http://www.swahilihub.com/image/view/-/2883872/medRes/1128213/-/jpww7h/-/TFHEKA2809.jpg

 

Soma shairi na ujibu maswali

Maonyesho ya Vitabu

Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Lukenya Academy Athi-River waelezewa na Bi Dorcas Bioto kuhusu Chuo Kikuu cha Kenyatta wakati wa Maonyesho ya Vitabu katika ukumbi wa Sarit Jijini Nairobi. Picha/ANTHONY OMUYA 

Na MWANDISHI WETU

Imepakiwa - Wednesday, March 7  2018 at  07:05

Kwa Muhtasari

Kusoma shairi lililotolewa na kujibu maswali.

 

USHAIRI

SOMA shairi lililotolewa na kujibu maswali ya shairi hilo:

Wanafunzi sikiliza, nawapa huu wasia,
Nataka kuwaeleza, mambo muhimu sikia,
Kwanza ninawapongeza, hapa mlikofika,
Hongereni, hongereni, hongereni kuhitimu.

Hapa mlikofika, kamwe msije bweteka,
Malengo kuyafikia huu ni mwanzo sikia,
Usije kuvizikia, vitabuvyo kwenye taka,
Hongereni, hongereni, hongereni kuhitimu.

Shuleni mmejifunza, masomo kwa uhakika,
Kiswahili ni cha kwanza, lugha hamkuichoka,
Kwa ari mkajifunza mbele kitawapeleka,
Hongereni, hongereni, hongereni kuhitimu.

Safari miaka saba, yenye raha na karaha,
Mlichopata si haba mwende nacho kwa furaha,
Hicho kidogo kibaba, kisilete majeraha,
Hongereni, hongeren, hongereni kuhitimu

Swali la 1
Mshairi anaposema “mlichopata si haba” ana maana gani?
A- Mlichopata si kilele
B- Mlichopata si kidogo
C- Mlichopata si duni
D- Mlichopata si dhaifu
E- Mlichopata si kibaya

Swali la 2

Vina katika ubeti wa pili ni vipi?
A- ha na ka
B- a na ka
C- ho na ho
D- ni na mu
E- u na v

Swali la 3

Wazo kuu katika shairi hili ni lipi?
A. Kuhitimu ni jambo muhimu
B. Elimu ya msingi ni bora zaidi
C. Kujiendeleza kielimu ni muhimu
D. Kiswahili ni somo la muhimu
E. Kuhitimu ni muhimu

Swali la 4

Kichwa kinachofaa kwa shairi hili ni kipi?
A. Ushairi kwa wahitimu
B. Kuhitimu ni fahari
C. Elimu ya Msingi
D. Wanafunzi wahitimu
E. Fahari ya kuhitimu

Swali la 5

Kinyume cha ‘karaha’ ni kipi?
A. Kero
B. Adabu
C. Furaha
D. Adhabu
E. Amani

Swali la 6

Neno “bweteka” kama lilivyotumika kwenye shairi hilo lina maana gani?
A. Kuridhika
B. Kudhihaki
C. Kudhoofka
D. Kudhalilika
E. Kudhihirika

Sehemu hii imenakiliwa kutoka kwa Necta