http://www.swahilihub.com/image/view/-/3174194/medRes/1310731/-/sq5p4t/-/blakauti.jpg

 

WASIOJULIKANA

Nguvu za umeme kupotea

Eneo zima la mji pamoja na viunga vyake usiku nguvu za umeme zikiwa zimepotea. Picha/HISANI 

Na BEATUS J. KUSAGA

Imepakiwa - Tuesday, May 8  2018 at  13:54

Kwa Muhtasari

Silaha anawapa nani?

Wasiojulikana.

 

HAWA ni kina nani?
Wanatoka nchi gani?
Lengo lao ni nini?
Ni binadamu au shetani?
Kiongozi wao ni nani?
Silaha anawapa nani?

Wasiojulikana.

Je wanaishi wapi?
Wanamiliki kipi?
Wanalipwa shingapi?
Kwanini hawaogopi?

Wasiojulikana.

Je ni Watanzania?
Nini tumewafanyia?
Mpaka wanatuua?
Wapi wanakotokea?
Nini wanadhamiria?

Wasiojulikana.

Wa mbili havai moja?
Kila kukicha vihoja,
Hebu tuungane pamoja,
Tuunde uhuru na umoja,

Wasiojulikana.

Kwani nini wanawaza?
Na nini tumewakwaza?
Kwanini wanatuliza?
Hawaoni wanatuumiza?
Lini watajituliza?

Wasiojulikana.

Iko wapi kauli yetu?
Laenda wapi taifa letu?
Je tukaishi kwenye misitu?
Kwanini hatuna utu?
Inapoteaje amani yetu?
Kwanini roho za kutu?
Eti kuna watu na viatu?
Heb vaeni viatu vyetu,
Hivi mnaishi huku kwetu?

Wasiojulikana.

Semeni nini tufate?
Je mtatupoteza wote?
Tusisikike popote?
Au asionekane yeyote?
Vipi tusiseme chochote?

Wasiojulikana

Hamjui tuna familia?
Hamtuoni tunalia?
Lini mtatuachilia?
Mbona tunapotea?
Je iko wapi njia?
Nini mnacho ashiria?

Wasiojulikana.

Ni kweli hamna huruma?
Ipi ni yenu dhima?
Mtafanya hivi daima?
Haijawahi kuwauma?

Wasiojulikana.

 

Beatus J. Kusaga
Sauti ya Kasuku

+255719368158