Ushirikiano na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA)

Na STEPHEN MAINA

Imepakiwa - Friday, October 7   2016 at  15:38

Kwa Mukhtasari

Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua katika mtandao wao kwa kutumia: www.necta.go.tz halafu bonyeza BRN na utapata maswali pamoja na majibu

 

“NIMEKUTANA na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dr Charles E. Msonde na kujadiliana naye kuhusu jinsi gani NECTA na Swahili Hub tunavyoweza kushirikiana katika ukuzaji wa Kiswahili kama vile kutumia maswali ya nyuma ya NECTA kwa kwa ajili ya wadau wa Kiswahili.

Alieleza kuwa NECTA wameacha utaratibu wa zamani wa kuchapisha vijitabu vyenye maswali ya mitihani iliyopita. Wanachofanya sasa ni kuchambua maswali ya wanafunzi kwa mitihani ya darasa la nne na la saba, kidato cha pili na cha nne. Uchambuzi wa maswali haya pamoja na mapedekezo hutayarishwa na kupakiwa katika tovuti wa ajili ya wateja mbalimbali.

Uchambuzi huu umechapishwa kwenye vitabu na kusambazwa mikoani na wilayani. Kwa hiyo wateja wanaweza kupata vitabu hivyo au kusoma kwenye tovuti.

Kwa taarifa zaidi tafadhali pakua katika mtandao wao kwa kutumia: www.necta.go.tz halafu bonyeza BRN na utapata maswali pamoja na majibu.”

STEPHEN MAINA
Mratibu wa Swahili Hub