http://www.swahilihub.com/image/view/-/3857924/medRes/1594073/-/kbyypb/-/ds.jpg

 

SIKU KUAGA UJANA

Bi Caren Anyango

Bi Caren Anyango, mkurugenzi na mwanzilishi wa Ujana Initiative Society, shirika linaloangazia jiinsi ya kusaidia vijana kujithamini na kujitegemea kwa kuwasaidia kunoa vipaji vyao. Picha/PAULINE ONGAJI 

Na RAYMOND NUSURA MGENI  (C) Malenga Wa Ubena 2018

Imepakiwa - Wednesday, April 11  2018 at  06:39

Kwa Muhtasari

Niliyoyaweza yale, muda huo sitaweza, 

Siku kuaga ujana, unapita haurudi.

 

NAFIKIRI siku hiyo, siku sinao ujana, 

Meno sina kibogoyo, macho hayaoni tena,

Mwili haunayo choyo, nguvu za ujana sina,

Siku kuaga ujana, unapita haurudi.

 

Huwa siwezi elewa, kuwa siku ipo yaja,

Mvi kichwa kitajawa, ujana hutaningoja,

Maisha yalokosewa, fainali hapo moja, 

Siku kuaga ujana, unapita haurudi.

 

Niliyoyaweza yale, muda huo sitaweza, 

Nitasema hapo kale, mengi nitayaeleza,

Kuzighani tungo zile, pengine nitaliwaza,

Siku kuaga ujana, unapita haurudi.

 

Ujana wafana mvuke, na moshi jikoni kama, 

Wasubiri tu utoke, huenda kitu kizima, 

Kazi nao ushikike, kushika hapo hugoma,

Siku kuaga ujana, unapita haurudi.

 

Kalamu haina wino, hapa nifikie mwisho,

Kijana sifa maono, ma’na una hitimisho, 

Kikomo kuna maneno, siku lipo kamilisho,

Unapita haurudi, siku kuaga ujana.

 

Raymond Nusura Mgeni 

+255 676 559 211, Dar es Salaam