http://www.swahilihub.com/image/view/-/3099934/medRes/1270158/-/upf4u3/-/dnkisii1808ert.jpg

MAVAZI YA WANAWAKE

Daraja Mbili

Wanunuzi wajaribu sidiria za mtumba katika soko la Daraja Mbili mjini Kisii mnamo Agosti 18, 2014. Picha/DENNISH OCHIENG 

Na MGENI WETU

Imepakiwa - Friday, March 9  2018 at  11:21

Kwa Muhtasari

Mavazi yenu aili, kuyavaaa mmegoma,

Mavazi ya kina mama, chanzo cha matamanio.

1

ENZI tulizokulia, zama zile za ujima,
Gauni walovalia, zilikuwa za heshma,
Mavazi ya asilia, yalikuwa ni alama,
Mavazi ya kina mama, chanzo cha matamanio.

2

Chanzo cha matamanio, mavazi ya kina mama,
Yabanayo makalio, na kiuno kutetema,
Sketi ta mpasuo, pembeni, mbele na nyuma,
Mavazi ya kina mama, chanzo cha matamanio.

3

Mfano ni bilausi, fupi wanazozipima,

Mgongo huacha wazi, mara anapoinama,

Na kitovu mbele wazi, anapotembea wima,

Mavazi ya kina mama, chanzo cha matamanio.

4

Mavazi ya kulalia, mchana wamwona vyema,
Tamaa yanachochea, rijali kukutazama,
Chambo akikurushia, vidole waumauma,
Mavazi ya kinamama, chanzo cha matamanio.

5

Mavazi yenu aili, kuyavaaa mmegoma,
Naa kuvaa suruali, gauni mmezitema,
Dhahiri kimaadili, wanawake mmezama,
Mavazi ya kina mama, chanzo cha matamanio.

6

Mwili wako mwanamke ubavu wangu gharama,
Huna budi ukumbuke, kuuhifadhi ni dhima,
Sio ovyo uoneke, kadamnasi ya ngoma,
Mavazi ya kina mama, chanzo cha matamanio.

7

Umeshafika wakati, itungwe sheria mama,
Iweze kuwadhibiti, wanawake maamuma,
Patolewe ithibati iwabane mahakama,
Mavazi ya kina mama, chanzo cha matamanio

8

Wanaume kimavazi, imara wamesimama,

Anayevaa shimizi,kichaa kwake lazima,

Aula umwite chizi, ilhali atagoma,

Mavazi ya kina mama, chanzo cha matamanio

9

Tamati yangu kauli, sitachoka kuwasema,

Chondechonde tafadhali, mngerudi mapema,

Mavazi yenu dhalili yaponda yenu heshima,

Mavazi ya kina mama, chanzo cha matamanio.

Mtunzi: Mgeni Wetu