http://www.swahilihub.com/image/view/-/3953310/medRes/1658764/-/t561msz/-/shahbal.jpg

 

MTUKUFU RAMADHANI

Suleiman Shahbal

Mgombea ugavana kaunti ya Mombasa kwa tiketi ya Jubilee Party, Suleiman Shahbal, afuturu pamoja na Waislamu Mei 30, 2017. Picha/MAKTABA 

Na QAMDULA MSIMBE CHAMIYAGO

Imepakiwa - Friday, June 2  2017 at  16:16

Kwa Muhtasari

Ni mwezi wa kuyapunga, matendo ya kishetani,

Mtukufu Ramadhani, ndio huyo -kaingia.

 

MWEZI HUU: Mtukufu Ramadhani,

Sio wa machapunga, wa kulakula njiani,

Ni mwezi wa kuyapunga, matendo ya kishetani,

Mtukufu Ramadhani, ndio huyo -kaingia.

 

MWEZI HUU: Mashetani, wamefungwa gerezani,

Wamefungwa wako ndani, nje hawaonekani,

Mwezi huu Rahmani, kaupa nyingi thamani,

Mtukufu Ramadhani, ndio huyo-kaingia.

 

MWEZI HUU: wa ibada, tumwombe sana Munani,

Si mwezi wa kawaida, Ukiandamana angani,

Utakapopita muda, sitegemee mwakani,

Mtukufu Ramadhani, ndio huyo-kaingia.

 

MWEZI HUU: tenda mema, kwa wa mbali na jirani,

Kisha kuwa na huruma, fanya watu hisani,

Mungu aliowanyima, huo ndio mtihani,

Mtukufu Ramadhani, ndio huyo-kaingia.

 

NAMALIZA: kuandika, Al-Qadr Jeilani,

Mwezi huu wa Baraka, wa amani na imani,

Si wa kucheza Bomboka, Msondo na Kiubani,

Mtukufu Ramadahni, ndio huyo-kaingia.

 

Qamdula Msimbe Chamiyago

Morogoro, Tanzania