http://www.swahilihub.com/image/view/-/3428152/medRes/1469769/-/e7ff0c/-/feda.jpg

 

NAMKUMBUKA MWALIMU

Mwalimu Julius Nyerere

Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, marehemu Mwalimu Julius Nyerere. Picha/MAKTABA  

Na IGNAS JOACHIMU KOMBA

Imepakiwa - Monday, October 24  2016 at  15:30

Kwa Muhtasari

Mjamaa mfahamu, Juliasi etu mwalimu,

Leo imenilazimu, kumkumbuka Mwalimu.

 

LEO siku imetimu kumkumbuka Mwalimu,
Naifahamisha kaumu hili tukio muhimu,
Ili wapate fahamu, na mafunzo ya kudumu,
Leo imenilazimu, kumkumbuka Mwalimu.

Hakupeda kudhulumu, na katu si mhujumu,
Alikuwa mtaalamu, tena wetu mhudumu,
Leo imenilazimu kumkumbuka Mwalimu.

Apendaye ukarimu, mgeni humkirimu,
Fikira zake zidumu, huyu mtu muhimu,
Usiawe na udumu kwa ajili ya kaumu,
Leo imenilazimu, kumkumbuka Mwalimu.

Ninamwomba rahimu aisaidie kaumu,
Kutimiza majukumu, tuzungushe gurudumu
Maisha tuyaataimu, upendo kwetu udumu,
Leo imenilazimu, kumkumbuka Mwalimu.

Tusijepata waazimukutotaka ya Mwalimu
Na nchi kuihujumu, tukose wa kulaumu,
Wajanja kututaimu, tukibaki humuhumu,
Leo imenillazimu, kumkumbuka Mwalimu.

Alituasa Mwalimu, sharia kuziheshimu,
Ili kweli tudumu, tusipatwe na hukumu,
Na daima tufahamu, ya halali na haramu.
Leo imenilazimu, kumkumbuka Mwalimu.

Mjamaa mfahamu,Juliasi etu mwalimu,
Udini sio mtamu, aliona ni haramu,
Hazikuwa zake mbinu, kuigawanya kaumu,
Leo imenilazimu, kumkumbuka Mwalimu.

Alimpisha kwa zamu, na Mwinyi alimkarimu,
Tukapata na nujumu, toka kwake Rahimu,
Twangara kama ruhamu, toka Hindi mpaka shamu,
Leo imenilazimu, kumkumbuka Mwalimu.

Upeowe kama mlizamu,mwenye wingi ufahamu,
Alikuwa maalumu na wala sintofahamu,
Kwa yale asiyotimu, kwani yeye binadamu,
Leo imenillazimu, kumkumbuka Mwallimu.

Kwa lgha ilo nudhumu, shairi nalihitimu,
Leo sina mengi humu, nalaga na kaumu,
Namuomba na rahimu, amrehemu Mwalimu,
Leo imenilazimu, kumkumbuka Mwalimu.

Na Ignas Joachimu Komba

Tanzania, Afrika Mashariki

Imepitiwa na kuidhinishwa na Stephen Maina