http://www.swahilihub.com/image/view/-/3174194/medRes/1310731/-/sq5p4t/-/blakauti.jpg

 

MAISHA YA ZAMA ZILE

Nguvu za umeme kupotea

Eneo zima la mji pamoja na viunga vyake usiku nguvu za umeme zikiwa zimepotea. Picha/HISANI 

Na TSEMBEA MAMBO ZUMA akiwa Mombasa

Imepakiwa - Tuesday, May 22  2018 at  16:13

Kwa Muhtasari

Maisha tunayoona, hivi sasa siku hizi,
Hayawezi kufanana, na ya zama hayawezi.

 

MAISHA tunayoona, hivi sasa siku hizi,
Hayawezi kufanana, na ya zama hayawezi,
Vijana tunawaona, tabia zao wapuzi,
Maisha ya zile zama, si sawa na siku hizi.

Yale tunayoyaona, kwa vijana siku hizi,
Adabu wote hawana, wengi wao majambazi,
Jelani wamejazana, mfano wa sisimizi,
Maisha ya zile zama, si sawa na siku hizi.

Hukaa wakizozana, kwa maneno ya upuzi,
Na wengine kupigana, kupatana hawawezi,
Maisha yale ya jana, yako wapi siku hizi?
Maisha ya zile zama, yako wapi siku hizi?

Hayo yalikwisha zama, na kurudi hayawezi,
Hasa kwa wetu vijana, hawa wa kisiku hizi,
Zimepita hizo zama, na kurudi haziwezi,
Maisha ya zile zama, yako wapi siku hizi?

Wavulana wasichana, tabia zao wafyozi,
Kwetu faida hawana, wamekataa malezi,
Mtapata tabu sana, mkiwapuza wazazi,
Maisha ya zile zama, yako wapi siku hizi?

TSEMBEA MAMBO ZUMA
Mombasa