http://www.swahilihub.com/image/view/-/4782502/medRes/2124995/-/b7mv3s/-/usailko.jpg

 

Aina za Mawasiliano

Usaili wa ajira

Usaili wa ajira. Picha/FOTOSEARCH 

Na MARY WANGARI

Imepakiwa - Friday, November 2  2018 at  09:06

Kwa Muhtasari

Zipo aina mbalimbali za mawasiliano.

 

TUMEKUWA tukiangazia mada kuhusu nadharia ya mawasiliano katika Kiswahili.

Katika makala iliyopita, tulianza kutazama kuhusu mabadiliko katika mawasiliano.

Mabadiliko mengine yanayojitokeza katika mawasiliano ni katika taarifa ambayo sasa inaweza kupitishwa kupitia mawimbi na ishara za kielektroniki.

Aina za mawasiliano

Mawasiliano yanaweza kuainishwa katika sehemu tatu jinsi ifuatavyo:

  • Mawasiliano ya ana kwa ana
  • Mawasiliano kati ya binadamu

  • Miondoko ya mwili

  • Toni ya sauti

Ingawa ushawishi wa mawasiliano unaweza ukabadilika kulingana na sababu tofauti mathalan  msikilizaji na msemaji, kwa jumla mawasiliano hulenga kutimiza lengo moja, hivyo basi katika baadhi ya matukio, huwa yanafanana kote duniani.

Mfumo wa ishara, kama vile sauti, kiimbo au uzito wa sauti wa sauti, ishara za mikono, uso, au ishara zilizoandikiwa  ambazo huwasilisha mawazo au hisia.

Swali nyeti ni je, ikiwa lugha inahusu kuwasiliana kwa ishara, sauti, mlio, ishara za uso na za mikono au ishara zilizoandikwa, mawasiliano ya wanyama yanaweza kuchukuliwa kama lugha?

Wanyama hawana lugha iliyoandikwa, lakini baadhi wanadhani mawasiliano ya wanyama yanaweza kuchukuliwa kama lugha ya namna yake.

Hata hivyo, madai hayo hupata pingamizi sana.

Lugha za binadamu zinazozungumzwa na kuandikwa zinaweza kufafanuliwa kama mfumo wa ishara almaarufu leksia na sarufi ambayo ishara hizo huzingatia.

Aidha, neno "lugha" pia hutumika kurejelea sifa bainifu za lugha.

Ni vyema kufahamu kwamba kujifunza lugha ni jambo la kawaida katika utoto wa binadamu.

Lugha nyingi hutumia mifumo ya sauti au ishara  ambazo huwezesha mawasiliano baina ya mtu na wenzake.

Kuna aina nyingi za lugha nazo huwa na sifa bainifu, ingawa nyingi ya sifa hizi huwa na upekee.

Isitoshe, hakuna mgawanyo dhahiri kati ya lugha na lahaja.

Kwa mujibu wa mwanaisimu Weinreich Max "lugha ni lahaja iliyo na jeshi la nchi kavu na la majini.

Lugha za kuundwa kama vile  tarakilishi na maumbo mbalimbali ya hisabati haziko chini  ya sifa bainifu zinazohusisha lugha za binadamu.

Mawasiliano kwa ishara/ kutazama

Huu ni mchakato wa kuwasiliana kwa njia ya kutuma na kupokea ujumbe usiohusisha maneno. Ujumbe kama huo unaweza kuwasilishwa kupitia ishara za uso au mikono, miondoko ya mwili au jinsi ya kukaa; ishara ya uso na kutazamana machoni, mawasiliano kwa njia ya vitu, kama vile mavazi,  jinsi ulivyotengeza nywele au hata kwa michoro, pia kupitia jumla ya njia zilizoandikwa hapo juu, kama vile mawasiliano kupitia tabia.

Marejeo

Mehrabian na Ferris (1967). "Inference of Attitude from Nonverbal Communication in Two Channels". Katika: The Journal of Counselling Psychology Vol.31, 1967, pp.248-52

Witzany, G. (2006 Plant Communication from Biosemiotic Perspective. Plant Signaling na Behavior 1 (4): 169-178.

Witzany, G. (2007 Applied Biosemiotics: Fungal meddelande. Katika: Witzany, G. (Ed). Biosemiotics in Transdisciplinary Contexts. Helsingfors, Umweb, uk. 295-301