http://www.swahilihub.com/image/view/-/4843998/medRes/2165166/-/10it2jxz/-/vipuli.jpg

 

Aina mbalimbali za mapambo na sehemu za mwili yanakovaliwa

Mtalii

Mtalii kutoka nchini Australia aangalia vipuli vikiuzwa Desemba 7, 2009 mjini Nakuru. Kipuli ni kisawe cha herini; pambo linalovaliwa masikioni. Picha/MAKTABA 

Na MARY WANGARI

Imepakiwa - Friday, November 9  2018 at  11:57

Kwa Muhtasari

Watu huvaa mapambo ama kwa sababu ya urembo na kujikwatua kwa kawaida au kuonyesha hadhi fulani katika jamii.

 

HAPA natoa ufafanuzi wa aina mbalimbali za mapambo.

 1. kanta - ni rangi nyeusi inayopakwa kwenye mvi (nywele nyeupe) ili nywele zionekana kama nyeusi, hasa na wale wasiopenda uzee.
 2. mkufu - ni kitu chembamba kama mnyororo kinachoundwa kwa madini kama dhahabu, fedha n.k kinachovaliwa shingoni.
 3. bangili - ni pambo la duara linalovaliwa mkononi na wanawake.
 4. herini au kipuli - ni pambo linalovaliwa kwenye ndewe la sikio.
 5. hina - ni rangi inayopakwa miguuni na mikononi mwa wanawake.
 6. kago au utanda - nio ushanga unaovaliwa kiunoni
 7. keekee - ni pambo linalovaliwa na wanawake mkononi kama kikuku au bangili.
 8. kigesi – ni bangili au kikuku kinachovaliwa na wanawake miguuni.
 9. kikuku  - ni pambo la duara linalovaliwa mkononi au mguuni.
 10. kipini - pambo linalovaliwa puani (sehemu ya juu)
 11. kishaufu, hazama au kikero –ni pambo la duara linalovaliwa puani (sehemu ya chini).
 12. mafuta - ni kitu kioevu kinachopakwa mwilini kwa makusudi ya kulainisha ngozi na kunukia vizuri.
 13. Marashi au manukato - haya ni kifurushi, maji au mafuta yanayonukia vizuri yanayoundwa kwa mawaridi na kemikali nyinginezo yanayopakwa mwilini hasa kwapani kwenye shingo na kadhalika.
 14. mshipi - ni mkanda unaovaliwa kiunoni.
 15. ndewe - ni tundu linalotobolewa kwenye sehemu ya chini ya sikio ili kuvaliwa mapambo ya sikioni.
 16. ndonya - ni tundu linalotobolewa katika sikio na mdomo wa juu au mdomo wa chini.
 17. nembo - ni chale zinazochanjwa usoni au kwenye sehemu nyingine za mwili. Nembo zilitumika kuonyesha kubaleghe(kuvunja ungo) kwa wasichana; kubainisha kabila au kuonyesha urembo tu.
 18. njuga - kengele ndogondogo zinazovaliwa shingoni, miguuni na mikononi hasa wakati wa kucheza ngoma za kitamaduni.
 19. nti - ni vijiti vidogo vinavyovaliwa na wanawake masikioni baada ya kutoga ndewe.
 20. nyerere - ni uzi mwembamba wa madini unaovaliwa mikononi na miguuni.
 21. pete - pambo la madini la duara linalovaliwa kidoleni.
 22. rangi ya kucha ni rangi inayopakwa kwenye kucha - hasa na wanawake
 23. tai  - nguo au kitambaa kilichoundwa ili kuvaliwa shingoni juu ya shati haswa wakati wa shughuli rasmi
 24. usinga - nywele za farasi au nyumbu zinazovaliwa mkononi bangili.

Marejeo

Swahili English dictionary

Kamusi ya TUKI