa TV na redio.

Hakuna hata mmoja, ajuaye kazi hio,
Ukenda kwake kioja, kumejaa maredio,
Na TV pamoja, za kufanya danganyio,
Mafundi wengi bandia, wa TV na redio.

Nikugusie kioja, kilonipata mwenzio,
Ilikuwa siku moja, ina kasoro redio,
Nikenda kwake mmoja, wa TV na redio,
Mafundi wengi bandia, wa TV na redio.

Ndio ikawa kimoja, yangu redio mwishowe,
Nilingoja nikangoja, nitengezewe isiwe,
Kila kukicha ni hoja, zinaelezwa zikawe,
Mafundi wengi bandia, wa TV na redio.

Supea zilizotajwa, heri mpya ninunue,
Pesa zangu zikafujwa, ili vitu anunue,
Hiki kile kikatajwa, hayo nilijionea,
Mafundi wengi bandia, wa TV na redio.

Wenzangu ndugu chungeni, hawa mafundi bandia,
Ni wengi sana mijini, mafundi nawaambia,
Hawaogopi ya nani, TV kuigungua,
Mafundi wengi bandia, wa TV na redio.

MWINYI HAJI MWALIMU

Lungalunga Mpakani