http://www.swahilihub.com/image/view/-/3502202/medRes/1524047/-/h2fie1z/-/desaa.jpg
Na MARY WANGARI
Imepakiwa - Friday, November 9 2018 at 10:07Kwa Muhtasari
Tunaendelea kutoa maelezo kuhusu aina za mavazi.
AINA ZA MAVAZI KATIKA KISWAHILI
Ukaya - kitambaa cha usoni.
Kizibao -koti fupi lisilo na mikono.
Blauzi - nguo ifananayo na shati.
Kimono -kanzu fupi ya mtindo wa Ujapani.
Suti - sketi au suruali pamoja na koti ziliozofanana kwa kitambaa na rangi.
Gauni - kanzu yenye marinda.
Bombo -kaptura. Suruali fupi iishiayo juu ya magoti au kwenye magoti. Pia huvaliwa na wanawake
Shati -vazi la sehemu ya juu ya mwili lililo na ukosi na mikono.
Sweta -fulana nzito ya sufi. Pia huvaliwa na wanawake.
Kitenge - Nguo mfano wa kanga.
Surupwenye au ovaroli -vazi la juu la kuzuia mavazi mengine yasichafuke wakati wa kazi. Pia huvaliwa na wanawake (bwilasuti)
Suruali -vazi la kiunoni hadi kwenye jicho la mguu lenye nafasi mbili za kupenyezea miguu. Pia huvaliwa na wanawake.
Joho - koti pana na refu lililo wazi sehemu ya mbele.
Kilemba -Kitambaa au nguo inayozungushwa kichwani (pia wanawake huvaa)
Jezi – ni vazi au nguo zinazovaliwa na wachezaji wanapocheza uwanjani, mathalani wachezaji wa kandanda, mpira wa vikapu, mpira wa wavu na kadhalika lengo kuu likiwa kutambulisha timu wachezaji wakiwa uwanjani.
Kufanya iwe rahisi kumtambua mchezaji akiwa uwanjani au akifanya kosa.
Mavazi ya ndani
Pia hufahamika kama kocho kwa jumla.
1. Chupi – mavazi ya ndani yanayovaliwa kufunika sehemu nyeti za wake kwa waume
2. Sidiria au kanchiri – mavazi ya wanawake yanayovaliwa kwenye sehemu ya kifua kufunika matiti
3. Shimizi/kamisi – vazi la wanawake linalovaliwa ndani ya mavazi mengine kama vile rinda au gauni
Aina za kofia
1. Chepeo – kofia kubwa yenye ukingo duara uliotokeza nje
2. Tarbushi/kitunga – kofia yenye shada la nyuzi ndefu.
3. Kidotia – kofia ya mtoto.
4. Bulibuli – kofia nyeupe iliyotiwa nakshi.
5. Boshori – kofia ya mtoto
Aina za mavazi ya kidini
Alba – ni kanzu inayotumiwa na yeyote anayehudumia katika ibada za madhehebu mbalimbali za Ukristo.
Amikto – ni kitambaa cheupe cha kitani chenye mikanda kinachotumika katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo ambapo watumishi wengine wanavaa kabla yamavazi mengine ya ibada.
Kwa kawaida amikto huvaliwa kichwani kisha inaachwa iangukie begani lengo likiwa hasa kufunika nguo za kiraia zisitokeze kutoka chini ya kanzu.
Marejeo
Mehrabian na Ferris (1967). Inference of Attitude from Non-verbal Communication in Two Channels". The Journal of Counselling Psychology Vol.31, 1967, pp.248-52.
Witzany, G. (2006 Plant Communication from Biosemiotic Perspective. Plant Signaling na Behavior 1 (4): 169-178.
Witzany, G. (2007 Applied Biosemiotics: Fungal meddelande. Katika: Witzany, G. (Ed). Biosemiotics in Transdisciplinary Contexts. Helsingfors, Umweb, uk. 295-301.