http://www.swahilihub.com/image/view/-/3291634/medRes/1377744/-/kepktnz/-/musesimu.jpg

 

Aina za Mawasiliano

Yoweri Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni kando ya barabara akiwa ameketi na akizungumza kwa simu Julai 12, 2016. Picha/HISANI 

Na MARY WANGARI

Imepakiwa - Monday, November 12  2018 at  07:41

Kwa Muhtasari

Mawasiliano ni muhimu katika kuafikia maendeleo katika jamii.

 

KATIKA makala iliyopita, tuliangazia mada kuhusu sifa zinazobadilika katika nadharia ya mawasiliano.

Tuliorodhesha aina mbalimbali ya mawasiliano.

Katika makala ya leo, tutachambua na kutathmini kwa kina kuhusu aina za mawasiliano maalum.

Kuna aina mbalimbali ya mawasiliano maalumu kama yalivyoorodheshwa:

 

Mawasiliano maalumu yanaweza kuorodheshwa katika aina anuwai jinsi ifuatavyo:

  1. Mawasiliano ya kiufundi au ya kitaalamu
  2. Mawasiliano ya mdomo
  3. Mawasiliano ya sayansi au ya kiteknolojia
  4. Mawasiliano ya kimkakati
  5. Mawasiliano ya kiununuzi
  6. Mawasiliano kwa umma
  7. Mawasiliano ya kusaidiwa
  8.  Mawasiliano ya grafiki
  9. Mawasiliano yanayofahamika kwa urahisi
  10. Mawasiliano yasiyo na ukatili

 

Mawasiliano ya mdomo

Mbinu hii inahusisha mchakato ambapo habari hupitishwa kutoka kwa mzungumzaji hadi kwa msikilizaji kupitia mdomo. Hata hivyo, vielezi vinaweza kutumiwa kusaidia katika mchakato huu.

Mpokezi au msikilizaji anaweza kuwa mtu mmoja,kikundi au hata hadhira. Ni vyema kufahamu kwamba kuna aina kadha za mawasiliano ya mdomo ikiwemo:

hotuba, mawasilisho, majadiliano miongoni mwa mengine.

Aghalabu hata hvyo, wakati wa mawasiliano ya ana kwa ana miondoko ya mwili na toni ya sauti huwa na athari kuu kushinda maneno halisi yanayosemwa.

Jambo la msingi kukumbuka ni kuwa maudhui au neno linalotumiwa silo litakaloamua sehemu ya mawasiliano mazuri ambapo kigezo muhimu ni jinsi ujumbe unavyowasilishwa kwa kuwa huwa na athari kubwa kwa msikilizaji.

Kama mzungumzaji, ni sharti uvutie na unase umakini wa hadhira na uhusiane nao.

Kwa mfano, watu wawili wanaosema kichekesho, mmoja wao anaweza kuifanya hadhira kuangua kicheko kutokana na miondoko mizuri ya kimwili na toni ya sauti.

Mtu wa pili anayewasilisha kichekesho kile kile kwa maneno yale yale anaweza kukosa kuibua hisia miongoni mwa hadhira na kuifanya imtazame tu.

Aidha, katika mawasiliano ya mdomo, inawezekana kutumia vielelezo ili kuwezesha kuwasilisha habari kwa usahihi zaidi.

Aghalabu tarakilishi huweza kutumia katika mawasilisho kama vile mihadhara ili kuwezesha au kuboresha mchakato wa mawasiliano.

Hata hivyo,  hatuwezi kuwasiliana kwa kutumia vielelezo pekee kwa sababu hayo hayatahitimu kuitwa mawasiliano yam mdomo.

Marejeo:  

Mehrabian na Ferris (1967). "Inference of Attitude from Nonverbal Communication in Two Channels". Katika: The Journal of Counselling Psychology Vol.31, 1967, pp.248-52.

Witzany, G. (2006 Plant Communication from Biosemiotic Perspective. Plant Signaling na Behavior 1 (4): 169-178.

Witzany, G. (2007 Applied Biosemiotics: Fungal meddelande. Katika: Witzany, G. (Ed). Biosemiotics in Transdisciplinary Contexts. Helsingfors, Umweb, uk. 295-301.