http://www.swahilihub.com/image/view/-/2585914/medRes/919607/-/h456z/-/mchumba2.jpg

 

MCHUMBA  NIMTAKAE

Bibi arusi amvisha pete bwana arusi

Bibi arusi amvisha pete bwana arusi. Picha/HISANI 

Na MFAUME HAMISI 'Mshairi Machinga' wa Dar es Salaam

Imepakiwa - Friday, April 13  2018 at  07:15

Kwa Muhtasari

Awe mwembamba kidogo, na mrefu kadhalika,

Mchumba ni  mtakae, ni wapi nitampata.

 

AWE mwembamba kidogo, na mrefu kadhalika,

Msambaa si mgogo, mwenye pesa za kuteka,

Si hitaji wa kidigo, wa lafudhi ya kudeka,

Mchumba ni  mtakae, ni wapi nitampata.

Moyo asiupe pigo, mwili ukadhohofika,

Sitaki mtega tego, wezi wakakamatika,

Kina mwalami na chogo, mauti yakawafika,

Mchumba nimtakae, ni wapi nitampata.

Aso mwendo wa mikogo, asiyependa kudeka,

Hatumii mkorogo, na mekapu kujipaka,

Ngozi asichole logo, ya njiwa,kenge na nyoka,

Mchumba nimtakae, ni wapi nitampata.

MFAUME HAMISI 'Mshairi Machinga' wa Dar es Salaam