Akisami

Na MARY WANGARI

Imepakiwa - Monday, November 5  2018 at  06:56

Kwa Muhtasari

Akisami ni nambari inayowakilisha sehemu fulani ya kitu kizima (fraction).

 

AKISAMI inaweza kuelezwa kama nambari inayowakilisha sehemu fulani ya kitu kizima (fraction). Katika akisami, ni lazima pawepo nambari ya juu na ya chini na hutenganishwa na kijistari cha alama ya mkwaju au mlazo (/).

Kwa mfano: 1/2 (one over two or half ) huitwa nusu.

Akisami hutumiwa kuonyesha sehemu ya kitu kizima. Kwa mfano, ukigawa kilo moja kwa vijisehemu vinne vinavyotoshana, kila kisehemu kitakuwa na uzani wa robo kilo (sehemu ya nne au moja ya nne ) ya kilo.

1/#

JINA

MFANO

1/2

nusu

1/2

nusu

moja ya mbili

1/3

thuluthi

2/3

thuluthi mbili

mbili ya tatu

1/4

robo

2/4

robo mbili

mbili ya nne

1/5

humusi

3/5

humusi tatu

tatu ya tano

1/6

sudusi

4/6

sudusi nne

nne ya sita

1/7

subui

6/7

subui sita

sita ya saba

1/8

thumuni

7/8

thumuni saba

saba ya nane

1/9

tusui

3/9

tusui tatu

tatu ya tisa

1/10

ushuri

6/10

ushuri sita

sita ya kumi

1/100

asilimia

72/100

asilimia sabini na mbili

sabini na mbili ya mia moja

 

Baadhi ya mifano kuhusu tarakimu ni kama ifuatayo:

Kwa mfano:

Andika akisami zifuatazo kwa maneno:

1.     240/295  - mia mbili arobaini ya mia mbili tisini na tano

2.     41/45  - arobaini na moja ya arobaini na tano

3.     26/51 -  ishirini na sita ya hamsini na moja

4.     59/74  -  hamsini na tisa ya sabini na nne

5.     1/5  -  humusi

Andika tarakimu zifuatazo kwa nambari

1.     sufuri - 0

2.     mia tatu ishirini na tano - 325

3.     sabini na tatu elfu, na mia nane hamsini na tatu- 73853

4.     mia tano sabini na nane elfu, na mia tatu hamsini na tisa - 578359

5.     mia sita tisini na sita milioni, na mia tisa tisini na nane elfu, na mia saba ishirini na tatu - 696998723

Andika nambari zifuatazo kwa maneno/herufi:

1.     4  -nne

2.     956 -  mia tisa hamsini na sita

3.     680 -  mia sita themanini

4.     4521903 -  milioni nne, na mia tano ishirini na moja elfu, na mia tisa na tatu

5.     100,000 – laki moja

Marejeo:

Swahili Oxford Living Dictionary